Na Amiri Kilagalila,Njombe

Viongozi wa dini na mila wilayani Wanging'ombe mkoani Njombe wametakiwa kutumia nafasi zao kuzungumza na wananchi walio kwenye maeneo yao umuhimu wa kulinda amani hasa katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi unaotarajia kufanyika hivi karibuni oktoba 28 mwaka huu.

Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Wanging'ombe Lauter Kanoni wakati akifungua mkutano wa kamati ya amani ya wilaya hiyo uliyofanyika leo kwenye wilaya hiyo.

Amesema kupitia kikao hicho ana imani kuwa wadau walioshiriki watakuwa mabalozi wazuri ambao watafikisha ujumbe wa kutunza amani hasa kipindi hiki kwa kuwa wanaaminika na wananchi.

Aidha amesema kuelekea uchaguzi mkuu wa madiwani, wabunge na raisi kwenye wilaya ya Wanging'ombe vyama vitakavyoshiriki ni vitatu ambavyo CCM na Chadema vitashiriki kwenye ngazi za ubunge na udiwani lakini chama cha CUF kitashiriki kwenye udiwani pekee.

"Kuna vyama vitatu vitakavyoshiriki kwenye uchaguzi wilayani hapa CCM,Chadema na CUF lakini kwa nafasi ya ubunge ubunge vitashiriki vyama viwili CCM na Chadema" amesema Kanoni.

Nao viongozi wa kidini kutoka madhehebu ya kikristo wa kiislamu wakiwemo Mchungaji Masaliwa Samsoni kutoka kanisa la Moraviani kutoka Igwachanya na shekhe wa wilaya ya Wanging'ombe  Mbaraka Mpanye wamewataka viongozi wa dini kuacha kujiingiza katika masuala ya kisiasa na badala yake wafanye kile wanachopaswa kufanya kwani kufanya hivyo ni kuwagawa wananchi na taifa kwa ujumla.

"Haitakuwa busara sana sisi watumishi wa mungu tukaacha lile ambalo mungu ametuita kulifanya tukaanza kuingia kwenye siasa kufanya hivyo tutawagawa waumini wetu" Amesema Samson.

"Asilimia kubwa ya wananchi wa Wanging'ombe waumini wetu lakini wana itikadi tofauti leo hii watumishi wa mungu tukiingia kwenye siasa itatuletea shida kwani wale tunaowangoza wana vyama tofauti" Amesema Shekhe Mbaraka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...