SIKILIZA WIMBO WAKE WA MWISHO  'YELLOW CARD'  
Freddy Supreme Ndala Kasheba akitumbuiza enzi za uhai wake katika Bustani ya Mnazi Mmoja miaka ya 90, wakati huo akiwa na Orchestra Safari Sound WANA OSS na mtindo wao wa 'Dukuduku'. Hapa alikuwa anaanza kupiga wimbo wa DUNIA MSONGAMANO katika mtindo wa  'Chunusi'. Hii ni mojawapo ya taswira nyingi za Ankal zilizokuwa zikipamba kurasa za Daily News enzi hizo za Black & White na ilizua utata kwani ilidhaniwa kuwa imefanyiwa utundu kwa kumtoa kiongozi na kumuweka mwanamuziki badala yake, wakiwa na imani kwamba mwanamuziki hawezi kuvutia umati namna hiyo. Ankal alipoonesha negative na kuthibitishwa kuwa ni picha halisi mambo yakaisha. 


Leo tunatimiza miaka saba toka kifo cha mwanamuziki mahiri Ndala Kasheba. 
Freddy Supreme au maarufu kwa wengi kama Ndala Kasheba alianza kujifunza gitaa akiwa na umri mdogo wa miaka 12, alipofika umri wa miaka 17 alikuwa tayari mwanamuziki mahiri wa Orchestre Fauvette, akiwa na wanamuziki wenzie kama Baziano Bweti na King Kiki. Mwaka 1968.

Kundi zima la watu tisa lilipanda mashua za walanguzi wa chumvi na kuvuka Ziwa Tanganyika toka Kongo hadi Tanzania kwa kupitia Kigoma. Kundi hili, Orchestre Fauvette,  lilitikisa anga za  Tanzania kwa vibao ambavyo wengi huvikumbuka mpaka leo, kama vile Fransisca, Vivi, Nono na Kalemie, Zula, Jacqueline

Kasheba aliweza kuimarisha jina lake zaidi alipolifanya maarufu gitaa la nyuzi kumi na mbili, mwenyewe akiliita nyuzi dazani, hasa alipoanza kulipiga kwa mtindo wa Dukuduku akiwa Safari Sound Orchestra. Pamoja na bendi hizo Kasheba pia alipitia  Safari Nkoy, Zaita Muzika, Kasheba group, pia alipita Maquis, na kwa wiki chache alipitia Tancut Almasi.
Kasheba alifariki 22 Oktoba 2004 akiwa na miaka 58.

MOLA AIWEKA MAHALI PEMA ROHO YAKE
AMINA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Nakumbuka kukutana na Ndala Kasheba miaka ya tisini pale Kawe Club. I have to say he was one of the best artist that I have ever known. Music never day,Kasheba ataishi milele.

    ReplyDelete
  2. Unajua Ankal,shughuli zake na twasira ya mafoto foto picha,yalizua utata mara nyingi sana sana,nakumbuka siku aliyopiga picha ndege iliyokua inavutwa na trekta pale uwanja ndege Dar,miaka ya 80s, alafu picha ingine iliyozua soo ni ile ya Unyagoni Zanzibar ! kuanzia hapo tulijua kuwa tunaye mtu asiye wa kawaida katika upigaji picha hapa Bongo

    ReplyDelete
  3. Kasheba tunakukumbuka! Hiki kibao kina ujumbe mkubwa sana!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...