"BIASHARA"
Showing posts with label BIASHARA. Show all posts
NAIBU Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dennis Londo amewataka wafanyabiashara wa Kariakoo jijini Dar es Salaam kutumia fursa ya uwepo wa tamasha la Kariakoo Festival kukuza biashara, uwekezaji na kutumia fursa ya masoko ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika kukuza masoko ya bidhaa zao.

Mhe Londo ameyasema hayo leo Septemba 25, 2026 jijini Dar es Salaam wakati akizindua rasmi tamashahilo kwa msimu wa tatu na kuongeza kuwa sekta binafsi ina mchango mkubwa wa takribani asilimia 70 kufanikisha Dira ya Nchi kwa Mwaka 2050 kwenye eneo la uunganishaji wa biashara na ongezeko la mnyororo wa thamani.

Mhe Londo amesema Serikali inatambua mchango mkubwa unaotolewa na Soko la Kariakoo kwani linachangia kwa kiasi kikubwa kwenye uchumi wa nchi, soko la ajira na mzunguko wa fedha na injini ya biashara.

Akizungumza kabla ya mgeni rasmi, Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo ya Masoko ya Kariakoo Bw.Jossam Mzava amesema umoja wa wafanyabiashara wa soko hilo umeweza kuwaunganisha wadau wote kwenye sekta ya biashara ndani na nje ya nchi kwa maslahi mapana ya kukuza mapato hapa nchini.

Tamasha hilo lililobeba kaulimbiu ya; 'Bei shwaa shwaaa' ikimaanisha bei imepunguzwa linawakutanisha wafanyabiashara mbalimbali kwa lengo la kujadili fursa mbalimbali na namna wanavyoweza kutumia masoko ya ndani na nje.

Katika hatua nyingine, Mhe Londo ameziagiza taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara kuanza kushiriki tamasha hilo ili kutoa fursa kwa wafanyabiashara kupata huduma na elimu juu ya upatikanaji wa leseni, ushindani wa kibiashara na nembo za ubora.









 Na Karama Kenyunko Michuzi tv 

MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umefanikiwa kukusanya jumla ya Sh150.04 bilioni kutokana na tozo za matumizi ya Daraja la Nyerere lililopo Kigamboni tangu kuanza kutumika kwake.

Makusanyo hayo yamepatikana katika kipindi cha kuanzia Mei 2016 hadi Juni 2026, kufuatia uzinduzi rasmi wa daraja hilo uliofanyika Aprili 2016.

Akizungumza leo, Septemba 21, 2026, katika kikao kazi na wahariri wa vyombo vya habari kilichoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba, amebainisha kuwa NSSF ilifadhili mradi huo kwa asilimia 100 badala ya asilimia 60 iliyopendekezwa awali.

“Mradi wa ujenzi wa daraja hilo uligharimu shilingi 345.20 bilioni, ambapo bilioni328.74 zilitumika moja kwa moja kwenye ujenzi na shilingi 16.46 bilioni zilitumika kuwalipa fidia wananchi waliopisha mradi.”

Ameeleza kuwa mpango wa uwekezaji uliwekwa kwa muundo wa kimkataba unaoelekeza fedha zote kurejeshwa ndani ya miaka 30 ya uendeshaji kupitia tozo.

Kutokana na mpango huo wa kurejesha uwekezaji ndani ya miaka 30, waendesha vyombo vya moto wanatarajiwa kuendelea kulipa tozo kwa takriban miaka 20 zaidi iliyobaki baada ya miaka 10 ya kwanza ya makusanyo kukamilika.

Amesema, katika kuhakikisha miundombinu hiyo inabaki katika ubora wa hali ya juu na salama kwa watumiaji wote, NSSF imetumia Sh25.81 bilioni kwa ajili ya gharama za uendeshaji, ulinzi pamoja na matengenezo ya mara kwa mara ya daraja hilo.

Aidha, Mshomba amesema kufuatia kuwepo kwa maoni na malalamiko kutoka kwa wananchi wanaoomba viwango vya tozo vipunguzwe zaidi, Serikali imeanza kupitia upya viwango vya tozo zinazolipwa na watumiaji wa daraja hilo.

Mshomba ameeleza kuwa Serikali imeunda timu ya wataalamu inayofanyia kazi suala hilo, na ripoti inatarajiwa kuwasilishwa serikalini hivi karibuni. Mchakato huu unafanyika ingawa viwango vya tozo za kuvuka tayari vilishawahi kushuka huko nyuma.

Timu hiyo inachambua hali halisi ili kutoa mapendekezo yatakayosaidia kuamua namna bora ya kuendelea na utaratibu wa tozo pamoja na kurejesha fedha zilizowekezwa. Miongoni mwa njia zinazotazamwa baada ya ripoti kuwasilishwa ni pamoja na uwezekano wa Serikali kuilipa NSSF fedha zilizowekezwa kwenye mradi huo.

Licha ya mchakato huo wa mapitio kuendelea, Mkurugenzi Mkuu alisisitiza kuwa makusanyo ya tozo na shughuli zote za daraja zinaendelea kama kawaida kwa mujibu wa mpango uliowekwa.

Ujenzi wa Daraja la Nyerere umeleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi na kijamii kwa kupunguza kero ya msongamano, kurahisisha usafiri kati ya Kigamboni na katikati ya jiji, na kuwa chachu ya ukuaji wa sekta za nyumba, biashara na utalii. NSSF imeahidi kuendelea kulisimamia kwa uwazi ili kulinda maslahi ya wanachama na Mfuko.





TCB Chief Executive Officer and Managing Director 
Adam Charles Mihayo



By Issa Michuzi


The Tanzania Commercial Bank (TCB) is again footing the bill for the annual gathering of board chairpersons and chief executives from public bodies, signing on as principal sponsor for the third year in a row.


The event, hosted by the Office of the Treasury Registrar, will take place in Arusha from 28 to 30 September.


TCB Chief Executive Officer and Managing Director Adam Charles Mihayo confirmed the support today, 9 September 2026, at a breakfast briefing with news editors at the Hyatt Kilimanjaro in Dar es Salaam. 


The bank, he said, is “honoured to participate in the important gathering and proud to serve as its principal sponsor for the third consecutive time.” 


He added, “We greatly appreciate the honour extended to us by the Office of the Treasury Registrar to participate in this important meeting.”


For Mihayo, the forum is no mere ceremony. Over three days, leaders from public institutions and corporations will swap experiences, audit their own performance, and hunt for workable ways to improve service delivery and deepen their contribution to national development.


He also pulled the media into that mission. 


When coverage is steady and clear, he said, Tanzanians can track the work of the Treasury Registrar and the bodies it oversees. “Better public understanding keeps those institutions moving toward greater transparency and accountability”, he added.


TCB’s lineage reaches back to 1925, when it opened as the Tanganyika Post Office Savings Bank. 


Today it is a full commercial bank, the government holding the majority stake, with other public institutions owning the rest. 


The bank offers retail, SME, corporate, treasury, and digital banking, and says its focus remains on innovative financial solutions and wider financial inclusion.


Renewing the sponsorship, the TCB chief adds, is one part of its broader promise to back efforts that strengthen public institutions and push Tanzania’s development agenda forward.

 BANK of Africa Tanzania imeingia makubaliano ya ushirikiano na kampuni ya CFAO Mobility  katika kuwezesha upatikanaji wa mikopo ya magari kwa watu binafsi, wataalam, wajasiriamali, wakulima na wafanyabishara mbalimbali nchini kote.


Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo jijini Dar es Saaam leo, Mkuu wa kitengo cha wateja wakubwa wa Bank of Africa Tanzania, Khalifa Zidadu, amesema ushirikiano huo unajibu hitaji linaloongezeka la kuwezesha upatikanaji wa mikopo ya  magari ili  kurahisisha usafiri, usafirishaji, biashara za utalii na huduma nyinginezo zinazozidi kupanuka zinazohitaji usafiri.

"Changamoto kwa wateja wengi sio lazima iwe hitaji la gari, lakini uwezo wa kukidhi gharama za awali huku ukiendelea kuwa na mtiririko wa pesa kwa biashara na matumizi mengineyo. Ushirikiano huu unashughulikia pengo hilo kwa kuchanganya chapa za magari zinazoaminika za CFAO na utaalamu wa magari na uwezo wa kutoa mikopo wa Bank of Africa Tanzania, na kuwapatia wateja njia  sahihi ya kukopa gari wanalohitaji bila kuwa na  shinikizo lisilo la lazima kwenye ukwasi wao,"Amesema Zidadu.


Ushirikiano huu umekuja wakati ambapo upatikanaji wa mkopo unaofaa unabaki kuwa kipaumbele muhimu kwa sekta ya biashara ndogo na za kati ya Tanzania. Bank of AfricaTanzania imeangazia mipango inayolenga kuboresha upatikanaji wa mikopo kwa biashara ndogo na za kati, hasa biashara zenye miradi inayoweza kutegemewa lakini haina  mali za kuweka dhamana inayowezesha kupata mkopo.


Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa CFAO Mobility Tanzania, Ali TIMIMI,  amesema ushirikiano huo utasaidia kufanya umiliki wa vyombo vya usafiri kuwa rahisi kwa kuwaunganisha wateja na magari sahihi kwendana na matakwa yao  na njia rahisi ya kupata mkopo kuweza kuyamiliki.

"Kwetu CFAO Mobility Tanzania, kumiliki usafiri wa kuaminika ni kichocheo muhimu cha fursa za kiuchumi. Kwa wateja wetu wengi, gari si njia tu ya usafiri; ni mali inayosaidia kuendesha biashara, kuwahudumia wateja wao, kukuza shughuli zao na kujenga thamani. Ushirikiano wetu na Bank of Africa Tanzania  unahusu kuwezesha uwepo wa  fursa ya kumiliki chombo cha usafiri,"alisema TIMIMI.


TIMIMI aliongeza kuwa  ushirikiano wa Bank of Africa Tanzania ambayo imebobea katika kutoa huduma za mikopo kwa wateja wake na utaalamu wa magari wa CFAO ambayo inauza aina mbalimbali za chapa za magari zinazoaminika utafanikisha kuunda  safari ya wateja waliounganishwa zaidi; kuanzia kuchagua gari sahihi hadi kupata mkopo unaohitajika kumiliki chombo na mchakato wa kukipata  ulio wa moja kwa moja, wa vitendo  unaokidhi mahitaji ya  wateja  wa pande zote mbili.

Naye, Mkuu wa kitengo cha wateja Binafsi wa Bank of Africa Tanzania, Asupya Nalingigwa, amesema huduma hii ya kuwezesha kukopa magari inawawezesha wateja  watakaokidhi vigezo kulingana na uwezo wao wa kulipa, kwa kipindi cha malipo cha hadi miezi 48, kwa ununuzi wa magari mapya kutoka CFAO.


Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya CFAO, Tharaia AHMED amesema kwamba mpango huo wa ushirikiano unafungua fursa za kiuchumi kwa wafanyabiashara , wakulima na wajasirimali katika usafirishaji wa bidhaa na huduma zao.

“Magari yetu ni yenye ubora wa hali ya juu na ya uwezo wa kutunza mazingira kwahiyo ni fursa ya kipekee kwa wakulima wanaosafirisha bidhaa kutoka shambani mpaka kwenye soko na wasafirshaji wa bidhaa mbalimbali nje ya nchini hii pia ni fursa kwao pia,” amesema Tharaia.


Na Said Mwishehe,Michuzi TV

KAMPUNI ya Jubilee Life Insurance Tanzania imezindua bidhaa tatu mpya za bima ya maisha zinazolenga kuwasaidia Watanzania katika uwekaji akiba, maandalizi ya elimu, ulinzi wa maisha na mahitaji mengine ya kifedha ya baadaye.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa bima hizo jijini Dar es Salaam Ofisa Mtendaji Mkuu wa Jubilee Life Insurance Tanzania, Helena Mzena, amezitaja bima walizozindua ni Fanaka Plus, Smart Education Insurance Plan na Akiba Flex.

“Kwa miaka zaidi ya 10 tumekua tukitoa suluhisho la bima za maisha ambazo kimsingi zinampa mteja wetu nafasi ya kutimiza malengo yake aliyojiwekea kama vile kusomesha Watoto Pamoja na kukuza biashara zao huku wakiwa na ulinzi wa maisha yao.

“Kwa kujali na kuzingatia matakwa ya Watanzania wote, kwa Pamoja kama taasisi tumeona ni vyema kuendelea kuboresha bidhaa zetu hizi ili kuwa na manufaa zaidi kwa wateja wetu,”amesema Mzena 

Akieleza zaidi amesema bima yao kwa ajili ya uwekezaji ambayo ilikua ikijulikana kama FANAKA LIFE PLAN, sasa inaitwa FANAKA PLUS ikiwa na maboresho zaidi yanayomhakikishia mteja wetu ongezeko la fedha zake, ulinzi wa maisha yake Pamoja na amani ya moyo akijua hakuna janga au changamoto itayozuia utimiaji wa ndoto zake, yote haya na mengine mengi sasa yanapatikana ndani ya FANAKA PLUS.

Pia amesema wameboresha bima yetu ya Maisha ya Akiba flex ambayo yenyewe inamruhusu mteja wao kuchangia kwa ajili ya mkataba wake wa bima ya maisha huku ikimpa uhuru wa machangio yake pale anapohitaji.

“Hatukuwaacha nyuma wazazi ambao wanajali elimu ya Watoto wao, na rasmi tunatambulisha kwenu SMART EDUCATION, hii ni bima ya maisha kwa ajili ya maandalizi ya ada ya mtoto, hapa mteja wetu anaweka akiba yake ili kuhakikisha ndoto za kielimu za Watoto wake zinatimia…

“Huku akiwa na ulinzi wa maisha yake na uhakika wa kwamba sisi Jubilee Life Insurance tutawajibika kutimiza ndoto hizo hata bila uwepo wa huyu mzazi,”amesema.

Ameongeza bima zote hizo ni uthibitisho wa kwamba sisi kama taasisi tunajali na kuthamini ndoto za wateja wetu na kuhakikisha ndoto hizo zinafikiwa bila stress zozote.”Sisi tunasema, Bima ya Maisha ni ya kila mmoja.”

Kwa upande wake mwakilishi wa Kamishna kutoka TIRA, Alex Rocky amesema ubora wa bidhaa za bima haupaswi kupimwa kwa idadi ya watu waliojiunga pekee, bali pia kwa kiwango ambacho bidhaa hizo zinawawezesha wananchi kuelewa na kutumia huduma za bima kwa ufanisi.

“Uelewa hujenga imani, na imani huongeza matumizi endelevu ya bima,” amesema.

Amesema Tanzania inaingia katika hatua muhimu ya kujenga familia zenye uwezo wa kustahimili misukosuko ya kifedha na taifa lenye uimara wa kifedha, huku bima ya maisha ikiwa na nafasi muhimu katika kulinda wananchi na kusaidia mipango yao ya muda mrefu.

Amesema matumizi ya lugha ya Kiswahili katika bidhaa hizo ni hatua muhimu katika kuongeza uelewa na ujumuishi wa huduma za bima nchini.

“Matumizi ya lugha inayoeleweka katika kutoa taarifa na elimu kuhusu bima huwawezesha wananchi kuelewa kwa usahihi faida, masharti na wajibu wao kabla na baada ya kujiunga na bima,” amesema.

Pia amesema bima ya maisha ni nyenzo muhimu katika kujenga usalama wa kifedha na uwezo wa kustahimili changamoto kwa mtu binafsi, familia na taifa kwa ujumla


Wafanyabiashara wa Tanzania wanaoagiza bidhaa kutoka China sasa wanaweza kuwalipa wazabuni wao moja kwa moja kwa kutumia Shilingi za Tanzania, bila kulazimika kwanza kubadilisha fedha hizo kuwa Dola za Marekani kabla ya kulipwa kwa Yuan ya China.

Huduma hiyo mpya ilikuwa miongoni mwa mada kuu katika Jukwaa la Biashara Tanzania na China lililoandaliwa na Stanbic Bank Tanzania katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam. Jukwaa hilo liliwakutanisha wafanyabiashara wa Tanzania, wawakilishi wa biashara kutoka China pamoja na taasisi mbalimbali za serikali na biashara kujadili fursa za kuimarisha biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China.

Mfanyabiashara wa Dar es Salaam, *Lulu Kheri*, alisema huduma hiyo itasaidia kupunguza changamoto za mabadiliko ya viwango vya fedha na gharama zinazoongezeka katika mchakato wa kufanya malipo ya biashara.

“Kinachotuhusu sisi wafanyabiashara ni kiwango cha kubadilisha fedha, gharama na uhakika kwamba mzabuni wetu atapokea malipo yake. Huduma hii inarahisisha mchakato na inaweza kusaidia kulinda faida yetu,” alisema Kheri.

Huduma ya malipo ya moja kwa moja ya *Shilingi ya Tanzania kwa Yuan ya China, iliyozinduliwa tarehe 12 Agosti 2026, inawezeshwa kupitia mfumo wa **Cross-Border Interbank Payment System (CIPS)*. Mfumo huo unapunguza hatua ya kubadilisha Shilingi kuwa Dola za Marekani kabla ya kubadilishwa kuwa Yuan, hivyo kupunguza gharama na kurahisisha mchakato wa malipo.

*Fredrick Max*, Mkuu wa Idara ya Biashara Stanbic Bank Tanzania, alisema huduma hiyo inalenga kutatua changamoto ya muda mrefu kwa wafanyabiashara wanaofanya biashara na China.

“Kwa muda mrefu, wafanyabiashara walilazimika kubadilisha Shilingi kuwa Dola za Marekani na baadaye kuwa Yuan. Huduma yetu ya moja kwa moja ya Shilingi kwa Yuan inaondoa hatua hiyo ya ziada, na kuwasaidia wateja kuokoa muda, kusimamia gharama na kufanya miamala kwa ufanisi zaidi,” alisema Max.

Aliongeza kuwa Stanbic Bank Tanzania, kupitia mtandao wa *Standard Bank Group* na ushirikiano wake wa kimkakati na *Industrial and Commercial Bank of China (ICBC)*, pia inasaidia biashara za Tanzania kupata wazabuni wa kuaminika nchini China na kufikia masoko ya wanunuzi wa China.

Katika mjadala wa jukwaa hilo, *Alfred Ngelula*, Mkuu wa Dawati la China (TISEZA), alisema kupunguza gharama za kubadilisha Yuan na Shilingi kunaweza kuongeza ushindani wa Tanzania katika kuvutia wawekezaji kutoka China.

Kwa upande wake, Benson Nkini Afisa Biashara Mwandamizi wa Tanzania Trade Development Authority (TanTrade), alisisitiza umuhimu wa Tanzania kuongeza mauzo ya bidhaa zilizoongezwa thamani katika soko la China.

Stanbic Bank Tanzania imeshiriki kuwapeleka wateja wake katika *China International Import Expo* kwa miaka minne mfululizo. Maonesho yanayofuata yanatarajiwa kufanyika Novemba 2026, yakitoa fursa kwa biashara za Tanzania kukutana na wanunuzi, wazalishaji na washirika wa kibiashara kutoka China.

Wafanyabiashara wanaweza kupata huduma ya malipo ya moja kwa moja ya Shilingi kwa Yuan kupitia matawi yote ya Stanbic Bank Tanzania, huku wateja waliopo wakitumia pia njia za kidijitali baada ya kukamilisha taratibu zinazohitajika.
Mkuu wa Idara ya Biashara na Wateja wa Kibiashara wa Stanbic Bank Tanzania, Fredrick Max, akizungumza na wafanyabiashara wa Tanzania na China pamoja na wadau mbalimbali katika Jukwaa la Biashara la Stanbic lililofanyika jijini Dar es Salaam. Jukwaa hilo lililenga kuwaelimisha wafanyabiashara kuhusu huduma ya malipo ya moja kwa moja kati ya Shilingi ya Tanzania na Yuan ya China, inayorahisisha miamala na biashara kati ya nchi hizo mbili.



Equity Group Holdings Plc imetangaza matokeo imara ya nusuya kwanza ya mwaka 2026, ikirekodi ongezeko la asilimia 32 la faida baada ya kodi kufikia TZS bilioni 841.75, kutoka TZS bilioni 640.1 zilizorekodiwa katika kipindi kama hicho mwakauliopita. Nchini Tanzania, Equity Bank Tanzania pia imeonyeshaukuaji imara baada ya kufikisha faida kabla ya kodi ya TZS bilioni 55.5, huku faida baada ya kodi ikikua kwa asilimia 82, ishara ya kuonesha kasi ya biashara, utekelezaji wenye nidhamuna kuongezeka kwa imani ya wateja katika soko.

Matokeo haya yanaonesha uimara wa Equity, uwezo wake wakukua katika mazingira ya biashara yanayobadilika namafanikio ya mkakati wake wa kutumia teknolojia kuboreshahuduma za kifedha. Ukuaji huu umechangiwa na kuimarika kwamapato, ufanisi wa uendeshaji, usimamizi thabiti wa viashiriavihatarishi na uwekezaji endelevu katika huduma za kifedhazinazoendeshwa na teknolojia, ambazo zinabadilisha namnawateja wanavyopata na kutumia huduma za benki.

Katika ngazi ya Equity Group , ukuaji huu unaakisi mafanikioya mageuzi ya muda mrefu ya taasisi hiyo kuelekea kuwa mtoahuduma za kifedha mwenye mifumo mbalimbali, ambaye nguzoyake kuu inajengwa kwenye teknolojia na uhusiano wa karibuna wateja. Equity inaendelea kuimarisha namnainavyowahudumia wateja kupitia mifumo ya kidijitali, matawi, mawakala na njia za malipo kwa wafanyabiashara.

Kwa Equity Bank Tanzania, matokeo ya nusu ya kwanza yamwaka yanaimarisha nafasi ya Benki katika kusaidia watubinafsi, wajasiriamali, Wafanyabiashara wadogo na wa kati, makampuni na taasisi za sekta ya umma. Matokeo hayayanaonyesha pia kuongezeka kwa imani ya wateja katika uwezowa Benki kutoa suluhisho za kifedha zinazogusa mahitaji halisiya kila siku, ikiwemo ukuaji wa biashara, malipo, akiba, mikopona usimamizi wa fedha.

Teknolojia imeendelea kuwa kichocheo muhimu cha matokeohaya. Katika Equity Group, asilimia 98.3 ya miamala yote ilifanyika nje ya matawi, huku asilimia 89.7 ya miamalaikichakatwa kupitia mifumo ya kidijitali. Mwenendo huuunaonyesha jinsi wateja wanavyozidi kuchagua huduma rahisi, salama na zinazopatikana kwa wakati wowote, na unaonyeshanafasi muhimu ya teknolojia katika kuongeza ufanisi, kuboreshahuduma na kurahisisha maisha ya wateja.
Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo hayo, MkurugenziMtendaji wa Equity Group, Dkt. James Mwangi, alisemamatokeo ya nusu ya kwanza ya mwaka 2026 yanaonyeshamafanikio ya safari ya muda mrefu ya Equity kujijenga kamataasisi ya kifedha ya kikanda, yenye huduma mbalimbali nainayowezeshwa na teknolojia.

“Matokeo yetu ya nusu ya kwanza ya 2026 yanaonyeshamafanikio ya mageuzi yetu ya makusudi kuelekea kuwa kundi la huduma za kifedha lenye huduma mbalimbali, linalowezeshwana teknolojia. Tunajenga taasisi iliyo tayari kwa siku zijazo, yenye uwezo wa kukua, iliyo salama na yenye kuleta matokeo, ikijengwa juu ya uwezo wa kidijitali, kuongeza ujuzi wawafanyakazi na utamaduni wa utekelezaji wenye nidhamu,” alisema.

Dkt. Mwangi aliongeza kuwa Equity inaendelea kujibadilishakutoka benki ya kawaida na kuwa taasisi jumuishi ya kifedhainayowezeshwa na teknolojia, yenye uwezo wa kukusanyamtaji, kuunganisha mifumo ya biashara na kuchochea ustawijumuishi na endelevu barani Afrika.

Kwa Equity Bank Tanzania, matokeo haya yanaweka msingiimara wa kuongeza kasi katika nusu ya pili ya mwaka 2026. Kipaumbele cha Benki kitakuwa kubadilisha kasi hii Ili kuwa nathamani kubwa zaidi kwa wateja, hususan kupitia suluhisho za malipo kwa wafanyabiashara zinazorahisisha makusanyo, kuongeza ufanisi wa biashara na kupunguza utegemezi wa fedhataslimu.
Miongoni mwa maeneo muhimu ya kimkakati ni Equity Lipa Namba, suluhisho linalowawezesha wafanyabiashara kupokeamalipo papo hapo, bila makato, kutoka benki yoyote au mtandaowowote wa simu, na kupata fedha zao wakati wowote. Kwa wafanyabiashara wadogo, wa kati na makampuni, hiiinamaanisha makusanyo ya haraka, mtiririko bora wa fedha, kupunguza hatari za kushughulika na fedha taslimu na kuwapawateja njia rahisi zaidi ya kulipa.

Kupitia Equity Lipa Namba, Benki inaendeleza ajenda yake yamageuzi ya kidijitali kwa kuwapa wafanyabiashara suluhisho la malipo linaloendana na mahitaji ya biashara za kila siku. Huduma hii inasaidia mauzo ya kila siku, makusanyo yawafanyabiashara na matumizi ya akaunti, huku ikichocheaukuaji wa amana, ukuaji wa biashara na matumizi mapana yamalipo ya kidijitali nchini Tanzania.

Pamoja na hilo, Equity Bank Tanzania itaendelea kuhamasishamatumizi ya Equity Mobile, huduma inayowawezesha watejakusimamia fedha zao kwa urahisi, kufanya miamala, kulipa bilina kupata huduma za benki mahali popote walipo. Benki pia itaendelea kuwekeza katika ulinzi kupitia bima, ili kuwasaidiawatu binafsi, wafanyabiashara na biashara kulinda kilewanachokijenga, kudhibiti vihatarishi na kukua kwa kujiaminizaidi.

Kuangalia mbele, Equity Bank Tanzania itaendelea kuwekamteja mbele, kuunga mkono ukuaji wa biashara na kuchangiamaendeleo ya uchumi wa Tanzania. Matokeo imara ya nusu yakwanza ya mwaka yanaimarisha dhamira ya Benki ya kutoasuluhisho za kifedha zilizo rahisi, za kidijitali na zenye ulinzi, ambazo zinaongeza thamani kwa wateja, wafanyabiashara, jamii, wanahisa na taifa kwa ujumla.


MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kikodi Ilala imefanya kikao na Washauri wa Kodi ambapo pande hizo mbili zimeeleza azma ya kuendelea kushirikiana katika kuwaelimisha walipakodi haki na wajibu wao.

Akizungumza katika kikao hicholeo Agosti, 18 2026, jijini Dar es Salaam, Meneja TRA Ilala, Musibu Shabani amesema kuwa TRA inatambua nafasi ya washauri wa kodi katika kuwasaidia wafanyabiashara kutimiza wajibu wao wa kikodi.

Aidha amewasisitiza kuendelea kushirikiana na TRA katika kuwajengea walipakodi uelewa wa haki walizonazo pamoja na wajibu wao wa kikodi.

“Mbali na kuwa wateja wenu, wafanyabiashara pia ni walipakodi wanaotegemewa katika kuijenga nchi. Kama wataalamu, tunapaswa kushirikiana katika kuwawezesha kutimiza wajibu wao ili ulipaji wa kodi usiwe mzigo kwao,” amesema Shabani.

Ameongeza kuwa milango ya TRA iko wazi katika kuhakikisha changamoto zote za kikodi zinazowakumba washauri wa kodi na wateja wao zinatatuliwa na kuwaahidi huduma bora.

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Washauri wa Kodi Tanzania (TATC) Sospeter Kibishi ameahidi kwa niaba ya washauri hao kuwa wataendelea kushirikiana na TRA kutoa elimu na kuimarisha uhusiano ili kuweka mazingira mazuri ya ulipaji wa kodi nchini.






Kinshasa, 17 Agosti 2026: Airtel Africa imeandika historia baada ya kuwa kampuni ya kwanza ya mawasiliano barani Afrika kuzindua kibiashara intaneti ya satelaiti kwa simu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ikifungua ukurasa mpya katika upatikanaji wa mawasiliano katika maeneo yasiyofikiwa na minara ya kawaida ya simu.

Huduma hiyo, inayotolewa kupitia ushirikiano kati ya Airtel Africa na Starlink, inawezesha wateja wenye simu janja zinazooana kupata huduma za mawasiliano katika maeneo ambayo hayafikiwi na miundombinu ya kawaida ya mawasiliano ya simu.

Starlink ina zaidi ya satelaiti 650 zinazosaidia huduma za mawasiliano ya moja kwa moja kati ya satelaiti na simu (satellite-to-mobile). Kwa sasa, huduma hiyo inalenga matumizi ya programu zinazotumia kiwango kidogo cha data, ikiwemo ujumbe wa WhatsApp, pamoja na SMS, bila kuhitaji wateja kuwa na vifaa maalumu au kifaa cha ziada.

Uzinduzi huo unafuatia makubaliano ya kimkakati yaliyotangazwa na Airtel Africa na Starlink mwezi Desemba 2025, pamoja na majaribio ya huduma za data na ujumbe nchini Kenya mwezi Machi 2026.

DRC imekuwa soko la kwanza la Airtel Africa na nchi ya kwanza barani Afrika ambako huduma ya intaneti ya satelaiti kwa simu  (Starlink Mobile) imefikia hatua ya kutolewa kibiashara.

Akizungumza kuhusu uzinduzi huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Airtel Africa, Sunil Taldar, alisema hatua hiyo ni muhimu katika kupanua upatikanaji wa mawasiliano barani Afrika.

“Uzinduzi wa kwanza kabisa wa kibiashara wa Starlink Mobile barani Afrika ni hatua muhimu kwa Airtel Africa kupitia ushirikiano wetu na SpaceX. Kwa kuunganisha mtandao wa Airtel wa ardhini na teknolojia ya satelaiti ya Starlink, tunapanua upatikanaji wa mawasiliano muhimu zaidi ya mipaka ya miundombinu ya kawaida ya simu. DRC inaongoza katika hatua hii muhimu ya maendeleo, na uzoefu unaopatikana hapa utasaidia katika kupanua huduma hii hatua kwa hatua katika masoko yetu, kwa kuzingatia idhini za mamlaka za udhibiti za kila nchi.

“Ninapenda kutambua kwa namna ya pekee na kutoa shukrani zangu kwa Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa msaada wake muhimu katika kufanikisha hatua hii, hususan kupitia Mheshimiwa Waziri wa Posta, Mawasiliano na Teknolojia Mpya ya Habari na Mawasiliano, Rais wa Mamlaka ya Udhibiti pamoja na timu zao.”

Taldar alisema uzoefu unaopatikana DRC utasaidia Airtel Africa katika kupanua huduma hiyo katika masoko mengine ya kampuni, kwa kuzingatia idhini na matakwa ya mamlaka za udhibiti katika kila nchi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel DRC, Thierry Diasnoma, alisema huduma hiyo ya satelaiti itaongeza fursa za mawasiliano katika nchi yenye eneo kubwa kijiografia, ambako baadhi ya wananchi wanaishi, kufanya kazi au kusafiri mbali na miundombinu ya kawaida ya mawasiliano.

“Huduma hii ya intaneti ya satelaiti kwa simu  inatoa safu ya ziada ya mawasiliano, ikisaidia wateja kuendelea kupatikana, kupata taarifa na kuwasiliana katika maeneo ambayo mtandao wa minara haupatikani,” alisema Diasnoma.

Huduma ya intaneti ya satelaiti kwa simu  inalenga pia kuwasaidia wasafirishaji na kampuni za usafirishaji na usambazaji, mashirika ya kibinadamu, wahudumu wa afya, wakulima, kampuni za uchimbaji madini na jamii zinazoishi katika maeneo ambayo hayajafikiwa kikamilifu na mitandao ya ardhini.

Aidha, teknolojia ya intaneti ya satelaiti kwa simu inaweza kuwa nyenzo muhimu katika mawasiliano ya dharura wakati wa majanga ya asili au pale ambapo mtandao wa kawaida unakatika kwa muda.

Kwa sasa, wateja wanaotaka kutumia huduma hiyo wanapaswa kuwa na simu janja ya Android yenye LTE inayooana na mfumo wa Starlink Mobile, pamoja na kifurushi cha data cha Airtel DRC kinachokidhi vigezo au huduma ya data roaming iliyowashwa.

Airtel imesema simu na vifaa vya kampuni ya Apple, vitawezeshwa kutumia huduma ya intaneti ya satelaiti kwa simu katika siku zijazo.

Wateja wanaokidhi vigezo wanaweza kujisajili kupitia MyAirtel App na kupata huduma ya majaribio bila malipo kwa siku 30 za kwanza.

Wateja wanaosafiri kwenda DRC na kujiunga na Airtel DRC wanaweza pia kujisajili kwa huduma hiyo ya majaribio baada ya kuamilisha huduma inayokidhi vigezo na kupakua MyAirtel App.

Baada ya kipindi cha majaribio, huduma itaendelea kupatikana kupitia vifurushi vya data vya Airtel vinavyokidhi masharti.

Airtel Africa na Starlink zimesema zinaendelea kuboresha huduma hiyo, huku uwezo wa ziada ukitarajiwa kuongezwa kadri teknolojia inavyoendelea kukua na idhini za udhibiti zinavyopatikana.

Uzinduzi huo unaiweka Airtel Africa katika nafasi ya kampuni ya kwanza ya mawasiliano barani Afrika kuanza kutoa intaneti ya satelaiti kwa simu kibiashara, huku ikiendelea kutumia teknolojia mpya kupanua wigo wa mawasiliano na kuongeza ujumuishwaji wa kidijitali barani Afrika.


 Airtel Money kwa kushirikiana na Buni,DTBI, Vocalize IoT Project na Techstar Innovation Hub* wamekutana na vijana kutoka vyuo vikuu na VETA nchi nzima kuwapa mafunzo ya Internet of Things - IoT na Digital Literacy.


Lengo ni moja tu: Kuwatengeneza vijana wawe wabunifu, waweze kujiajiri na kuzalisha ajira kupitia uchumi wa kidijitali. Hawataki tena vijana wawe watumiaji tu, wanataka wawe watengenezaji wa teknolojia zitakazotatua matatizo ya jamii.


Akizungumza na vijana hao, Meneja wa Huduma za Kifedha na Miamala ya Kigeni wa Airtel Money, Bi. Rita Nyamwehura alisema kampuni imeamua kuwekeza kwa vijana kwa sababu ndio chachu ya ukuaji wa uchumi.



"Airtel tumejikita kuhakikisha huduma zetu zinawafikia Watanzania popote walipo, mijini na vijijini, kwa njia salama, rahisi na yenye uhakika. Tunaamini teknolojia za kidijitali ni chachu ya ukuaji wa uchumi na fursa kwa vijana. Kupitia ushirikiano huu, tunataka kuwawezesha vijana kutumia ubunifu wao kutengeneza suluhisho zinazogusa maisha ya kila siku ya Watanzania," alisema Nyamwehura.


Pia aliwataka vijana watumie kikamilifu huduma za Airtel Money kama vile kununua vifurushi, kulipia bili, Lipa Namba na huduma nyingine ili waelewe jinsi teknolojia inavyoweza kuunganishwa na biashara.


Kwa upande wake, Bw. Elia Kinshaga kutoka JATEC ambaye ni Business Development Manager alisema mafunzo haya yanalenga kuwapa vijana uwezo wa kubuni teknolojia za IoT katika sekta za maji, usalama, usafirishaji, afya na utoaji wa huduma.


Alitoa mfano wa mita janja za maji zinazolipiwa kabla ya matumizi. Amesema teknolojia hizo zinapunguza upotevu wa mapato na kuongeza uwazi.


Kinshaga pia alifichua kuwa kupitia ushirikiano wa Airtel na DTBI kumekuwepo na Fursa Labs zenye vifaa vya kisasa vya TEHAMA - kompyuta, intaneti na maabara za ubunifu. Moja ya matunda yake ni mfumo wa Visomo unaomilikiwa na MagilaTech. Mfumo huu umesaidia wanafunzi wa VETA kusoma mtandaoni na sasa unatumika Tanzania, Dubai na DRC.


"Nawahimiza vijana kujiamini, kutumia maarifa wanayopata na kuendelea kubuni bidhaa na huduma za kidijitali zitakazochochea ajira na kuongeza tija," alisisitiza Kinshaga.


Mmoja wa washiriki, Levina Chifiye kutoka St. Joseph College of Engineering and Technology alisema mafunzo hayo yamefungua akili yake. 


"Nimeelewa jinsi IoT inavyoweza kutumika kwenye usalama, usafirishaji na mifumo ya malipo. Pia Airtel Money API zitatuwezesha kuunganisha malipo kwenye miradi yetu ya kiteknolojia," alisema Levina.


Ushirikiano huu unaonyesha wazi kuwa mustakabali wa Tanzania upo mikononi mwa vijana wenye ubunifu na teknolojia.