Semina iliyofanyika wiki Hii jumamosi tarehe 25 Agust imefana sana,ambapo iliudhuriwa na watu wengi kutoka kada mbalimbali rai wa Tanzania na baadhi watanzania lakini walio nje ya nchi,Mwendeshaji na msimamizi wa semina hiyo Mr Deogratius Kilawe  amesema kuwa kafurahishwa sana na mwitikio wa Watanzania kuanza kuchangamkia Semina mbalimbali ambazo lengo lake kuwapatia maarifa watanzania ili waweze pambana vema na utandawazi.
Pia hii imempa motisha aweze fanya tena semina wiki lijalo Hapo Hapo Mbezi garden Hotel Inayokwenda kwa Jina "how to improve your memory"(Jinsi ya kuboresha utunzaji wa kumbukumbu kichwani) Hii ni kutokana kuwepo na hii dunia ya watu kuwa busy na kazi Hivyo kama usipokuwa makini Unaweza sahau ahadi mbalimbali na mipango Hivyo maarifa yanahitajika ambapo wiki lijalo wazungumzaji watakuwa Dr Rugola Mtandu(medical doctor/masters degree holder) na Mr Shadrack Ntuha (Visionary).
Deogratius Kilawe akiwezesha semina hapa Mbezi beach garden.
Wadau walio hudhuria seminar wakichangia mada



Gillsant kutoka Popote media(Chief marketing officer) akitoa mada kwa semina.
Deogratius Ntundu kutoka Art media ltd  akiwa anawezesha semina

Washiriki

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Duniani kuna vijimamhoz! I hope huyo anaefundiha watu ku make money online yeye ni milionea tayari. Yasije yakawa ya kipofu kumuongoza njia kipofu. Hizi semina huyo ziko majuu na ukihudhuria huwa mwisho mnaambiwa mjisajili ili kufundihwa. Kujisajili ni $250. Hapo ndio watu huwa wanaingia mitini.

    ReplyDelete
  2. jamaa angeandika how to make money online na akamwaga sela how to do it?

    How to make money online halafu anaongelea kuhusu memory?

    Sasa wasiohudhuria watafaidika vipi?

    Andunje

    ReplyDelete
  3. Mdau wa kwanza, nakubaliana na wewe. Hapa UK mimi nilijaribu haya mambo nikakwama. Kuna kampuni walitaka niuze bidhaa zao lakini walinipa sharti la kulipia kwanza. Sasa mimi nikawaambia wanikopeshe katika faida nitakayopata nitawalipa. Waligoma kunipa mkopo!!

    ReplyDelete
  4. mbona wengine wamelala?

    ReplyDelete
  5. Jamani fundisheni watanzania kutumia rasilimali za uhakika walizonazo, Ardhi kwa Kilimo cha kisasa, Ufugaji wa kisasa na jinsi ya kujitosheleza kwa mahitaji badala ya kuwategemea wachina wawamwagie bidhaa hadi vijiti vya kuchokonolea nyama kwenye meno. Nyie mmekaza to make money online hadi lini? Hayo mambo ndio yanazidi kutufanya wabongo tupende mession town badala ya kufanya kazi na kuzalisha mali. Nyie wasomi si mnaona wachina, wabrazil nk, kwa nini hamuwaelezi watzania wafanye hivyo wabadili maisha mmekazana kuwafundisha michoro michoro tu. Ahaaaa sio hivyo jamani, tusaidiane kiukweli sio kupotezana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...