Zaidi ya wakulima 2000 mkoani Mwanza wanatarajiwa kunufaika na kilimo cha umwagiliaji mwaka mzima baada ya Serikali kuwagawia pampu za kisasa 164.
Wakulima hao ambao asilimia 70 ni vijana, wanatoka katika vikundi 125 vinavyotoka kwenye wilaya sita za mkoa wa Mwanza.
Akikabidhi pampu hizo leo Alhamisi kwa niaba ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda, Mkuu wa Wilaya ya Magu, Jubilate Lawuo amesema pampu hizo zitaongeza kasi ya uzalishaji wa mazao mbalimbali kwa wakulima na kuchangia katika mapinduzi ya kilimo mkoani humo.
Amesisitiza kuwa ugawaji wa pampu hizo unapaswa kuenda sambamba na utoaji elimu kwa wakulima kutoka kwa maofisa ugani waliosambazwa katika kata na vijiji mkoani humo.
Aidha, amewaasa wakulima kutumia pampu hizo kwa lengo lililokusudiwa ili kuleta matokeo chanya katika shughuli zao za kilimo.
Kwa upande wake Mwakilishi kutoka Tume ya Umwagiliaji mkoa wa Mwanza, Mhandisi Said Kambi amesema pampu hizo zilizogharimu jumla ya shilingi bilioni 1.1 zitagawanywa kwa vikundi 125 vya wakulima.
“Mkoa wa Mwanza una hekta 40,000 zinazofaa kwa kilimo cha umwagiliaji lakini ni hekta 3,300 zimeendelezwa kwa ajili ya kilimo hicho. Hivyo ujio wa pampu hizi utasaidia kuongeza kasi ya uzalishaji wa mazao katika kipindi chote cha mwaka.
“Ili kulinda mazingira na kuzuia kilimo cha pembezoni mwa vyanzo vya maji, zimefungwa mipira yenye urefu wa zaidi ya mita 60 kutoka kwenye vyanzo vya maji, mifereji au mabwawa,” amesema.
Kila pampu ina uwezo wa kusukuma mita za ujazo 80 hadi 100 za maji kwa saa, hatua inayoiwezesha kumwagilia hadi ekari 40 kwa siku, huku uwepo wa magurudumu ukiwezesha urahisi wa kuzihamisha.
Naye Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Magu, Edward Kihamba mbali na kuishukuru serikali kwa kuwapatia pampu 47 katika wilaya hiyo, pia ameahidi kushirikiana na madiwani wenzake kuhakikisha maofisa ugani wanatoa elimu inayotakiwa katika matumizi ya pampu hizo.
NMB, BUNGE KUWAKUTANISHA ZAIDI YA 1,000 MICHEZONI DODOMA
Na Mwandishi Wetu, Dodoma.
ZAIDI ya washiriki 1,000 kutoka Bunge, wizara 14 na taasisi 10 wanatarajiwa kushiriki NMB Bunge Bonanza 2026 litakalofanyika Jumamosi jijini Dodoma, baada ya NMB Bank Plc kukabidhi udhamini wake wathamani ya Sh milioni 210 ikiwemo vifaa vya michezo kwa ajili ya mashindano hayo.
Mwenyekiti wa Bunge Bonanza na Mbunge wa Makete, Festo Sanga, amesema mwaka huu Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu, amealika wizara 14 na taasisi nyingine 10. Idadi ya washiriki inatarajiwa kuwa kubwa kuliko miaka iliyopita, huku akiongezea bonanza hilo litafanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari John Merlini, jijini Dodoma, Jumamosi, Agosti 29, 2026.
Mshauri Mwandamizi wa Kitengo cha Biashara za Serikali Benki ya NMB, Vicky Bishubo, amesema benki inaunga mkono michezo kwa sababu ya mchango wake katika afya, mshikamano na tija kazini. Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na mipira, makombe, track suti za michezo, fulana na medali.
Spika Zungu anatarajiwa kuwa mgeni rasmi. Kabla ya bonanza kuanza, wabunge watafanya matembezi yatakayoanzia Chuo cha Mipango saa 12:00 asubuhi.
Ingawa ushindani mkali unatarajiwa kutoka kwa timu za Bunge, wizara, taasisi na NMB, Sanga alisema lengo kuu ni kuwavuta watumishi kwenye mazoezi, kujenga mshikamano na kuongeza uelewa kuhusu kinga dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza.
BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo (Ijumaa, Agosti 28, 2026) limemthibitisha Mheshimiwa Deogratius Ndejembi kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mheshimiwa Ndejembi amepitishwa kwa asilimia 100 ya kura zote 324 zilizopigwa na waheshimiwa wabunge, ambapo amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa imani aliyoionesha kwake kwa kumteua kuwa Makamu wa Rais na katika nafasi nyingine mbalimbali za uongozi.
Pia Mheshimiwa Ndejembi amelishukuru Bunge kwa imani kubwa waliyompa kiasi cha kumpigia kura kwa asilimia mia moja.
Mapema akiwasilisha hoja ya kuthibitisha uteuzi wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Mheshimiwa Deogratius Ndejembi anatosha na ni mtu sahihi wa kumsaidia Mheshimiwa Rais katika nafasi ya Makamu wa Rais,
akiitaja kuwa ni nafasi yenye dhamana na majukumu makubwa katika uongozi wa nchi.
"Majukumu hayo yanahitaji mtu mwenye uzoefu wa uongozi, uelewa mpana wa shughuli za Serikali, uwezo wa kufanya kazi kwa karibu na Rais, busara katika kushughulikia masuala ya kitaifa, pamoja na uwezo wa kuratibu na kufuatilia utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya Serikali," amesema Dkt. Mwigulu.
"Mheshimiwa Rais amemteua Mheshimiwa Deogratius John Pancras Ndejembi kwa kuzingatia, pamoja na mambo mengine, uzoefu alioujenga katika uongozi wa kisiasa na katika nafasi mbalimbali za Serikali," ameongeza Waziri Mkuu.
Dkt. Mwigulu amesisitiza kuwa uzoefu wa uongozi alionao Mheshimiwa Deogratius Ndejembi unadhihirisha kuwa ni mtu sahihi kutumikia wadhifa wa Makamu wa Rais.
"Mheshimiwa Deogratius John Pancras Ndejembi si mgeni katika uongozi wa Umma na katika siasa za nchi yetu. Kabla ya kuwa Mbunge, Mheshimiwa Ndejembi alihudumu kama Mkuu wa Wilaya katika Wilaya ya Kongwa. Mheshimiwa Spika, baada ya kuchaguliwa kuwa Mbunge, Mheshimiwa Ndejembi ameendelea kuaminiwa na Mheshimiwa Rais na kupewa majukumu mbalimbali ndani ya Serikali."
"Amehudumu katika nafasi ya Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora; Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu; Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, kabla ya kuhudumu kama Waziri wa Nishati," ameongeza Waziri Mkuu.
Dkt. Mwigulu amesema katika kipindi ambacho amehudumu ndani ya Serikali, Mheshimiwa Ndejembi ameonesha uwezo wa kubeba majukumu mbalimbali na kufanya kazi katika sekta zenye mahitaji na changamoto zinazotofautiana, akisisitiza kuwa uzoefu huo ni muhimu kwa Makamu wa Rais ambaye, kwa nafasi yake, anatakiwa kuwa tayari kumsaidia Rais katika masuala mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano na kutekeleza majukumu yoyote atakayokabidhiwa kwa mujibu wa Katiba.
"Kwa kuzingatia majukumu ya Kikatiba ya Makamu wa Rais niliyoyaeleza, pamoja na uzoefu wa kisiasa, kiutawala na kiutendaji wa Mheshimiwa Deogratius John Pancras Ndejembi, Serikali inaamini kuwa ana uwezo wa kutekeleza kwa uaminifu na ufanisi majukumu ya nafasi ya Makamu wa Rais na kumsaidia Mheshimiwa Rais katika kuendeleza shughuli za Serikali na maendeleo ya Taifa letu," amefafanua Dkt. Mwigulu.

Tahadhari hiyo imetolewa na Bayer Tanzania kupitia kampeni yake ya kitaifa ya uhamasishaji kwa wakulima inayolenga kuongeza uelewa kuhusu umuhimu wa kutumia na kuhakiki mbegu halisi kabla ya msimu wa kilimo.
Kampeni hiyo inayojulikana kama “DEKALB Mafanikio Shambani” imeendelea Mkoani Morogoro baada ya kuzinduliwa mapema mwezi huu, ikiwa na lengo la kuwafikia wakulima katika maeneo mbalimbali nchini na kuwapatia elimu kuhusu mbegu bora na suluhisho za kisasa za kilimo.
Mkurugenzi wa Bayer Tanzania, Sango Mwinyi, alisema matumizi ya mbegu zisizothibitishwa yanaweza kuwaweka wakulima katika hatari ya kupoteza uwekezaji wao, hasa katika kipindi ambacho kilimo kinakabiliwa na changamoto zinazotokana na mabadiliko ya tabianchi na hali ya hewa isiyotabirika.
“Wakulima wanapaswa kuwa makini wanaponunua mbegu na kuhakikisha wanazihakiki kabla ya kupanda. Bila kupata taarifa sahihi na kufanya uhakiki, wakulima wanaweza kununua na kupanda mbegu zisizo sahihi na hatimaye kupoteza sehemu kubwa ya uwekezaji wao kutokana na mavuno duni,” alisema Mwinyi.
Alisema wakulima wadogo, ambao ni sehemu muhimu ya mfumo wa chakula nchini, wanahitaji kupata taarifa sahihi ili kufanya maamuzi sahihi kuhusu pembejeo wanazotumia katika mashamba yao.
Kwa mujibu wa Mwinyi, mabadiliko ya tabianchi yameongeza umuhimu wa wakulima kutumia mbegu zilizothibitishwa na zinazofaa kwa mazingira husika ili kuongeza uwezekano wa kupata mavuno yenye uhakika.
“Wakulima wadogo wanaendelea kukabiliwa na changamoto kubwa zinazotokana na mabadiliko ya tabianchi na hali ya hewa isiyotabirika. Katika mazingira haya, matumizi ya mbegu zilizothibitishwa ni muhimu zaidi kwa sababu zinawasaidia wakulima kuongeza tija na kujenga ustahimilivu wa kilimo,” alisema.
Kupitia kampeni hiyo, Bayer inahamasisha matumizi ya aina tano za mbegu chotara za mahindi za DEKALB, ambazo zimetengenezwa kwa kuzingatia maeneo mbalimbali ya kilimo nchini, ikiwemo maeneo yenye mvua chache na yale yenye uwezo mkubwa wa uzalishaji.
Mbali na elimu kwa wakulima, kampeni hiyo pia imeambatana na promosheni yenye zawadi mbalimbali kwa wakulima wanaonunua na kuhakiki mbegu halisi za DEKALB. Zawadi hizo ni pamoja na pampu za kunyunyizia dawa za mgongoni, simu janja, mashine za kupandia mahindi zinazoendeshwa kwa mkono, pikipiki, mifumo ya umeme wa jua na mashine za kumenya mahindi.
Aidha, wakulima wawili watakaobahatika watajishindia gari aina ya Toyota pick-up kila mmoja mwishoni mwa kampeni hiyo.
Ili kushiriki, wakulima wanatakiwa kununua mbegu za DEKALB kutoka kwa wauzaji wa pembejeo walioidhinishwa, kisha kukwangua kibandiko cha TOSCI kilichopo kwenye kifungashio ili kupata namba ya kipekee ya uhakiki.
Baada ya hapo, mkulima anatakiwa kupiga *148*52# na kuingiza namba ya uhakiki yenye tarakimu 12. Baada ya mbegu kuthibitishwa, mkulima atapokea ujumbe mfupi wa uthibitisho na kuingizwa moja kwa moja kwenye droo ya promosheni.
Mwinyi, ambaye pia ni Kiongozi wa Biashara ya Sayansi ya Mazao nchini Tanzania katika Bayer East Africa, alisema kampeni hiyo inalenga zaidi kumwezesha mkulima kufanya uamuzi sahihi kabla ya kuwekeza katika uzalishaji.
“Kila msimu wa kilimo ni uwekezaji mkubwa kwa kaya za wakulima. Hivyo, kuhakikisha mbegu ni halisi na zenye ubora kabla ya kupanda ni hatua muhimu ya kulinda uwekezaji huo. Tunawahamasisha wakulima wasinunue mbegu kwa kuangalia bei pekee, bali wahakikishe pia uhalali na ubora wake kabla ya kupanda,” alisisitiza.
Kampeni ya DEKALB Mafanikio Shambani inatarajiwa kudumu kwa miezi minne, ikilenga kuongeza uelewa miongoni mwa wakulima kuhusu umuhimu wa kutumia mbegu zilizothibitishwa, kuongeza tija ya kilimo na kuchangia katika kuimarisha usalama wa chakula nchini.

Mkurugenzi wa Bayer Tanzania Sango Mwinyi ( mwenye namba 8) akiwa kwa picha ya pamoja na wadau wa mbegu kutoka Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) na wakulima wa mkoa wa morogoro, pamoja na wauza pembejeo kutoka Morogoro wakati wa uzinduzi wa kampeni yake ya kitaifa ya uhamasishaji kwa wakulima ili kuwaongeza uelewa kuhusu umuhimu wa kutumia na kuhakiki mbegu halisi kabla ya msimu wa kilimo inayofahamika kama “DEKALB Mafanikio Shambani’’. Uzinduzi huo umefanyika katikati ya wiki hii.
Na Mwandishi Wetu, Dodoma Kamati ya Bajeti ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar imeupongeza Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa kazi kubwa inayofanya katika kuimarisha mifumo ya utoaji wa huduma za bima ya afya nchini, pamoja na ushirikiano wake na Mfuko wa Huduma za Afya Zanzibar (ZHSF).
Pongezi hizo zimetolewa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe. Mariam Hamis Said, wakati Kamati hiyo pamoja na Menejimenti za ZHSF na NHIF ilipotembelea Makao Makuu ya NHIF kwa ajili ya kujifunza namna Mfuko huo unavyoendesha na kutoa huduma kwa wanachama.
Mhe. Mariam amesema ziara hiyo imekuwa na mafanikio makubwa, kwa kuwa Kamati imepata fursa ya kuelezwa na kujionea kwa vitendo mifumo na huduma zinazotolewa na NHIF, kupitia ziara kwenye Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH).
Pamoja na kutoa pongezi kwa NHIF, Kamati hiyo ilipata fursa ya kutaka kufahamu kwa kina masuala mbalimbali yanayohusu uendeshaji na maendeleo ya Mfuko, ikiwemo namna NHIF inavyopambana na udanganyifu, utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote, pamoja na hatua zinazochukuliwa kuhakikisha wanachama wanapata huduma bora na kwa wakati.
Aidha, Kamati ilitaka kufahamu namna matumizi ya TEHAMA yameboresha utendaji wa NHIF na kusaidia kupunguza gharama za uendeshaji, pamoja na namna uwekezaji unavyosaidia kuimarisha Mfuko.
Masuala mengine yaliyotiliwa mkazo ni pamoja na vyanzo vya mapato ya Mfuko, viashiria vinavyotumika kupima mafanikio na uendelevu wa NHIF, pamoja na mafunzo na uzoefu ambao Mfuko umeupata katika kipindi cha miaka 25 ya utekelezaji wa majukumu yake.
Amesema ushirikiano kati ya NHIF na ZHSF umeleta matokeo makubwa katika hatua mbalimbali za uanzishaji na uendelezaji wa ZHSF, huku akieleza kuwa uzoefu na msaada uliotolewa na NHIF umeiwezesha Zanzibar kuanza na kuendelea vizuri katika safari ya kuimarisha huduma za bima ya afya.
“Kamati inapongeza NHIF na ZHSF kwa mashirikiano makubwa wanayoyafanya ambayo yamewezesha ZHSF kuanza na kuendelea vizuri,” amesema Mhe. Mariam.
Ameongeza kuwa kazi iliyofanywa na NHIF katika kusaidia uanzishaji wa ZHSF ilihitaji uvumilivu na kujitolea kwa kiwango kikubwa, akieleza kuwa Zanzibar imenufaika na uzoefu wa NHIF katika kujenga mfumo wa bima ya afya.
“Kazi iliyofanywa na NHIF ni kazi iliyofanyika kwa uvumilivu mkubwa, lakini kwa kutubeba Zanzibar katika uanzishaji wa Mfuko wetu,” amesema.
Aidha, Mhe. Mariam ameipongeza Menejimenti ya NHIF kwa kuwawezesha kutembelea Hospitali ya Benjamin Mkapa, ambako wamejionea namna wanachama wa NHIF wanavyopokelewa na kuhudumiwa.
Amesema ziara hiyo imewapa fursa ya kuona kwa vitendo ubora wa huduma zinazotolewa, hususan huduma za kibingwa na kibingwa bobezi, ambayo ni mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, katika kuboresha huduma za afya nchini.
“Tumejionea namna wanachama wa NHIF wanavyopokelewa na kuhudumiwa. Hakika kazi hii ni kubwa na nzuri ambayo kwa ujumla tunaipongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Samia Suluhu Hassan, ambapo huduma za kibingwa na kibingwa bobezi zinapatikana hapa nchini,” amesema. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Dkt. Irene Isaka, amesema Mfuko utaendelea kushirikiana kwa karibu na ZHSF ili kuhakikisha wananchi na wanachama wanapata huduma bora za afya kwa wakati na kwa ufanisi.
Dkt. Isaka amesema NHIF itaendelea kutoa ushirikiano unaohitajika kwa ZHSF, hususan katika maeneo ya uzoefu, mifumo ya utoaji huduma na masuala mengine ya kitaalamu, kwa lengo la kuimarisha huduma za bima ya afya kwa wananchi wa Zanzibar.
Amesema ushirikiano huo ni sehemu ya dhamira ya NHIF ya kuhakikisha huduma za afya zinapatikana kwa wananchi popote walipo nchini, huku mifuko hiyo ikiendelea kujifunza na kubadilishana uzoefu katika kuboresha huduma kwa wanachama.
Ziara hiyo imefanyika ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha ushirikiano na kubadilishana uzoefu baina ya taasisi zinazohusika na utoaji wa huduma za bima ya afya Tanzania Bara na Zanzibar.
Bima ya Afya kwa Wote, Jiunge Sasa!














.jpeg)






.jpeg)

.jpeg)




.jpeg)

.jpeg)


.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)