-Apongeza ajira 722 kwa Watanzania kupewa msukumo;

-Asema biashara ya mauzo nje kwa sasa imeelekea kwenye ajira za nje

Doha, Qatar

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Judith Kapinga leo ameshiriki ziara ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanini Mhe Dkt Mwigulu nchemba kutembelea kampuni ya serikali ya usafirishaji ya MOWASALAT inayotoa huduma ya usafiri kwa umma nchini Qatar.

Katika ziara hiyo Mhe Kapinga amefurahishwa na kampuni ya nchini humo ya MOWASALAT kuajiri i vijana 722 wa Kitanzania katika nafasi mbalimbali, ikiwa ni fursa muhimu kwa Watanzania kupata ajira, kuongeza ujuzi na uzoefu katika soko la ajira la kimataifa.

Mhe. Kapinga amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kuweka mkazo katika huduma ya kuwekeza kwa vijana wenye elimu ili kuongeza ajira, kukuza ujuzi na kuongeza mapato ya Taifa. 

Aidha, ameitaka TANTRADE kuweka mkazo zaidi katika kutambua na kukuza fursa za kuwekeza kwenye huduma  na kuifanya kuwa miongoni mwa viashiria muhimu vya utendaji  katika kuongeza mauzo ya huduma za Tanzania katika masoko ya kimataifa.






Na Ashura Mohamed, Kilimanjaro

SERIKALI imesisitiza dhamira yake ya kuendelea kuthamini na kuimarisha miundombinu rafiki kwa watu wenye ulemavu, ili kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo ya taifa.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Raymond Mangwala, aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu, katika kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Viziwi Duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Halmashauri ya Manispaa ya Moshi.

Mangwala amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuweka mazingira wezeshi kwa watu wenye ulemavu, ikiwemo kupitia mikopo isiyo na riba inayotolewa na halmashauri kwa kutenga asilimia 10 ya mapato yake, ambapo asilimia mbili hutengwa kwa ajili ya watu wenye ulemavu.

“Serikali haitawaacha nyuma watu wenye ulemavu. Tunawahimiza mjitokeze kwa wingi kuchangamkia fursa hii ya mikopo. Ni mtaji unaoweza kuwakomboa kiuchumi na kuwawezesha kuanzisha miradi ya kujitegemea,” amesema Mangwala.

Katika hatua nyingine, Mangwala amezitaka taasisi za fedha nchini, ikiwemo Benki ya CRDB, kubuni huduma rafiki na kurahisisha upatikanaji wa mikopo kwa watu wenye ulemavu, hususan viziwi ambao mara nyingi hukumbana na changamoto za mawasiliano.

Akizungumza katika maadhimisho hayo, Meneja Ujumuishi na Fursa Sawa kutoka Benki ya CRDB, Cresensia Grace Kajiru, amesema benki hiyo itaendelea kuweka mazingira wezeshi na rafiki kwa watu wenye ulemavu wa kusikia.

“Kwa kutambua kuwa kila ifikapo Septemba 26 ni Siku ya Viziwi Duniani, sisi kama Benki ya CRDB tunaendelea kuweka mazingira wezeshi, siyo tu kwa kutoa huduma za wakalimani wa lugha ya alama katika matawi yetu yote, bali pia kuwafundisha wafanyakazi wetu kwa vitendo lugha ya alama ili mteja kiziwi akifika ahudumiwe moja kwa moja bila kikwazo,” amesema Kajiru.

Kwa upande wake, Katibu wa Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) Tawi la Kilimanjaro, Polkarip Josephati Mwacha, akisoma risala kwa mgeni rasmi, amesema licha ya juhudi zinazofanywa na Serikali, viziwi bado wanakabiliwa na changamoto kubwa katika sekta ya elimu.

Amesema ukosefu wa walimu wenye ujuzi wa kutosha wa lugha ya alama pamoja na vifaa saidizi umechangia viziwi wengi kukosa elimu bora, hali inayowaweka katika mazingira magumu ya kushindana katika soko la ajira na kushiriki kikamilifu katika shughuli za kijamii na kisiasa.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA), Tungi Mwanjala, ameiomba Serikali kuharakisha mchakato wa kuridhia na kusaini Mkataba wa Afrika wa Haki za Watu Wenye Ulemavu, ili kulinda na kutetea haki zao kwa mujibu wa sheria za kimataifa.

Kwa upande wake, Mbunge wa Viti Maalumu vya Watu Wenye Ulemavu, Nassiriya Nassir Ali, ameipongeza Serikali kwa kuendelea kuweka mazingira wezeshi kwa watu wenye ulemavu, huku akiwataka viziwi kutumia ipasavyo fursa zinazotolewa na Serikali ili kujiletea maendeleo.

Maadhimisho hayo yalihudhuriwa na wadau mbalimbali, wakiwemo Benki ya CRDB, viongozi wa Serikali, taasisi za kifedha, makundi mengine ya watu wenye ulemavu pamoja na wananchi.





TIMU ya Taifa ya Serbia itakuwa mwenyeji wa timu ya taifa Uholanzi katika mchezo wa UEFA Nations League 2026/27, utakaopigwa Jumapili, Septemba 27, katika Uwanja wa Rajko Mitić jijini Belgrade.

Mchezo huo wa Kundi A2 unatarajiwa kuanza majira ya saa 19:00 usiku, huku timu zote zikiwa na nafasi ya kusaka matokeo muhimu katika hatua hii ya ligi.

Timu hii ya taifa ya Serbia itaingia kwenye mchezo huo ikiwa na jukumu la kutumia faida ya kucheza nyumbani ili kuhakikisha kupata pointi mbele ya mashabiki wake. Timu hiyo iko katika kundi moja na mataifa ya Uholanzi, Ujerumani pamoja na Ugiriki, hivyo kila mchezo una umuhimu katika safari ya kumaliza nafasi za juu kwenye msimamo wa kundi.

Kwa upande wa Uholanzi, mchezo huo utakuwa sehemu ya mwanzo wa kipindi kipya chini ya kocha mpya Xavi Hernandez. Kocha huyo ameeleza kuwa anataka timu yake icheze kwa kasi, kufanya kazi kwa bidii na kuchukua hatua ya kulazimisha mchezo, huku Virgil van Dijk akiendelea kuwa nahodha wa kikosi hicho.

Uholanzi pia imepangwa kukutana na Serbia tena Oktoba 4, lakini safari hii ikiwa nyumbani, jambo linalofanya mchezo wa Belgrade kuwa muhimu katika kuanza kujenga nafasi zao ndani ya Kundi A2.

Meridianbet inasema kuna michezo kama Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli. Ingia katika kasino ya mtandaoni ya Meridianbet na ujiokotee mkwanja mapema. Jiunge sasa au Tembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Ratiba ya kundi hili pia inaonyesha kuwa Serbia baada ya mchezo huu itakutana na Ujerumani ya kocha Jurgen Kloop mnamo Oktoba 1, wakati Uholanzi itasafiri kucheza na Ugiriki siku hiyo hiyo.

Kwa ujumla, mchezo huu kati ya Serbia dhidi ya Uholanzi unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na ubora wa timu zote mbili na umuhimu wa pointi katika kundi hilo.

Macho yatakuwa kwa namna Serbia itakavyotumia uwanja wa nyumbani na jinsi Uholanzi itakavyoanza kutumia mbinu mpya zitakazo kuwa chini ya Xavi katika kampeni ya michuano ya Mataifa ulaya (Uefa Nations League).

Karibu Meridianbet ambapo Kipindi hiki ambacho timu za taifa kutoka maeneo mbalimbali duniani zipo kwenye majukumu yao, kuna michezo mikubwa inayosubiriwa na mashabiki, ikiwemo UEFA Nations League, mechi za kufuzu AFCON 2027 na michezo mingine ya kimataifa Bila kusahau Odds kubwa na machaguzi kibao kwenyekila mchezo.

BAHARI kubwa imechafuka, upepo unavuma na safari ya kutafuta hazina inaanza. Kwa wapenzi wa michezo ya kasino wanaotafuta burudani iliyojaa msisimko, Pirates Power kutoka Meridianbet inakualika kupanda jahazi na kuanza safari ya kipekee katikati ya bahari yenye siri na hazina zilizofichwa. Huu si mchezo wa kawaida, bali ni safari inayochanganya burudani, changamoto na nafasi ya kupata ushindi mkubwa huku kila raundi ikifungua ukurasa mpya wa matukio.

Kwenye safari hii, kila mzunguko wa mchezo unaweza kuwa hatua muhimu kuelekea kwenye hazina kubwa. Pirates Power inakupa nafasi ya kushinda hadi mara 5,000 ya dau lako, jambo linaloongeza msisimko kila unapozungusha. Ukiwa kama nahodha wa jahazi lako, kila raundi inakupa fursa ya kuendelea kusaka mchanganyiko unaoweza kubadili kabisa safari yako. Ni mchezo unaowaleta pamoja wale wanaopenda burudani ya kasi na changamoto za kusisimua katika ulimwengu wa sloti.

Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Lakini bahari ya Pirates Power imejaa zaidi ya mawimbi na hazina. Mchezo huu una mistari 20 ya ushindi na njia 6 za kushinda, hivyo kila raundi inaweza kuleta mchanganyiko tofauti wa alama unaoweza kuzalisha ushindi. Alama za Wild zina uwezo wa kuongeza ushindi mara mbili, huku Scatter zikifungua milango ya raundi za bonasi zenye zawadi zinazoongeza ladha ya safari.

Na kama hiyo haitoshi, ndani ya bahari hii kuna hazina kubwa zaidi zinazowasubiri mabaharia jasiri. Mini, Major na Grand Jackpot ni sehemu ya mvuto wa Pirates Power, zikiongeza ladha ya kusaka zawadi kubwa ndani ya mchezo. Kila raundi inabeba mshangao wake, na safari inaweza kubadilika ghafla pale alama zinazotafutwa zinapojitokeza. Hivyo, kwa anayependa kuingia kwenye ulimwengu wa michezo yenye mandhari ya kipekee na msisimko wa kila mzunguko, jahazi la Pirates Power liko tayari kuondoka.

Sasa ni wakati wa kuchukua nafasi yako kama nahodha wa kweli na kuanza safari yako ya Pirates Power kupitia Meridianbet. Panda jahazini, pitia mawimbi ya bahari ya hazina na furahia kila raundi huku ukifuatilia fursa za ushindi zinazopatikana ndani ya mchezo. Kumbuka, kila safari ina hadithi yake, na katika Pirates Power, kila raundi inaweza kuwa mwanzo wa tukio jipya.
Mradi mkubwa wa Maji wa Miji 28 unaotekelezwa katika Kijiji cha Mavuji kilwa Masoko umekamilika na wananchi wameanza kupata huduma ya maji na kuondokana na changamoto ya magonjwa kama kipindupindu ulokua unawakumba mara kwa mara kutokana na adha ya maji.

Baada ya kufunguliwa kwa tone la kwanza la Mradi huu mkubwa wa kihistoria, Wananchi wameupokea mradi huu kwa furaha na shangwe huku wazee wakimuombea Dua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan.

Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso (Mb) ametembelea mradi huo nakujionea utekelezaji wake uku akisema maunganisho mapya ya huduma ya maji kwa wananchi wa Mavuji ni siku Saba tu.

Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mavuji, kilwa Masoko , Lindi baada ya kukagua mradi mkubwa wa Maji wa Miji 28, amesisitiza kwa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa mazingira Kilwa Masoko (KIMUWASA) na Mamlaka zote za maji nchini huduma ya kuunganishiwa maji majumbani isizidi siku Saba.

Mradi huu mkubwa wa Maji wa Miji 28 Kilwa umegharimu kiasi cha Fedha Shilingi Bilioni 44 za kitanzania na umefikia asilimia 94.3 ya utekelezaji wake na tayari umeanza kutoa huduma kwa wakazi wa Kijiji cha Mavuji huku ukitegemewa kuwanufaisha wakazi zaidi ya 59,983 ambapo lita milioni 5 .5 za maji zitazalishwa kwa siku kutoka kwenye chanzo cha Mto Mavuji.









NA MWANDISHI WETU, TANGA

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Kihongosi, amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ni kiongozi mwenye uwezo mkubwa ndani ya Bara la Afrika, mvumilivu na mchapakazi.

Kihongosi ameyasema hayo wakati akihutubia mamia ya wananchi wa Tanga katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Lamore, ikiwa ni hitimisho la ziara yake mkoani humo ya kukagua uhai wa Chama pamoja na utekelezaji wa Ilani ya CCM ya 2025–2030.

Amesema Rais Samia ameithibitishia dunia kuwa wanawake wanaweza kuongoza nchi kwa ufanisi na kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ndani ya muda mfupi.

“Rais Samia ni kiongozi mwenye uwezo mkubwa, si Tanzania pekee bali pia ndani ya Bara la Afrika. Ni mvumilivu, mchapakazi, mwenye hofu ya Mungu, anayesikiliza na kutatua kero za wananchi,” amesema Kihongosi.

Amesema utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini, ikiwemo mkoani Tanga, ni miongoni mwa ushahidi wa juhudi za Serikali katika kuendeleza maendeleo ya Taifa.

Ametaja baadhi ya miradi hiyo kuwa ni ujenzi wa Bandari ya Tanga, ukarabati na upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Tanga pamoja na ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR).

Aidha, Kihongosi amewataka wananchi kuendelea kumuunga mkono Rais Samia katika jitihada za kuwatumikia Watanzania na kuhakikisha Taifa linaendelea kupata maendeleo endelevu.







Na George Maziku, Mbogwe

DIWANI Kata ya Bukandwe, iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Mbogwe, mkoani Geita Paulo Raphael Sahani amewalaumu wazazi katika shule ya msingi Kanegere, iliyopo kijiji cha Kanegere wilayani humo, kwa kuitelekeza shule hiyo na kusababisha uchakavu mkubwa.

Diwani huyo ametoa lawama hizo jana Alhamisi, Septemba 24, katika sherehe za mahafari ya 22 ya wanafunzi waliohitima darasa la saba mwaka huu, ambapo diwani huyo alikuwa mgeni rasmi.

Alisema kuwa wazazi na wananchi wa kijiji cha Kanegere wameacha kujitolea kuchangia maendeleo ya shule yao, badala yake jukumu hilo wamewaachia wawekezaji wa sekta ya madini waliopo kijijini hapo, ambao hatahivyo diwani huyo alidai hawasomeshi watoto wao katika shule hiyo.

"Sisi viongozi, walimu, kamati ya shule na wazazi wa shule hii kwa ujumla wetu tumefeli kabisa kuihudumia shule yetu. Tumeitelekeza kabisa na kuifanya ichakae na kukosa hadhi ya kuitwa shule inayotegewa kutoa elimu bora kwa watoto wetu. Tumewaachia wawekezaji jukumu la kuhudumia shule yetu lakini wao hawana watoto wanaosoma hapa", alisema diwani Sahani.

"Lazima tubadilike, tuanze kuchangia shule yetu sasa. Wazazi wa watoto wanaohitimu darasa la saba wachangie angalau mfuko mmoja wa saruji kwa ajili ya maendeleo ya shule hii, haiwezekani mtoto akae hapa miaka saba halafu aondoke hivi hivi bila kuchangia chochote, na katika kipindi hicho inawezekana ameharibu miundombinu ya shule kama milango, madirisha au ameharibu bati kwa kutupa mawe kwenye paa, hii siyo sawa hata kidogo", alifafanua Sahani.

Sahani alisema kuwa kuanzia mwakani kutakuwa na mabadiliko makubwa ambapo kila mzazi wa mtoto anaehitimu darasa la saba katika shule hiyo atatakiwa kuchangia angalau mfuko mmoja wa sementi kwa ajili ya ukarabati na umaliziaji wa majengo ya shule ya Kanegere.

"Tuanze mwakani kwasababu tutakuwa na wahitimu wengi, kwa maana wanafunzi waliopo leo darasa la sita na la tano watahitimu pamoja. Tunaweza kuwa na wahitimu kati ya 300 mpaka 400, hivyo tunaweza kupata mifuko 300 mpaka 400 ya saruji na kuweza kumalizia baadhi ya majengo yetu na kufanyia ukarabati mengine", alisisitiza diwani huyo.

Wakati huo huo diwani huyo amewatolea wito watu wote waliosoma shule ya msingi Kanegere kuikumbuka shule hiyo kwa kuchangia maendeleo yake.

Diwani huyo ambaye pia alihitimu darasa la saba katika shule hiyo mwaka 2004, aliahidi kuwatafuta na kuwaunganisha watu wote waliohitimu shuleni hapo kati ya mwaka 2004 mpaka 2010 ili waweze kuchangia ujenzi na ukarabati wa shule yao kama shukrani kwa mafanikio yao ya leo.

"Napenda kutangaza kupitia mahafari haya kwamba katika mahafari ya mwaka ujao, wahitimu wote wa shule hii wa kuanzia mwaka 2004 mpaka 2010 ndio watakuwa wageni rasmi na mimi ndiye mwenyekiti wa kamati ya maandalizi hayo, nitawatafuta kila mahali walipo na kuwashawishi wachangie yao", alibainisha diwani huyo.

Aliongeza, "Lazima tufanye kazi mchana na usiku ili kurejesha haraka hadbi ya shule yetu, inatubidi turudishe shukrani zetu kwenye shule iliyotusomesha. Inakuwaje tutoe fungu la kumi kanisani halafu tushindwe kuchangia shuleni", alihoji diwani huyo.

Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi waliohitimu darasa la saba shuleni hapo mwaka huu walielezea furaha yao pamoja na matumaini yao ya baadaye.

"Najisikia vizuri na nina furaha sana kufikia hatua hii. Malengo yangu ni kuendelea na masomo ya sekondari na chuo ili niweze kutimiza ndoto zangu za kuwa rubani wa ndege", alisema Janeth Emmanuel (14) mmoja wa wahitimu wa mwaka huu.

Nae mhitimu mwingine Gaudencia William (13) alisema kuwa ana imani kubwa kwamba atafaulu mtihani wake wa darasa la saba na kuendelea na masomo ya sekondari na hatimaye kutimiza lengo lake la kuwa daktari wa binadamu.

"Mimi nataka kuwa daktari wa kutibu watu, naamini nitafaulu kwenda sekondari na nikifikaa huko nitasoma masomo ya sayansi kwasababu nayapenda na ninayaweza", alijigamba Gaudencia.







Na Janeth Raphael - MichuziTv 

Serikali imesema ipo katika mashauriano ya kufanya marekebisho ya baadhi ya vifungu vya Sheria ya Ndoa kwa lengo la kukabiliana na tatizo la ndoa za utotoni na kuhakikisha watoto wa kike wanapata fursa ya kuendelea na elimu bila vikwazo.

Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Juma Zuberi Homera, amesema hatua hiyo inalenga kuweka mazingira yatakayowawezesha mabinti kuendelea na masomo kuanzia ngazi ya awali hadi kidato cha sita, huku wakilindwa dhidi ya ndoa za utotoni na ukatili wa kijinsia.

Dkt. Homera ameyasema hayo jijini Dodoma wakati wa programu ya “Sema na Waziri”, ambapo alieleza kuwa Serikali inaendelea na mashauriano kuhusu mabadiliko ya sheria hiyo ili kushughulikia changamoto zinazowakabili watoto wa kike.

Amesema Serikali inatambua umuhimu wa elimu katika kumwezesha mtoto wa kike kujenga maisha yake na kufikia ndoto zake, akisisitiza kuwa uwekezaji katika elimu na mitaji ni miongoni mwa nguzo muhimu za kuwawezesha wasichana kujikwamua kiuchumi.

Katika hatua nyingine, Dkt. Homera amepongeza juhudi zinazofanywa na Plan International Tanzania katika kutetea na kulinda haki za watoto wa kike, akiahidi kuwa Wizara itaendelea kushirikiana na taasisi hiyo katika kukabiliana na ukatili wa kijinsia na kuwawezesha mabinti walio katika mazingira magumu.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Plan International Tanzania, Jane Sembuche, amesema takwimu zinaonesha kuwa asilimia 29.1 ya wanawake wenye umri wa miaka 20 hadi 24 waliolewa kabla ya kufikisha miaka 18, hali ambayo imekuwa na athari katika fursa zao za elimu na maendeleo ya kiuchumi.

Sembuche ameitaka Serikali kuharakisha mchakato wa marekebisho ya Sheria ya Ndoa ili kuweka miaka 18 kuwa umri wa chini wa ndoa kwa wote, akieleza kuwa hatua hiyo itasaidia kulinda haki za watoto na kuchangia utekelezaji wa malengo ya Dira ya Tanzania 2050. 



NA MWANDISHI WETU

SERIKALI imeishukuru Benki ya NMB kwa kuendelea kudhamini Tamasha la Kariakoo ‘Kariakoo Festival 2026’, huku ikiipongeza kwa Huduma na Bidhaa Bunifu zinazochochea ukuaji kiuchumi miongoni mwa wafanyabiashara nchini, zikiwemo NMB SME’s Credit Card na Mshiko Fasta.

Shukrani na pongezi hizo zimetolewa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dennis Londo, wakati akizindua msimu wa tatu wa Kariakoo Festival 2026, jukwaa la linalowakutanisha wafanyabiashara na wanunuzi wa ndani na nje, likiratibiwa na Kampuni ya One Voice Events na kudhaminiwa na Benki ya NMB.

Kariakoo Festival 2026 imezinduliwa Ijumaa Septemba 25 na jukwaa hilo litafanyika hadi Septemba 27, ambapo Naibu Waziri Londo amewataka washiriki kulitumia vema kufanikisha safari ya mabadiliko ya kisekta kuelekea Uchumi Usiotegemea Pesa Taslimu (cashless economy).

Mkuu wa Idara ya Biashara ya NMB, Alex Mgeni, alisema kupitia jukwaa la Kariakoo Festival, benki yake imezileta huduma bora na rafiki kwa wafanyabiashara na wajasiriamali, ikiwemo SME’s Credit Card, NMB Mkononi, NMB Tap to Pay, NMB Lipa Namba na Mshiko Fasta.

Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Kariakoo (JWK), Severine Mushi, naye aliishukuru Serikali kwa kuweka mazingira wezeshi ya kufanya biashara nchini, kiasi cha kuzivutia taasisi za fedha kama NMB, kuwekeza kufanikisha matukio yanayowakutanisha wadau wa biashara kitaifa na kimataifa.





Na Victor Masangu, Kibaha

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Kibaha Mjini, Ramdhani Kazembe, amewataka vijana nchini kuwa wazalendo, kudumisha amani na kuachana na tabia ya kukaa vijiweni, badala yake wajitokeze kushiriki kikamilifu katika michezo na mazoezi kwa ajili ya kujenga afya zao.

Kazembe ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa mgeni rasmi katika Bonanza la Tangini Season One, lililofanyika Kibaha, kwa niaba ya Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Pwani, Alhaj Mussa Mansour.

Amesema kushiriki katika michezo na mazoezi ni muhimu kwa vijana kwa kuwa husaidia kuimarisha afya ya mwili na akili, huku pia ikisaidia kupunguza hatari ya kupata magonjwa yasiyoambukizwa.

Aidha, Kazembe amesema Alhaj Mansour ameahidi kushirikiana bega kwa bega na viongozi wa klabu za Jogging katika Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha, ambapo amepanga kukutana nao kwa ajili ya kuweka mikakati madhubuti ya kuendeleza na kuunga mkono mchezo huo.

Amesema ushirikiano huo pia utasaidia kuwawezesha vijana kutumia fursa mbalimbali za kiuchumi, ikiwemo mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri kwa ajili ya kuwawezesha kujikwamua kiuchumi.

“Napenda kuwapongeza kwa dhati wanachama wa Tangini Jogging pamoja na vilabu vyote ambavyo vimeshiriki kikamilifu katika bonanza hili. Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Pwani amenituma kuja kumwakilisha na amesema yupo pamoja nanyi na ataendelea kushirikiana na vijana katika kuendeleza klabu za Jogging,” amesema Kazembe.

Kwa upande wake, Mratibu wa Bonanza la Tangini Season One, Ally Gombati, amesema lengo la kuandaa bonanza hilo ni kuwakutanisha vilabu mbalimbali vya Jogging ili kufanya mazoezi kwa pamoja, kujenga na kuimarisha afya, sambamba na kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuendeleza sekta ya michezo.

Gombati amesema wameona umuhimu wa kuwaunganisha vijana kutoka maeneo mbalimbali ili kujenga misingi ya umoja na mshikamano, huku wakiwakumbusha umuhimu wa kulinda amani ya nchi na kufanya mazoezi kwa ajili ya afya zao.

“Tumeamua kuandaa bonanza hili ambalo tumeliita Tangini Bonanza na tumeweza kuvishirikisha vilabu vya Jogging zaidi ya 30 kutoka maeneo mbalimbali ya Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha pamoja na maeneo mengine jirani ya Jiji la Dar es Salaam, ikiwemo E-FM Jogging, Clouds Jogging, Tangini Jogging pamoja na Jogging nyingine kutoka maeneo mbalimbali,” amesema Gombati.

Nao baadhi ya wanachama wa Tangini Jogging Club wamesema bonanza hilo limewapa fursa ya kukutana na kufahamiana na watu kutoka maeneo mbalimbali, huku mazoezi hayo yakitarajiwa kuwasaidia kuimarisha afya zao na kupunguza hatari ya kupata magonjwa yasiyoambukizwa.

“Kwa kweli tunapenda kutoa shukrani zetu za kipekee kwa uongozi wa Tangini kwa kuona umuhimu wa kuandaa bonanza hili ambalo limetukutanisha na wenzetu kutoka maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Kibaha pamoja na Jiji la Dar es Salaam. Tumeweza kukimbia pamoja na kubadilishana mawazo mbalimbali kuhusu michezo na masuala ya maendeleo,” wamesema.

Bonanza la Tangini Season One limewakutanisha wanamichezo kutoka klabu mbalimbali za Jogging za Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha na maeneo mengine ya Jiji la Dar es Salaam, likiwa na lengo la kujenga urafiki, kudumisha umoja na mshikamano, kuimarisha afya na kujikinga na magonjwa yasiyoambukizwa.



WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba ameipongeza Serikali ya Qatar kwa kufanikiwa kuwa na matumizi makubwa ya teknolojia kwenye usafiri wa umma na hasa matumizi ya nishati safi.

Ametoa pongezi hizo leo (Jumamosi, Septemba 26, 2026) jijini Doha, Qatar mara baada ya kupokea taarifa ya uendeshaji wa kampuni ya usafirishaji ya MOWASALAT kutoka kwa Waziri wa Uchukuzi wa Qatar, Sheikh Mohammed bin Abdullah bin Mohammed Al Thani.

Waziri Mkuu ambaye ameanza ziara ya kikazi ya siku tatu nchini humo, amesema ubunifu wao umesaidia kuondoa msongamano wa magari barabarani kwa sababu usafiri wa umma ni wa uhakika.

"Nyumbani tunalo tatizo la msongamano wa magari na kupitia teknolojia mnazotumia, Tanzania inaweza kujifunza mbinu mlizotumia ili nasi tuweze kukabiliana nalo," amesema.

Waziri amesema amefurahi kuona kampuni yao inatumia nishati safi kwa sehemu kubwa. "Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kinara wa nishati safi barani Afrika, na hii ni hatua nzuri kwetu. Tunatarajia kuwa wenyeji wa AFCON 2027, kwa hiyo itatufaa sana," amesema.

Waziri Mkuu ameishukuru kampuni hiyo kwa kuwaajiri Watanzania 722 katika nafasi mbalimbali. "Ni fursa kwa vijana wetu kukuza ujuzi na kujifunza teknolojia mbalimbali."

Mapema, Waziri wa Uchukuzi wa Qatar, Sheikh Mohammed bin Abdullah bin Mohammed Al Thani alimweleza Dkt. Mwigulu kwamba kampuni hiyo inatoa huduma za usafiri wa abiria kwa kutumia mabasi, taxi, usafiri kwa wanafunzi, matukio binafsi, ya kitaifa na ya kimataifa.

"Kwa mwaka 2025, kampuni yetu imetoa huduma kwa watu milioni 42. Tunayo magari 1,200 na njia za magari (routes) tulizonazo ni 128. Asilimia 70 ya magari yetu yanatumia umeme na kutokana na ubora na uhakika wa huduma zetu, tumeweza kuyatoa barabarani magari 12,363," alisema.

Alisema kutokana na teknolojia walizonazo, magari yao yanakuwa yanakaguliwa kwa mfumo wa kielektroniki. Yamewekewa mfumo unaowezesha kubaini changamoto kwa haraka badala ya kusubiri kufanyiwa ukaguzi na mafundi," alisema.