-Wanufaika wamshukuru Rais Dk.Samia kwa kuwajengea uwezo kiuchumi


Na Mwandishi Wetu, Ilemela

MRADI wa ufugaji samaki kwa njia ya vizimba katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, mkoani Mwanza, umeendelea kufungua fursa za kiuchumi kwa kaya zenye kipato duni, kuwaongezea kipato walengwa na kuwasaidia kujikwamua dhidi ya umaskini.

Mradi huo unaotekelezwa na wanachama wa vikundi vya Maligana Kasafu na Temeke, vilivyopo Mtaa wa Kae Ndogo, Kata ya Kigongo, unawawezesha walengwa kutumia fursa ya uwepo wa Ziwa Victoria kuendesha shughuli za uzalishaji mali na kuboresha maisha yao.

Akizungumza kuhusu mradi huo, Mratibu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii(TASAF) katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela David Macha amesema vikundi hivyo vilibuni wazo la kufuga samaki kwa njia ya vizimba baada ya kutambua kuwa mazingira yao ya kuishi karibu na ziwa ni fursa muhimu inayoweza kutumika kuongeza kipato.

Amesema awamu ya kwanza, vikundi hivyo vilipatiwa Sh milioni 34 kupitia TASAF, fedha zilizotumika kutengeneza vizimba viwili, kununua vifaranga vya samaki na chakula kwa ajili ya kuendesha shughuli za ufugaji.

Amefafanua baada ya kuanza ufugaji, vikundi hivyo vilifanikiwa kuvuna samaki na kupata mapato ya takribani Sh milioni 27, mafanikio yaliyowapa motisha ya kuendelea na mradi huo ili kuongeza kipato na kuimarisha shughuli zao za kiuchumi.

“Baada ya mavuno, wanachama waliamua kuendeleza uwekezaji katika ufugaji wa samaki kwa kutumia sehemu ya fedha zilizopatikana, huku kiasi kingine kikitumika kusaidia shughuli nyingine za wanachama, ikiwemo kukopeshana kwa ajili ya mahitaji na shughuli za kujipatia kipato.”

Pia amesema ufugaji samaki kwa njia ya vizimba ni fursa inayoweza kusaidia kuongeza upatikanaji wa samaki katika mazingira ambayo yamekuwa yakikabiliwa na changamoto ya upungufu wa samaki, huku ukiwawezesha walengwa kujenga msingi wa kujitegemea kiuchumi.

Amefafanua TASAF imekuwa ikisaidia kaya zenye hali duni kupitia shughuli mbalimbali za uzalishaji mali, zikiwemo ufugaji na kilimo cha bustani, kwa lengo la kuongeza kipato cha kaya na kuboresha ustawi wa jamii.

Amebainisha kabla ya kuanza kunufaika na miradi hiyo, baadhi ya walengwa walikuwa wakikabiliwa na changamoto ya kukosa uhakika wa chakula cha kutosha kwa siku, lakini kwa sasa shughuli za kiuchumi wanazofanya zimewasaidia kuboresha upatikanaji wa mahitaji yao ya msingi.

“Wanufaika wa Mradi huu kwa sasa wamepunguza utegemezi, kuimarisha uwezo wa kuhudumia familia zao na kuhakikisha watoto wanapata fursa ya kuendelea na masomo, ikiwemo elimu ya juu.Jumla ya walengwa 30 wanahusishwa na shughuli hizo ambazo zimechangia kubadilisha maisha yao.”

Macha amesema baadhi ya walengwa ambao awali walikabiliwa na changamoto za kiuchumi na kutengwa katika jamii sasa wameendelea kujenga uwezo wa kujitegemea kupitia shughuli za uzalishaji mali, hali inayoongeza nafasi yao ya kushiriki kikamilifu katika maendeleo.

“Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela itaendelea kusimamia miradi inayotekelezwa katika eneo hilo ili kuhakikisha inakuwa endelevu na kuleta matokeo yaliyokusudiwa, sambamba na juhudi za Serikali katika kuboresha maisha ya wananchi.”

Kwa upande wake mnufaika wa TASAF, Modesta Makonya amesema mradi wa ufugaji samaki kwa njia ya vizimba umemsaidia kuboresha maisha yake na familia yake, ikiwemo kupata kipato na kujenga nyumba kupitia shughuli za uzalishaji mali.

Amesema walianza kufikiria shughuli mbadala za kiuchumi baada ya kuelekezwa kuwa mpango wa kunusuru kaya maskini katika awamu waliyokuwa wananufaika nayo ungefikia mwisho.

Amefafanua walikaa pamoja na kuanzisha kikundi cha wanawake, ambacho baadaye kilipata msaada wa Serikali kupitia TASAF, chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kupatiwa fedha Sh milioni 34 zilizowawezesha kuanzisha mradi wa ufugaji samaki kwa njia ya vizimba.

“Baada ya kupata fedha hizo, tuliweka vizimba viwili, kila kimoja kikiwa na samaki 650. Tulifanya shughuli za ufugaji na tulipofikia wakati wa kuvuna, tulifanikiwa kupata mapato ya takribani Sh milioni 29, jambo lililotupa moyo wa kuendelea na mradi huo,” amesema Makonya.

Ameongeza mafanikio ya mavuno ya kwanza yaliwafanya kuendelea na awamu ya pili ya ufugaji, ambapo walitumia Sh milioni 22.4 kwa mahitaji mbalimbali ya mradi, huku wakiendelea na maandalizi ya kuongeza uzalishaji ili kupata mapato makubwa zaidi katika mavuno yajayo.

Amesema pia manufaa ya TASAF yameonekana pia kwa walengwa wengine ambao wameanzisha shughuli mbalimbali, zikiwemo ufugaji wa mbuzi, bata na kuku, kilimo cha mboga za majani na biashara ya dagaa, hatua zinazowasaidia kuongeza kipato na kuimarisha maisha ya familia zao.


Na George Maziku, Kahama

Uongozi wa mgodi wa dhahabu wa Mwime 2 Gold Mine uliopo katika mtaa wa Ilindi, kata ya Zongomera, wilayani Kahama, mkoa wa Shinyanga umewataka vijana wilayani humo kuchangamkia fursa za kazi zilizopo katika mgodi huo badala ya kukaa bure vijiweni huku wakilalamikia serikali kwa ukosefu wa kazi.

Hayo yameelezwa na afisa uhusiano wa mgodi huo Christopher Bundala mwisho wa wiki iliyopita alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mgodini hapo.

Bundala alisema kuwa mgodi wake umekuwa mkombozi kwa watanzania wengi wasiokuwa na ajira ambapo zaidi ya watu 5000 wengi wao vijana wamenufaika, kwa njja mbalimbali.

"Nataka kutumia fursa hii kuwaasa watanzania wenzangu hususani vijana kuacha kukaa bila kazi kwenye vijiwe na kulalamikia serikali kwa kukosa ajira, waje hapa mgodini kwetu na migodi mingine ili wajiajiri, wasikae huko kupanga maandamano ambayo hayana maana", alisisitiza Bundala.

Alifafanua kuwa wanaonufaika na mgodi huo ni wachimbaji, wauzaji wa zana za uchimbaji, mamalishe, watoa huduma ya usafiri wa watu na mizigo, wafanyabiashara mbalimbali wakiwemo wenye maduka na nyumba za kupangisha.

Kuhusu uwezeshaji wa makundi maalum ya wanawake na walemavu, Bundala alisema mgodi wake umewawekea utaratibu na mazingira mazuri ya kujitafutia na kufanya kazi za kuwapatia kipato.

"Mgodi wetu unawajali wanawake na walemavu ambao katika hali ya kawaida hawawezi kumudu mikikimikiki ya uchimbaji dhahabu kwasababu ni kazi za kutumia nguvu zaidi", alieleza Bundala.

Aliongeza, "Kwahiyo tumezingatia sana hali hiyo kwa kuweka utaratibu wa kuwaruhusu kuokota mawe ya dhahabu katika eneo letu la leseni na wanapokusanya mawe ya kutosha tunawagongea mihuri bure ili kuwawezesha kutoa mizigo yao kupeleka makarashani kusaga", alifafanua Bundala.

Nao baadhi ya wanawake na walemavu wanaofanya kazi katika mgodi huo waliusifu uongozi wa mgodi wa Mwime 2 kwa kuwajali na kuwasaidia kujipatia kipato.

"Sisi tunaushukuru uongozi wa. mgodi huu wa Mwime 2 kwa kutujali. Wanatupatia mawe ya bure na pia wanaturuhusu kupita hapa na pale mgodini kuokoteza mawe na kutugongea mizigo yetu ili tukasage makarashani", alisifu Ashrafu Juma ambaye ni mlemavu.



WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Tanzania inalenga kuwa miongoni mwa wazalishaji 10 bora wa chakula duniani kutokana na uwekezaji ambao umefanyika kwenye sekta ya kilimo.

“Matarajio yetu ya muda mrefu yameelezwa katika Dira ya Maendeleo Tanzania ya 2050. Chini ya lengo la kwanza, Tanzania inalenga kuwa mzalishaji mkuu wa chakula barani Afrika na miongoni mwa wazalishaji 10 bora wa chakula duniani,” alisema.

Waziri Mkuu ameyasema hayo jana (Alhamisi, Oktoba 22, 2026) wakati akitoa mada kuu kwenye mjadala kuhusu Mustakabali wa Kilimo barani Afrika katika Mkutano wa Kimataifa wa Norman E. Borlaug (Borlaug Dialogue) unaoendelea katika Kituo cha Mikutano cha Iowa, jijini Des Moines, Marekani.

Aliwaeleza washiriki wa mkutano kwamba chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Serikali iliongeza bajeti ya Wizara ya Kilimo kutoka shilingi bilioni 294 za Tanzania kwa mwaka 2021/2022 hadi shilingi trilioni 1.241 katika mwaka 2025/2026. “Hii inadhihirisha jinsi sekta ya kilimo ilivyopewa kipaumbele kama injini ya mabadiliko ya kiuchumi, utengenezaji wa ajira, usalama wa chakula na lishe, ukuaji wa viwanda na mauzo ya nje.”

Kutokana na jitihada hizo, Waziri Mkuu alisema Tanzania imefanikiwa kufikia kuwa na utoshelevu wa chakula wa asilimia 130. “Hii inaonesha uwezo wetu kukidhi mahitaji ya kitaifa ya chakula unaongezeka na kuweza kuzalisha ziada kwa masoko ya kikanda na kimataifa,” alisema na kuongeza: “Mauzo yetu ya nje ya kilimo yaliongezeka kutoka dola za Marekani bilioni 2.1 mwaka 2021/2022 hadi kufikia dola bilioni 3.7 mwaka 2024/2025.”

Alisema nchini Tanzania, kilimo kinabaki kuwa nguzo ya mageuzi ya kiuchumi kwa kuwa hivi sasa inachangia asilimia 24.6 ya Pato la Taifa, inaajiri asilimia 65 ya nguvu kazi na inazalisha takriban asilimia 30 ya mapato ya mauzo ya nje na malighafi kwa viwanda nchini.

Alitumia fursa hiyo kumpongeza Mshindi wa Tuzo ya Chakula Duniani wa mwaka 2026 Prof. Huub Lelieveld kwa mafanikio aliyopata akisema kwamba yanaikumbusha dunia kuwa usalama wa chakula haupatikani tu wakati chakula kinapopatikana. “Ukweli wa kisayansi ni kwamba chakula ni lazima pia kiwe salama, chenye lishe na kinachoweza kupatikana kwa bei nafuu.

Prof. Lelieveld ni mwanasayansi wa Uholanzi ambaye amekuwa akijihusisha na masuala ya usalama wa chakula. Ametangazwa kuwa mshindi wa mwaka 2026 na Taasisi ya Tuzo ya Chakula Duniani (World Food Prize Foundation).

Akizungumzia kaulimbiu ya mjadala huo isemayo “Kabla Njaa Haijatushinda”, Waziri Mkuu alisema inahitaji uharaka, lakini uharaka lazima uambatane na matumaini. “Afrika siyo tu bara linalokabiliwa na changamoto za usalama wa chakula bali pia ina uwezo mkubwa wa kuwa mchangiaji mkubwa wa usalama wa chakula duniani. Na Tanzania inakusudia kuwa sehemu ya mabadiliko hayo,” alisisitiza.

“Acha tuwekeze kwa wakulima, na tuwekeze pia katika sayansi. Tuwekeze kwa vijana na wanawake. Tuwekeze katika mifumo thabiti ya chakula. Na zaidi ya yote, tuwekeze katika uwezo wa kilimo barani Afrika. Kwa kweli, kabla ya njaa haijatushinda, tuchukue hatua, tuwekeze na tuvumbue pamoja. Tujenge mifumo ya chakula inayoweza kulisha vizazi vya sasa na vijavyo,” alisisitiza.

Katika hatua nyingine, Mwanzilishi na Mhariri Mkuu wa Jarida la Chakula, Kilimo, Lishe na Maendeleo la Afrika, Prof. Ruth Oniang’o alisema anaamini ndani ya muda mfupi ujao, Tanzania itakuwa mfano kwa mataifa mengine kutokana na hatua inazopiga kwenye kilimo.

Prof. Oniang’o alikuwa akichangia mada ambapo alisifu jitihada za serikali zilizofanyika ikiwemo uwekezaji mkubwa katika miundombinu, kubuni miradi ya Jenga Kesho Bora (BBT) na kuwatumia maafisa ugani.

Waziri Mkuu ameambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Ngwaru Maghembe, Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde, Balozi wa Tanzania Washington, Dkt. Elsie Kanza na watendaji wengine wa Serikali.











Na Janeth Raphael -MichuziTv

Vijana wanaoshiriki katika sekta ya kilimo wamezitaka Serikali na wadau wa maendeleo kuweka mazingira rafiki yatakayowawezesha kupata mitaji, ardhi, pembejeo na masoko ili kunufaika na fursa za ajira na ujasiriamali zinazopatikana katika sekta hiyo.

Wito huo umetolewa wakati wa kongamano la siku mbili la National Youth Parliamentary Dialogue on Agrifood Systems Transformation, linalofanyika Oktoba 23 na 24, 2026, katika Hoteli ya Morena, Dodoma, likiwakutanisha vijana, Wabunge, wawakilishi wa Serikali na wadau wa kilimo kujadili namna ya kuwawezesha vijana kushiriki kikamilifu katika mifumo ya chakula na biashara za kilimo.

Donald Mezambwa, Programu Ofisa wa Vijana, Jinsia na Maendeleo ya Ujasiriamali kutoka AGRA Tanzania, amesema kongamano hilo linalenga kubaini vikwazo vinavyowakabili vijana na kutafuta suluhisho kwa kushirikiana na watunga sera. Ameeleza kuwa kupitia mradi wa YEFA, unaofadhiliwa na Mastercard Foundation kwa miaka mitano, vijana wanalengwa kupata fursa za ajira kupitia kilimo na mifumo ya chakula.

Mezambwa amesema pamoja na changamoto za mitaji na gharama za uzalishaji, vijana wengi wanakosa taarifa muhimu kuhusu taratibu za biashara za mipakani, ikiwemo Simplified Trade Regime (STR), inayorahisisha biashara ndogo za bidhaa zenye thamani isiyozidi Shilingi milioni mbili kwa kuzingatia masharti husika. Amesisitiza umuhimu wa kuwawezesha vijana kupata taarifa na ujuzi utakaowasaidia kupanua biashara zao.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Tavia Agribusiness Company Limited, Charles Constantine Masasi, amesema upatikanaji wa ardhi, mitaji na masoko ni nguzo muhimu kwa vijana wanaotaka kuwekeza katika kilimo. Ameeleza kuwa kampuni yake ilinufaika na programu ya Building a Better Tomorrow (BBT) tangu mwaka 2023 na kupata mkataba wa Serikali mwaka 2024 wa kuzalisha mbegu, huku ikiomba ekari 30 kupitia Halmashauri ya Kibaha kwa ajili ya kilimo cha mboga na matunda.

Masasi amebainisha kuwa gharama kubwa za pembejeo zinaendelea kupunguza tija kwa wakulima, akitolea mfano wa mbolea inayouzwa kati ya Shilingi 80,000 na Shilingi 120,000 kwa mfuko, huku bei ya mahindi wakati mwingine isilingane na gharama za uzalishaji. Pia ameshauri mifumo ya mikopo kuzingatia uwezo wa mwombaji na uhalisia wa mradi, badala ya kutegemea historia ya mikopo pekee, hali inayoweza kuwanyima baadhi ya vijana fursa za kuanzisha au kupanua biashara.

Akizungumzia hatua za Serikali, Msimamizi wa Programu ya BBT katika Wizara ya Kilimo, Clephine Josephat, amesema Serikali inaendelea kuwawezesha vijana na wanawake kwa kuwapatia ardhi, mitaji, huduma za ugani na masoko.

Ameeleza kuwa kilimo kinachangia zaidi ya asilimia 24 ya Pato la Taifa na kuajiri zaidi ya asilimia 75 ya Watanzania, huku Serikali ikipanga kuanzisha mashamba 20 katika mikoa 10 ya Tanzania Bara. Aidha, Shilingi bilioni sita zimetengwa katika mwaka wa fedha husika kupitia Mfuko wa Pembejeo za Kilimo (AGITF) kwa ajili ya mikopo ya uwekezaji.

Josephat amesema ifikapo mwaka 2030, programu ya BBT inalenga kuchangia upatikanaji wa ajira milioni 1.6, kuweka ekari 340,000 katika uzalishaji na kupanua wigo wa programu hiyo hadi vijiji 12,000 vya Tanzania Bara.

Kwa ujumla, kongamano hilo linajadili pia namna ya kuimarisha mchango wa Bunge katika utungaji wa sera, ugawaji wa bajeti na usimamizi wa programu za kilimo, huku likitoa nafasi kwa vijana, wakiwemo wanawake vijana na vijana wenye ulemavu, kuwasilisha mapendekezo yatakayoboresha upatikanaji wa fursa.

Washiriki wanatarajia kuweka vipaumbele vya pamoja na mpango wa utekelezaji unaohusisha vijana, Serikali na Bunge ili kuhakikisha maazimio yanageuzwa kuwa hatua madhubuti za kuongeza ajira, kipato na ushiriki wa vijana katika maendeleo ya kilimo nchini.








• In 2024, the Coca-Cola system contributed USD 3.6 billion in value-added economic activity across the COMESA region.

• The Coca-Cola system and its value chain supported over 458,200 direct and indirect jobs across the region in sectors including agriculture, manufacturing, retail, transport, and services.

• The system spent almost USD 1.5 billion on goods and services from suppliers in COMESA member countries, driving local industry growth and economic resilience.

Dar-es-Salaam, Tanzania, 23 October 2026 – During the 19th COMESA Business Forum, a major economic platform for promoting trade and regional integration, the Coca-Cola system unveiled the results of a new study showcasing its significant economic contributions to the COMESA region. The study was conducted by global consultancy Steward Redqueen and highlights the transformative role Coca-Cola plays in fostering economic progress, creating employment, and supporting local industries.

“As this study shows, the Coca-Cola system continues to deliver substantial economic impact in COMESA, creating opportunities through local partnerships, investments, and supply chains,” said Luis Felipe Avellar, President of Coca-Cola's Africa Operating Unit . “The 19th COMESA Business Forum is an important platform to showcase how businesses like those that comprise the Coca-Cola system contribute to sustainable economic development in Africa.”

The 19th COMESA Business Forum has brought together leaders from across the region to discuss trade, innovation, and economic growth. Coca-Cola’s active participation as a key collaborator demonstrates its alignment with the forum’s mission of building stronger economic ties across the region’s 21 member countries.

The study revealed that the Coca-Cola system, incorporating its network of bottlers, suppliers,

Distributors, and retailers, contributed USD 3.6 billion to the region’s combined GDP in 2024, representing 0.3% of COMESA’s GDP. Through direct employment and its value chain, the system supported over

458,200 jobs.

“For every direct job created by the Coca-Cola system in COMESA, an additional 28 jobs are supported throughout the regional economy,” noted Avellar.

In addition to its employment multiplier, the Coca-Cola system’s integration within local economies fuels industrial and community advancement. The report highlighted that Coca-Cola spent almost USD 1.5 billion on suppliers across the COMESA region in 2024, benefitting industries like sugar production, manufacturing, packaging, and logistics.

“The Coca-Cola system operates as a critical economic engine across the COMESA region, empowering local suppliers, retailers, and distributors to thrive,” said Alfred Olajide, Vice President of East and Central Africa Operations at Coca-Cola. “The 19th COMESA Business Forum provides a meaningful opportunity to underscore our commitment not just to delivering beverages, but also driving innovation, collaborations, and sustainable development in the region.”

Beyond economic contributions, the Coca-Cola system continues to champion sustainability and

Community development initiatives in the region. Several COMESA member states benefit directly from the Coca-Cola system’s Africa Water Stewardship Initiative, a nearly USD 25 million program that addresses water-related challenges across 20 African countries by 2030.

The study leveraged a robust Multi-Regional Input-Output (MRIO) model to capture the Coca-Cola system’s impact across its activities, including operations, local procurement, and extensive value chain linkages. The findings demonstrate how Coca-Cola drives ripple effects through the economy, from agriculture to retail, illustrating the company’s strategic role in driving regional development.

Avellar concluded: “The 19th COMESA Business Forum reaffirms the importance of collaboration in achieving sustainable and inclusive economic growth. We are proud to collaborate with COMESA in building stronger economies and better futures for the communities we serve.”
Alfred Olajide, the Vice President of East and Central Africa Operations at Coca-Cola During speaks during the 19th COMESA Business Forum which is a major economic platform for promoting trade and regional integration. During the Forum, the Coca-Cola system unveiled the results of a new study showcasing its significant economic contributions to the COMESA region

Benki ya NMB kwa kushirikiana na CMC Agri Limited imezindua kampeni ya Korosho Yangu, Benki Yangu mkoani Mtwara, itakayowezesha vyama vikuu vitano vya ushirika kushindania matrekta, AMCOS kushindania pikipiki na wakulima mmoja mmoja kupata fursa ya zawadi za fedha kwa kuongeza amana benki katika msimu wa korosho wa 2026/2027.

Akizindua kampeni hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Donald Msengi, amesema matrekta hayo yanaweza kusaidia kupunguza changamoto za usafirishaji wa pembejeo na korosho katika maeneo yenye miundombinu duni. Ameitaka NMB kutoa elimu kuhusu masharti ya kampeni na mikopo, huku akiishauri kuangalia uwezekano wa kuwasaidia wakulima kupata mikopo ya kulipia bima ya afya kabla ya mavuno.

Mkuu wa Idara ya Kilimo Biashara wa NMB, Nsolo Mlozi, amesema matrekta hayo yatawezesha usafirishaji wa korosho, kunyunyizia dawa na maandalizi ya mashamba, huku washindi wakipatikana kwa kuzingatia kiwango cha amana, miamala na masharti ya kampeni.

Meneja wa CMC Agri Limited Tanzania, Stuart Leishman, amesema matumizi ya zana za kisasa ni muhimu kuongeza tija ya kilimo, huku Mwenyekiti wa MAMCU, Alhaji Azam Mfaume, akieleza kuwa kampeni hiyo itachochea ushindani wa vyama vya ushirika katika kuongeza amana na kuwasaidia wakulima kupata huduma bora za kilimo.












VIJANA wa leo wanapenda vitu vya kisasa, vya haraka na vyenye msisimko, na Meridianbet kwa kushirikiana na EGT Digital wanakuletea Spin Legends Tournament ya milioni 4. Sasa unaweza kufurahia michezo ya kasino ya kidigitali yenye muonekano wa kuvutia na ubora unaoendana na teknolojia ya sasa huku ukiwa kwenye kinyanganyiro cha kuondoka na sehemu ya fungu hili la milioni 4.

Kila mchezo unaohusika kwenye mashindano haya umeundwa kukupa uzoefu tofauti kila unapocheza. Kuanzia michoro ya kisasa hadi uchezaji mwepesi usio na usumbufu, EGT Digital imeweka viwango vipya vya burudani ya mtandaoni kwa wapenzi wa kasino. Na kila unapocheza unazidi kukusanya alama na kujiweka nafasi ya juu ya msimamo wa mashindano.

Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya MERIDIANBET au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Miongoni mwa michezo inayoshiriki kwenye michuano hii ni ile inayovutia wachezaji wengi ikiwemo Sugartime, Sugarville, Ventura Panda, Aztec Rush, Vampire Night na mingine mingi sana. Kila mmoja una mtindo wake wa kipekee unaoongeza hamasa na kufanya kila raundi kuwa ya kusisimua zaidi huku yote ikiwa na nafasi sawa za kukusogeza kileleni mwa msimamo.

Kupitia Meridianbet, unaweza kushiriki mashindano haya kwa urahisi ukiwa mahali popote na wakati wowote. Mfumo wake salama na rahisi kutumia unakupa uhuru wa kufurahia burudani bila usumbufu huku ukijaribu bahati yako ya kuondoka na mamilioni kupitia kwenye michezo unayoipenda.

Usikose nafasi ya kuwa sehemu ya mapinduzi haya ya kidigitali. Jiunge na Meridianbet leo, ingia kwenye ulimwengu wa EGT Digital, shiriki Spin Legends Tournament na ujionee mwenyewe burudani ya kisasa yenye msisimko na nafasi za kuondoka na ushindi mkubwa.


KWA dau dogo tuu unaweza ukatengeneza zaidi ya Mamilioni, mechi kibao za ushindi zipo kwaajili yako. Unasubiri nini sasa? Ingia kwenye akaunti yako na uanze safari yako ya ushindi leo.

EPL kuendelea kwa mechi moja siku ya leo ambapo Ipswich atakuwa nyumbani kukipiga dhidi ya Nottingham Forest ambao wapo nafasi ya 19 kwenye msimamo wa ligi, huku mwenyeji yeye yupo nafasi ya 10 kwenye msimamo wa ligi, hivyo hii ni mechi ngumu kwelikweli.

Ipswich Town itakuwa na faida ya kucheza nyumbani katika uwanja wa Portman Road, jambo linaloweza kuipa hamasa ya kuanza mchezo kwa kasi na kutafuta bao la mapema. Hata hivyo, itahitaji kuwa makini katika safu yake ya ulinzi, ambayo imekuwa ikiruhusu mabao katika baadhi ya michezo yake ya hivi karibuni.

Chukua mkwanja kupitia michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Kwa upande wa Nottingham Forest, timu hiyo itahitaji kutumia uzoefu wake na uwezo wa wachezaji wake wa kushambulia ili kupata matokeo mazuri ugenini. Uwepo wa Morgan Gibbs-White unaweza kuwa muhimu katika kutengeneza nafasi za kufunga na kuunganisha safu ya kiungo na washambuliaji. Jisajili hapa.

Mara ya mwisho kukutana Forest waliondoka na ushindi, hivyo hii ni nafasi ya wenyeji kulipa kisasi. Odds kubwa zipo hapa.

Kule Ujerumani pia BUNDESLIGA kuna mechi moja kali kati ya VFB Stuttgart dhidi ya Borussia Monchengladbach ambapo mwenyeji anaonekana kuwa na nafasi nzuri zaidi ya kupata ushindi katika uwanja wa MHPArena.

Stuttgart imeonyesha kiwango kinachobadilika katika ligi, lakini ushindi wake wa hivi karibuni dhidi ya Paderborn na Slovan Bratislava unaweza kuongeza kujiamini kwa kikosi hicho.

Kwa upande wa Borussia Monchengladbach, changamoto kubwa imekuwa safu ya ulinzi ambayo imekuwa ikiruhusu mabao mengi. Timu hiyo itahitaji kucheza kwa nidhamu, kupunguza makosa ya kujilinda na kutumia mashambulizi ya kushtukiza kupata nafasi za kufunga. Pamoja na hali hiyo ngumu, Monchengladbach bado inaweza kuwa hatari ikiwa Stuttgart itaacha nafasi nyingi nyuma. Suka jamvi lako hapa.

Halikadhalika kule ITALIA, SERIE A itaendelea ambapo Torino atakiwasha dhidi ya AC Monza huku tofauti ya pointi kati yao hadi sasa ni pointi 3 huku kila imu ikiwa inahitaji kupata ushindi mnono siku ya leo.

Torino inaingia katika mchezo huu ikiwa na morali nzuri baada ya kuifunga Parma mabao 3-0, huku Giovanni Simeone akifunga mabao mawili na Ché Adams akiongeza bao jingine. Timu hiyo imekusanya pointi 10 katika mechi zake tano za mwisho, jambo linaloonyesha kuwa imeanza kupata mwendelezo mzuri wa matokeo.

Kwa upande wa Monza wao, ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Cagliari umeongeza kujiamini kwa kikosi hicho kabla ya safari ya kwenda kukutana na Torino. Gustavo Varela alikuwa miongoni mwa wachezaji waliofanya vizuri kwa kufunga mabao mawili, huku Jay Robinson pia akichangia katika ushindi huo. Je nani kuondoka na ushindi siku ya leo?. Suka jamvi hapa.

Taharuki imetanda katika Kitongoji cha Saburi, kilichopo Makuyuni, Wilaya ya Monduli mkoani Arusha, kufuatia mgogoro wa ardhi unaohusisha wananchi na mwekezaji anayedaiwa kutaka kubomoa makazi yao.

Wananchi  wameeleza kwa uchungu hali wanayopitia kutokana na mgogoro huo, wakidai kuwa kundi la watu waliokuwa na silaha za jadi, likiambatana na tingatinga, lilifika eneo hilo kwa lengo la kubomoa nyumba zao.

Kwa mujibu wa maelezo ya wananchi hao, baadhi yao walijitokeza kuzuia zoezi hilo, hali iliyofanya   kukamatwa kwa baadhi ya wakazi ambao wanadaiwa kushikiliwa mahabusu kwa zaidi ya siku 20 bila kufikishwa mahakamani.

Aidha, baadhi ya wananchi wanadaiwa kuishi mafichoni kutokana na hofu ya kukamatwa, huku familia zikiendelea kukabiliwa na sintofahamu kuhusu usalama wa makazi yao na hatima ya mgogoro huo.

Wananchi hao wanaiomba Serikali na mamlaka husika kuingilia kati ili kuchunguza madai hayo, kuhakikisha haki inatendeka na kupata ufumbuzi wa kudumu wa mgogoro huo bila kuhatarisha maisha na makazi yao.







Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) imewajengea uwezo Wabunifu wa Majengo na Wakadiriaji Majenzi kuhusu mazingira ya haki katika mchakato wa zabuni za umma, ili waweze kudai haki zao pindi wanapoona hawakutendewa haki kwenye michakato ya zabuni za umma walizoshiriki.

Mkuu wa Sehemu ya Huduma za Sheria PPAA, Bi. Agnes Sayi akizungumza na waandishi wa Habari kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa PPAA, pembezoni mwa Mkutano Mkuu wa Sita wa Wabunifu wa Majengo na Wakadiriaji Majenzi, ulioandaliwa na Bodi ya Usajili wa Wabunifu wa Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) Jijini Arusha amesema lengo PPAA kushiriki maonesho hayo ni kutoa elimu kuhusu haki katika mchakato wa zabuni za umma.

“Sheria ya ununuzi wa Umma ya Mwaka 2023, iliweka sharti la lazima kuwa ununuzi wote wa umma ufanyike kieletroniki katika mfumo wa NeST, baada ya sharti hilo PPAA ilijenga Moduli ndogo ya kupokea na kushughulikia malalamiko na rufaa ambapo imekuwa na mchango mkubwa kwa taasisi nunuzi na waabuni,” amesema Bi. Sayi

Bi. Sayi ameongeza kuwa, awali kabla ya kuanza kwa matumizi ya Moduli ya kuwasilisha Malalamiko na rufaa, wazabuni ambao hawakuridhika na uamuzi wa Maafisa Masuuli na Taasisi Nunuzi walilazimika kuwasilisha malalamiko au rufaa zao moja kwa moja katika ofisi za PPAA, Dodoma. Jambo lililokuwa linatumia muda, gharama, kupotea kwa baadhi ya nyaraka za zabuni na kuchangia kupunguza misingi ya uwazi na uwajibikaji kwa pande zote mbili.

“Baada ya kuanza rasmi kwa matumizi ya Moduli hiyo imerahisisha uwasilishaji wa malalamiko na kutoa fursa kwa wazabuni wengi zaidi ikiwa ni pamoja na kuokoa muda, gharama, kuongeza uwazi na uwajibikaji katika mchakato ya ununuzi wa umma na Utunzaji wa kumbukumbu za malalamiko na rufaa kwa usahihi na urahisi,” amesema Bi. Sayi

Aidha, Bi. Sayi alifafanua kuwa mazingira ya haki katika mchakato wa zabuni za umma ni yale yanayohakikisha kuwa washiriki wote wanatendewa kwa usawa na bila upendeleo. Alisisitiza kuwa mazingira hayo yanapaswa kuzingatia sheria, kanuni na masharti yaliyowekwa katika nyaraka za zabuni, huku yakipinga vitendo vya rushwa na kuhakikisha uwazi na uadilifu katika mchakato mzima wa ununuzi wa umma.

Sanjari na matumizi ya Moduli, PPAA imefanikiwa kuanzisha huduma ya Mkutano kwa njia ya Mtandao “Video Conference” ambapo hutumika kusikiliza mashauri kwa wahusika walioshindwa kufika moja kwa moja katika Ofisi za PPAA kwa ajili ya kusikiliza mashauri yalilowasilishwa mbele yake.

Bi. Sayi ameongeza kuwa huduma ya Video Conference imetoa fursa ya kuwasikiliza wahusika wa shauri walioshindwa kufika PPAA kutokana na sababu mbalimbali na kuiwezesha Mamlaka ya Rufani kutekeleza jukumu lake la msingi la utatuzi wa migogoro itokanayo na michakato ya ununuzi wa Umma. 

“Kwa sasa baadhi ya mashauri yameshasikilizwa kwa kwa “video conference” na baadhi ya washiriki wakiwa katika mikoa mbalimbali ya Tanzania na wengine kutoka katika mataifa ya Afrika Kusini, Nigeria, Poland, India na China,” amebainisha Bi. Sayi

Katika hatua nyingine, Bi. Sayi ameongeza kuwa PPAA imenzisha matumizi ya Programu ya Simu ya Mkononi “Mobile App” kwa lengo la kuwawezesha wazabuni kuwasilisha malalamiko na rufaa dhidi ya maamuzi yanayotolewa katika michakato ya ununuzi wa umma. Hatua hii inalenga kupunguza gharama za kupata haki pamoja na kuharakisha utatuzi wa migogoro.

Bi. Sayi amewasihi Wabunifu wa Majengo na Wakadiriaji Majenzi na wadau wengine kuzingatia sheria na kanuni za ununuzi wa umma ili kuiwezesha Serikali kuwa na mfumo wa ununuzi unaochochea ushindani, matumizi bora ya fedha za umma na utekelezaji wenye mafanikio wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Mkutano Mkuu wa Sita wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu wa Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) ulioanza tarehe 20 – 23 Oktoba, 2026 umeongozwa na Kaulimbiu: Kuijenga Tanzania tunayoitaka kuelekea 2050: Kuimarisha Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa kwa Mazingira Endelevu ya Ujenzi