Kivutio cha Maporomoko ya Maji ya Napuru, kilichopo katika Shamba la Miti Meru jijini Arusha, kinachosimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), kimetwaa tuzo ya ubora katika vivutio vya asili na utalii wa maporomoko ya maji katika tuzo za East Africa Sustainability and Conservation Excellence Awards (ESCEA) 2026.

Tuzo hiyo ilikabidhiwa kwa TFS jana Oktoba 31, 2026, katika hafla iliyofanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, na Mkurugenzi wa Huduma Saidizi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), Mohamed Ally, aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa wakala huo, Dkt. Andrew Komba.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mohamed alisema tuzo hiyo ni utambuzi wa mchango wa TFS katika uongozi, ubunifu na juhudi za kuendeleza uhifadhi wa mazingira, matumizi endelevu ya rasilimali za asili na maendeleo endelevu katika Afrika Mashariki.

Kwa upande wake, Afisa Utalii wa Shamba la Miti Meru, Mhifadhi Masanja Kayanogu Juma, alisema tuzo hiyo ni chachu kwa TFS kuendelea kuimarisha juhudi za kulinda na kuhifadhi rasilimali za misitu zinazowezesha kuibua na kuendeleza vivutio vya utalii wa ikolojia.

Shamba la Miti Meru ni miongoni mwa maeneo yenye fursa za utalii wa ikolojia jijini Arusha, likiwa na Maporomoko ya Maji ya Napuru kama kivutio chake kikuu, kinachovutia wageni wanaotafuta uzoefu wa utalii unaotegemea urithi wa asili.

Hafla ya utoaji wa tuzo hizo iliwakutanisha viongozi wa Serikali, wafanyabiashara, wataalamu wa uhifadhi wa mazingira, wawekezaji, wadau wa utalii na wawakilishi wa mashirika mbalimbali kwa lengo la kutambua mafanikio katika uhifadhi na kuimarisha mahusiano ya kibiashara.










By Jacob Kasiri, Dar es Salaam.

Tanzania National Parks (TANAPA) has received two prestigious honours at the East Africa Conservation Excellence Awards 2026, recognising its contribution to wildlife protection, biodiversity conservation and environmental sustainability.

TANAPA won the Outstanding National Parks Conservation Company of the Year Award, while Ruaha National Park received the Excellence in Wildlife Conservation and Protected Area Management – National Park Award 2026. The awards were presented during a ceremony held at Serena Hotel in Dar es Salaam on Saturday October 31, 2026.

Guest of Honour Mohamed R. Ally, Director of Business Support Services, representing Dr. Andrew M. Komba, Chief Executive Officer of the National Food Reserve Agency (NFRA), commended TANAPA for its conservation leadership. He noted that the institution had continued to protect rare and endangered biodiversity, ensuring threatened species survived and their populations increased despite growing conservation challenges.

He also highlighted Ruaha National Park’s contribution to food security, noting that its conservation efforts help protect vital water sources supporting irrigation and rainfall, thereby strengthening agricultural production and food availability.

Receiving the awards on behalf of TANAPA Conservation Commissioner Massana Mwishawa, Ruaha National Park Commanding Officer, Assistant Conservation Commissioner Emmanuel Moirana, said the recognition would motivate the institution to strengthen conservation efforts and ensure natural resources continued contributing to national economic growth, environmental sustainability and food security.

Tanzania has 21 National Parks, including internationally renowned destinations such as the Serengeti, Nyerere, Ruaha and Tarangire, as well as Mount Kilimanjaro. These protected areas preserve vital ecosystems, support diverse wildlife populations and contribute significantly to tourism, employment, investment and the national economy.

The awards followed an evaluation by the East Africa Conservation Excellence Awards Committee, recognising organisations contributing to conservation, biodiversity protection, climate action and sustainable development. The honours also acknowledge the dedication of TANAPA’s workforce, government institutions, communities and development partners in safeguarding Tanzania’s natural heritage for present and future generations.







Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amewasili mkoani Kilimanjaro leo, Jumapili, Novemba 1, 2026, kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika ibada ya uzinduzi wa jengo jipya la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Nshara, wilayani Hai.

Waziri Mkuu amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu. Baadaye, alipowasili kanisani, amepokelewa na Mkuu wa KKKT, Askofu Dkt. Alex Malasusa, pamoja na Mkuu wa KKKT, Dayosisi ya Kaskazini, Askofu Dkt. Fredrick Onael Shoo.






Vifijo, nderemo na shangwe zilisikika mara baada ya Emilian Ngatunga na Witness Mshigeni kuhitimisha sherehe za ndoa yao ndani ya hifadhi ya Ngorongoro.

Wawili hawa ilikuwa chaguo lao la kipekee kwa ajili ya kuanza safari mpya ya maisha yao ya ndoa kufanya sherehe yao ya harusi katika eneo hili lenye mandhari ya kuvutia ambapo kuliifanya siku yao kuwa ya pekee zaidi, yenye furaha na kumbukumbu zisizosahaulika ambazo watazithamini maisha yao yote.

Wakielezea furaha yao, maharusi hao wameonesha kufurahishwa na uamuzi wao wa kuchagua Ngorongoro kuwa sehemu ya kufungia ndoa yao, wakieleza kuwa walipata uzoefu wa kipekee na usioweza kusahaulika.

“Kiukweli Ngorongoro ni sehemu ya pekee kuhitimisha harusi, mapenzi yetu yamekuwa moto moto kwa kufika hapa ni raha juu ya raha, mahaba juu ya mahaba”, walisema wapendao hao.

Ngorongoro inajulikana sana kutokana na historia yake hasa chimbuko la binadamu wa kale na wengine husema kwamba kutokana na historia yake inawezekana tunda la mti wa kati lililiwa katika eneo hilo.














-Kampuni yapanga kupanua huduma na kuimarisha matumizi ya huduma za kidijitali ili kusaidia mawakala kukuza biashara zao

Mixx Tanzania inapanga kupanua huduma zinazopatikana kupitia mtandao wake wa mawakala zaidi ya 270,000 nchini, ili kuwaongezea fursa za kipato nje ya kamisheni wanazopata kutokana na miamala ya kuweka na kutoa fedha.

Mipango hiyo ni sehemu ya dhamira ya kampuni kuimarisha ushirikiano na mawakala wake kwa kupanua fursa za biashara, kuimarisha mawasiliano na kuongeza matumizi ya huduma za kidijitali katika shughuli zao za kila siku.

Akizungumza katika hafla ya ‘Mixx Wakala Brunch’ iliyofanyika Dar es Salaam leo iliyoadhimisha miaka 16 ya ushirikiano na mawakala, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mixx Tanzania, Bw. Louis-Olivier Favot, alisema mtandao huo sasa unawahudumia Watanzania takribani milioni 28.

“Tangu enzi za Tigo Pesa hadi leo Mixx, ninyi ndio mmetusaidia kujenga biashara hii. Mnafungua biashara zenu mapema na kufunga usiku, mkiwahudumia wateja kila siku. Mnahakikisha fedha taslimu, salio na chenji vinapatikana, huku jamii ikiendelea kuwaamini,” alisema Favot.

Alisema kampuni inapanga kuongeza huduma katika vituo vya mawakala ili kupanua vyanzo vyao vya mapato na kuwawezesha kukidhi mahitaji zaidi ya kifedha ya wateja.

“Tunapanga kuongeza huduma kupitia vituo vyenu ili muweze kupata kipato, nje ya kamisheni za kuweka na kutoa fedha,” alisema.

Upatikanaji wa fedha taslimu na floti unaendelea kuwa muhimu katika shughuli za mawakala. Upungufu wake unaweza kuwazuia kukamilisha miamala, hivyo kuwakosesha kamisheni na kuwalazimu wateja kutafuta huduma katika vituo vingine.

Kupitia huduma ya Bustisha Wakala, iliyoanzishwa kwa kushirikiana na Benki ya KCB Tanzania, zaidi ya mawakala 7,000 tayari wanapata msaada wa kuongeza salio la kuendeshea biashara zao kila siku. Favot aliwahimiza mawakala wengi zaidi kutumia huduma hiyo ili kuimarisha uwezo wao wa kuwahudumia wateja.

Kampuni pia iliangazia App ya Mixx Wakala, inayowawezesha mawakala kusimamia miamala na kufuatilia mwenendo wa biashara zao kidigitali kupitia simu. Favot alisema Mixx itaendelea kuboresha huduma zake kwa kuzingatia maoni ya mawakala na kuwasaidia kunufaika zaidi na huduma zinazopatikana.

Katika mipango yake kuelekea mwaka 2030, Mixx inalenga kuwawezesha mawakala wengi zaidi kutumia zana za kidijitali kusimamia biashara zao na kuwahudumia wateja wengi zaidi.

Aidha, Favot alisema kutakuwa na mikutano ya mara kwa mara kati ya mawakala, yeye mwenyewe na timu ya uongozi wa kampuni. Mikutano hiyo itawapa mawakala nafasi ya kuwasilisha changamoto, kupendekeza maboresho na kujadili namna ya kuimarisha ushirikiano wao na Mixx.

Kampuni pia itakuwa ikipitia mara kwa mara masharti ya biashara na ushirikiano wake na mawakala ili kuhakikisha pande zote zinanufaika na juhudi za mawakala zinatambuliwa ipasavyo.

Favot aliwataka mawakala kuendelea kutoa maoni kuhusu uzoefu wao, changamoto wanazokutana nazo katika vituo vyao na huduma zinazohitajika na wateja, ili kusaidia kampuni kuboresha huduma zake.

Kwa upande wake, John Mkwizu, wakala wa Mixx anayefanya shughuli zake eneo la Magomeni, Dar es Salaam, alieleza umuhimu wa upatikanaji wa salio na matumizi ya zana za kidijitali katika biashara yake.

“Wateja wanatutegemea kupata fedha zao wanapozihitaji. Ninaposhindwa kukamilisha muamala, wanalazimika kutafuta wakala mwingine, nami ninakosa kamisheni. Upatikanaji wa salio la uwakala unaniwezesha kuendelea kuwahudumia, huku App ya Mixx Wakala ikinirahisishia usimamizi wa miamala yangu ya kila siku.

“Kama wakala, nataka kutoa huduma za kuaminika, kuwafanya wateja warudi tena na kupata kipato cha kutosha kukuza biashara yangu,” alisema Mkwizu.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mixx Tanzania, Louis-Olivier Favot, akizungumza na mawakala wa Mixx (hawapo pichani) wakati wa hafla ya Mixx Wakala Brunch iliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Hafla hiyo iliadhimisha miaka 16 ya ushirikiano na mawakala, ambapo kampuni ilitangaza mipango ya kupanua huduma kupitia mtandao wake wa mawakala zaidi ya 270,000 ili kuwaongezea fursa za kipato. Kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Njia mbadala za Kidigitali na Usambazaji - Mixx Tanzania, Bw. Innocent Mosha.





 

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imewataka Makarani Waongozaji Wapiga Kura katika kata ya Nonde iliyopo Halmashauri ya Jiji la Mbeya Mkoani Mbeya kutekeleza majukumu yao kwa weledi.
 
Hayo yamebainishwa leo Oktoba 31, 2026 na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele wakati akizungumza na watendaji hao alipotembelea mafunzo yao ya siku moja ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya uchaguzi Mdogo wa Udiwani katika Kata ya Nonde unaotarajiwa kufanyika tarehe 04 Novemba,2026.
 
Jaji Mwambegele  amewasisitiza washiriki hao  kufanya kazi kwa weledi na kwa kuzingatia Sheria na Kanuni ili kuufanya uchaguzi huo kuwa huru na wa haki.
 
Awali kabla ya ufunguzi wa Mafunzo haya, washiriki hao waliapa kiapo cha kutunza siri na kile cha kujitoa uanachama wa chama cha siasa ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa haki na weledi.
 
Uchaguzi huo utafanyika ikiwa ni miongoni mwa kata  kata 11 za Tanzania Bara ambazo ni Lugenge, Halmashauri ya Mji Njombe; Bargish, Halmashauri ya Mji Mbulu; Makole, Halmashauri ya Wilaya ya Muheza; Mwera, Halmashauri ya Wilaya ya Pangani na Oldonyosambu, Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro.
 
Nyingine ni Igalula iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Uyui; Shelui, Halmashauri ya Wilaya ya Iramba; Mvumi, Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa; Nyarero, Halmashauri ya Wilaya ya Tarime na Ilolangulu, Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe.






Na Said Mwishehe,Michuzi TV

TANZANIA inatarajia kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Wabunge Wanawake kwa mwaka 2026 wa Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu.

Akizungumza leo Oktoba 31,2026 jijini Dar es Salaam Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mussa Zungu amesema mkutano huo muhimu unatarajiwa kuwa na washiriki zaidi ya 300 kutoka nchi 12 za Ukanda wa Maziwa Makuu na unatarajia kuanza Novemba 2 mwaka katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Julius Nyerere.

“Na utawakutanisha viongozi wakuu na wadau mbalimbali ili kujadili masuala yenye maslahi ya pamoja katika kukuza maendeleo, amani, na ushirikiano wa kikanda. Mgeni rasmi katika ufumguzi wa mkutano huo ni Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

“Viongozi wengine mashuhuri watakaohudhuria hafla ya ufunguzi ni pamoja na Judith Suminwa Tuluka ambaye ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambaye ni mgeni maalum; Adao Francisco Correia de Almeida ambaye ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Angola naRais wa Jukwaa la Kibunge la Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu;

“Wengine ni Amason Jeffah Kingi ambaye ni Spika wa Bunge la Seneti la Kenya, Jacob Oboth – Oboth ambaye ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Uganda, Aime Boji Sangara ambaye ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Zubeir Ali Maulid ambaye ni Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar na Malungo Chisangano ambaye ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Zambia.”

Zungu amesema mkutano huo unafanyika chini ya kauli mbiu isemayo ‘Amani na maendeleo kwa ajili ya Ukanda wa Maziwa Makuu.Lengo lake kuu ni kuimarisha ushirikiano na kuongeza mchango wa wanawake katika maamuzi, Diplomasia ya kibunge, amani, usalama na maendeleo endelevu kwenye Ukanda wa Maziwa makuu.

Aidha, Mkutano huo ni fursa muhimu ya kuimarisha mshikamano na ushirikiano miongoni mwa nchi wanachama, pamoja na kujadili mikakati ya kukabiliana na changamoto zinazoukabili ukanda wetu.

Vilevile, amesema Tanzania kuwa Mwenyeji wa Mkutano huo kunaleta taswira chanya kwa nchi yetu kuendelea kuaminiwa na mataifa mengine kama nchi yenye amani na inayoendeleza na kutambua misingi ya utawala bora chini ya Uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Ametoa mwito kwa Watanzania wote kushirikiana kwa pamoja ili kuhakikisha wageni wanapokelewa kwa bashasha, upendo, na ukarimu uleule unaoitambulisha nchi yetu duniani. Hiyo ni fursa adhimu ya kuwaonesha utamaduni wetu tajiri, mshikamano wetu thabiti, na uzuri wa kipekee wa Tanzania yetu.

“Kila mmoja wetu na awe balozi mwema kwa kuonesha heshima, nidhamu ya hali ya juu, usafi wa mazingira yetu, na moyo wa dhati wa kuwajali wageni wetu. Wewe ukiwa kama Mtanzania simama kama balozi, ili kila mgeni atakayeondoka, aondoke na kumbukumbu nzuri na zisizosahaulika mioyoni mwao kuhusu Tanzania.”


TANZANIA inatarajiwa kuwa kitovu cha biashara na uwekezaji katika sekta ya kilimo cha hotikacha barani Afrika kupitia jukwaa la kimataifa la HortiLogistica Africa 2026, litakalowakutanisha wakulima, wawekezaji, wafanyabiashara, wanunuzi wa kimataifa, wasafirishaji na wadau mbalimbali wa mnyororo wa thamani wa mazao ya mboga, matunda na maua kutoka ndani na nje ya nchi.

Jukwaa hilo linatarajiwa kufanyika kuanzia Novemba 8 hadi 10 mwaka 2026 katika viwanja vya TGT, mkoani Arusha, likiwa na lengo la kuunganisha wazalishaji wa mazao ya hotikacha na masoko ya ndani na kimataifa, pamoja na kuweka mazingira bora ya kuvutia mitaji na teknolojia mpya katika sekta hiyo.

HortiLogistica Africa 2026, inayoandaliwa na Asasi Kilele ya Sekta Binafsi inayojishughulisha na kuendeleza na kukuza sekta ya hotikacha nchini (TAHA), kwa kushirikiana na Serikali kupitia Wizara ya Kilimo, inatarajiwa kukutanisha wakulima, wasafirishaji, wanunuzi, teknolojia, vionhozi, wafanyabiashara na wataalamu kutoka zaidi ya nchi 40 duniani.

Umuhimu wa jukwaa hilo hauishii katika maonesho pekee, bali linatoa fursa ya kujenga mahusiano ya kibiashara kati ya wakulima na wanunuzi wakubwa wa kimataifa, kupata mikataba ya kuuza mazao nje ya nchi, kuvutia wawekezaji na kubadilishana teknolojia zitakazosaidia kuongeza uzalishaji na ubora wa mazao.

Aidha, jukwaa hilo linatarajiwa kufungua fursa katika maeneo mbalimbali ya mnyororo wa thamani wa hotikacha, yakiwemo uzalishaji wa kisasa, upatikanaji wa mbegu bora, pembejeo, vifaa vya kilimo, teknolojia za umwagiliaji, uhifadhi wa mazao, ufungashaji, usafirishaji na huduma za ugavi wa kimataifa.

Katika eneo la biashara ya kimataifa, uwepo wa wanunuzi, wasafirishaji na wawekezaji utatoa nafasi kwa wakulima na kampuni za ndani kupata taarifa za mahitaji ya masoko ya nje, viwango vya ubora vinavyohitajika na namna ya kukidhi masharti ya usafirishaji wa mazao kwenda kwenye masoko mbalimbali duniani.

Pamoja na hayo, matumizi ya teknolojia za kisasa za uhifadhi na usafirishaji wa mazao katika mifumo ya cold chain yanatarajiwa kuwa miongoni mwa maeneo muhimu ya majadiliano, hatua inayoweza kusaidia kupunguza upotevu wa mazao baada ya kuvunwa na kuongeza ushindani wa bidhaa za Tanzania katika soko la kimataifa.

Kwa upande mwingine, jukwaa hilo ni fursa muhimu kwa vijana na wajasiriamali kuingia katika biashara zinazohusiana na hotikacha, ikiwemo huduma za usafirishaji, usindikaji, ufungashaji, uuzaji wa pembejeo, teknolojia za kilimo na huduma za kifedha.

Aidha, Serikali imekuwa ikitambua sekta ya hotikacha kama eneo lenye uwezo wa kuchochea uwekezaji, kuongeza mapato ya wakulima, kukuza biashara ya nje na kupanua wigo wa ajira kwa Watanzania.

Kupitia HortiLogistica Africa 2026, Tanzania inalenga kutumia nafasi yake ya kimkakati katika ukanda wa Afrika Mashariki na fursa za miundombinu ya usafiri na masoko ili kujenga mazingira yatakayoiwezesha nchi kuwa kitovu cha biashara na usambazaji wa mazao ya hotikacha barani Afrika.

Kaulimbiu ya jukwaa hilo ni “Bridging Markets, Cultivating Prosperity”, ikimaanisha kuunganisha masoko na kukuza ustawi kupitia kilimo, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na kuendeleza sekta ya hotikacha.

Hivyo, HortiLogistica Africa 2026 inatarajiwa kuwa jukwaa muhimu la kuunganisha uzalishaji na masoko, ambapo mafanikio yake yatapimwa pia kwa uwezo wa kuzalisha mikataba ya biashara, uwekezaji mpya, teknolojia na fursa endelevu kwa wakulima na wafanyabiashara wa Tanzania na Afrika kwa ujumla.




WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo (Jumamosi, Oktoba 31, 2026) ameongoza Kikao cha Kamati ya Katiba, Sheria na Bunge ya Baraza la Mawaziri.

Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Spika, bungeni jijini Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu Mkuu Kiongozi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, mawaziri na naibu mawaziri wa wizara mbalimbali.



Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar na Mlezi wa Mkoa wa Katavi, Ndg. Abdi Mahamoud Abdi, amewapongeza viongozi wa mkoa huo kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kuimarisha maendeleo na kutekeleza maelekezo ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Serikali.

Ndg. Abdi ametoa pongezi hizo leo, Oktoba 31, 2026, alipotembelea mabanda ya Maonesho ya Wiki ya Mwanakatavi 2026 yanayofanyika katika Viwanja vya Mizengopinda, Kata ya Kabungu, Wilaya ya Tanganyika, mkoani Katavi.

Akiwa katika ziara hiyo, Ndg. Abdi amewasilisha salamu kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, huku akipongeza juhudi za maendeleo zinazotekelezwa katika mikoa mbalimbali nchini, hususan Katavi.

Amesema ameridhishwa na namna maonesho hayo yanavyowezesha wananchi kupata huduma mbalimbali, kuwasilisha kero zao kwa wahusika na kupata ufumbuzi wa changamoto zinazowakabili katika maisha yao ya kijamii na kiuchumi.

Aidha, ameupongeza ubunifu wa kuanzishwa kwa Kituo cha Huduma kwa Pamoja (One Stop Center), kinachorahisisha upatikanaji wa huduma za usajili na nyaraka kwa wafanyabiashara kupitia halmashauri.

Vilevile, amegusia umuhimu wa ubunifu unaolenga kuboresha maisha ya nyumbani, kuimarisha afya na kudumisha usalama wa mazingira.