▪️ Aeleza hatua tatu za kuharakisha miradi ya barabara nchini

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesisitiza kuwa hukumu za mahakama lazima ziheshimiwe na kutekelezwa kwa mujibu wa sheria, akisema mtu asiyeridhika na uamuzi wa mahakama anapaswa kutumia taratibu za kisheria kuupinga badala ya kuzuia utekelezaji wake.

Ameyasema hayo leo, Jumamosi, Novemba 21, 2026, wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Mtongani, Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha, mkoani Pwani.

Kauli hiyo imefuatia malalamiko ya Omari Rajabu Mganga, mkazi wa Kata ya Janga, aliyedai kushinda kesi ya ardhi katika Mahakama Kuu lakini bado anakabiliwa na mgogoro baada ya eneo hilo kudaiwa kuuzwa kwa mtu mwingine.

“Maelekezo ya mahakama hayawezi kupindishwa pindishwa kwa njia isiyo ya kisheria,” amesema Dkt. Mwigulu.

Ameelekeza afisa wa sheria na Jeshi la Polisi kuhakiki nyaraka za kesi hiyo na, iwapo hukumu itathibitisha madai ya mlalamikaji, kushirikiana na Mkuu wa Wilaya kuhakikisha anakabidhiwa eneo hilo kwa mujibu wa sheria.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema Serikali imeweka vipaumbele vitatu vya kuharakisha utekelezaji wa miradi ya barabara nchini, ambavyo ni kurejesha kasi ya miradi iliyokwama kutokana na changamoto za malipo, kutoa fedha za awali kwa wakandarasi wenye mikataba na kukamilisha taratibu za miradi ambayo wakandarasi wamepatikana lakini mikataba haijasainiwa.

Amesema zaidi ya Sh. bilioni 330 zimepelekwa kwenye mifuko ya barabara katika kipindi cha takribani mwezi mmoja, kufuatia utaratibu wa kuelekeza fedha moja kwa moja kwenye mifuko hiyo ili kuharakisha utekelezaji wa miradi.

Aidha, ameelekeza mkandarasi wa barabara ya Mlandizi–Stesheni ya SGR (Ruvu), yenye urefu wa kilometa 23, kulipwa fedha za awali ili kuharakisha kuanza kwa ujenzi, huku akizitaka mamlaka husika kukamilisha masuala ya uthamini na fidia ili kuondoa vikwazo vya utekelezaji wa mradi huo.








*Makamu wa Rais Kufungua maadhimisho ya mwaka mmoja wa maendeleo ya vijana nchini

Na Mwandishi Wetu
SERIKALI imesema imeendelea kutekeleza programu mbalimbali zinazolenga kuwawezesha vijana kiuchumi, kijamii na kuwajengea uwezo wa kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya taifa.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Joel Nanauka, amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu maadhimisho ya mwaka mmoja ya mafanikio ya vijana yatakayohusisha taasisi mbalimbali za Serikali.

Amesema maadhimisho hayo yatafanyika Novemba 23, mwaka huu, katika Ukumbi wa Super Doll, Dar es Salaam, na kufunguliwa na Makamu wa Rais, Deogratius Ndejembi.

Nanauka amesema maadhimisho hayo yatakuwa fursa ya kuonesha mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha mwaka mmoja, ikiwemo shughuli mbalimbali zinazofanywa na vijana ambazo zimekuwa chachu ya kujiajiri na kuunda ajira kwa wengine.

Amesema katika kipindi hicho, Ofisi ya Maendeleo ya Vijana imepiga hatua katika kuratibu na kusimamia utekelezaji wa programu zinazolenga kuwawezesha vijana kiuchumi, kijamii, pamoja na kuwajengea uwezo wa kushiriki katika shughuli za maendeleo ya taifa.

Ameeleza kuwa afua zilizotekelezwa zimejikita katika uwezeshaji wa vijana kiuchumi, malezi na makuzi, elimu ya uraia na uzalendo, pamoja na kuimarisha uratibu na ushirikiano na wadau mbalimbali wa maendeleo ya vijana nchini.

Aidha, amesema maadhimisho hayo yatatoa fursa ya kuonesha misingi iliyowekwa katika kuimarisha mifumo ya uratibu, ushirikishwaji na uwezeshaji wa vijana, huku yakibainisha vipaumbele vya utekelezaji wa majukumu kwa kipindi kijacho.

Amesema hatua nyingine muhimu iliyofikiwa ni kuanzishwa kwa mifumo inayolenga kurahisisha upatikanaji wa taarifa, huduma na fursa kwa vijana, ikiwemo Mfumo wa Uwezeshaji Vijana (Youth Empowerment System – YFS), ambao katika kipindi cha majaribio umefanikiwa kusajili vijana 110,155 kabla ya kuzinduliwa rasmi.

“Katika mfumo wa uwezeshaji wa vijana, ofisi inalenga kurahisisha upatikanaji wa taarifa za huduma na fursa zinazotolewa na Serikali pamoja na wadau, na kuwaunganisha vijana na taasisi zinazotoa huduma hizo,” amesema.

Vilevile, amesema katika maadhimisho hayo kutazinduliwa Mfumo wa Uratibu wa Maendeleo ya Vijana utakaowezesha taasisi za Serikali na wadau kupanga, kutekeleza na kufuatilia kwa pamoja programu za maendeleo ya vijana.

Amesema maadhimisho hayo yenye kaulimbiu ‘Mwaka Mmoja, Vijana Pamoja’ yatahusisha maonesho ya bidhaa, huduma na ubunifu wa vijana, pamoja na ushuhuda wa vijana walionufaika na fursa mbalimbali za uwezeshaji.

Fursa hizo ni pamoja na mitaji, mikopo, zabuni za Serikali, kilimo cha umwagiliaji, ufugaji wa samaki na shughuli za viwanda.ki na shughuli za viwanda
Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha Vijijini

WAZIRI Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa soko la kisasa la Mlandizi, wilayani Kibaha Vijijini, mkoani Pwani, lenye thamani ya Sh bilioni 7.7, huku akimuagiza mkandarasi kukamilisha mradi huo ifikapo Desemba mwaka huu.

Aidha, amewahakikishia wakandarasi nchini kuwa kuanzia sasa hakutakuwa na kisingizio cha kuchelewesha miradi kutokana na kutolipwa fedha, akisisitiza Serikali imeweka kipaumbele katika ulipaji wa madeni ya wakandarasi ili kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati.

Akizungumza Novemba 21, 2026, wakati wa ziara ya kikazi wilayani Kibaha Vijijini na mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero za wananchi, Mwigulu aliiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha kuhakikisha gharama za vizimba katika soko hilo hazipandishwi kupita kiasi ili kuepusha kuwakimbiza wafanyabiashara kwa gharama kubwa za upangishaji.

Akizungumzia changamoto ya kusuasua kwa ujenzi wa barabara ya Makofia-Mlandizi-Mzenga, Waziri Mkuu aliagiza mkandarasi alipwe fedha zinazostahili ili kuendelea na kazi, akieleza kuwa fedha za miradi ya maendeleo, hususan barabara zinazotekelezwa na TARURA na TANROADS, zimeanza kupewa kipaumbele katika utaratibu wa malipo.

“Kuanzia tulipoanza mwaka wa fedha Julai 2026, fedha za miradi ya maendeleo, hasa ya barabara za TARURA na TANROADS, zinakwenda kwenye mifuko ya barabara, hakutakuwa na kusuasua kwa mradi ulioanza utekelezaji, kipaumbele ni kuanza kulipa wakandarasi waliopo site, walioondoa mitambo na wale wanaostahili malipo ya awali,” alisema.

Kuhusu fidia, Mwigulu alisisitiza umuhimu wa wananchi wanaopisha miradi kulipwa kwa wakati ili kupunguza migogoro inayoweza kukwamisha utekelezaji wa miradi, akifafanua kuwa Serikali inatambua umuhimu wa miundombinu, ikiwemo barabara, katika maendeleo ya wananchi.

Alieleza kuwa ucheleweshaji wa baadhi ya miradi ya barabara haukutokana na uzembe, bali ulitokana na Serikali kuelekeza nguvu na rasilimali katika kukamilisha mradi mkubwa wa kimkakati wa Bwawa la Mwalimu Nyerere, Rufiji, uliokamilika kwa gharama ya Sh trilioni 6.

Mhandisi wa Mkoa, Charles Kabeho, alisema ujenzi wa soko la Mlandizi umefikia asilimia 93, ukiwa na vizimba 770 na majengo manne, huku mradi huo ukitarajiwa kunufaisha wananchi 800.

Alieleza kuwa hadi sasa Sh bilioni 5.132 zimetolewa kwa mradi huo, ambapo mkandarasi amelipwa Sh bilioni 4.543 na majengo yote yako katika hatua za umaliziaji.

Naibu Waziri wa TAMISEMI (Afya), Jafar Seif, alisema mkandarasi ameongezewa muda wa utekelezaji kulingana na makubaliano, hadi Desemba 25 mwaka huu.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, alisema barabara inayounganisha Mlandizi-Makofia hadi Maneromango yenye urefu wa kilomita 100 imegawanywa katika vipande vitatu vya utekelezaji, ambavyo ni Makofia-Mlandizi, Mlandizi-Ruvu na Ruvu-SGR-Maneromango.

Alisema kipande cha Makofia kuunganisha barabara kuu, usanifu umekamilika na hatua ya ulipaji fidia imefikia Sh bilioni 8.959, huku Hazina ikiendelea na maandalizi ya malipo.

Kasekenya alieleza kuwa kipande cha Mlandizi-SGR-Ruvu chenye urefu wa kilomita 23 kinatarajiwa kugharimu Sh bilioni 60.250, ambapo mkandarasi ameanza maandalizi na Serikali inaandaa malipo ya awali, huku kipande cha Ruvu-Maneromango usanifu wake ukiwa umekamilika na wananchi wakidai fidia ya Sh bilioni 13.

Awali, Mbunge wa Kibaha Vijijini, Hamoud Jumaa, aliishukuru Serikali kwa juhudi za kuinua sekta mbalimbali na kutenga fedha kwa ajili ya kukamilisha miradi ya maendeleo jimboni humo, huku akitaja changamoto zinazowakabili wananchi kuwa ni ujenzi wa barabara ya Makofia-Mlandizi-Mzenga kwa kiwango cha lami, ulipaji fidia na mkandarasi kukamilishiwa malipo.

Aliomba Ofisi ya Waziri Mkuu kuangalia ombi la Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha kupandishwa hadhi na kuwa Mamlaka ya Mji.














Na Karama Kenyunko, Michuzi TV
ONGEZEKO la magonjwa yasiyoambukiza limeendelea kuhitaji juhudi za pamoja katika kuhamasisha jamii kufanya mazoezi mara kwa mara, kuzingatia lishe bora na kufuatilia hali zao za kiafya ili kujikinga na magonjwa hayo.

Katika kuunga mkono juhudi hizo, Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kimekusanya washiriki zaidi ya 700 katika matembezi na mbio za hisani za msimu wa tano zilizofanyika katika kampasi ya chuo hicho jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika shughuli hiyo, Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Bruno Sunguye, amepongeza uongozi wa MUHAS kwa kuandaa matembezi hayo akisema yamewakutanisha wahitimu wa miaka mbalimbali, wanafunzi, wafanyakazi na wadau wa afya kutoka maeneo mbalimbali nchini na nje ya nchi.

Amesema shughuli hiyo inaunga mkono juhudi za Serikali kupitia Wizara ya Afya za kuhamasisha wananchi kufanya mazoezi, kuzingatia milo bora na kufahamu hali zao za kiafya ili kupunguza hatari ya magonjwa yasiyoambukiza.

“Tunawapa hamasa iwe mfano kwa vyuo vingine kuweza kuwa na matukio kama haya ili kwa pamoja tuweze kutengeneza jamii ambayo inakuwa na afya njema na katika harakati za kupambana na magonjwa yasiyoambukiza,” amesema.

Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa MUHAS, Profesa Appolinary Kamuhabwa, amesema chuo hicho kitaendelea kutumia matembezi hayo kuhamasisha jamii kujali afya kwa kuwa magonjwa yasiyoambukiza yanaendelea kuongezeka.

Amesema mwitikio wa washiriki umeendelea kuimarika, ambapo katika msimu huu wamefikia zaidi ya 700, wakiwemo washiriki kutoka Marekani, Ujerumani na Sweden.

Amesema MUHAS pia inaendelea kuboresha miundombinu ya mazoezi katika kampasi yake ya Muhimbili, ikiwemo ujenzi wa uwanja wa kisasa wa michezo, ukumbi wa mazoezi (gym) pamoja na vyumba vya kuogea na kubadilishia nguo ili kurahisisha ushiriki wa watu katika mazoezi.

Profesa Kamuhabwa amewahimiza wananchi kutumia huduma za uchunguzi wa afya zinazotolewa na taasisi za afya za chuo hicho ili kufahamu hali zao na kupata huduma wanapobainika kuwa na changamoto za kiafya.

Naye Rais wa Convocation ya MUHAS, Marsha Macatta-Yambi, amesema matembezi hayo yana nafasi ya kuwaunganisha wahitimu, wanafunzi na wafanyakazi wa chuo hicho, huku yakiimarisha uhusiano wao na chuo hata baada ya kuhitimu.

Amesema msimu wa tano umeonesha maboresho katika ushiriki na udhamini, huku washiriki wakifikia takribani 700 na vifaa vya ushiriki vikiuzwa vyote.

Ameongeza kuwa mapato yanayopatikana kupitia shughuli hiyo huelekezwa katika kusaidia maendeleo ya chuo, ikiwemo kuimarisha mazingira ya wanafunzi na utekelezaji wa mipango mbalimbali kupitia Mfuko wa Uwekezaji wa Ali Hassan Mwinyi wa MUHAS (Ali Hassan Mwinyi MUHAS Endowment Trust Fund).

Amesema matembezi hayo pia yamekuwa fursa ya wahitimu na wanafunzi kukutana, kukumbushana walikotoka na kuendelea kuchangia maendeleo ya chuo hicho.

MUHAS imekuwa ikiandaa matembezi na mbio hizo za hisani kwa misimu mitano mfululizo, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuhamasisha jamii kufanya mazoezi na kujenga utamaduni wa kujali afya.





Afisa wa Huduma Mpya za Kifedha wa Vodacom M-Pesa, Sylivester Lukeka(kulia), akielekeza wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakati wa hafla ya UDSM Freshers Connect iliyofanyika chuoni hapo, Novemba 20, 2026. Kupitia hafla hiyo, Vodacom Tanzania iliwahamasisha wanafunzi wapya kutumia teknolojia na huduma za kidijitali kama nyenzo muhimu za kujenga ujuzi, kujiongezea kipato na kujiandaa kwa fursa za ajira na ujasiriamali. 

Aidha, kampuni hiyo iliwatambulisha wanafunzi kwenye mpango wa TECHSTART, unaowawezesha kupata mafunzo mbalimbali ya Microsoft bila malipo ili kuwajengea ujuzi wa kidijitali. Sambamba na hilo, wanafunzi walielimishwa kuhusu huduma ya M-Wekeza ya Vodacom M-Pesa, inayowapa fursa ya kuanza kuwekeza na kujenga utamaduni wa kuweka akiba kwa ajili ya maisha yao ya baadaye. Hatua hiyo ni sehemu ya dhamira ya Vodacom Tanzania ya kuwawezesha vijana kushiriki na kunufaika na fursa zinazotokana na ukuaji wa uchumi wa kidijitali nchini.
Afisa wa Huduma Mpya za Kifedha wa Vodacom M-Pesa, Sylivester Lukeka (kushoto), akisikiliza swali kutoka kwa mmoja wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakati wa majadiliano yaliyofanyika katika hafla ya UDSM Freshers Connect, Novemba 20, 2026. Kupitia mazungumzo hayo, wanafunzi walipata ufafanuzi kuhusu huduma ya M-Wekeza na fursa za kujenga ujuzi wa kidijitali kupitia mpango wa TECHSTART, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Vodacom Tanzania za kuwaandaa vijana kutumia fursa za ajira, ujasiriamali na uchumi wa kidijitali.

Mkuu wa Idara ya Bei za Bidhaa na Makundi Maalumu ya Wateja wa Vodacom Tanzania, Gemma Vedasto Kamara akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakati wa hafla ya UDSM Freshers Connect iliyofanyika Novemba 20, 2026. Kupitia hafla hiyo, Vodacom Tanzania iliwahamasisha wanafunzi wapya kutumia teknolojia na huduma za kifedha za kidijitali kujenga ujuzi, kujiongezea kipato na kujiandaa kwa fursa za kiuchumi. 

Kampuni hiyo pia iliwatambulisha wanafunzi kwenye mpango wa TECHSTART, unaowawezesha kupata mafunzo ya Microsoft bila malipo, pamoja na huduma ya M-Wekeza inayowapa fursa ya kuanza safari ya uwekezaji na kujenga utamaduni wa kuweka akiba kwa ajili ya maisha yao ya baadaye.

Mkuu wa Idara ya Bei za Bidhaa na Makundi Maalumu ya Wateja wa Vodacom Tanzania, Gemma Vedasto Kamara (kulia), pamoja na Afisa wa Huduma Mpya za Kifedha wa Vodacom M-Pesa, Sylivester Lukeka (kushoto), wakimkabidhi zawadi mmoja wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (katikati), wakati wa hafla ya UDSM Freshers Connect iliyofanyika chuoni hapo Novemba 20, 2026.

Kampuni hiyo pia iliwatambulisha wanafunzi kwenye mpango wa TECHSTART, unaowawezesha kupata mafunzo ya Microsoft bila malipo, pamoja na huduma ya M-Wekeza inayowapa fursa ya kuanza safari ya uwekezaji na kujenga utamaduni wa kuweka akiba kwa ajili ya maisha yao ya baadayea kupata mafunzo ya Microsoft bila malipo, pamoja na huduma ya M-Wekeza inayowapa fursa ya kuanza safari ya uwekezaji na kujenga utamaduni wa kuweka akiba kwa ajili ya maisha yao ya baadaye.
Mkuu wa Idara ya Bei za Bidhaa na Makundi Maalumu ya Wateja wa Vodacom Tanzania, Gemma Vedasto Kamara (wa tano kutoka kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam waliokamilisha mafunzo ya muda mfupi kupitia mpango wa TECHSTART, wakati wa hafla ya UDSM Freshers Connect iliyofanyika chuoni hapo, Novemba 20, 2026. Wanafunzi hao walionesha vyeti vyao kwa kutumia simu zao kama ishara ya mafanikio baada ya kukamilisha mafunzo hayo, yanayolenga kuwajengea ujuzi wa kidijitali kupitia kozi fupi za Microsoft. Kupitia hafla hiyo, Vodacom Tanzania iliendelea kuonesha dhamira yake ya kuwawezesha vijana kwa kuwapatia fursa za kujifunza, huku pia ikiwahamasisha kutumia huduma ya M-Wekeza kujenga utamaduni wa kuweka akiba na kuwekeza kwa ajili ya maisha yao ya baadaye.

Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakiwahudumia wanafunzi katika banda la kampuni hiyo wakati wa hafla ya UDSM Freshers Connect iliyofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Novemba 20, 2026. Kupitia hafla hiyo, Vodacom Tanzania ilitoa elimu kuhusu matumizi ya huduma zake za mawasiliano na fedha kwa njia ya kidijitali, ikiwahamasisha vijana kutumia teknolojia kurahisisha shughuli zao za kila siku, kujenga tabia ya kuweka akiba na kutumia fursa mbalimbali za kiuchumi.


BURUDANI ya kasino mtandaoni ndani ya Meridianbet inazidi kupamba moto kufuatia kuwasili kwa mchezo mpya wa Jolly Jolly Bonanza kutoka Expanse, unaoleta ladha mpya ya burudani kwa wapenzi wa michezo ya kasino. Mchezo huu unakuja na mazingira ya kuvutia yaliyojaa furaha, msisimko na matukio yanayoufanya kila mzunguko kuwa sehemu ya burudani na ushindi.

Kupitia Jolly Jolly Bonanza, wachezaji wanapata nafasi ya kuingia katika ulimwengu wa burudani unaochanganya mvuto wa mchezo na msisimko wa kila unapocheza. Ni mchezo uliotengenezwa kwa lengo la kuongeza ladha ya kipekee katika safari yako ya kufurahia michezo mbalimbali inayopatikana ndani ya kasino ya Meridianbet.

Kinachoufanya mchezo huu kuwa wa kuvutia zaidi ni jina lake lenyewe, Jolly Jolly, linaloashiria furaha na burudani. Kila unapofungua mchezo na kuanza kuzungusha, unajiandaa kufurahia mazingira yake ya kipekee huku ukigundua kile ambacho mchezo huu mpya umekuandalia.

Expanse, kupitia ubunifu wake katika sekta ya michezo ya kasino, imeendelea kuleta chaguo mbalimbali za burudani kwa wachezaji. Safari hii, Jolly Jolly Bonanza inaongeza chaguo jipya ndani ya Meridianbet, ikiwapa wapenzi wa michezo ya kasino sababu nyingine ya kuchunguza burudani inayopatikana kwenye jukwaa hilo.

Sasa ni wakati wa kuipa nafasi burudani mpya! Tembelea Meridianbet, fungua sehemu ya kasino na ugundue Jolly Jolly Bonanza. Ingia kwenye mchezo, jifunze namna unavyochezwa na ufurahie kila hatua ya safari hii mpya ya burudani.

Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Usibaki nyuma wakati furaha imeanza rasmi! Jolly Jolly Bonanza imewasili na kukuletea msisimko mpya unaosubiri kugunduliwa. Chagua burudani yako, zungusha na ufurahie ladha ya mchezo huu mpya kutoka Expanse. Jolly Jolly Bonanza ipo ndani ya Meridianbet! Jiunge leo kwenye burudani, zungusha na ufurahie ushindi wa Jolly Jolly.

JE unajua kuwa mkwanja mrefu unakusubiri wewe pekee siku ya leo?. Mechi zipo nyingi sana na machaguo unayoyataka pia yapo. Suka jamvi lako la ushindi na uibuke bingwa sasa.

Ligi pendwa Duniani, EPL itaendelea ambapo mapema kabisa vijana wa Enzo Maresca Manchester City watakuwa Etihad kumenyana vikali dhidi ya Fulham ambao ni moja ya timu ngumu kweli kukabiliana nayo.

City hii ni mechi ambayo wanahitaji kushinda na wanaitazama kwa jicho tofauti sana kwani wametoka kupoteza mechi 3 mfululizo kwenye ligi na kushuka hadi nafasi ya 3 huku wageni wao wakiwa nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi wakiwa na pointi zao 10.

Hii ni mechi ambayo Maresca na vijana wake inabidi waamke kwani mbio za ubingwa zinazidi kuwa ngumu, na Meridianbet wao wanampa nafasi kubwa ya kushinda City pale nyumbani kwake. Je wewe unampa nani?. Beti hapa.

Pesa ipo kwenye michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Nao mabingwa watetezi wa ligi Arsenal watakuwa ugenini kusaka poinrti 3 muhimu dhidi ya Newcastle United ambao msimu huu haujawa mzuri sana kwao kwani mpaka sasa wamekusanya pointi 12 kwenye mechi 10 ambazo wamecheza.

Mara ya mwisho kukutana The Gunners waliondoka na ushindi hivyo hii ni mechi ya wenyeji kulipa kisasi. Lakini je wataweza kuambulia hizo pointi 3 mbele ya vijana wa Arteta ambao wanasifika kuwa na safu bora ya ulinzi?. Tengeneza jamvi hapa.

LALIGA pale tutaangazia mechi ya Real Madrid dhidi ya Celta Vigo ambapo vijana wa Mourinho wanatazamia kupata ushindi kwenye mechi hii ili waendelee kushikilia nafasi ya 2 ambayo wapo, huku wageni wao wanataka ushindi wavuke nafasi waliyopo.

Vijana wa Mourinho wameendelea kuwa na tawkimu nzuri za kushinda na sasa hii ni mechi nyingine wanayotaka kupata matokeo ili kujiweka sawa kwenye mbio za ubingwa, huku mechi hii ikipewa machaguo zaidi ya 1000 pale Meridianbet. Je unangoja nini kutandika jamvi lako la ushindi?.

Lakini pia unaweza ukapiga pesa nzuri kwenye mechi za ligii kuu ya ITALIA, yaani SERIE A ambapo vinara wa ligi Lazio watakuwa nyumbani kupepetana dhidi ya US Lecce hii ni moja ya mechi ambayo vijana wa Gattuso wanahitaji kupata ushindi kuendelea kujikita kileleni.

Ikumbukwe kuwa Lazio msimu huu hawapo kwenye mashindano yoyote ya Ulaya hivyo nguzu zao zote wanaziwekeza kwenye ligi na mpaka sasa haijapoteza mechi yoyote kwenye ligi. Mgeni wake yupo nafasi ya 14 akiwa amepoteza mechi 7 hadi sasa kwenye ligi.

ODDS KUBWA zipo kwenye mechi hii. Je wenyeji wataendelea kujikita kileleni kwa kupata ushindi na mechi hii?. Jisajili sasa.

Kule LIGUE 1 Ufaransa mechi kibao zipo na sisi tutawatazama mabingwa watetezi wa ligi, PSG ambao watakuwa ugenini dhidi ya OGC Nice ambao wao wapo nafasi ya 6 kwenye msimamo wa ligi baada ya kukusanya pointi zao 17.

Msimu uliopita vijana wa Enrique walishinda mechi zote mbili za ligi walizokutana, huku licha ya timu hiyo kuwa na majeraha za baadhi wa wachezaji muhimu bado inaendelea kuonesha ukubwa wake kwa kushinda mechi kubwa. Beti yako unampa nani leo?. Tandika jamvi hapa.



Na Karama Kenyunko, Michuzi TV
MASHIRIKA yasiyo ya kiserikali (NGOs) nchini yametakiwa kubuni vyanzo vya ndani vya mapato na kuimarisha ubia na sekta binafsi ili kupunguza utegemezi wa ufadhili kutoka nje na kuhakikisha uendelevu wa shughuli zake za kijamii.

Wito huo umetolewa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya Jukwaa la Sita la Mwaka la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, litakalofanyika jijini Dodoma kuanzia Novemba 25 hadi 28, 2026.

Dkt. Gwajima amesema changamoto ya utegemezi wa wafadhili, masharti magumu ya upatikanaji wa fedha na kutotabirika kwa ufadhili ni miongoni mwa mambo yanayohitaji majadiliano ya kina ili kupata suluhisho litakalowezesha mashirika hayo kuendelea kutoa huduma kwa jamii.

Amesema kutokana na hali hiyo, jukwaa la mwaka huu limejikita katika kaulimbiu isemayo, “Fikra Mpya Kuhusu Uendelevu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali: Ubunifu, Ubia na Upatikanaji wa Rasilimali Fedha Kupitia Vyanzo vya Ndani.”

Katika jukwaa hilo, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi, huku washiriki takribani 3,500 kutoka serikalini, sekta binafsi, washirika wa maendeleo, vyombo vya habari na mashirika yasiyo ya kiserikali wakitarajiwa kushiriki.

Dkt. Gwajima amesema zaidi ya mashirika 8,000 yaliyosajiliwa nchini yanatoa huduma katika sekta mbalimbali zikiwemo afya, elimu, maji, kilimo, uhifadhi wa mazingira, uwezeshaji kiuchumi, haki za binadamu, usawa wa kijinsia na ulinzi wa kijamii, hali inayodhihirisha umuhimu wa sekta hiyo katika maendeleo ya Taifa.

Amesema mchango wa mashirika hayo ni muhimu zaidi katika kipindi hiki ambacho Tanzania imeanza kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, iliyozinduliwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Julai 17, 2025.

Ameeleza kuwa Wizara hiyo iliandaa Juni 2026 Mkakati wa Kitaifa wa Mageuzi ya Kijamii na Maendeleo ya Mtaji Watu katika kufikia malengo ya Dira 2050, unaojulikana kama Jamii Ajenda Dira 2050, unaoongozwa na falsafa ya “Familia Imara, Jamii Imara, Taifa Imara.”

Kwa mujibu wa Waziri huyo, jukwaa hilo ni la sita tangu kuanzishwa kwake mwaka 2021 na litatoa fursa kwa wadau kujadili mafanikio, changamoto na fursa za ufadhili, pamoja na kubadilishana uzoefu kuhusu namna bora ya kuimarisha uendelevu wa mashirika hayo.

Amesema mijadala itafanyika Novemba 25 na 26 katika Ukumbi wa Urio Executive, huku kilele cha jukwaa kikifanyika Novemba 27 katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete.

Aidha, Novemba 28 kutakuwa na mbio za hisani katika Uwanja wa Jamhuri, utoaji wa huduma za afya kwa wakazi wa Dodoma, shughuli za uwajibikaji kwa jamii pamoja na maonesho ya bidhaa na shughuli zinazotekelezwa na mashirika na wadau wa sekta binafsi.

Dkt. Gwajima ametoa wito kwa taasisi za serikali, mamlaka za serikali za mitaa, sekta binafsi, washirika wa maendeleo, mashirika yasiyo ya kiserikali, vyombo vya habari na wananchi kujitokeza kushiriki jukwaa hilo ili kuongeza maarifa na kujenga mikakati ya pamoja ya kuimarisha sekta hiyo

MASHIRIKA yasiyo ya kiserikali (NGOs) nchini yametakiwa kuimarisha uendelevu wa shughuli zao kwa kutumia ubunifu, kujenga ubia na kutafuta rasilimali fedha kupitia vyanzo vya ndani ili yaweze kuendelea kutoa mchango katika kutatua changamoto zinazokabili jamii.

Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NACONGO), Jasper Makala, amesema hayo leo, Novemba 20, 2026 wakati akielezea maandalizi ya Jukwaa la Mwaka la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali 2026, ambalo kaulimbiu yake inajikita katika uendelevu wa mashirika hayo kupitia ubunifu, ubia na upatikanaji wa rasilimali fedha kutoka vyanzo vya ndani.

Makala amesema mashirika hayo yanafanya kazi katika sekta mbalimbali zikiwemo elimu, maji, afya, mazingira na nishati, hivyo yanahitaji kuwa endelevu ili kuweza kushirikiana na Serikali pamoja na sekta binafsi katika kutatua changamoto zilizopo katika maeneo hayo.

Amesema ubunifu na ubia ni miongoni mwa maeneo yatakayojadiliwa katika jukwaa hilo, ikiwemo matumizi ya teknolojia katika kukuza uendelevu wa mashirika na kuongeza mchango wake katika utekelezaji wa ajenda za kitaifa na kimataifa, ikiwemo Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2050.

Ameeleza kuwa katika eneo la ubunifu, washiriki watapata fursa ya kuona mtambo unaozalisha nishati ya haidrojeni kwa kutumia maji kwa ajili ya kupikia, ikiwa ni sehemu ya kuonesha mchango wa mashirika hayo katika kuunga mkono ajenda ya nishati safi ya kupikia nchini.

Amesema hatua hiyo inaendana na mkakati wa Serikali wa kuhakikisha ifikapo mwaka 2034, angalau asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia.

Aidha, amesema jukwaa hilo litawakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo wa sekta binafsi na taasisi za fedha kwa ajili ya kujenga ubia utakaosaidia mashirika yasiyo ya kiserikali kufikia uendelevu wa kifedha na kiutendaji.

Ameongeza kuwa kutakuwa na mbio za hisani zitakazolenga kukusanya fedha za kuanzisha mtaji wa awali wa Mfuko wa Pamoja wa Ruzuku kwa ajili ya kusaidia mashirika yasiyo ya kiserikali, huku akiwahimiza waandishi wa habari kutumia nafasi yao kuutaarifu umma kuhusu jukwaa hilo na umuhimu wake.
Shirika la Posta Tanzania kupitia Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini limeendelea kuimarisha uwezo wake katika kusimamia na kupima utekelezaji wa majukumu yake kwa kutembelea wizara mbalimbali za Serikali kwa lengo la kujifunza mifumo ya kidijitali inayotumika katika ufuatiliaji na tathmini ya utendaji kazi.

Miongoni mwa Wizara zilizotembelewa ni Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Wizara ya Ujenzi, Wizara ya Afya pamoja na Wizara inayosimamia masuala ya vijana.

Akizungumza kupitia Posta TV, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini wa Shirika la Posta Tanzania, Bi. Zahra Kitara, amesema ziara hiyo imekuwa na manufaa makubwa kwa Shirika kutokana na fursa ya kujifunza namna taasisi hizo zinavyotumia mifumo ya kidijitali kukusanya taarifa, kufuatilia utekelezaji wa majukumu na kupima utendaji kazi.

Amesema maarifa yaliyopatikana kupitia ziara hiyo yatasaidia Shirika kuimarisha usimamizi wa utendaji kazi, kufuatilia utekelezaji wa mipango yake na kuhakikisha malengo yaliyowekwa yanafikiwa kwa ufanisi.

Aidha, amesema matumizi ya mifumo hiyo yanatarajiwa kuwa na manufaa kwa wananchi kwa kuimarisha ufuatiliaji na ubora wa huduma mbalimbali za kiposta wanazopatiwa, kupitia usimamizi madhubuti wa utekelezaji wa majukumu ya Shirika.














Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, akipokea mkoba wenye machapisho na taarifa mbalimbali kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kutoka kwa Afisa Uhusiano Mkuu wa Mfuko huo, Bi. Queen Edward, alipotembelea banda la PSSSF katika Kongamano na Maonesho ya Sekta ya Majengo na Uwekezaji wa Ardhi (Tanzania Real Estate Expo and Forum – TAREX 2026), katika Ukumbi wa Superdome, Masaki, jijini Dar es Salaam, Novemba 20, 2026.


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, akipokea mkoba wenye machapisho na taarifa mbalimbali kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kutoka kwa Afisa Uhusiano Mkuu wa Mfuko huo, Bi. Queen Edward, alipotembelea banda la PSSSF katika Kongamano na Maonesho ya Sekta ya Majengo na Uwekezaji wa Ardhi (Tanzania Real Estate Expo and Forum – TAREX 2026), katika Ukumbi wa Superdome, Masaki, jijini Dar es Salaam, Novemba 20, 2026.



Dar es Salaam


WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, ameipongeza na kuitambua kazi nzuri inayofanywa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), katika kusimamia shughuli zake na kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Pongezi hizo amezitoa leo Novemba 20, 2026, alipotembelea banda la PSSSF katika Kongamano na Maonesho ya Sekta ya Majengo na Uwekezaji wa Ardhi (Tanzania Real Estate Expo and Forum – TAREX 2026), yanayofanyika kwa siku tatu jijini Dar es Salaam, ambapo alikuwa mgeni rasmi.

Akizungumza wakati akiwa katika banda hilo, Mhe. Dkt. Nchemba aliipongeza PSSSF kwa kazi nzuri inayofanya na kuhimiza kuendelea na juhudi hizo.

“Hongereni sana, natambua kazi nzuri mnayofanya. Endeleeni hivyo hivyo,” alisema Mhe. Waziri Mkuu.

Kwa mujibu wa Afisa Mwandamizi toka Idara ya Uwekezaji, Milki na Usimamizi wa Majengo wa PSSSF, Bw. Arnold Kagaruki, ushiriki wa PSSSF katika kongamano na maonesho hayo unatokana na nafasi yake kama mdau muhimu katika sekta ya majengo na uwekezaji wa ardhi, kupitia uwekezaji wake katika miradi mbalimbali ya majengo na ardhi nchini.

“ Kuna uwekezaji unaowagusa moja kwa moja wanachama na wananchi kama vile majengo ya kibiashara, nyumba na viwanja; lakini pia Mfuko umewekeza kimkakati ambapo kwa kushirikiana na Kituo cha Mikutano cha Kimataifa AICC, PSSSF imewekeza katika ujenzi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mount Kilimanjaro International Convention Centre Jijini Arusha ambapo ujenzi umeanza” alisema.

Kongamano na maonesho hayo yanawakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya majengo na uwekezaji wa ardhi, wakiwemo waendelezaji wa miradi ya majengo, wawekezaji, taasisi za kifedha, mamlaka za udhibiti pamoja na watoa huduma za kitaalamu kutoka Tanzania Bara, Zanzibar na Kenya.

Kupitia jukwaa hilo, PSSSF inalenga kuonesha mchango wake katika maendeleo ya sekta ya majengo na uwekezaji wa ardhi, kutangaza fursa zinazotokana na uwekezaji wake, kuimarisha mahusiano na wadau mbalimbali, pamoja na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu shughuli na huduma zinazotolewa na Mfuko, Alisema Bw. Kagaruki.




Haijawahi kutokea wanafunzi 90 kupelekwa kusoma nje ya nchi na Serikali kwa wakati mmoja. Kupitia Programu ya Samia Scholarship Extended, vijana hao wanakwenda Algeria kupata maarifa na ujuzi katika fani za sayansi na teknolojia, hatua inayochangia utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014, Toleo la 2023, na Dira 2050 kwa kujenga rasilimali watu yenye umahiri wa kuchochea maendeleo endelevu.

Akizungumza Novemba 20, 2026, jijini Dar es Salaam, wakati wa kuwaaga wanafunzi hao, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, amesisitiza kuwa wamechaguliwa kwa ufaulu wao katika masomo ya sayansi kidato cha sita, bila upendeleo. “Mmechaguliwa kwa sababu mmekuwa nyota katika mitihani yenu,” amesema, akifafanua kuwa ufadhili huo si mkopo, bali ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kuwaendeleza vijana wenye uwezo mkubwa.


Prof. Mkenda amesema uwekezaji katika sayansi na teknolojia unalenga kuijengea Tanzania uwezo wa kuendeleza sekta zake kwa kutumia wataalamu wake. Akitolea mfano reli, ameeleza kuwa kuwa na reli ni maendeleo, lakini kuweza kuijenga wenyewe ndiyo msingi wa maendeleo endelevu, huku akiwahimiza wanafunzi wengine kusoma kwa bidii ili kunufaika na fursa zinazotolewa na Serikali.


Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Wanu Hafidh Ameir, amesema wanafunzi hao wamebeba matumaini ya Taifa katika kuimarisha uwezo wa nchi kwenye sayansi na teknolojia. Amewataka kuitumia fursa hiyo kujijengea maarifa na ujuzi watakaoutumia kutatua changamoto za jamii na kuchangia maendeleo ya Tanzania baada ya kuhitimu masomo yao.

“Mmetumwa na Taifa. Taifa zima limewatuma,” amesisitiza Mhe. Wanu, akiwataka vijana hao kusoma kwa bidii, kutii sheria za Algeria, kudumisha maadili na uzalendo, pamoja na kusaidiana licha ya kwenda katika vyuo tofauti. Aidha, amewaomba wazazi kuendelea kuwashauri na kuwaombea watoto wao ili wakamilishe masomo na kurejea salama kulitumikia Taifa.

Naye Balozi wa Tanzania nchini Algeria, Mhe. Mobhare Matinyi, amesema manufaa ya ushirikiano wa elimu kati ya nchi hizo yanaonekana kupitia wahitimu wanaohudumu kama madaktari bingwa, wahadhiri, wahandisi na wataalamu wa TEHAMA nchini na katika kampuni za kimataifa. Amesema mafanikio hayo yanaonesha ubora wa elimu inayotolewa Algeria na umuhimu wa kuendelea kutumia fursa hizo kuandaa wataalamu wanaohitajika kwa maendeleo ya Tanzania.


Mwenyekiti Mwenza wa Kamati ya Ushauri ya Programu ya Samia Scholarship, Prof. Raphael Chibunda, amesema kamati inashirikiana na Wizara pamoja na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kutafuta nafasi katika vyuo bora duniani. Amewahimiza Watanzania waishio nje ya nchi, hasa wanaofanya kazi katika vyuo na taasisi za kimataifa, kutumia uzoefu na mahusiano yao kusaidia kuongeza fursa za masomo kwa vijana wa Kitanzania.

Akitoa ushuhuda wake, mnufaika wa programu hiyo, Hosea Gideon Ngalama, aliyesoma Shule ya Sekondari Kimamba iliyopo Kilosa, mkoani Morogoro, amemshukuru Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kumwezesha kuendelea na elimu kupitia ufadhili huo. Amejivunia kutoka katika shule ya Serikali na kupata nafasi hiyo, akieleza kuwa inaonesha namna Serikali inavyowajali vijana na kuwawezesha kutimiza ndoto zao za elimu.