Na Lydia Churi-Dodoma 

Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Mohamed Awadh leo amefungua Mafunzo ya kuwajengea uwezo wawakilishi wa habari wa Mahakama walioko kwenye kanda za Mahakama Kuu na Mahakama za Mikoa na kuwataka washiriki hao kujifunza namna ya kutoa taarifa za Mahakama zilizo sahihi ili kuboresha suala zima la utoaji wa haki kwa wananchi.

Akifungua mafunzo hayo mjini Dodoma, Jaji Awadh amesema Mahakama ya Tanzania kupitia Mpango Mkakati wake wa miaka mitano (2015/16-2019/20) inalenga kujenga imani ya wananchi kwa Mahakama na kuimarisha ushirikishwaji wa wadau katika shughuli zake ambapo kwa kuwapatia mafunzo wawakilishi wa habari ni moja ya mikakati ya kufanikisha jambo hilo. 

Mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo wawakilishi wa habari wa Mahakama walioko kwenye kanda za Mahakama Kuu na Mahakama za Mikoa yanawahusisha Watumishi wa Mahakama wakiwemo Maafisa Habari, Maafisa Utumishi, Maafisa Tawala, Maafisa Tehama pamoja na Wasaidizi wa Kumbukumbu.

Aidha mafunzo hayo pia yanawahusisha Maafisa Habari wa Taasisi ambazo ni wadau wa Mahakama ya Tanzania zikiwemo Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Tume ya Kurekebisha Sheria, Wizara ya katiba na Sheria na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto. 

Alisema mafunzo hayo yatasaidia kuimarisha utoaji wa habari za mahakama kwa wananchi kwa kuwa Maafisa hao watajengewa uwezo utakaowawezesha kuandika taarifa za mahakama zitakazoongeza uelewa kwa wananchi juu ya maboresho yanayoendelea kufanyika na hatimaye kurejesha imani ya wananchi kwa Mhimili huo.

Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dodoma Mhe. Mohamed Awadh akifungua Mafunzo ya kuwajengea uwezo wawakilishi wa habari za Mahakama walioko kwenye kanda za Mahakama kuu ya Tanzania na kwenye Mahakama za Mikoa yaliyoanza leo mjini Dodoma. Kushoto ni Mshauri Mwelekezi wa Mawasiliano kutoka kitengo cha Usimamizi wa Maboresho ya Mahakama (Judiciary Delivery Unit- JDU) Dkt. Cosmas Mwaisobwa na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano wa Mahakama ya Tanzania Bw. Nurdin Ndimbe.
Maafisa Habari, Maafisa Tawala, Maafisa Utumishi, Maafisa

Tehama na Wasaidizi wa Kumbukumbu wanahudhuria mafunzo hayo. Mafunzo hayo pia yanahudhuriwa na Maafisa habari kutoka baadhi ya Taasisi ambazo ni wadau wa Mahakama zikiwemo Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Tume na Tume ya Kurekebisha Sheria. 
Baadhi ya Washiriki wa Mafunzo wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dodoma Mhe. Mohamed Awadh akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washirikiwa Mafunzo ya kuwajengea uwezo wawakilishi wa habari za Mahakama walioko kwenye kanda za Mahakama kuu ya Tanzania na kwenye Mahakama za Mikoa yaliyoanza leo mjini Dodoma. Mafunzo hayo pia yanahudhuriwa na Maafisa habari kutoka baadhi ya Taasisi ambazo ni wadau wa Mahakama zikiwemo Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Tume na Tume ya Kurekebisha Sheria. 
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dodoma Mhe. Mohamed Awadh akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washirikiwa Mafunzo ya kuwajengea uwezo wawakilishi wa habari za Mahakama walioko kwenye kanda za Mahakama kuu ya Tanzania na kwenye Mahakama za Mikoa yaliyoanza leo mjini Dodoma. Mafunzo hayo pia yanahudhuriwa na Maafisa habari kutoka baadhi ya Taasisi ambazo ni wadau wa Mahakama zikiwemo Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Tume na Tume ya Kurekebisha Sheria.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...