Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
KAMPUNI ya Simu za Mkononi ya Vodacom imepata leseni ya masafa ya mawasiliano katika bendi ya 700MHZ baada ya kuibuka mshindi katika mnada wa masafa hayo.

Vodacom ilishinda masafa hayo kwa jumla ya bei dola za Kimarekani 1,0005,000 ambapo masafa hayo yatalipiwa kodi kila mwaka dola za Kimarekani 40,000.

Akizungumza baada ya Vodacom kupata leseni Waziri wa Ujenzi , Mawasiliano na Uchukuzu Mhandisi Isaac Kamwelwe amesema kuwa TCRA imekuwa ikifanya kazi nzuri ambapo imetoa gawio la sh.bilioni 81.Amesema kuwa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) kuhakikisha Vodacom inatekeleza masharti ya leseni yanatekelezwa kama ilivyokusudiwa katika utoaji wa huduma ya mawasiliano.

Kamwelwe ameiataka TCRA kuendelea na utaratibu wa kugawa masafa kwa njia ya mnada kutokana na faida ya kiuchumi kwa fedha inayopatikana kuendeleza miundombinu ya huduma za simu za mikononi na data zenye kasi kubwa , ubora , kupunguza gharama za uwekezaji.Nae Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhadisi James Kilaba amesema kuwa kuna njia mbalimbali za ugawaji wa masafa ikiwemo kutoa masafa kwa anayewahi kuomba pamoja na njia ya mnada.

Amesema masafa ya simu za mkononi ya faida katika kuendeleza huduma za simu za mkononi na data zenye ubora ,kupunguza gharama za matumizi ya huduma za mawasiliano kwa mtoa huduma ya masafa hayo.Kilaba amesema faida nyingine ni kukuza na kuchochea ubunifu wa huduma mpya na matumizi ya teknolojia za habari na mawasiliano pamoja na serikali kupata mapato kutokana na mauzo ya masafa hayo.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mamlaka ya Mawasiliano  Tanzania (TCRA) Mhandisi  James Kilaba  akimkabidhi Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Plc Hisham Hendi, leseni  ya Masafa ya 700MHz,  iliyotolewa na  Mamlaka hiyo kwa kampuni ya Vodacom  baada ya kuibuka mshindi katika mnada ulioendeshwa na TCRA mwezi Juni mwaka huu. Hafla hiyo imefanyika  jijiji Dar es Salaam.   Wapili kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa  Kitengo cha Sheria wa Vodacom Tanzania Plc, Olaf Momburi na Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti (Head of Regulatory Affairs) wa Kampuni hiyo Ngayama Matongo.
 Waziri wa ujenzi ,Uchukuzi, na Mawasiliano, Mhandisi Isaac Kamwelwe akiupongeza uongozi wa Vodacom  wakati wa hafla ya  kukabidhiwa leseni ya masafa ya 700MHz, iliyotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Vodacom ilibuka mshindi  wa mnada wa  masafa ya Mawasiliano uliofanywa na TCRA. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Hisham Hendi, Kaimu Mkurugenzi wa kitengo cha Sheria Olaf Momburi na Mkuu wa kitengo cha Udhibiti (Head of Regulatory Affairs) wa Vodacom Tanzania Plc Ngayama Matongo.

 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini TCRA, Mhadisi James Kilaba akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na utoaji wa leseni ya masafa kwa kampuni Vodacom katika hafla iliyofanyika Ukumbi wa TCRA jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Hisham Hendi, akiongea wakati wa hafla ya  kukabidhiwa leseni  ya masafa ya 700MHz, iliyotolewa na  Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kampuni hiyo baada ya kuibuka mshindi katika Mnada uliondeshwa na TCRA mwezi Juni mwaka huu. Hafla hiyo imefanyika  jijini Dar es Salaam.  
 Mkurugenzi, Mambo ya Watumiaji na Viwanda (DCIA) wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Raynold  Mfungahema (kushoto) akiteta jambo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom  Tanzania Plc, Hisham  Hendi wakati wa hafla ya kukabidhiwa  leseni ya Masafa ya Mawasiliano katika bendi ya 700MHz iliyotolewa na  Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) baada ya Vodacom  kuibuka mshindi katika mnada ulioendeshwa na TCRA. Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania Plc  wakiwa kwenye hafla ya kampuni hiyo kukabidhiwa leseni ya Masafa ya Mawasiliano katika bendi ya 700MHz iliyotolewa na  Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) baada ya Vodacom  kuibuka mshindi katika mnada ulioendeshwa na TCRA. Hafla hiyo imefanyika Makao makuu ya TCRA jijini Dar es Salaam.
Waziri wa ujenzi, Uchukuzi, na Mawasiliano, Mhandisi Isaac Kamwelwe (kushoto)akimpongeza kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa  Vodacom Tanzania Plc, Hisham Hendi wakati wa hafla ya  kukabidhiwa Leseni ya Masafa ya 700MHz, na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) iliyofanyika makao makuu ya Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam, Vodacom ilibuka mshindi  wa mnada wa  masafa ya Mawasiliano  uliofanywa na TCRA. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...