Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii

WAFANYAKAZI wawili wa Kampuni ya Simu ya Airtel na wengine tisa, leo January 15, 2019 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kujibu mashtaka saba yakiwemo kuingilia mifumo ya mawasiliano ya Airtel.

Akisoma hati ya mashtaka Wakili wa Serikali Ester Martin akisaidiana na Erick Shija amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Kelvin Mhina, amewataja washtakiwa hao kuwa ni Erick Fidelisi, Zephaniah Maduhu, Anthony Masaki, Lumuli Stanford, Ndeshiwonasiya Malle, Davis Waseda, Goodluck Nyakira, Michael Onyango, Sylvester Onyango, Rodgers Laizer na Nancy Mwenda.

Katika kosa la kwanza imedaiwa, kati ya Septemba 9 na Desemba 24 mwaka 2018 ndani ya Jiji na Mkoa wa Dar es Salaam washtakiwa kwa pamoja walikula njama ya kutenda kosa la wizi. Shtaka la pili imedaiwa siku na mahali hapo, washtakiwa hao huku wakijuwa kuwa ni kinyume cha sheria walijaribu kutenda kosa la wizi.

Pia imedaiwa mahakamani hapo kuwa katika shtaka la tatu, washtakiwa Laizer na Mwenda kwa makusudi na kinyume cha sheria walisababisha Kuingilia mfumo wa mawasiliano wa Kampuni ya simu ya Airtel bila ya kuwa na kibali. Aidha katika shtaka la nne imedaiwa washtakiwa wote, wanadaiwa kutoa taarifa za mfumo wa mawasiliano kinyume cha sheria.

Imedaiwa kuwa washtakiwa Laizer na Mwenda wanadaiwa kutoa taarifa ya mfumo wa mawasiliano ya kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel kwa watu ambao hawahusiki na kampuni hiyo kinyume cha sheria.Katika shtaka la sita imedaiwa pia, siku na mahali hapo washtakiwa hao waliingilia ufanyakazi wa
mfumo wa mawasiliano wa kampuni ya simu ya Airtel bila ya kuwa na idhini.

Wakati katika shtaka la saba, imedaiwa washtakiwa walipokea taarifa kupitia kompyuta bila idhini ya kampuni ya Airtel.Hata hivyo washtakiwa Wamekana kutenda makosa hayo na washtakiwa Masaki, Stanford, Waseda na Mwenda walifanikiwa kupata dhamana huku wengine wakirudishwa rumande kwa
kushindwa kutimiza masharti ya dhamana. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Januari 29 kwa ajili ya kutajwa upelelezi bado haujakamilika.
 WAFANYAKAZI wawili wa Kampuni ya Simu ya Airtel na wengine tisa, leo January 15, 2019 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kujibu mashtaka saba yakiwemo kuingilia mifumo ya mawasiliano ya Airtel.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...