KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA WANNE WA TUKIO LA MAUAJI.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu wanne waliofahamika kwa majina ya:-
1.      JAPHET YAHAYA NGUKU [37] Mkazi wa Msewe – Igurusi Wilaya ya Mbarali
2.      AGATHA FRANCIS [30] Mkazi wa Mbalizi.
      3. ANDREW ANGANILE MWAMBULUMA [43] Mkazi wa Mapinduzi - Mbalizi
      4. MEJA JOTAM SANGA @ MESIA [48] Mkazi wa Ikonda Mkoa wa Njombe kwa tuhuma za mauaji ya mtoto wa miaka sita [06] aitwaye ROSE JAPHET Mkazi wa Kijiji cha Msewe, Wilayani Mbarali.

Ni kwamba mnamo tarehe 03.05.2019 majira ya saa 21:00 usiku huko Kijiji cha Msewe kilichopo Kata ya Igurusi, Tarafa ya Ilongo, Wilaya ya Mbarali, Mkoa wa Mbeya katika msitu wa hifadhi wa Chimala Mtoto aitwaye ROSE JAPHET [06] alikutwa ameuawa kwa kunyongwa shingo na kukatwa kanyagio la mguu wa kushoto pamoja na kiganja cha mkono wa kushoto ambapo kanyagio la marehemu limekutwa limefukiwa huko Mbalizi, Wilaya ya Mbeya Vijijini.

Chanzo cha tukio hili ni tamaa ya kupata utajiri ambapo baba mzazi wa marehemu aitwaye JAPHET YAHAYA NGUKU alimtoa mwanae kwa ANDREW ANGANILE MWAMBULUMA ambaye ni mfanyabiashara kwa malipo ya Tshs 5,000,000/= ili auwawe na kisha kukatwa kanyagio la mguu wa kushoto na kiganja cha mkono wa kushoto na kupatiwa mfanyabiashara huyo ili apeleke kwa mganga aitwaye MEJA JOTAM SANGA @ MESIA [48] ili amtengenezee ndagu (dawa ya utajiri) ili afanikiwe katika  biashara zake za Shule anayoimiliki iitwayo Shule ya Sekondari Ushindi iliyopo Mbalizi.
  
KUPATIKANA NA MALI YA WIZI GARI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu wawili waliofahamika kwa majina ya:-
1.      ABRAHAM NSAJIGWA [37] Mkazi wa Forest
2.      FESTO ZAKARIA [35] Mkazi wa Ilemi
Kwa tuhuma ya kupatikana mali ya wizi gari lenye namba ya usajili T.899 DCW aina ya Noah rangi nyeusi.
Watuhumiwa wamekamatwa mnamo tarehe 12.05.2019 saa 02:00 usiku huko maeneo ya Isanga, Kata ya Isanga, Tarafa ya Sisimba, Jijini Mbeya. Gari hiyo iliibwa huko Temeke Mkoani Dar es Salaam ambapo baada ya tukio hilo, taarifa zililifikia Jeshi la Polisi na kuanza msako na jana kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa wakiwa na gari hilo.

TAARIFA YA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA KATIKA MAENEO MBALIMBALI YA MKOA WA MBEYA.

Kutokana na mvua zilizoanza kunyesha tangu tarehe 29/04/2019 hadi sasa Mkoani Mbeya zimesababisha uharibifu wa nyumba na mali yakiwemo mazao mbalimbali hasa katika Wilaya ya Rungwe na Kyela.

Katika Wilaya ya Rungwe huko Mtaa wa Igamba, Kata ya Bulyaga, Tarafa ya Tukuyu Mjini mvua iliyonyesha usiku wa tarehe 12.05.2019 zimesababisha hatari ya kuweza kuleta majanga ikiwemo kubomoka kwa nyumba za wakazi wa maeneo hayo.

Katika Wilaya ya Kyela mvua hizo zimesababisha uharibifu wa makazi ya watu na majengo hasa Shule ya Msingi Mwaya iliyopo Kata ya Mwaya kwani imezingirwa na maji. Pia maeneo ya Kata ya Mwaya na Tenende mvua zinazoendelea kunyesha zimesababisha nyumba zilizopo maeneo hayo kuzingirwa na maji.

           Imetolewa na:
 [ULRICH O. MATEI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...