Na Woinde Shizza Michuzi Tv, Arusha 

MRADI wa ujenzi wa njia za kusafirisha Kenya-Tanzania Power Interconnection (KTIPIP)ZTK wa laini kubwa ya msongo wa kilovolti 400 inayoanzia Singida na kupitia Babati nakuja mkoa wa Arusha hadi Namanga utanufaisha vijiji vyote ambavyo vimepitiwa na mradi huo na havina umeme Kwani Serikali imeahidi kuvitapatiwa umeme. 

Hayo yamebainishwa na Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga wakati akikagua mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ,ambapo amebainisha kuwa kwa nchi yetu huo ni mradi mkubwa na ulianza kutekelezwa tangu mwaka 2016 ambapo mradi wa kwanza kama huo ulianza kutekelezwa ulianzia Dodoma kuja hadi Singida ila pia ulipelekwa hadi Shinyanga na sasa utaanzia Singida na utapita mkooani Arusha hadi Namanga na kisha kuvuka upande wa nchi ya Kenya. 

Ameema miradi hiyo inayohusu njia ya kusafirisha Umeme kwa kilovolti 400 ni mradi wa kwanza kutekelezwa katika nchi yetu ambapo awali njia za kusafirisha umeme za juu kabisa kwa Tanzania zilikuwa kilvolti 220 lakini kutokana na uhitaji wa umeme katika nchi yetu pamoja na vile ambavyo Rais Magufuli alivyoelekeza tunatakiwa kuwa na viwanda na nchi yetu kuwa katika uchumi wa kati, 

Ambapo ameelekeza kwamba kunatakiwa kuwa na meme wa kutosha na wa uhakika na wa bei nafuu, hivyo ni lazima kuwepo na vyanzo vya umeme wa uhakika.

"Navyanzo hivyo tunavyo na tukianza na kile cha Rufiji ambapo kinazalisha megawatt 2115 lakini pia tunamiradi mingine ya Misumo, Kinyerezi na yote ni yakuzalisha umeme na imeshakamilika ,sasa kazi kubwa ya njia hizi za umeme nikusafirisha umeme huu kutoka katika hivi vyanzo vya umeme na unasafirishwa kwa ajili ya kwenda mikoani kwa watumiaji.

"Na mradi wa Rufiji ukikamilika tutajenga njia yakusafirisha umeme kutoka Rufiji kupita Chalinze mpaka Dodoma na ukishafika Dodoma utaunganishwa na hii njia .Tunafahamu hii njia kwa nchi yetu ni muhimu sana maana inaunganisha mitandao ya umeme ya nchi za Kenya ,Ethiopia mpaka huko Sudan.Pia itaunganisha na mitandao ya umeme upande wa Kusini ambapo upande huo itaunganisha Zambia, Namibia, Afrika Kusini, Angola mpaka nchini Congo,"amefafanua Luoga

Amesema mradi huo unafaida nyingi ikiwemo kuwa na umeme wa kutosha katika nchi yetu,pia utatuunganisha na nchi za jirani na tutakuwa na uwezo wa kuuza umeme katika nchi hizo za jirani na kwamba nchi yetu itakapo kuwa na umeme wa kutosha tutakuwa na nafasi na uwezo wa kuuza umeme huu nchi za nje kama Kenya ,Zambia mpaka Ethiopia.

"Na mradi huu ni wamanufaa sana kwetu ukiacha tu katika suala la uchumi wa vijana lakini pia utatusaidia kupata mapato kutokana na kuuza kwa umeme katika nchi za nje,"amesema.Pia amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa wakandarasi ili wakandarasi hao wasipate changamoto.Pia wawe tayari kupokea umeme kwani vijiji vyote vilivyopitiwa na mradi huo watapatiwa umeme.

Kwa upande wake Mratibu na Msimamizi wa Mradi huo kutoka Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi Peter Kigadye, amefafanua mradi huo wanaamini utakamilika kwa wakati kama ambavyo wamekubaliana na wakandarasi ambao tayari wapo kazini na vifaa vyote muhimu vimefika na kazi ya kusimika nguzo imeanza.

Amesema Tanzania imebarikiwa kwai itakuwa na sehemu tatu za mradi huo ambapo ya kwanza ni mradi wa Backborn ambao umejengwa katikati ya nchi yetu na ulikuwa na kilomita 670 inaanzia Shinyanga hadi Iringa wakati sehemu ya pili ni kuunga kutoka Singida hadi mpakani na Kenya ambapo kuna kituo kimoja kinachoitwa Isinya.

Amesema kwa upande wao watakwenda vizuri kwani kila kipande cha ujenzi wa mradi kuna mkandarasi wake na kila mmoja yupo hatua mbalimbali za ujenzi."Kupitia watalaam wetu tumekuwa tukifuatilia hatua kwa hatua na wakati huo huo wapo watalaamu wengine ambao nao wanafanya kazi hiyo hiyo kuhakikisha kila kinachofanyika kimezingatia mahitaji na vigezo vya viwango vya ubora,"amesema Mhandisi Kigadye.

Amesema kuwa mradi huo wa njia ya umeme ya Kenya-Tanzania Power Interconnection (KTIPIP)ZTK, unatarajiwa kukamilika Aprili mwaka 2020 na anaamini mradi huo utakapo kamilika nchi yetu itaingia kwenye biashara ya umeme na hakutakuwa na tatizo la umeme tena.
Mratibu na Msimamizi wa Mradi huo kutoka Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi Peter Kigadye,akitoa maelezo ya kotii cha kupoozeshea Umeme cha Legur wakati Kamishna wa Umeme alipofanya ziara. 
Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga akiuliza Jambo wakati alipikuwa akikagua ujenzi wa nradi wa kukagua Umeme uliopo katika Kijiji cha Legur
Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga akiuliza Jambo wakati alipikuwa akikagua ujenzi wa nradi wa kukagua Umeme uliopo katika Kijiji cha Legur

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...