Na Said Mwishehe,Michuzi TV

ALIYEKUWA Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais -Muungano na Mazingira Januari Makamba amemua kuvunja ukimya baada tu ya Rais Dk.John Magufuli kumuondoa kwenye baraza lake la mawaziri.

Mapema asubuhi ya leo Rais Magufuli ametangaza kumtengua Januari Makamba katika nafasi hiyo na kuteua Mbunge wa Jimbo la Kibakwe George Simbachawene kushika nafasi hiyo huku Mbunge wa Nzega Mjini Hussein Bashe akiteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Kilimo.

Hivyo baada ya uamuzi huo Januari Makamba kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika hivi " Kwa kweli nimeyapokea mabadiliko yaliyofanywa kwa moyo mweupe kabisa kabisa.Nitasema siku zijazo."

Katika maelezo yake hayo Januari Makamba ameamua kuambatanisha na picha yake akiwa na Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili Mzee Alhaj Ali Hassan Mwinyi.

Kwa kukumbusha tu taarifa ya Ikulu iliyotolewa leo Julai 21 ,mwaka 2019 ilisema Rais Magufuli amemteua George Simbachawene kuwa Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais ,Muungano na Mazingira .Simbachawene anachukua nafasi ya Januari Makamba ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Wakati huo huo Rais Magufuli amemteua Mbunge wa Nzega Mjini Hussein Bashe kuwa Naibu Waziri wa Kilimo.Bashe anachukua nafasi hiyo iliyokuwa awali inashikiliwa na Innocent Bashungwa ambaye siku za karibuni aliteuliwa kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...