Mlio ughaibuni mjue Dar International Airport in jina jipya

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. ya mkapa na mwinyi ziko wapi na ni kwanini imebadilishwa jina. inatia kichefuchefu

    ReplyDelete
  2. Kila kitu ni mwl nyerere,imeanza kuchefua kweli, kama hujaona hili wewe ni kipofu wa mawazo. Wengine watapewa lini vitu kwenye majina yao, namaanisha watu kama Mkwawa, mirambo, mangi na wenzao wa rika lao?

    ReplyDelete
  3. Na kweli! Kwani kina Sitti binti Saad, Marijan Rajabu, Mbaraka Mwinshehe na wengineo hawana hadhi ya kukumbukwa? Mimi ningefurahi kama uwnja huo ungepewa jina la Bi Kidude. "BI KIDUDE INTERNATIONAL AIRPORT".

    Da Mija.

    ReplyDelete
  4. Hata mimi nakubali kuwa Uwanja wa Ndege wa Bi Kidude ni jina safi. Akina Sitti binti Saad nani anawakumbuka? Nyerere tunamheshimu (pamoja na makosa aliyokuwa nayo) lakini haina maana kuwa nchi yetu haina watu wengine wa kuwaenzi.

    Lakini Michuzi tunakushukuru kwa taarifa unazotupa kwa picha. Kazi nzuri sana.

    ReplyDelete
  5. Kila kitu Nyerere tu, bwana Michuzi huoni hata wewe ungestahili jina lako litumike?Yaani mie tangu niko shule ya msingi nakusikia kwenye fani yako inakuwaje wanakusahau. Kila kitu Nyerere tu, hivi kama sio wewe tusingepata habari nyingi kwa picha.

    ReplyDelete
  6. Hili linahitaji uchambuzi wa kina kabisa.
    Nkya

    ReplyDelete
  7. Nelson Mandela siku hizi anakataa jina lake lisitumike sehemu zingine kwani anafikiri inatosha. Labda hata Nyerere angalikua hai angalifanya vivyo hivyo.

    Au mnaonaje tuibadili Tanzania nzima iitwe Nyerere maana tusipate taabu ya kutafuta 'landmarks.' Halafu Daily News tuiite Michuzi. Sio kejeli. Huyu ndugu nimemjua kuwa mfotoaji tokea mareheme mwalimu wangu ananifundiha kusema a e i o u.

    ReplyDelete
  8. Halafu ukimtizama anaonekana bado yanki...saingine anaweza kutuzaa.

    ReplyDelete
  9. Bado Ali Hassan Mwinyi Airport, na Benjamin Mkapa Airport...nadhani U-Politically Correct umeingia Tanzania.

    Nadhani kuna watu ambao watachukia kwa vile wanakumbuka walivyokuwa wananyanyaswa customs kwa vile waliingia nchini na dawa ya mswaki, sabuni, sharti, shuka, mpya, viatu mtoni, nk...lakini enzi hizo ilikuwa 'hali halisi'.

    Mwalimu Nyerere alikuwa 'Baba wa Taifa' lazima akumbukwe. Na watu wasishangae kama miaka ijayo jina lika badilishwa tena.

    ReplyDelete
  10. Dada Chemi, you made my day. tuwasiliane basi jamani, issamichuzi@gmail.com. huku mambo kama kazi

    ReplyDelete
  11. Ndugu Michuzi,
    Kuna taarifa zimechapishwa Darhotwire kuwa uwanja huu wa J.K. Nyerere huwa unafungwa jua linapozama .[ref: http://darhotwire.com/dar/Habari/2005/12/07/13317.html ]
    Hebu tupe uhakika kama hii ni kwlei. Manaake sijawahi kusikia *International* airport inayofungwa !! Ati!

    /Freddie

    ReplyDelete
  12. Uwanja huu jamani haufungwi kuchapo. ndege zote za kimataifa zaingia na kuondoka usiku.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...