Rais Kikwete na Makamu wake Dr Ali Mohamed Shein na wake zao, Salma Kikwete (mwenye gauni jekundu) na Mwanamema Shein (na mtandio) wakiwa na wasanii wa bongoflava Ikulu Dar hivi majuzi. Watoto wa Jah Kaya mnawaona, huyo aliye kama mzungu ni msichana Keisha anayekuja juu kwa sauti nyororo, na ni albino wa kwanza kuwa nyota wa muziki nchini. Nyuma ya Rais na Makamu ni Mheshimiwa Temba wa Wanaume Family. Nyuma ya Mama Kikwete ni Juma Nayure, Mbele ya Rais ni Bushoke akiwa kati ya Mandojo na Domokaya. Banana Zoro amekula njano karibu na Rais. Samahani kwa kuichelewesha picha hii muhimu. Maneno yenu yamenikuna na nadhani kwa pamoja twaweza kuendeleza hii kasi mpya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. dear michuzi,

    kwa kweli inatia moyo kuona kuwa raisi wa sasa ameunganika sana na sehemu kubwa ya walalahoi na wavuja jasho wa nchi hii. hata hivyo, imeonekana kuwa kujua tatizo ni jambo moja na kulitatua ni jambo jingine! tunasubiri vitendo haswa katika kuwakwamua wananchi milioni 38 kutoka umasikini. kwa kuanza angalau kila mvuja jasho na apewe haki yake!

    cheers

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...