Washikaji wakigombea dizeli ilomwagika baada ya ajali ya tenka la mafuta na daladala jana 28/12/05 pale 'machinjioni' chang'gombe Dar. Watu wawili walipoteza maisha kwenye ajali hiyo. Hapa stori ni kwamba ajali iliyohusisha tenka la mafuta lilipata ajali sehemu za Tukuyu na jamaa waliofakamia mafuta ya dezo walikufa kwa moto baada ya mmoja wao kuamua kuwasha fegi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. tunashukuru michuzi! hizi ndio aina ya picha tunazizihitaji zaidi. hii inaonyesha ni jinsi gani kwa watanzaia walio wengi maisha yao hayana thamani kutokana na ukweli kuwa ni fukara! hiyo diseli ikilipuka unadhani mtu atapona kweli? kawaida hayo mambo huwa si ya kupimbilia!

    sasa basi ningependekeza hiyo picha na mheshimiwa aione ili ajue ugumu wa kazi inayomkabili!

    cheers

    ReplyDelete
  2. Michuzi 'uwage' unatembelea Mbeya siku mojamoja kupiga tupicha kuna sehemu mwanana za haja kupiga picha kule. Pale palipotokea ajali ile ya kusononesha sio Tukuyu. Anyway unakuwa dakika kama 30-40 hivi kufika "Took-You". Lakini si wewe tu. Watu kibwena huchanganya kati ya Rungwe na Tukuyu. Kama Songea na Ruvuma,Sumbawanga na Rukwa, Bukoba na Kagera na Musoma na Mara.

    Hilo la jiografia mosi. Pili ajali ile watangazaji kama Renfred Masako walipatia umaarufu. Umaarufu wa nini panapo damu na roho kutoka. Ingawaje ni kweli watu waliagamia kama 'ndafu', lakini mkongwe huyu wa habari alikosa tafsida alipolichomoa neno 'ndafu' kama lilivyo live kumaanisha 'watu'.


    Now the bottom line of my comment is, umasikini tuliotopewa nao ndio unatufanya tufanye kazi za hatari hata ikiwa ni za chap-chap. Mafuta ya kuendeshea mitambo ni ya hatari sana. Hivi tulikosa nini sisi kwa Mungu hata tuteseke namna hii? Kama kweli ile hekaya ya kwenye baibo eti yule mtoto aliyemcheka babaye alipokuwa uchi ndio inahusisha Africa na ufukara huu, Leo kwa niaba ya wa-Afrika wote namuomba atusamehe. Tumeteseka vya kutosha tokea enzi za Utumwa wa aina aina hata sasa.

    Jamani sikufuru hapa. Hivi kama Mumgu ndio huyuhuyu, Why others are driving posh limos from birth to death while others wanawakiwa na jua, wanateketezwa na Malaria, Ukimwi, kipindupindu from birth to death.

    Nina mengi ya kusema lakini yatosha. Nimekua na hisia zilizonifanya nichanganye viluga hapa na pale.

    ReplyDelete
  3. Naona vijana wanavyojiajiri, tatizo lipo ni kwa magari yatakayotumia dizeri iliyojichanganya na mchanga.
    Dennis

    ReplyDelete
  4. Jamaa wanakomba mafuta utafikiri Mmarekani Iraq!

    F MtiMkubwa Tungaraza.

    ReplyDelete
  5. Yaani jamaa hawaogopi kupigwa picha wala nini. Wao wanaendelea kuchota tu.

    ReplyDelete
  6. Hii ni ishara mbaya ya wazi inayodhihirisha njaa kuu waliyo nayo watanzania.

    ReplyDelete
  7. nilisoma pale kama sio www.ippmedia.com ni www.uchaguzitanzania.com kuwa ilibidi polisi wafyatue risasi nadhani kumi hewani ili kusambaza hao ndugu zetu kwenye kisima cha mafuta. kumbe vibaka nao walianza!

    cheers

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...