Mbunge mteule wa Mbinga Capt. John Komba akiongoza kundi lake la Tanzania One Theatre (TOT) katika kutumbuiza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. kwa kweli hapo kuna uwezekano wa mambo mawili. la kwanza ni kupotea njia kwani huyo bwana inawezekana kaupata kwa sababu ya kipaji chake cha kuburudisha na sio uwezo wa kufanya kazi na kutatua matatizo wa milioni 38 walio masikini. la pili labda anaweza kuishawishi serikali kuamzisha sheria inayoruhusu sanaa za kulipwa hivyo kuwasaidia watanzania!

    ReplyDelete
  2. lakini labda kitu kimoja! huko CCM matumbo makubwa ni fasheni?

    ReplyDelete
  3. Mimi nadhani nafasi aliyopatiwa ni kama njia ya kulipa fadhila kwa juhudi zake za miaka nenda rudi kukipigia debe chama tawala.

    Lakini nasikia huyu bwana ni swahiba wa karibu sana mr JK,au ndo kwasababu ya kupenyezwa kwenye kura za maoni na hatimaye kuukwaa uheshimiwa????

    2010 msishangae Khadija kopa naye akaibuka kwa ari pya na kasi mpya.MICHUZI tunakuomba ukikutana nae DOM umuulize kama atatundika Track zake na kua mtu wa SUTI tu au mwendo mdundo na achimenengule!!!

    Najua nilivyosema achimenengule nimemkuna sana michuzi kwani LEADERS amekua kama mwanachama wa kudumu kwenda kusakata sebene kila mwisho wa wiki!!!!!!!!

    ReplyDelete
  4. Uliposema achimenengule umetukuna wengi bwana fikrathabiti.Hasa unapokua thousands of miles away from home. Kuhusu suti na traksuti kila moja ina sehemu yake. Komba atajua mwenyewe we 2 put wat taip ofu cloth is needed. Au la watamfundisha wanaojua kama hafundishiki watamshauri, kama hashauriki watamnunulia suti na kumtumia kama zawadi.

    ReplyDelete
  5. Uliposema achimenengule umetukuna wengi bwana fikrathabiti.Hasa unapokua thousands of miles away from home. Kuhusu suti na traksuti kila moja ina sehemu yake. Komba atajua mwenyewe we 2 put wat taip ofu cloth is needed. Au la watamfundisha wanaojua kama hafundishiki watamshauri, kama hashauriki watamnunulia suti na kumtumia kama zawadi.

    ReplyDelete
  6. Kama alivyosema Msaki, nadhani huyo bwana kaupata kwa sababu ya kuimba na wala si kwa sababu ya uwezo wa kuongoza. Angalia kuwa hawezi kuongoza kikosi chake cha TOT (watu wasiozidi hamsini) sawasawa, je ataweza kuongoza watu zaidi ya laki tatu?

    Nimesema hawezi kuongoza TOT kwa sababu kashindwa kuwanunulia sare sahihi badala yake kawavika track-suit za timu ya taifa ya Brazil ambazo huenda ni mitumba.

    ReplyDelete
  7. Tuanalo tatizo watanzania hasa tunapochagua mabomu kuongoza nchi lazima nchi ilipuke.Komba ana elimu gani ukilinganisha na ulimwengu wa sayansi na teknolojia tunaoishi sasa.Na siyo kuwa ni yeye tu tuna makomba wangapi kwenye serikali yetu wanaoishi kwa hisani.Khadija kopa naye ni mjumbe wa halmashauri kuu ya ccm,chombo kinacho mteue rais wa watu millioni 38.Utakapo mweleza maswala ya uchumi atakujibu nini sana atakuwa chombo cha kutunga nyimbo za mipasho tu.Olee wa nchi yetu Tanzania ambayo inakuwa kama Mzazi aliye jenga nyumba sasa wakati ana karibia kufa akaanza kubomoa dirisha akauza kesho anauza mlango mwisho nyumba inabaki pagala kisha anwaachia urithi wanae,hawa viongozi wetu wasiotaka kuachia vijana walete mabadiliko watatuachia picha ya nyumba iliyo namna gani?si wameisha uza kila kitu sasa wanatuachia nchi isiyo na kitu.
    Vijana mko wapi? hamhitaji kujiunga na vyama vya siasa(upinzani)maana vimeisha kuuawa,namatakiwa kuja tuungane tuingie ndani ya ccm ili damu mpya ilete mapinduzi ya kweli tusipofanya hivyo nchi inakufa si mumesikia kina Ngombale bado wamo hadi wafie vitini,Msekwa kaangushwa juzi hapa lakini bado alikuwa ananyemelea.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...