
Uzuri wa kazi hii ni kuwa na fursa ya kukutana na watu mashuhuri mbalimbali. hapa niko na Mzee Kenneth Kaunda alipotembelea bongo karibuni. nilifanya nae mahojiano marefu na ya kusisimua. Hakika ni mojawapo ya siku ambazo sintosahau kwani alikuwa kama babu kwa matani na ucheshi. hata kahawa aliinuka na kunitilia kikombeni na kuniungia sukari. nilipomwambia nataka 'sweet' akaniambia 'too much sweet becomes bitter'. kwa vile mie umombo not reachable naomba mnitafsirie maana na maana halisi ya ujumbe huo.
Michuzi wewe kubonga kinyaki hakunihakikishii kuwa ni mnyaki lakini naomba unifanyie kauchunguzi hapo Bongo ukipenda eti wanyaki (hasa kule Kyela kwa bibi yangu Ndimbumi) wanapenda sana sukari nyingi kunako vinywaji vyao. Yawezekana kweli kwani hata mimi bila vijiko vi-4 au zaidi kikombe cha chai hakipandi babake.
ReplyDeleteMzee Kaunda alikuja kutoa mada hapa afrika kusini kwenye Chief Albert Luthuli Memorial Lecture. bado ana afya yake na ni mtu mwenye imani na ubuntu wa hali ya juu sana. hata hivyo alikiri kuwa wao waliwekeza nguvu nyingi kuikomboa afrika toka ukoloni. pia alikiri kuwa ni jukumu la viongozi wa sasa kujitahidi kuwakomboa watu wake kutoka umasikini! je museveni na mugabe hilo wanalijua? je JMK yuko teyari kukabiliana na makunyanzi yatakayomshawishi asirudi kwenye ukombozi wa siasa na kukazana na ukombozi dhidi ya umasikini na haswa wa watu wake (watanzania) na si afrika na dunia kwa ujumla?
ReplyDeleteNaungana na Mark katika changamoto aliyoitoa kwa viongozi wetu hawa wa Africa wanaoichukulia siasa kama ajira ya kudumu.
ReplyDeleteBwana michuzi nakuheshimu sana katika fani yako ya uandishi napenda kutoa wito utumie fursa uliyonayo kutumegea fikra ang'avu kutoa kwa wazee wetu kama akina Kaunda pindi upatapo fursa ya kukutana nao na sio uishie tu kusema umekutana nao na kunywa gahawa.
Tueleze wao kama wakongwe katika ulingo huu wa kisiasa wanaonaje mustakabali wa bara letu na harakati zinazofanywa na viongozi wake katika kuleta ukombozi wa maisha bora?
wandugu wapendwa,
ReplyDeleteniliongelea habari ya mhadhara uliotolewa na KK fuata kiunganishi hiko ili kuisoma. chukua muda kupita pita na kwenye makala za hawa waheshimiwa wengine na labda pia kulinganisha walau umakini katika utendaji na ufuatiliaji wa mambo pia uzalendo na wa serekali yetu ya nyumbani. - kumbuka hawa wana miaka 10 tu ya uhuru ukilinganishwa na sisi ambao tuna miaka 44.
http://www.ukzn.ac.za/publications/jca%20167%20LUTHULI%20PUBLICATION.pdf
cheers
Huyu mzee na falsafa yake ya humanism ndicho kilimfanya waive na baba wetu wa taifa. Inabidi wazee kama hawa tuendelee kuwaenzi.
ReplyDeleteGood job, Michuzi. I hope utatuwekea insight zake humu na sisi tufaidi.
NI SAWA BWANA SEMKAE, kuna hayo mambo ya juu juu na utu na kutawala. lakini kuna gharama kubwa kama ya kuua demokrasia ambako mwalimu alifanya na pia kudumaza mawazo na uono wa watanzania inabidi pia tuyafichue, tuyaelewe na halafu tuyarekebishe! tusiangalia kunakong'ara tuu - hakuna msaada sana!
ReplyDelete