kikosi kizima cha mabingwa wa soka tanzania bara dar young africans.
waliokaa toka shoto: ben mwalala, john baraza, nadir canavaro, dekilojo chambua (kocha msaidizi), jack chamangwana (kocha mkuu), abuu ramadhani, ahmed mkweche na edwin mukenya.

kati toka shoto: benjamin haule, mohamed banka, adbul mtiro, waziri mahadhi, maridadi bukenya, gaudence mwaikimba, yusuph khamis, amir kihemba, gulla joshua, andrew carlos, lulanga mapunda na mbarouk suleiman.

juu toka shoto: Deo lucas, shardack isajigwa, salum athumani, razak siwa (kipa wa makocha), suphian juma (daktari), herry morris, celdo mwaipopo, ramadhani wasso na said maulid.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Hivi Yanga wameshafungua kashop kakuuzia jezi na calender pale Jangwani?

    ReplyDelete
  2. Chama hili nilikuwa nalizimia sana enzi zile.Mojawapo ya ushenzi wa ughaibuni hususani Marekani ya kaskazini ni kwamba mambo ya soka huyaoni kabisa.Nakumbuka enzi zile za kuparamia ukuta au kuingia taifa fungulia ng'ang'a ili mradi tu uone japo dakika tatu za mwisho.Kuna siku niliparamia ukuta,kabla sijafika juu akatokea FFU kuangalia chini mwingine kanisimamia na jibwa lake.Wakaniambia nichague kusuka ama kunyoa.Nikawaambia kusuka ni kupi na kunyoa ni kupi.Kusuka ni kupanda juu nikale virungu au kushuka chini anikamatishe jibwa lake kidogo.Hebu hisi nilichagua nini au ungekuwa wewe ungechagua nini?

    ReplyDelete
  3. Jeff,

    Sasa hujatumalizia wewe ulisuka au kunyoa? Acha kutuweka kwenye suspense bwana.

    ReplyDelete
  4. bwana msangi inaonyesha we ni mtu wa kuparamia sana! umeparamia mpaka umefika marekani ya kaskazini, wee kiboko!

    ReplyDelete
  5. Ee bwana wee!!! Watoto wangu mwenyewe hao Wanjano wa Jangwani. Wakina- Michuzi na Simba yenu mwaka huu mlie tu.

    Jeff sikujua pia umo katika fani ya uchekeshaji. Nami natamani kujua kuwa ulisuka ama ulinyoa. Au uliziacha hivyohivyo tu.

    Kati ya masaibu ya kuishi Amerika ya Kaskazini ni kukosa raha ya soka. Hii mijamaa bwana haijui cha Manchesta, Aseno wala Chelsii. Yameng'anga'nia Giants (chama langu hapa mtoni) na wengine. Tofauti na wabongo wengine, I can't just wait to go back home to cheer for Yanga like I am demon-possessed.

    ReplyDelete
  6. Hivi hii ni timu ya soka mbona kinaonekana kama kikosi cha majambazi ya Bongo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...