jenerali banza stone mwana wa masanja akiingia ukumbini diamond jubilee na trupu lake la twanga pepeta kuzinduz albamu ya mtu pesa. hivi sasa twanga wako oman kwa ziara ya mwezi mmoja. wamembeba tena ali choki. banza na masfiri diouf wamebaki kwa sababu ambazo haziajaelezwa, ingawa watu wanasema banza na diouf wamesusa kwa kuwa choki karudishwa kwa dau kubwa kama mchezaji wa kulipwa!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Ehee sasa hizo bunduki walizoshika ndizo zinatumiwa na majambazi au hapo walikuwa wanaigiza nini? Nambie pia kama kuna kibwagizo yaani Rapu ya ujambazi maana wasanii huwa hawakawii kuchomeka vimaneno.

    ReplyDelete
  2. Hilo la kusononeka kwao kwa kurejeshwa Ali Choki kwa dau kubwa mosi. Kwani ninavyoifahamu Twanga Pepeta Msafiri Diof na Banza Stone wameinyanyua sana katika miaka ya hivi karibuni hata inatisha. Sasa iweje mtu ambaye aliondoka kwa kejeli arudishwe kwa wallet nene wakati watiifu wanalia njaa?

    Lakini pili nahisi hawa jamaa hawajaenda Oman kwa sabau ya tabia zao. 'Ufaza' unawafanya hata wasiheshimu kazi yao. Msafiri na Masanja ni walevi wa kupindukia hata wakati fulani wanashindwa kupanda jukwaani na kuwasononesha mashabiki wao tunaoenda kunako maonyesho yao kuwatazama. Kama hili ndilo lililochukua nafasi basi watajifunza kuwa na 'nizamu'

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...