
kumbe wanablogu nanyi mmo!
kwenye maktaba yangu nimekuta picha hii ya kihistoria. kutoka kushoto ni Abdallah Ezza (mpwawe Gema aliyekuwa mpiga gitaa wa Afrosa), katikati ni Hayati Patrick Pama Balisidya, na mwisho ni F MtiMkubwa Tungaraza. Picha ilipigwa mjini Helsinki wakati Marehemu alipoenda kushiriki katika tamasha la Etnosoi mwaka 1993.
Bila blogu hizi picha tungeziona wapi? Safi kama Michuzi.
ReplyDeleteBrother Michuzi tunashukuru sana kwa kutuletea burudani hizi. Hii ni changamoto kwa wapigapicha wetu wa Kibongo, kuwa habari zinatengezwa na wasomaji sio wanakazania picha za viongozi wakila kuku kwa mikono kwenye mahoteli makubwa au wakiingia kwenye state dinner na designer suit.
ReplyDeleteTAMASHA JEMA,
Dennis- Denmark
Unaona Bwana, siku zote mii nasikia tu Mtimkubwa Mtimkubwa!! kumbe ni huyu swahiba wangu wa zamani sana. Siku hizo tulikuwa tunamwita "Sujaroro" huyu Bwana alikuwa burudani ya pekee na ni furaha kwamba yumo humu.
ReplyDeleteFadhil
Abdallah Ezza yuko wapi sasa?
ReplyDeleteezza yuko helsinki, yeye ni alwatan wa jiji pia ni rizevu wa Bongo FC. ni vigumu kwa mtanzania yoyote anayepita helsinki kutomuona ezza, kwa bahati mbaya naona hamkukutana.
ReplyDeleteAsante Mti kwa taarifa. Nikija tena lazima nikutane naye.
ReplyDelete