waziri mkuu wa tanganyika julius kambarage nyerere akiwa na mwenyeji wake joni f. kenede ndani ya ikulu ya marekani julai 16, 1963. nadhnani jamaa alieomba snepu hii ataridhika. maombi maalumu yanakaribishwa, nna picha karibu za matukio yote muhimu ya bongo. nasikia kuna mnaoguna, je napata nini? hakika napata raha nikisikia nyie mwapata raha kwa hili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. asante sana bwana michuzi,! sasa leo nitammaliza mzungu mmoja hapa ughaibuni,,,!alikuwa ajui kuwa nyerere alishakutana ndani ya white house na the most loved president of all time jfk!
    respect mr michuzi. nitakuja tena na ombi lingine lakini leo pumzika.

    ReplyDelete
  2. Inasikitisha kwamba toka mwaka 1963 hatujakuwa watu wa muhimu tena kupata ukaribisho mwingine wa "official state visit" kwenye Hekalu Jeupe. Asante Michuzi - sasa tutafutie ile ya Nyerere alipokwenda state visit Buckingham Palace (miaka ya sabini nadhani). Na huko hatujaalikwa tena, japokuwa Blair na Mkapa walikuwa buddy-buddy kiasi kile! Damn...

    ReplyDelete
  3. Michuzi, historia hutunzwa kwa njia mbalimbali. Moja ya njia hizo ndio hii ya picha. Na teknolojia ya blogu inatuwezesha kuona picha hizi na hata watakaokuja baada ya miaka 500. Unachofanya hapa Michuzi ni kuwa unaandika historia kwa kutumia picha. Na tunaambiwa kuwa picha moja huzidi maneno elfu moja!

    Unajua Nyerere alipokwenda Marekani alikuwa mvaa suti. Kisha akaja kwenda Uchina. Akaingia Uchina na suti akarudi na mavazi ya kijamaa. Una picha za alipokwenda Uchina na aliporudi?

    ReplyDelete
  4. Jamjuah,
    Andika kwenye blogu yako ili tuweze kuitazama. Hivi sasa hatuwezi kuiona maana hujaweka chochote. Tafadhali. Karibu sana.

    ReplyDelete
  5. Baada ya kutoka white house bwana mkubwa akaamua kwenda Uchina na kubadili mwelekeo sijui alichukizwa na nini Mzee Huyu basi haya kila mwanadamu kaja na mapungufu yake na ujasiri wake ni pale kutubu pele ya wananchi wake

    ReplyDelete
  6. Mungu awalaze pahala pema peponi ndugu hawa (Julius na Joji). Amen

    ReplyDelete
  7. jamaa wanadai kuwa hawa jamaa walikuwa marfaki sanaaa wakati hamna lolote urafiki utokee wapi waki kila mtu anajuwa kwa nyerere kenda kuomba ah!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...