Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Sasa mbona Michuzi usemi hii ilikuwa wapi? Isaac Mgwasa

    ReplyDelete
  2. ooooopps! samahani washkaji...hii ni jana usiku pale ikulu kwenye dhifa ya kitaifa kwa heshima ya rais wa visiwa vya comoro aliyekuja jana hio hio kwa ziara ya siku 5. wakulu walichepuka kuteta jambo

    ReplyDelete
  3. caption:

    "Sasaaa wazee nipeni maarifa. Mliibaje hela za serikali bila wananchi kujua?"

    ReplyDelete
  4. Michuzi hii inafurahisha kwa kiasi fulani.Unajua ni nchi chache sana Afrika ambazo maraisi wastaafu wana bahati ya kukutana na rais aliye madarakani.
    Hapa Uganda pamoja na nchi kuwa na marais wa zamani zaidi ya saba haijawahi kutokea picha kama hii.
    Sijui ndio matunda ya Nyerere au ndio tusemeje?

    ReplyDelete
  5. Ni kweli kinadharia ingekuwa hivyo yaani bwana JK angefaudu hekima na busara za waliopita. Lakini wacheni kusifia ujinga pamoja na kuwa sisi tumeweza kujikokota katika demokrasia ya kupishana kiti cha urais, lakini utendaji wetu wa kazi pumbafu kabisa. Huyo Mwinyi alifanya nini Bongo, sefuri. Mkapa naye sefuri, huyu Kikwete naye tuone tutafika wapi. Afrika bado, lakini tutafika. - Mpambalioto

    ReplyDelete
  6. niko na wewe mbalioto, unasema kweli tupu. wanatuyeyusha tu.hawa ndio waharibifu namba wani.
    Tanzania tuombe mungu CCM igawanyike, tupate vyama viwili vyenye nguvu, labda maendeleo yatakuja. hawa wanapeana ofisi tu.

    eti JK alipiga kampeni mpaka akazirai,,,,, ni juu ya nini si angekaa nyumbani kwake na mkwewe wakala bia taratiibu,badala kujisumbua bureee.
    watanzania tunahitaji wapinzani wa kweli, kwa faida ya taifa. jamjuah

    ReplyDelete
  7. Mpambalioto usiongee ili mradi tu. Mkapa kafanya mengi, soma statistics. Kabla yake tulikuwa hatujui hata jinsi ya kukusanya revenue!

    ReplyDelete
  8. Mk,
    Kweli vita ni mbaya hakuna mfanowe. Lakini kusingizia amani watu wakaacha kufanya vitu vya maana eti tu kwa sababu tuna amani ni upuuzi usiopimika. Tulitarajia amani iendane na maendeleo. Nchi inayojivunia amani huku watu wake wana mgao wa umeme wa masaa 18 kwa siku ni upuuzi. Kudai amani ipo wakati nchi imekumbwa na balaa kubwa la njaa nayo ni mahoka nyingine.
    Iwapi basi tofauti yetu na hao Somalia, Burundi, DRC kama matatizo yanayo sababishwa na vita ndio hayo hayo tuliyonayo sisi? Tena hatujasikia njaa wala migao ya umeme huko kwenye nchi hizo, kulikoni sisi?
    Namalizia kwa kusema kukusanya kodi bila faida zake kuonekana ni uzushi. Barabara za lami ambazo hata si highway hata hivyo, Mkapa kazikuta. Mlandizi-Arusha ilikuwepo, Mlandizi-Mbeya ilikuwepo, Msamvu-Dodoma ilikuwepo, Makambako- Songea ilikuwepo, Sasa hizo barabara mnazopigia kelele Mkapa kajenga ni zipi? Yes alikuwa anakusanya kodi, zimefanya nini?
    Kaliwa.

    ReplyDelete
  9. Mwaona jinsi BWM anavyotoa jasho shingoni? Ulabu huo!!!

    ReplyDelete
  10. mmh jamani tupunguze maneno makali kwa waheshimiwa wetu, hakuna aliyekamilika, hata kama ungekuwa wewe ukapewa huo uraisi ama achilia mbali huo uraisi, ukatibu kata tu ungeanza ujasilia mali kwako kwanza

    ReplyDelete
  11. hii ngoma ileile midundo tafauti, hakuna jipya , ikiwa watu ni walewale.

    ReplyDelete
  12. We MK sidhani kama hata wewe una amini hayo unayoyasema!! Sikiliza inaelekea kabisa we ndio wale wasomi wa Kiafrika wanakaa sana darasani na ukimuuliza swali anaanza kutoa jinsi vitabu vinavyosema. We kama una vita na unakuwa maskini na ukiwa huna vita pia unakuwa maskini kama uko vitani au ndio umepigwa mabomu juzi kuna faida gani kujivunia AMANI!!!!??? Wacheni lazima tukue kidogo. Nitakupa mfano nafikiri watu wote tunakubalina vifo Bongo sasa vimezidi yaani ukirudi Bongo ukiulizia fulani yuko wapi usishangae ukiambia huyo tawile zamani gani!!!! Wachana na hiyo hiyo "Amani" yetu kwa miaka 40 tunakabiliwa na tatizo la maji mpaka leo hatujalifumbua, tatizo la umeme nalo. Watu kibao wanakufa kwa magonjwa yenye kinga na dawa kama typhod wacheni!!!! Utasema kuna faida ya kuwa na Amani??!!! Tungekuwa tunasonga mbele na kula kuku kweli lakini mimi nakwambia tunazidi kuwa maskini na unajua umaskini unaleta UFALA. Kwa hiyo Wabongo sasa hivi ni MAFALA kuliko hata enzi ya Mchonga sababu hatuna kitu tumebaki kubabaika vitu vya kifala kama simu za mikono. Lakini unajua hata siku mja HUWEZI KUUPUZA UKWELI UKIUUPUZA UTAKUUMIZA, basi mshikaji kama Makaburu walishindwa kule Azania basi kaa chonjo hata Bongo kinaweza waka moto. Watu anachoka na pole pole unaona watu wanazidi kuwa majasiri ujambazi kibao. Basi pole pole huo upuuzi wenu wa kuwa tuna Amani watu wataona haina mpango, ngoja tuwafuate huko huko Mikocheni.

    Mpambalioto

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 13, 2006

    TAFUTA DUNIA NZIMA VIONGOZI WANAOFANANA TABIA NA MATENDO KAMA WAPO!MWINYI ANGEWEZA KUENDELEA MKAPA PIA:UONGOZI UNABADILISHWA ILI KUTUMIA KIPAJI KINGINE,YAPO MAZURI YA NYERERE,MWINYI,MKAPA NA KIKWETE ATAFANYA YAKE!MUNGU HAKUTAKA MTU MMOJA AWE NA KILA KITU(SELF CONTAINED)
    NASI KAMA NCHI TUNAYO YA KUJIVUNIA!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...