jk akiwa na witness manwingi ambaye ni miss utalii bongo na pia miss utalii africa 2005. jana alishika nafasi ya miss personality. hapa ni ikulu ambapo jk alikaribisha wahiriki wote mia na ushee hiyo jumamosi mchana na jioni mkewe mama salma alikuwa mgeni rasmi ambapo miss south africa Henri Van Schalkwk ndie aliyetangazwa miss tourism model of the world 2006 kwenye ukumbi wa ubungo plaza jana usiku

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. jk mtu wa totoz kishenzi,lazima afanye vitu vyake hapo

    ReplyDelete
  2. hayo majukumu yalivyomkalia hadi nyweleni unafikiri atakumbuka mambo ya totoz....subutuuu!!!!!

    ReplyDelete
  3. Swala sio Totos, Rais wa nchi anatakiwa awe na heshima na adabu! yasije yakamkuta ya Clinton na Monica …….

    ReplyDelete
  4. Huu ndio ule upuuzi wa hali ya juu, Rais wa nchi hauwezi kupiga picha na mwanamke kama hawala yako vile!!!

    Mwanamke pamoja na Rais wanaonesha (body language)kama wanatakana!! Pia Kingine ebu angalia wameshikana mikono!!!

    Sijui wasaidizi wa Ikulu siku hizi wanafanya kazi gani!! Au ata mshauri wa Raisi sijui alikuwa wapi!!

    Utafikiri alikuwa anataka kumpiga busu!! Mama Kikwete akiona hii picha lazima aone wivu akikaa kimya basi kwakuwa mumewe kalamba dume (Uraisi) anaogopa kualibu!!

    Aibu bwana, Michuzi Siku nyingine mshauri Raisi mambo haya yasirudiwe tena. Akumbuke yeye sio tena waziri wa mambo ya nje bali ni Raisi wa nchi.

    Kupiga picha na mwanamke waweza kupiga picha lakini sio za namna hizi.Aibu tupu.

    Naona nibaki Anonymous maana hawa watu wote wananijua.

    ReplyDelete
  5. jamani ni kwa upendo tu!

    hao ni kaka na dada tu! Jk ni kaka yetu na sie ni wadogo zake, na huyo ni dada yetu! wote tunapendana, na wale wadogo zetu wengine walio kule kajunjumule anawependa pia, na wale wamasai aliowapa maji siku ile anawapenda pia...na wale wanaokufa njaa, anawapenda pia si umesikia mambo ya harambee la njaa la juzi??

    upendo hua chuki, huua uhasama, huua ukatili huua uovu..

    ila hapo huyo dada ndio kidogo alikuwa dakika tatu mbele, mkuu amewahi kumdhibiti kwa mkono!

    michuzi, hizi picha taratibu lakini ukizingatia kuwa wote sisi ni binadamu, na tuna hisia! - mhifadhi hifadhi mkulu wetu!

    nabakia anony kwa leo

    ReplyDelete
  6. huyu ni mtu hatari sana kwenye mambo ya totoz,, ukitaka muulize babu seya na wanae,,,safari hii atakekanyaga anga zake atakutwa baharini aliwe na samaki.

    ReplyDelete
  7. Nywele za bandia

    ReplyDelete
  8. Hata kama ana nywele za bandia bado yuko fresh sana. Hata huku marekani wakina Beyonce wana nywele za bandia.

    ReplyDelete
  9. Na kweli ukichunguza utagundua jk kauwahi mkono..kwi kwi..kwi.. michuzi watupa raha!!!!!

    ReplyDelete
  10. Jamani mbona wengine mnamuandma rais kiasi hiki. Nae anaupendo. Mbona hapa mtoni watu wanafikia hata kubusiana. Mawazo yangu hapa rais kaonyesha upendo tu. Naungana na Anony mmoja hapo juu kuwa pamoja na timetable lake kuwa gumu rais wetu ni mtu simpo. Jamani naye anapenda kufurahisha roho yake. Anatupenda wote hata wale wa kule Kajunjumele.

    ReplyDelete
  11. maji ni maji tu...hata yakichemka vipi yatarudi hali yake ya ubaridi. JK ni JK tu hata akiwa Rais kuna matendo yake ya siku zote yatabaki kama yalivyo.

    ReplyDelete
  12. halafu mmesahau, hivi kweli kuna kipindi ambacho raisi ameita walalahoi ikulu?? hapo anashabikia walalahoi kunyanyuka!! ni nini tunachopaswa kukasirika? ni kwa upendo tu!!

    pia mmesahau kuwa yeye mwenetu hajabanwa na taratibu za kimagharibi..kiimani yeye bado ana allowance kubwa tu ya kuongeza...hadi wanne!! mbona Mzee Ruksa alikuwa anafanya mambo? - cha maana ni kutenga kazi na indivijo zake!! ambazo kila mtu anazo!!

    ReplyDelete
  13. RAIS ANASHAURIWA NA WAREMBO LAZIMA TUENDELEE AWAMU HII.JJ

    ReplyDelete
  14. Ni mfano mzuri lakini mbona sijasikia raisi akikaribisha ikulu wasomi kama vile wahadhiri wa vyuo vikuu au watu wengine muhimu?
    Bado sijaridhika kabisa. Warembo sio role model kwa maendeleo ya nchi kabisa.
    Hapa rais kachemsha amenikera.

    ReplyDelete
  15. TATIZO KUU LA RAIS WETU LABDA NI KUWA MTU WA KUPENDA ATTENTION, KWA HIYO JK ANALIWEZA KWELI KWELI.NAONA BADO YUKO KWENYE KAMPENI{MTU WA WATU INCLUDING WAREMBO)JJ

    ReplyDelete
  16. Jamani, naomba kutofauti... nadhani muda haujafika, ni siku hata mia hazijaisha tangu atawale, hiyo miss Utalii imefanyika siku hiyo, na siku hiyo akampongeza walau kupozi kwa picha..si ni jambo jema??. tusisahau hii kitu ina impact kubwa kiuchumi...kwa kuwaita kwake wahusika woote wa miss utalii, ikulu, inafagilia Tanzania, na si nimesikia kwa miaka kadhaa itafanyikia hapa?? JK alikuwa na kazi ya kuwashawishi wakuu wa hiyo kitu kuwa hawakukosea kuteua Tanzania!! huko serekalini, si ndio sasa wanapigana shule Arumeru? kwani hata wakati wa kampeni si aliishaahidi kufagilia tafiti? kama wasomi si ndio maprofesa na madaktari(hata kama feki) wamejaa serekalini? je hao waserekali WAPROTOKALI tumewahi kusikia wakikiri kuwa kuna tatizo serekalini zaidi ya kudai wapewe ushahidi wa rushwa?? si waliunda PCB halafu wakamtoa meno?? tumesikia raisi yoyote wa TZ akikiri maslahi ya watumishi wake ni mabovu...kumbe wanakata cha juu wanakula kinachobaki... watafiti wa mambo ya siasa wanaoheshimika mfano Prince Bagenda waliishampa JK 100 % ndani ya siku 65 za utawala....yaani hili halihitaji shule kwani hata watoto wa chekechea wameishaliona....jamani sijawa mkali..na si mkereketwa / mfurukutwa..ila ni vizuri tukawa tofauti na wanasiasa ambao wao hata zuri watalisema kuwa baya...mbona hatutoi heko kwa mema yake pia?...naomba nimfanyie uwakili kama nilivyomfanyia Saidi Mwema... tumpe muda na tumsaidie JK!!

    ReplyDelete
  17. TUMEPATA RAIS MWINGINE ANAYESHAURIWA NA MKEWE.
    TUMEMPA KAZI YA KUONGOZA NCHI NA SIO KWENDA KUKUMBATIANA NA WAREMBO NA KUULIZANA RANGI ZA CHUPI.

    WATU HAWANA CHAKULA HUKO, WENGINE TUMEONA HAPO HAWANA VITABU,MAJAMBAZI YAMEZIDI KILA KONA MJINI NA VIJIJINI , MADAKATARI NDIO KWANZA WANALILIA MALIPO, WALIMU NAO HOI.
    NIE YAKE HUYU RAIS ILIKUWA NI ARI MPYA BIBI MPYA.

    NI BORA KUALIKA WANAFUNZI WA SHULE WAKAONE JINSI RASI ANAVYOFANYA KAZI, WANGEJIFUNZA MENGI.

    ReplyDelete
  18. TAFADHALI JULIA HALI YA WANANCHI KWANI WALIPOKUCHAGUA WALIKUWA NA IMANI YA KWAMBA UTAONGOZA NCHI BILA YA KUANGALIA TOFAUTI ZA WATU. WAPE KAZI MCHAHARA WA KUTOSHA, HAPO UMASIKINI NA DHULUMA ITAPUNGUA, KWANI TANZANIA NI NCHI NZURI, BORA, IMARA, YENYE WANANCHI WENYE IMANI NA RAISI PAMOJA NA BENDERA YAO. PLEASE DONT LETS US DOWN WE BEALIVE IN YOU.MAY GOD BLESS TANZANIA, AMEN.

    ReplyDelete
  19. Hawa watu wasiokua na majina wananitia wasiwasi sana juu ya fikra zao!!!!

    Nani hajui kua sekta ya utalii ina mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa taifa lolote duniani ikiwemo Tanzania???Mimi nadhani aliyofanya JK ni kama sehemu ya kumpongeza mshiriki wetu aliyenyakua taji katika mashindano hayo makubwa ya urembo duniani!!!

    Naamini kua wenzetu wa ughaibuni wakisikia Miss PERSONALITY ametokea Tanzania wanaweza kuingiwa na shauku ya kuja kutembelea nchi yetu kitu ambacho kitatuingizia fedha za kigeni ambazo kwa upande mmoja zitasaidia kuujenga uchumi wetu na kukabiliana na matatizo lukuki yaliyo mbele yetu.

    Kwanini tuwe na fikra finyu kuhusu uhusiano wa karibu wa mheshimiwa rais na wanawake???Hakuna mtu asiyependa hawa viumbe na kua nao karibu pia hakuna maana kua una uhusiano wa kimapenzi nao!!!!

    Mbona MAKENE alivyokua waziri mkuu wa DARUSO alikua nao karibu sana lakini hatukua na mashaka yoyote juu ya ukaribu huo???

    ReplyDelete
  20. wewe kweli ni fikralegevu, na wala huo udhabiti sijaona.
    yaani wewe unawaza kwamba mtu/mtalii anaweza kufunga safari ya kuja bongo, kwa sababu kasikia eti miss personalty!ni mtanzania.kweli hizi ndizo fikra dhabiti au,,,,,?wasomi wetu mnatuangusha kweli.

    Rais alimuwa amemisi vitu vyake, akaona awaalike wachuwachu au kaa wewe ulivyowaita viumbe,afarijike na roho yake.
    kama ni kutangaza utalii kuna njia kibao tena zinazoweza kuleta mafanikio na sio mamisi ndani ya state house.

    ReplyDelete
  21. Kuendelea kubishana na wewe ni kupotezeana muda tu.Ila cha msingi jaribu kubadilika kwani umeshakua!!

    ReplyDelete
  22. IKULU NI MAHALI PATAKATIFU,JK.NYERERE

    ReplyDelete
  23. usifanye mchezo na ikulu bwana fikrapotofu, inaonyesha ujawahi kufika pale wewe. tuulize sisi tumeishi sana pale wakati wa mwalimu.na palikuwa patakatifu kweli kweli, hakuna mambo ya kucheza bongodalisalaaaaam pale.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...