mojawapo ya majengo ya zamani ya dar ni posta ya zamani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Jengo hili ni la kihistoria. Natamani wangekuwa analikarabati ipasavyo. Hata hivyo mimi ni nani wa kusema? Ngoja nizime kibatari.

    ReplyDelete
  2. Unajua sisi tuna tabia ya kuvunja majengo ya zamani hata yale ambayo yako kwenye orodha ya majengo ya kihistoria ili kuwapa wazungu nafasi ya kujenga majengo ya vioo yanayofanya walalanjaa kuamini kuwa uchumi unakua ingawa hata kazi ya kusafisha humo ndani wanaweza wapewe majirani zetu toka Kenya.

    Aisee Michuzi, kuna picha sijui unaweza zipata...nyingine labda ulikuwa hujazaliwa. Picha za: Malcolm X alipokuja Bongo (alikaa hoteli iliyokuwepo karibu na kiplefti cha mnara wa saa), Angela Davis, Walter Rodney (aliyeandika How Europe Underdeveloped Africa), Horace Campbell (aliyeandika Rasta and Resistance: From Marcus Garvey to Walter Rodney). Nadhani itabidi mambo ya kuingia maktaba yenu, sio?

    ReplyDelete
  3. Duu!!kaka Michuzi haya Mambo ya kuliza...hasa kwa sisi tulioko huku
    Ughaibuni..Lots of memories...
    Malcom X alikuja Bongo?..

    ReplyDelete
  4. wazungu ndio waliojenga majengo yote tulionayo mnayodai ni ya kihistoria.hebu amka we ndesanjo.

    ReplyDelete
  5. kwani bwana anony historia maana yake nini?

    ReplyDelete
  6. kbc Y thang mnaonana? unakumbuka don Bosco youth festival 1992 au 1993 - youth for peace? unawakumbuka Tripple M + T boys & Edutainment? nadhani kuna haja tuwe tunakutana tujikumbushe zile good times!! naona kama siku hizi starehe zimekwisha vile!!

    nadhani anony aliteleza kidogo kwenye definition ya historia!! ngojea nikumbushe zamani sana nilifundishwa fomu one!! ni kumbukumbu ambazo hupitishwa kwa kuandikwa au kusimuliwa zikiwa na lengo la kutujulisha tulikotoka, kitu ambacho ni muhimu kutufahamisha wapi tuliko na ni wapi tunakwenda!! historia huwa na maana zaidi ikiwa itatupa uwezo mzuri wa kuamua ni wapi tunakwenda na tufanyeje tufike kwani tuna mifano yote ya nyakati, kuliko kutafuta wa kumlaumu (hii ni ya kwangu)...... Jana Koffi Annan alikuwa Afrika ya kusini akihutubia wakuu alisema mambo matatu..muhimu

    1. Kuacha tabia ya kuwalaumu wakoloni kwa kila kitu, na badala yake kutafuta masuluhisho ya matatizo yetu (mimi huita matumizi mabaya ya historia)....nadhani Japan na China waliligundua hili mapema....

    2. alizitaka nchi za Afrika zenye uwezo kama SA, kupambana kujenga uwezo kimaendeleo na kwa kushirikiana na nchi zingine zinazoizunguka (majirani) bila kuzinyonya...na

    3. kusisitiza kuwa bado ni suala la msingi kuuendelea na nia ya kuwa na nafasi zaidi baraza la usalama la UN...

    ReplyDelete
  7. Braza ndesanjo unaandika ukweli tupu,wakiona majumba ya vioo wanajua mambo ndio basi, tumeshaendelea, kumbe bado tunashika mkia.
    Pia nimefurahi sana kujua kuwa hata wewe bwana ndesanjo unamkubali bwana benjamin zephaniah(Fearless Rastaman)

    kuhifadhi historia yetu ni muhimu sana, watoto wetu waone na wajue historia ya nchi yao, sio luvunja na kujenga majengo ya vioo, wakati tunamaeneo kibao yamejaa vichaka.
    jamjuah.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...