kinama wakibongo wakienda nje ya nchi kwenye ziara

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. mama zetu hawa safi sana, sio viruka njia vya siku hizi

    ReplyDelete
  2. Bwa Michuzi, hapo namwona Anti yangu (wa tatu kutoka kushoto kwa mtazamaji). Shukrani kwa picha.
    Zipo baadhi ya scholarship ktk blogu yangu ya yahoo kwa zipitieni zinaweza kuwa msaada kwa yeyote.

    ReplyDelete
  3. enzi hizo bwana vimini kwenda mbele hakuna mruzi wala sh sh sh leo ukivaa malaya......na joto zima huna budi kutinga nguo ndefu haya maisha ya kuishi kuangalia nani anasema nini TAABU KWELI KWELI!!

    ReplyDelete
  4. PONGEZI KWA KAZI NZURI UNATUFIKISHA MBALI. ENDELEA KUTOA VITU VYA ENZI HIZO KUTOKA 1950s - 1980s. AHSANTE.

    ReplyDelete
  5. Anony #2, utafikiri ulikuwemo kichwani mwangu. Hivyo vimini wacha kabisa tena wakati huo ambapo hawakuwa wameanza kuiga ya Ughaibuni. Leo hii ati watu wanajifanya utamaduni wakati kabla ya 1884 wengi wa babu zao walikuwa wanatembea utupu. Sasa jamami huo utamaduni unaanzia vizazi vitatu vilivyopita?

    ReplyDelete
  6. Hizi mini zilipigwa maruku kabisa mwaka 76. Hii picha ilipigwa kabla ya hapo

    ReplyDelete
  7. hongera sana michuzi, hii picha ni ushahidi tosha kuwa mama zetu walikuwa hawashikiki kwa vimini lakini siku hizi ndio wanaongoza katika kuvipiga vita. Namuunga mkono anony# 4 watanzania inabidi tubadilike mtu huna uhuru kuvaa nguo uipendayo kisa utapigiwa miluzi barabarani, uhuru maana yake nini????????

    ReplyDelete
  8. Subi, mbona hata mimi huyo ni shangazi yangu, Mbona baba mkubwa na Baba mdogo hawana mtoto anaitwa Subi? Na kwa baba yangu ndo kabisa! Au una maana ya shangazi kama wasemavyo wazungu?

    ReplyDelete
  9. wazazi wanapiga makelele kutokana na dunia ya sasa na ya hapo mwanzo ni tofauti watoto ama wasichana wakivaa hivyo wanabakwa si tanzania tu ni baadhi ya nchi nyingi wanapiga vita nguo hizo kwani zinatamanisha wanaume wanaopenda uzinzi hasa walevi,wavuta bangi,wanaotumia madawa ya kulevya,ukimwi na hata ambao hawatumii chochote ila ni ushetani unaowatuma kufanya hivyo, na mengi ambayo kwa sasa yamezidi mno kupita kiasi tofauti na enzi hizo na ndio maana wazazi kwa uchungu wa watoto wao wanajaribu kuwalinda watoto wao kwa kuwakataza mavazi hayo, si pia unaona msichana akivaa hivyo hana raha akipita barabrani jinsi atakavyo fanyiwa nadhani ni mfano bora wakuona amzazi akataze ama wale wengi wanao tumia vazi hilo kama ni lakuuza mwili wao kwa hiyo msichana mwingine akipita kama akivaa vazi kama hilo wanaume watadhani nae anauza mwili wake kumbe sivyo nimaamuzi ya mtu kuvaa hivyo na si kwa kujiiuza kutokana na wale wanaotumia kwa mabaya.

    ReplyDelete
  10. Hivi naona kama Edda Sanga na Maria Shaba wamo kwenye hiyo picha... Walikuwa ma Spring Chicken!

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 15, 2006

    Vimini vipo toka enzi..Lakini leo dada zetu wakivaa wanabakwa,kulikoni?

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 17, 2006

    MAADILI!JANDO NA UNYAGO HAKUNA,MNASEMA NA UTANDAWAZI VILE!?

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 19, 2006

    Yule mama wa tatu kutoka kushoto kwako ni mchaga!Wa pili kulia na wapili kushoto wote wanyakyusa,kama unabisha muulize Michuzi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...