gari la waziri wa maji. magari yote ya mawaziri yameandikwa namna hii, kwa mfano waziri wa fedha ni wf na wa miundo mbinu ni wwmm. je gari la waziri asiye na wizara maalum litaandikwaje?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. wanatumia mapesa kibao kununua magari ya kifahari wakati mwananchi mwenyewe anabaki masikini na kufa masikini afrika bwana hasara tupu.Angalia mataifa ya ulaya au amerika viongozi wanatumia mgari ya kawaida tu.viongozi wote wa afrika wana matumizi yasiyo ya msingi.opotevu tu wa pesa za mtanzania.badala ya kupeleka ktk mahospitali ili uduma nzuri iongezeke au kupeleka hizo pesa mahali pengine ktk huduma za jamii wao wananunua mavx na gx, ujinga mtupu.

    ReplyDelete
  2. Hivi hiyo picha kwenye spear tire ni K-lynn au? Kama ndiyo yeye basi huyu waziri atkuwa anamind totoz.

    ReplyDelete
  3. Sasa kaka barabara za Tanzania na Ulaya unaweza kulinganisha, nunua Volvo watambelee kama hujazitupa kila baada ya miezi 6

    ReplyDelete
  4. acha upuuzi wewe, kusamehewa madeni sio kutumia pesa kama Bongo ni USA kuna magari kibao ya pesa rahisi na sio hii migari ya mamilioni wao wanunua migari wakati raia wa bukombe ana ata cent ya kununulia dawa haya ndo maendeleo.hii migari ipo kila kona ktk kila wizara sasa we uoni ni upotezeshaji wa pesa zetu za madafu.nyie ndo mnabaki kusema siku itafika tu hali itabadilika, itabadilika lini wakati mnatumia kama matajiri na hapa bado alijaenda kumchukua bibi wa nje wa waziri au kutumika nje ya masaa ya kazi.upuuzi tu wa afrika ndio mnao endekeza na kesho mnaenda kukopa tena!madeni kibao, matumizi mabaya, watoto kila siku wanazaliwa na kufa, watoto na watu wazima kila siku wanakufa na njaa au kutokuwa na pesa ya kupeleka ndugu, jamaa, n.k hospitalini, huduma za jamii mbovu, njaa, umeme alafu waziri, mbunge, raisi wanaishi kifahari kuliko ata huyo raia aliye wachagua.huu ni ujinga au umelidhika na khali ya maisha ya bongo?

    ReplyDelete
  5. Kwanza serikali hainunui hayo magari kwa bei ya reja reja, kumbuka hilo.

    Naomba uniambie unataka watumie magari gani ambayo yanaweza kushahimiri vishindo vya barabara za Tanzania. Unataka watumie nini, Mark II mayai?

    Unataka wizara ngapi zimetumie gari moja? Mawaziri wawe wanapakizana au?

    Kusamehewa madeni haiusiani na matumizi dogo wewe kajifunze uchumi, Na hiyo USA ndio inaongoza dunia kwa madeni na matumizi.

    ReplyDelete
  6. acha uongo wewe brazil ndio inaongoza kwa madeni na matumizi.

    ReplyDelete
  7. uchumi watu wamesoma mpaka kichwa kinataka kupasuka

    ReplyDelete
  8. Taratibu kaka Brazil inaongoza Debt to GDP ratio @ 48%($200B), lakini total debt bado ni USA($9T) Naongea vitu ninavyoelewa.

    Kichwa kinapasuka eeh, nilikuwa nimesahau kuwa hata Mrema anadigrii siku hizi.

    ReplyDelete
  9. baada ya kuenda ktk internt ehe acha kuzungumzaa stori za zamani angalia upya brazil ndio ina ongoza kwa madeni.nina uhakika ninachosema sema na kazi zangu ni za ktk hii nyanja.

    ReplyDelete
  10. Kama huna namba tafadhali kaa kimya tuongee watu tunaojua tunachokisema, internet si wote tunayo sasa kinachokushinda nini?

    ReplyDelete
  11. Badala ya kutumia mabillioni kununua magari ya kifahari yanayoweza kuhimili barabara mbofu mbofu, kwanini wasitumie mabilioni hayo kutengeneza barabara ili magari mabofu bofu nayo yaweze kujihimili?

    Akili ni nywele na Tanzania kuna wenye vipara wengi!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...