haya mambo yalipotea kwa muda, sasa yamerudi tena kwa kasi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 29, 2006

    hawa ni akina matonya nini????

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 29, 2006

    tuwekee na picha ya kinje akiwa pamoja na mademu zake wote watatu

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 29, 2006

    Michuzi,
    Hali kama hii inatukumbusha kazi kubwa iliyopo mbeleni mwetu.Hawa hawapo hapo kwa mapenzi yao.Dawa sio kuwafukuza bali kuangalia kiini chake ambacho ni hali duni za kimaisha.

    ReplyDelete
  4. Jeff,
    Hawa watu waone hivi hivi, wana mashamba ya maana Dodoma tena wana kipaji cha kupanga ratiba zao, ikifika kipindi cha kilimo hurudi Dodoma na kusaidiana kulima, mazao yakianza kukua wengine wanabaki kuangalia mashamba na wengine wanakuja mjini kukusanya. Na wanapokuwa mjini wazazi huwapangia ratiba kwamba wewe utaenda wapi na wewe wapi na tena ni marufuku kunawa uso..Jamaaa wana hela kama hawana akili nzuri. Kuna kipindi nilifanya kazi na watoton waishio katika mazingira magumu huko ndiko niliko yajua yote haya.

    Mimi naona cha msingi ni kutafuta njia ya kuwakomboa kifikra ili wao wenyewe wakubali kubadilika na si kuwalazimisha kubadilika.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 29, 2006

    Kama ni kweli wana mashamba ya maana basi hayo mashamba hayawasidii kitu maana hiyo kazi ya omba omba na kulala nje kwenye baridi na mbu usiku ni mateso makubwa, siamini kabisa kama kweli wana hela hakafu wanaendelea kuteseka namna hiyo.....

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 29, 2006

    Mimi siamini kuwa kweli ombaomba wana shida. Huu ni utaratibu wa maishatu wamejiwekea hawa ndugu kama njia ya kujiongezea kipato. Nasikia kuna wengine mpaka wamejenga huko kigamboni kwa hela hii hii ya kuomba. Tunatakiwa tubuni means ya kuwaelimisha ili waachane na hii tabia.

    ReplyDelete
  7. jamani tutazame picha hiyo hapo juu na kisha tujiulize kama tunadhani huyo mtoto na mwenzaqke mgongoni na mwingine chini kama wanamiliki mashamba ya maana Dodoma ama kwingine Tanzania? Tutafakari pia kuhusu maana halisi ya mashamba ya maana katika nchi yetu? Tukitazame kilimo kilivyotupwa na kudhalauliwa, tuangalie masaibu ya watanzania wanaoishi vijijini na kisha tufikiri kuhusu bei za mazao na adha kama ukame! Kisha tufunge safari ya kuingia katika miji ya Tanznaia na kuona idadi ya watu inayoongezeka huko? Sababu ni zipi wakati zamani tuliambiwa kuhamia vijijini lakini wajanja wakajichimbia mijjini na kufanya maisha ya anasa huko huku wakisahau kaya zilizo vijijini? Wakati huo huo tutazame nini kinafanya hata serikali kuogopa kuhamia Dodoma? Omba omba, machinga, wanaofanya biashara ya ngono nk nyingine za muundo huo ni kutokana na ukata unaokithiri kadri siku zinavyoongezeka. Naungana na Jeff kuhusu kufanya tafakari ya mzizi wa tatizo na kisha kujiuliza ni nani kati yetu anayehitaji serikali kumuinua kimaisha kati yangu na huyo mdogo wangu anayeombaomba hapo huku kaka yake akikaa dirishani na kujikausha.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 30, 2006

    Kuna ujumbe kwenye hiyo picha kwetu sie watanzania. Naungana na bwana Jeff na Mr. Makene na je ni kitu gani kifanyike kutatuta tatizo hili?

    ReplyDelete
  9. Kamjadala kanakwenda vizuri,

    Makene nimekupata lakini ninakuhakikishia watu hawa wana fedha kuzidi mwananchi mwenye mshahara wa kima cha chini.

    Kama Bwana Grill alivyosema, kwamba huu ni utaratibu tu waliojipangia, ni kweli watu hawa karibu wote wanaishi Kigamboni tena kwenye nyumba zao si za kupanga. Hao ambao hulala barabarani huwa ni danganya toto ili kuuhakikishia umma kwamba wana shida, na sio kama siku zote hulala hao hao hujiwekea zamu, leo familia hii kesho hii.

    Lakini bado nakubaliana na Jeff pia kwamba kipo kiini cha yote haya hadi watu kuamua kuwa MIRIJA. Nimeukumbuka leo msemo wa Nyerere "MIRIJA".

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 30, 2006

    Kupanga mbinu ya kuwasaidia kujikomboa kimawazo ni sawa kabisa lakini kwa vile hawa wanachukulia hali hii kama sehemu ya shughuli katika maisha yao itachukuwa muda sana kukubali,nilibahatika kufika UK wakati fulani pale serikali inahudumia watu wa makundi mbalimbali lakini bado waombaji wapo mitaani kuomba zaidi, kumbe jamani kazi ipo kubadili fikra za omba omba.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 30, 2006

    sitegemei hao watoto wanajipangia kuwa omba omba, nahisi hao ni watoto wa omba omba na kuna uwezekano mkubwa na ako katoto kaliko bebwa mgogongoni kakawa omba omba na watoto wa hao watoto pia watakuwa omba omba(snow balling). Mzunguko utaendelea na bila serikali kuangalia hili suala inasikitisha kuwa watoto wengi watajikuta kwenye tatizo hilo. Huyo kaka wa chenji alobakisha ni ya moja baridi break point!!!

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 30, 2006

    daa huu umaskini wetu! haya hapo mtoto kambeba mtoto mwenzie, hivi maisha ya watoto hao yatakuwaje kiukweli mwenye moyo wa kuwasaidia awasaidie tuu,lakin unama sana

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 30, 2006

    Tupunguze kuzaa zaa kama sungura! Uzazi wa mpango ni muhimu sana. Omba omba akizaa watoto 7 wakati hana hela ya kumpeleka hata mmoja shule, wote wataishia kuwa omba omba.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 31, 2006

    Naomba yeyote anayewaangalia hawa watoto ajitahidi mdomo wake usiropoke kashfa.Jaribu kufumba macho na kufikiri;umeoa na umewazaa hao watoto,lakini kutokana na ulimwengu wa sasa uliojaa shida na magonjwa wewe na mkeo au mumeo mnafariki na kuwaacha hawa watoto;labda wewe na mkeo huko dar mlikuwa mnaishi kwa kubangaiza aina fulani ya maisha.
    Mimi nawaangalia hawa machozi yananitoka!Mungu atupe watu wake maarifa.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 02, 2006

    MLIOKO UGHAIBUNI WATUMIENI NDUGU ZENU PESA. MMEWATUPA SAAAAAAAAAAAAANA. WENZENU TUNATUMA TAFADHALI.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...