kituo kipya cha mabasi cha kijitonyama makumbusho kinachochukua nafasi ya kituo cha mwenge. watu wa mwenge hivi sasa inabidi wadunde kwa mguu tokea hapo makumbusho ambako ni mwisho kwa mabasi yatokayo mjini. si zogo hilo lililopo!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 25, 2006

    Vipi facilities kama vyoo, vioski na sehemu ya kivuli kwa wangojea mabasi vipo?ama kwa vile ni eneo wazi basi ni kiyuo, hii ni dhihaka sana ndio maana tunakuwa nyuma siku zote bila kutengeneza stendi za maana.Pale Ubungo kama si UDA sijui tungepajemga kwa miaka mingapi na kwa design gani.Maskini TZ!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 26, 2006

    Sipati picha halisi yab daladala za mwenge - tazara, posta/kariakoo - kupitia manzese/sinza (shekilango road), yatakuwa yaishia au yanapaki wapi! Jamani hebu wazeni kabla ya kutenda! Fanyeni maandalizi ya jambo/kitu kabla hamjaamua kulazimisha watu kufanya kile mnachotaka! Maana wengine tutabakia haah! Gerald Hando na Fina Mango mpooooooo!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 26, 2006

    HIVI TANZANIA TATIZO NI NINI?HATUNA WATAALAMU,UMASIKINI,RUSHWA,UZEMBE AU NINI?SIELEWI KWA VIPI WATU WANAKURUPUKA TU KUTOA MAELEKEZO BILA KUPANGA KWANZA,INASIKITISHA!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 28, 2006

    Michuzi mbona unapotosha watu walio mbali na nyumbani? Kwani ina maana magari yalipokuwa yakifika Mwenge wote waliokuwa wakiyapanda walikuwa wakiishi Mwenge? Mbona kuna magari ya Kariakoo Tegeta yanayopitia Mwenge? Mbona jamaa wa Makumbusho, kijitonyama ambao ni wengi kuliko wa Mwenge wamefurahia hiyo dili ya Serikali? Muulize Nsyesu akuambie!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 28, 2006

    We michuzi nawewe hebu acha hizo, ina maana hakuna mabasi ya tgt? sasa hao waendao mwenge si wapande hayo ya tegeta?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...