washiriki wa miss tanzania ya kwanza nchini hoteli ya kilimanjaro. mshindi aliibuka bibie theresa shayo (namba 5), ila baada ya hapo mashindano yakapigwa marufuku kwa dhana kuwa kinyuma na maadili ya mtanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 24, 2006

    Je hivi sasa mambo ya umiss yako sawa na maadili ya kitanzania?! Feministic organisation zote zinapinga haya mambo kwa kusema kwamba ni kumdhalilisha mwanamke!Yaani umbo na uzuri kutumika kama chombo kujikimu kimaisha!Nadhani machangudoa nao kwao umbo ni chombo cha kujitafutia maisha!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 24, 2006

    NIMEIONA HIYO MICHUZI,KUMBE WACHAGA(KASKAZINI HAWAJAANZA LEO KUPRESENTI FANI?)SAFI SANA!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 24, 2006

    Hapana,mashindano ya uzuri ni kumtukuza MUNGU na KUMKASHIFU pia!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 24, 2006

    Hao ndio walikuwa warembo kweli kweli, no wigi, no mkorogo just beauty.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 24, 2006

    Na mpaka leo ni kinyume na maadili basi tu Afrika hakuna msimamo. Waafrika Mahanidhi wa akili

    ReplyDelete
  6. Unajua 'beauty' ni neno binafsi, kila mtu ana viwango vyake. Ila kimaadili, ni wazi kwa kuzingatia mila ya mwafrika, basi hawa mamiss wa leo si wazuri kabisa.
    Nani anabisha?

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 24, 2006

    Pembe wewe ni exception unakubali kujitukana mwenyewe. FUNY!!!!!!!!

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 24, 2006

    Nyie Waafrika mnadakia mambo tu kama kasuku. Mila sijui za Mtanzania sijui Mwafrika ndio zipi? Nguo mmeanza kuvaa miaka mia moja iliyopita leo mnajifanya ati siyo mila yenu kukaa nusu uchi. Hebu tizameni picha ya Michuzi kuhuzu Wanyasa na ngoma yao kwenye blogu hii halafu mlinganishe kati ya hao na hawa ma miss nani wanajidhalilisha. Ujambazi, wizi, rushwa ndio havikuwa mila zetu lakini wapi, watu wanapenda hayo mradi mtu upate pesa badala ya kupiga vita hayo tunabakia na kushughulishwa na trivial matters.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 24, 2006

    ANONY 6:16 PM INAONEKANA ULIKAA DARASANI NA ULIELIMIKA!MORE THAN EXCELLENT!

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 24, 2006

    Acheni madomo kaya...kukandia vitu msivyovijua, wengine humo kwenye shindano utakuwa ni mashangazi zenu, mama zenu wakubwa au ata mama zenu kabisa...

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 24, 2006

    katika blogu hii haipiti siku bila watu kubishana au kutoa lugha chafu sijui ndio utamaduni?

    kwanini msijieshimu wote na kuweza kutoa comment za msingi zitakazo wasaidia wabongo wote? alafu utakuta wengine wana elimu zao na wengine wapo majuu na ndio hapo utajua kwamba kuwa na elimu au kuwa huku majuu sio kubadilika tabia na kuelimika.

    badilisheni mawazo na tabia zenu, mkiiendelea kuchangia visivyo eleweka au matusi ndio itakuwa kama sheria kwenu na hako katabia kitakwenda mpaka kwa watoto wenu au jamii yenu nzima.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 24, 2006

    We Anony wa saa 10:55PM unaweza kutupa ufanunuzi zaidi kuhusu comments za maana. Wengine matusi kwao ndio kitu cha maana humu duniani na yanawasaidia sana. Ni vigumu sana watu wote kuwa na interest ya aina moja. Hata ingekuwa ni blog inayotembelewa na marais watupu duniani matusi yasingekosekana. Kila mtu ana interest yake wala haina uhusiano na level ya elimu kabisa.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 25, 2006

    Unajua saa zingine ukinyamaza unaonesha una busara sana kuliko kuongea vitu ambavyo havimake sense.

    Mimi sikubaliani na lugha ya matusi hata siku moja, lakini kitendo cha kusema huyu anaongea pumba yule yuko majuu sijui nani msomi na nani hakusoma ni kuonyesha mapungufu yetu tu. Kwa vile hukubaliani na maoni ya watu wengine haimaanishi wao ni wajinga na wewe ni mjanja.

    Kama kweli mna nia njema na hao mnaowaona wajinga dawa yake ni wewe kutoa point ambazo zinakuwa na nguvu kiasi cha kumbadilisha unayemuona mjinga ili awe mwelevu kama wewe.

    Siku zote mwanga huonekani kizani, hebu na onyesheni mianga kizani badala ya kutumia miwani ya mbao ili uone gizani.

    ReplyDelete
  14. Bwana Michuzi, mbona wenzetu watoa maoni katika blogu yako kwa kawaida huwa wanajificha nyuma ya hii anonymous?

    Ni kuwa na haya/uoga au ni vipi mbona wenzetu hawajitambulishi?

    Sura mpya ya blogu yako ni makini kabisa na kama kawaida picha na maelezo ni kuvutio kikuu kabisa kwangu!

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 25, 2006

    katika blogu hii haipiti siku bila watu kubishana au kutoa lugha chafu sijui ndio utamaduni?

    kwanini msijieshimu wote na kuweza kutoa comment za msingi zitakazo wasaidia wabongo wote? alafu utakuta wengine wana elimu zao na wengine wapo majuu na ndio hapo utajua kwamba kuwa na elimu au kuwa huku majuu sio kubadilika tabia na kuelimika.

    Kingine utakuta picha imewekwa watu wana anza kuzungumzia maisha binafsi ya huyo mtu, kumtukana, kumtolea maneno ambayo mengine hayana ukweli wowote ule.

    Mkumbuke hii blogu ina angaliwa na watu wa kila umri na kila cheo. wapo watoto na wakubwa hivyo basi tuijenge hii jamii kwa kutoa comment za busara na zisizo na matusi au kukashifiana.

    badilisheni mawazo na tabia zenu, mkiiendelea kuchangia visivyo eleweka au matusi ndio itakuwa kama sheria kwenu na hako katabia kitakwenda mpaka kwa watoto wenu au jamii yenu nzima.

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 25, 2006

    Akiey acha kuleta zakuleta, Wewe kuandika hilo jina ndio kumekufanya usiwe anonymous? hakuna anayekufahamu na hakuna anayeweza kudhibitisha kwamba hilo ama ni jina lako au silo. Cha muhimu hapa ni lugha nzuri basi. Wewe unafikiri watu wote wakijitambulisha kwa majina ambayo hata hatuna hakika kama ni yao au hata hutujali kuyafahamu na bado wakaendelea na lugha zao chafu itasaidia nini?

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 25, 2006

    AKIEY hakufikiria na kuanalaizi ulichoandika hapo juu. Tunakuomba ukae chini ufikirie kwanza ndipo utoke upya. Haya fikiria vizuri validity ya ulichoandika na utoke tena upya karibu sana!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 26, 2006

    Kukaa kimya si ujinga, mbona mimi nina point za nguvu lakini sijazitoa?

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 26, 2006

    ETI MWAYEGO ANONI 11:41 AM,HATA MIMI SIZITOI ILA NINAZO KIBAO!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...