mtaalamu wa kilimo wa brazil akimueleza dk asha-rose migiro mbinu za ukulima wa zao la muhogo, ambao ni moja wa vyakula mama vya wabrazil. pamoja na soka nchi hii ina maendeleo makubwa kwenye kilimo, viwanda na biashara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 16, 2006

    Michuzi kisamvu wanakijua hao?

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 16, 2006

    Michuzi,
    Sasa jamani hata kilimo cha mihogo tunahitaji wataalamu kutoka nje? Kama Dr. Migito angekuwa na nafasi angeenda Serengeti, Mara. Huko angepata utaalamu zaidi wa jinsi ya kulima mihogo manake ndio zao tunalitegemea kule.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 16, 2006

    kweli kabisa zemarc uliyosema hapo juu, unajua watu wengine wanatabia ya kujifanya wanajua kila kitu wakati hawajui.

    umenena na busara sana leo hii.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 16, 2006

    SASA HAPO INABIDI SERIKALI IPELEKE ANGALAU WAKULIMA WACHACHE KUJIFUNZA NA SIO ALIVYOONA MINGIRO KUWA INATOSHA,ANGALAU MMOJA MMOJA KUTOKA SEHEMU ZINAZOLIMA MHOGO KAMA ZAO KUU LA CHAKULA;NA WAKIRUDI KUTOKA HUKO,WASAIDIWE PEMBEJEO ILI WAWAFUNDISHE WENGINE KWA VITENDO.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 16, 2006

    Huyu waziri ameenda na wataalamu au ameenda peke yake. Maana safari kama hizi angekuwa anaandamana angalau na mabwana shamba wawili hivi kutoka zile sehemu zinazolima hili zao kwa wingi.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 16, 2006

    Mimi naona suala hapa sikujifunza kulima mhogo, kwani hiyo mihogo ninayoiona hapo afya yake ni mbofumbofu kulinganisha na mihogo inayopatikana huko Nyang'hwale au Kasamwa. Mihogo mitatu tu inaweza kutoa debe la unga, lakini hii hapa mmh! Labda wanachoweza kutufundisha ni jinsi ya kuhifadhi ziada au kusindika kwa matumizi ya baadaye. Lakini kwa kilimo hawaoni ndani.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 16, 2006

    Ninyi kuhusu muhogo tunavyolima kule serengeti sina haja ya kujifunza kuoka kwa mto yoyote kwani nina uhakika tunafanya vizuri zaidi kuliko watu wangine. Piga uwa nitajifunza vitu vingine lakini sio kulima muhoga kutoka Brazil.

    Itakuwa ni suala la kupotezeana muda na mali kama tunaenda kutafuta utaala nchi za nje wakati sie wenyewe tunao ujuzi hapa hapa Tz. Anony 11:50 nakubaliana na wewe kabisa mihgo mitatu tunayolima home inaonekana kuwa na afya kuliko hiyo ya wabrazil, labda kama hao wabrazil wamkuza hiyo mihogo kwa wiki 1

    ReplyDelete
  8. jamani hawa wabrazil wanatisha sio kwenye soka tu, bali hata mambo memngine ikiwa ni pamoja na kilimo na ufugaji.

    hapa brazil dr migiro alikuja kutia sahihi mkatabaw a ushirikiano wa kudumu na nchi hii katika masuala mbalimbali, hivyo baada ya hapo milango itakuwa wazi kwa wataalamu wa sekta mbalimbali kuja kujifunza.

    mnaoona hakuna haja kuja mbali kote huku kujifunza ukulima wa muhogo mmekwenda adijojo. hawa jamaa wamefanya utafiti na kugundua aina kama 12 za mihogo na idadi hiyo hiyo ya matumizi, ikiwa ni pamoja na nguvu za nishati.

    hivyo ndugu zetu wa sengerema mihogo ina faida nyingi zaidi ya kujaza tumbo. kwa ushirikiano huu bongo tuna nafasi ya kujifunza mengi toka huku...

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 17, 2006

    Michuzi hiyo yuca mitamu kishenzi,jaribu kula utatuambia utamu wake kama nini

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 17, 2006

    kwa miaka yote tunaona picha za mawaziri wetu kutia saini mikataba, mambo yako pale pale tu.hizi safari ndefu wakubwa wanajitungia ili wapate pesa(alawansi ) za safari,mwezi mzima safarini anatengeneza kaa dola elfu kumi hivi or more,watu wanabaki wakizani bosi anakula rushwa,kumbe alawansi za kitunga. nyie tanzania na brazili wapi na wapi.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 18, 2006

    Maswala ya kupigana picha za kutabasamu na kusaini mikataba imepitwa na wakati sasa tunataka kujua mikataba hiyo ina faida gani na itaendeshwaje. swala la kuwatuma wakulima wakajifunze nalo laweza kuwa ni kupoteza muda kwani nao watakuwa wanaangalia alawansi tu. Ni hawa viongozi wetu kuwa serious katika "implementation"

    ReplyDelete
  12. Jamani hata hapa tuna mbegu bora kibao za mazao kama mihogo mahindi viazi maharage na kadhalika, kama unataka kusadiki hayo nenda kituo cha utafiti kilimo cha uyole mkoani mbeya uone ma Dr wanavyo breed mbegu pale, tatizo ni kwamba hazisambazwi kwa wakulima ipasavyo zinaishia vijiji vya karibu

    Nenda mpwapwa kuna mbegu bora ya ng'ombe inayojulikana kama mpwapwa breed imegunduliwa tangu miaka ya 60lakini wala haijasambazwa kwa wakulima mpaka leo

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 18, 2006

    Waziri wa Kilimo anafanya nini? Kazi yake inafanywa na Waziri wa Mambo ya Nje? Au haruhusiwi kusafiri nje ya nchi?

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 19, 2006

    WAZIRI WA KILIMO WA TANZANIA,HUYO NDIO KIUNGO CHETU KWA WIZARA ZOTE NJE YA NCHI,HUYO NI LAZIMA AJUE KWANZA.(ATIE SAINI MIKATABA YA KUANZISHA USHIRIKIANO)HAUKUWEPO KATIKA MAMBO HAYO,ANGEKWENDAJE?

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 20, 2006

    Hapo ndio tunapokosea sasa mbinu za ukulima wa muhogo ilitakiwa aelezwe bwana shamba hapo sio Migiro ili aweze kuwasaidia wakulima....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...