dada wa kibongo akanashejoan mwanga (katikati, nyuma) akiwa wu qiao huko hebei, china, akishiriki kwenye tamasha la china-afrika. dada huyu, ambaye sasa amerudi nyumbani baada ya kuhitimu mafunzo ya mazingaombwe, sarakasi na lugha ya kichina kwa miaka 4, sasa amefungua kampuni yake ya maonesho na amepanda chati kichizi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 12, 2006

    aji hongera sana! na pole sana!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 14, 2006

    Katika moja ya makusanyo yangu ya picha nilikuwa na picha ya kikundi cha taifa cha sarakasi kikishuka kwenye meli wakitokea China, mwaka 1973/4. Nilibahatika kukiona kikundi kile kwenye maonyesho yao ya awali kabisa kwenye ukumbi wa Msimbazi. Pia nilibahatika kukiona tena kwenye maonyesho yake ya mwisho kwenye ukumbi Diamond kabla kikundi kuvunjwa 1980.

    Kwa sudi hiyo hiyo baadhi ya wanasarakasi wa kikundi cha taifa k.m. Marehemu Mwalimu Thomas Umila na David Twalib wakaja kuwa walimu wangu nilipokuwa Chuo cha Sanaa Bagamoyo. Kwa sudi hiyo hiyo hadi leo hii ninapoandika nina kusudio la kumuinua tena Bingwa Khamis Nyota moja wa mabingwa waliokuwa kwenye kikundi cha taifa cha sarakasi.

    Nina hamu sana ya kujua wapi walipo na wanafanya nini akina Lipi, George, Rajabu Ubwa,Abuu, Edison "Tyson" Mwamakula -mara ya mwisho nilisikia habari zake akiwa Moshi au Arusha, Nobert Mhanga -mara ya mwisho niliongea naye akiwa Sweden na alikuwa kabadili kibao na kuwa Medicine Doctor, Ada Mfungo -mara ya mwisho nilimuona akiwa na Muungano Cultural Troupe, Safi Omar, Shangwe, Mary Materego na wengineo wote!

    Muhidin, tafadhali naomba upekue kule masijala halafu utuletee ile picha ya wale jamaa wakishuka toka China.

    Dada Joan hongera kwa mafanikio na tafadhali waenzi waliokutangulia akina Safi Omar, Ada Mfungo, Shangwe, Mary Materego na wengineo.

    Ni miye maridhiya,
    F MtiMkubwa Tungaraza.

    ReplyDelete
  3. Kulikuwa na jamaa fulani, Roderick Ndomba, naye alienda kusoma China miaka ile kuwa mwana sarakasi. Kama una habari zake tafadhali nipashe.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 15, 2006

    Pia alikuwepo Faustin Kibingwa -mara ya mwisho nilimuona Uwanja wa Taifa alipokuwa anachezea Nyota Nyekundu.

    Njia rahisi ya kupata taarifa za hawa jamaa ni kwa kumpata Mwalimu Rajabu Ubwa. Kama kuna mtu anajua anuani, namba ya simu, au namna nyingine yoyote ambayo itawezesha kumpata Mwalimu Rajabu tafadhali tuunganishie.

    Shukran jaazillah.

    Masalaam,

    F MtiMkubwa Tungaraza.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 17, 2006

    China kutoa mafunzo ya sarakasi kwa vijana kutoka Afrika

    --------------------------------------------------------------------------------

    cri
    Wasikilizaji wapendwa, mliyosikiliza sasa hivi ni muziki ya maonesho maalumu ya sarakasi, yaliyofanyika tarehe 14 mwezi Septemba kwenye Jumba la Maonesho ya michezo ya sanaa la Tianqiao la Beijing. Maonesho hayo mazuri yaliyofanywa na wasanii kutoka Sudan, Ethiopia, Tanzania na Kenya, yaliwafurahisha watazamaji.

    Sarakasi ni sanaa inayopendwa na nchi za Afrika. Katika miaka ya 70 na 80 ya karne iliyopita, China iliwahi kutoa mafunzo kwa vikundi kadhaa vya wachezaji wa sarakasi kutoka kwenye nchi za Afrika. Baada ya kurudi nyumbani kutoka China, wachezaji hao waliunda vikundi vya sarakasi na kufanya maonesho nchini mwao na katika nchi za nje, na kushiriki kwenye mashindano ya kimataifa ya sarakasi na kusifiwa sana. Baada ya kuanzishwa kwa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika, ushirikiano kati ya pande hizo mbili umeingia kwenye kipindi kipya. Kwa msingi wa baraza hilo, kutokana na matakwa ya nchi za Afrika, wizara ya utamaduni ya China imeanzisha tena mradi wa kutoa mafunzo ya sarakasi kwa vijana wa Afrika. Kuanzia mwaka 2002, wizara ya utamaduni ya China iliifanya shule ya sarakasi ya Wuqiao ya Hebei iwe kituo cha kutoa mafunzo kwa wanasarakasi kutoka nchi za Afrika. Hadi sasa shule hiyo imewaandaa wanafunzi 36 kutoka Tanzania, Kenya, Ghana na Ethiopia, na maonesho yaliyofanyika tarehe 14 hapa Beijing yalifanywa na kikundi cha tatu cha wanafunzi wa shule ya sarakasi ya Wuqiao.

    Mabalozi wa nchi mbalimbali za Afrika nchini China walialikwa kutazama maonesho hayo, wakiwemo balozi wa Kenya Bi. Ruth Solitei na kaimu balozi mdogo wa Tanzania Bw. Augustine Ngonyani. Bi. Solitei alisema, Kenya inaishukuru sana China kwa juhudi zake za kutoa mafunzo kwa wasanii wa sarakasi wa Afrika, akisema:

    Viongozi hao walifurahishwa na maonesho hayo mazuri. Kabla wachezaji hao kupanda jukwaani, wanaonekana ni watu wa kawaida, lakini wakati wanapokuwa jukwaani wote walikuwa wasanii hodari, wanaonesha vizuri kila sehemu ya mchezo, kwa mfano, sehemu moja inaoneshwa mtu mmoja akiwabeba watu watatu, lakini yeye mwenyewe alisimama kwenye ubao uliowekwa kwenye gurudumu. Kwa mtu wa kawaida ni vigumu sana kusimama kwenye ubao uliowekwa kwenye gurudumu, sembuse kuwabeba watu watatu. Muziki wa Afrika, na wachezaji wa Afrika wenye ukarimu mkubwa, vyote vimeipatia sarakasi ya jadi ya China sura mpya.

    Wakati maonesho hayo yalikuwa yakiendelea, makofi makubwa kama hayo yalisikika mara kwa mara. Watu kutoka nchi mbalimbali waliwasiliana kwa macho na kutikisa vichwa mara kwa mara wakifurahia maonesho hayo, wakati huohuo sarakasi imekuwa lugha moja inayotumika kote duniani.

    Baadhi ya wachezaji hao waliwahi kupata mafunzo ya sarakasi kwenye nchi zao, lakini mafunzo hayo hayakuwa kamilifu sana, baada ya kujifunza nchini China, kiwango chao cha sarakasi kimeinuka kwa udhahiri. Kitu cha kawaida kama vile bakuli, kofia, kiti, na meza kikifika mikononi mwao, kitabadilisha sura yake, hali hiyo inawafurahisha sana watazamaji, na pia imewafanya wafahamu zaidi sarakasi.

    Kabla maonesho hayo hayajaanza, mwaandishi wetu wa habari alipata fursa ya kukutana na wasanii hao, mkubwa kabisa ana umri wa miaka 18, na mdogo kabisa ana umri wa miaka 12, ni kama mwanafunzi wa shule ya msingi. Walipozungumzia maisha hapa China, wote walifurahi na kukubali kuongea na mwandishi wetu wa habari.

    Kati ya watoto hao wanaopendeza, kuna msichana mmoja mrembo mtanzania anayeweza kuongea vizuri kichina, anaitwa Joan Mwanga. Aliendesha maonesho hayo kwa kichina, wakati maonesho hayo yalipofika katikati, aliimba wimbo mmoja unaoitwa Mapenzi yangu kwako ni kama Mwezi, ambao uliwafurahisha sana watazamaji. Alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa, kichina chake kinatokana na kuishi kwake China kwa miaka mitatu, na wachezaji hao pia wanaweza kuongea kidogo Kichina, kwa kuwa wana vipindi vya kujifunza Kichina kila wiki. Alisema, wasanii hao watarudi nyumbani kwao muda mfupi baada ya maonesho, lakini yeye atabaki hapa China kuendelea na mafunzo.

    Konsela wa wizara ya utamaduni ya China Bi. Zhang Jiping alifahamisha kuwa, katika miaka 25 iliyopita mbali na kuanzisha kituo cha kutoa mafunzo ya sanaa kwa watu wa nchi za Afrika, China imepeleka wataalamu katika nchi mbalimbali za Afrika kutoa mafunzo ya uchoraji, dansi na sarakasi, hatua hiyo imekaribishwa na nchi za Afrika. Kaimu Balozi mdogo wa Tanzania Bw. Augustine Ngonyani alisema:

    Sarakasi ni sanaa ya jadi ya China, walimu wa sarakasi hawakubali kumfundisha mtu yeyote, lakini wachina wanatoa mafunzo ya sarakasi kwa watu wa Afrika, hali hiyo inathibitisha kwa mara nyingine kuwa, watu wa Afrika ni marafiki na ndugu wa wachina!

    Imenukuliwa na,

    F MtiMkubwa Tungaraza.

    ReplyDelete
  6. mary materego yupo germany kwa sasa anafanya kazi katika circus moja inaitwa AFRICA!AFRICA!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...