Christliche Negerfamilie in Moschi
One of the many pictures from the history files. This one dates back to German colonial times (prior 1919) Translation: A Christian Black Family in Moshi

Magogoni creek enzi za Mjerumani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Enzi hizi mvua ikigoma kunyesha walikuwa wanaenda kwenye mapango wanachinja mbuzi na kufanya tambiko, kabla hawajamaliza mvua hiyoooo, sasa hivi thubutu mtachinja hata ngombe wote mvua hamna, mvua itoke wapi wakati miti yote tumegeuza milango, madirisha, stuli, vigoda, mkaa nk.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 21, 2006

    michuzi,tuwekee picha kama hizi zinazoonyesha tanzania miaka hiyoo wakati wa ukoloni au miaka ya mwanzo baada ya uhuru....napenda historia na picha kama hizi zinatukumbusha mambo mengi ya siku zilizopita...tukipata picha kama za maeneo ya kati ya dar-es-salaam,oysterbay,sinza,masaki'kichangachui'zitanoga mnooo

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 21, 2006

    Michuzi,
    hiyo picha ya waafrika wa kwanza kwanza kukubali uongo wa Wajeremani ni rekodi nzuri sana ya kihistoria. Ukitazama nyuma ya familia hiyo utaona majani ya "isale." Isale ni jani linaloheshimika sana katika utamaduni na mila ya Wachagga. Jani hili hutumika kwenye mitambiko, kesi, n.k. Hutumika pia kuashiria kuwa nyumbani kwa fulani kuna pombe ya mbege. Ukiweka jani hilo katika njia inayoelekea nyumbani kwako (kwa huko Moshi huitwa "kichumini.") watu wanajua kuwa wakija kwako watapata kata ya mbege.

    Iwapo kuna mtu umemkosea sana sana. Unataka kumuomba msahama. Ukienda kwake ukiwa na jani hili lazima akusamehe. Isale ni jani muhimu sana katika kupatanisha na kutatua ugomvi. "Wasomi" wanaotatua ugomvi katika nchi za Afrika wangekuwa wanaheshimu mila na tamaduni zetu wangekuwa wanatumia mbinu za kitamaduni na kimila kutatua magomvi. Wengi hutumia mbinu na nadharia walizosoma katika madarasa ya vyuo vikuu nchi za magharibi wanashindwa kujua umuhimu wa kutumia vitu kama isale.

    Jani hili ni moja ya alama zilizokuwa katika bendera ya wachagga enzi zileeeee.....

    Haya, somo la historia na utamaduni kwa chati...Asante Michuzi.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 21, 2006

    Lakini Ndesajo si unajua hasara na faida za wakoloni?

    ReplyDelete
  5. Unajua kwa wenzetu, wangeweza kutrace na kujua hawa watu descendants wao leo hii ni akina nani na wako wapi TZ. Ila tulivyo bongo hata wajukuu wa hii familia hawajui kuna picha za babu wa babu yao.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 21, 2006

    Nakuunga mkono "Picha zetu"

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 21, 2006

    Na wewe Simba nenda kaone faida na hasara za wakoloni!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 22, 2006

    Bwana michuzi usipotoshe maana halisi. "Christliche Negerfamilie in Moschi" maana yake ni "Familia ya nyani ya kikristo Moshi" na wala sivyo kama ulivyotafsiri wewe. Cha ajabu ni kwamba watu waliotudhania kuwa sisi ni nyani wametuletea mafundisho na kwa upumbavu hao wazee waliotutangulia wakayakubali. Upumbavu zaidi ni sisi vizazi vya sasa pia bado tunaendelea kuamini upumbavu huohuo.

    ReplyDelete
  9. emergency poison, bora umesema ukweli maana huyo anony muongo mkubwa.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 22, 2006

    Nilivyomuelewa huyo aliyesema kuwa tafsiri ni "familia ya nyani" alikuwa anakejeli akimaanisha kuwa wakoloni hao walikuwa wakituchukulia kuwa sisi ni nyani. Naona hii ni kejeli yeye ukweli fulani.
    Hii ni tafsiri yangu ya maoni yake. Kama nimekosea anaweza kunisahihisha.

    ReplyDelete
  11. basi siku nyingine ajue watu watafikiria vibaya maana hiyo tafsiri aliyotupa Michuzi ndiyo sahihi. Yaani mnafikiria huko kwenye maktaba watu wataweka caption inasema 'familia ya nyani?'

    ReplyDelete
  12. Kigerera kwa bahati nzuri mimi ni mwana mazingira na nina mashamba ya miti, pia ninajua jinsi watu wa zamani walivyokuwa wanahifadhi mazingira kwa imani zao, mkoa wa Tanga ndio unaoongoza kwa hifadhi ya misitu na hii inatokana na wao kuendekeza ushirikina (samahani)kwa hiyo misitu yenye vyanzo iliwekewa mila kali na watu wanaogopa mpaka leo hii kuigusa, kwa hiyo hapo nilikuwa najaribu kuoanisha vitu vyote viwili, niliongelea imani na hali halisi

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 31, 2006

    Wewe Simba ni michanganyiko ya maisha hiyo ndio inakufanya uamini hivyo unavyoamini! Usipoangalia utawehuka bwana mdogo shauri yako! Face reality, mimi kama muislamu hapa Tanzania, na expiriences zangu zote za kusafiri global hii, wale wanaoamini na kuabudu vitu vya ajabu, ajabu kama wewe, asilimia kubwa maisha yao sio kama wale wanaobudu biblia. Ukiangalia kwa makini utachunguza there is a lot of love and care katika biblia, kuliko kwenye ubuda, uhindu, uislam, mizimu, n.k
    Ndio maana wanaoabudu biblia always huwa wanaishi afadhali kuliko sisi.
    Mfano mdogo hapa Tanzania, watu wanaoishi bora ni waikristo kuliko waislam! Dunia ya leo hii kisiasa wanyama wanaoongoza ni sisi waislam.
    Tumetawaliwa na waislaam na waikristo, leo hii, misaada mikubwa inatoka wapi? Kwa wazungu au waarabu?
    Sasa hata kama tulidanganywa na wakoloni ni sawa, is too late now! Sasa wewe kwa ushauri wako unataka waafrica wote tuabudu mizimu yetu ya zamani, au wote tuwe waislaam kama mimi, si africa yote itakuwa kama Somalia?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...