kibopa wa kwaliti grup yusuf manji akitia sahihi mkataba wa kuifadhili yanga. mwenye buluu ni francis kifukwe, anayeanguka kwa niaba ya yanga

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Naona yanga wanachukua sehemu ya Mabilioni yao waliyochangia NSSF

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 03, 2006

    tunashukuru sana kwa kuweka picha ya huyu jamaa anaesumbua wabongo, Hapa kisha ona ulaji mwingine wa kufadhili yanga. Kama mnavyo jua kuna njia nyingi za kupata msamaha wa kodi.

    ReplyDelete
  3. Hii mikataba inatisha. Mwisho wa siku tusije tukaambiwa Klabu imebinafsishwa kutokana na vipengele vya mkataba.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 03, 2006

    Huu lazima huwe feki kabisa labda kama atabadilika sina uhakika make jamaa nasikia siyo mchezo. naona ametafuta umaarufu tena huyu mzee. washauri wake wako smart kabisa.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 04, 2006

    Huyu jamaa ni smart kwelikweli, baada ya kile kimbembe chake cha NSSF na Viwanja wa Chang'ombe kaamua kutafuta sympath kwa walalahoi. Kama kuna mtu anataka wajuba wamtoe roho amseme vibaya huyu jamaa sasa.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 05, 2006

    Hii tamaa ya pesa itatupeleka pabaya Watanzania. Sasa hii klabu yangu imeingia mkataba na huyo ponjoro mbona itakuwa mbinde.
    Huyu bwana kabla ya kukubali kuingia naye mkataba wowote tungesubiri kwanza asuluhishe ile kesi yake na Bw. Mengi.
    Hapa anatafuta umaarufu tu na kujijenga kwa walalahoi. Na kweli kama mtoa maoni hapo juu aliposema, sasa hivi ukimsema vibaya huyu ponjoro wajuba wanaweza kukutoa roho!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 06, 2006

    Mtumeeeeee hivi hana haya huyu mtu ni chori yaani mwizi wa kimataifa, kila maoni yaliyotoka hapa ni ya ukweli kabisa, kubadilika bwana hawezi huyu, huo mkataba ni feki, huyu jamaa sio mchezo, na naona ni shapu kweli ana washauri wa uhakika, yaani baada ya kasheshe ya NSSF na Chan'gombe sasa yuko kwa walala hoi. Haya tutasikia siku moja club imebinafsishwa kutokana na vipengeli vya mkataba, jamani kama wazungu wanavyosema ALWAYS READ SMALL PRINTS I hope wamesoma kwa makini nakala zote, lakini SINA IMANI NAO KABISA. Samahani.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 13, 2006

    Bwana Grill amezoza kweli, huyu mtu alikuwa wapi siku zote hizi yanga hakuiona? Shenzi taip tu huyu, ni MWIZI JAMANI, na ni kweli bwana Grill waTZ waluluga wamezoea kuburuzwa tu. ngojeni na maforena kibao hasa wa-Sauzi. haya ngojeni huko mbeleni TUTA-TAWALIWA, natabiri. Mwalimu NYERERE huko alipo peponi naona anasikitika sana mana alipinga sana haya mambo. lakini wamelowea sana na wameanzisha biashara kibao ambazo wanakuja na watu wao, wanauza vitu chipu, walalahoi wenzetu ajira hamna. Na waziwazi unakwenda mahotelini, mtanzania mwenzio anakuvuka na kumsevu forena kwanza , tunanyanyasika katika nchi yetu. Haya!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 14, 2006

    Grill huyu jamaa wakati anasaini mkataba unaona kabisa hana raha. Ni kama vile analia.Hebu mhangalie vizuri. Hapa kilichoko kichwani ni jinsi gani atarudisha hela yake yuko tayari kuwabebesha mzigo wowote hili pesa yake irudi. Mpaka akurupushwe ndio akimbilie yanga? inamaana yanga ni kimbiliao la wanaotafuta hauweni. Mimi nina wasi na mikataba ya presha. ndio maana nafikiria yanga tumeingiliwa. Samahani wapenzi wengine wa yanga inawezekana mkafikiri kuwa atatukomboa au namchukia. yangu macho.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...