stesheni ya reli dodoma

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. wakati picha ya chini ikionesha jinsi viongozi wa kiafrika wakionesha matumizi yao mabaya ktk pesa za taifa na wananchi, Picha ya juu inaonesha hali halisi ya mtanzania wa chini kabisa ilivyo na mazingira yake yanayo mzunguka. Je kuna Kiongozi yoyote aliye na uchungu na jamii hii ya kitanzania? Au ndio aliye shiba hamjui mwenye njaa? Viongozi wa Kiafrika nina jua baadhi yenu mna angalia hii blog hacheni kusahau mlipotoka na muwekeza nguvu zenu ktk kuondoa umasikini wa mtanzania mlipa kodi.

    ReplyDelete
  2. hapo juu nakusapoti kabisa yaani hadi hasira. Bwana Michuzi TAFARADHI SANA Tunaomba ufanye juu chini hawa viongozi wetu wapate ujumbe wetu hii nchi imezidi kutunyanyasa kiwaziwazi na kufaidi wao tu. Wanang'ara mafuta manzingira yanakuwa ya hali hii hebu ona shetion au kijiji gani makao makuu loo bora tubaki huku tulipo. Bunge haina Blog???watafute tutoe michango yetu !@!!!

    ReplyDelete
  3. Michuzi kwanza naomba nikupongeze kwa taaluma yako ya photojournalism, mimi nipo TOBAGO, nimemshirikisha rafiki yangu kuona picha hizi kadiri ya maoni ya wenzangu hapo juu, na majuzi tu tulikuwa tuansoma juu ya hotuba ya JK pale MZA kuhusu kukandia film ya Darwin's Nightmare, yaliyoonyeshwa katika film hiyo juu ya MZA hayana tofauti na usambamba wa picha zako hizo, ni hali mojaa katika mazingira tofauti na watendaji tofauti, nasikitika kwamba hali hizi mbili zinaweza kukanushwa na viongozi kuwa ni uongo wakati tunaachotakiwa kufanya ni kutumia "uongo" huo kujenga maisha bora kwa kila Mtanzania. Asante sana Michuzi.

    ReplyDelete
  4. Je mama kama huyu aliyeonyeshwa na michuzi hapo juu anaweza kumudu gharama za kumpatia mwanae elimu ya chuo kikuu ambaye amefaulu katika kiwango cha daraja la pili(DIVISION TWO)??????

    Kutowapatia vijana mikopo ya elimu ya juu waliofaulu katika daraja hilo kunafanya porojo za kuondoa umaskini nchini mwetu kua NDOTO!!!!

    ReplyDelete
  5. Ukivuka hatua hamsini kushoto utakuta hoteli wanayolala hao first class citizens.
    Wameikarabati kwa bei mbaya wakati wananchi wanaumia

    ReplyDelete
  6. Nakubaliana na nyie wote, pia stesheni inatilisha aibu kwa wageni. Hivi kweli tunaweza kusema hapa ni makao makuu. wapakae rangi basi.

    ReplyDelete
  7. Bwana Michuzi unapo chukua hizi picha kama ya huyu mama unapata ruhusa yake kuiweka katika blog yako? Sidhani kama huyo mama anapendezwa na kitendo chako cha udhalilishaji kumweka hadhalani dunia nzima imwone. Jaribu kuweka utaratibu wa kuwapiga picha watu, ni vema pia hawa watu unaowapiga wakakubari kupigwa picha naukawaeleza bayana matumizi ya hizo picha. Nadhani unalielewa hilo kwa kina kabisa.

    ReplyDelete
  8. kaka anony hapo juu nimekuelewa na nakutaka radhi. yaani, ingawa nilipata 'b' kwenye midia law, uelewa wangu mdogo unaniambia kwamba sijakosea, hasa kwa vile hiyo ni kweli biyondi rizonebo daut kuwa huyu mama alikuwa stesheni ya dodoma, ambayo ni sehemu ya pabliki, na sijamdhalilisha kwa kuwa hiyo ni hali halisi na ina pablik interesti kama ambavyo maoni mengine (ya maana zaidi ya yako) yanavyonena... samahani inglishi iz not richebo mwenzio, vinginevyo ningeng'anga zaidi.

    pia hebu fikiria nikiwa mpirani ama dansini ama hata mtaani na nataka kuomba ruhusa kabla ya kupiga picha itakuwaje...

    ReplyDelete
  9. nakubaliana na wewe mzee michuzi, sidhani kama umekosea kwa picha kama hii. Kuna wakati kulikuwa na heated discussion kuhusu kupiga picha za watu in public na sheria ikaconclude kwamba in public, unaweza kupiga picha kama hizi, especially kama hazina interest ya kuzifanyia biashara.

    Hata hivyo, nadhani zile picha ulizopiga kwenye club dodoma ungeomba ruhusa. Mimi kama ningetokea kwenye zile picha bila ruhusa yangu ningeweza kukushitaki, na uwezekano wa kushinda ni mkubwa.

    ReplyDelete
  10. Hii picha ya Dodoma railway station inaonyesha ni jinsi gani wakubwa wanavyotumia pesa vibaya. Angalia magari ya Wabunge, Jengo la Bunge and compare them with the Railway Station? These people are not working for you and I in Dodoma or Dar! They're working for themselves!

    ReplyDelete
  11. mimi nakubaliana na watu wote waliotoa maoni yao hapo juu.lakini natatizwa kidogo na ni hatua gani tunayoichukua ili kuona haya mambo yote yanayotuumiza yanafanyiwa kazi.
    ukweli ni kwamba hawa wabunge wote whether ni vijana au wazee wengi wao wapo kwa faida zao.sasa watanzania mimi nadhani as a group ambayo imekusanywa pamoja kupitia kwenye hii blog ya bwana michuzi tufikirie nini cha kufanya ili kuyaondoa haya maonezi yote yanatokea ndani ya nchi hii.
    kuna anon hapo juuu ameongelea suala wanafunzi wa watoto masikini kupata division two na kutolipiwa fee?
    kwa hili mimi nimechanganyikiwa kabisa maana wakati mheshimiwa kikwete anatangaza sera zake wakati wa uchaguzi moja wapo ilikuwa ni maisha bora kwa kila mtanzania.sasa hili la kutowapatia elimu ndugu zetu linaangukia wapi?
    sielewi kwa kweli.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...