Home
Unlabelled
makwetta
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
miaka 30 yote na sijawahi kumsikia, yaani watu kama hawa inaonyesha hawajafanya lolote la maana bungeni na hawastahili kuwepo, in short watolewe ! michuzi mie nadhani huyu ndio utachukua nafasi yake 2010 !
ReplyDeletewewe mtoa maoni hapo juu anony 10:24 sijakuelewa, unasema hujawahi kumsikia au hajafanya lolote. Kama wewe bado kinda uliza kati ya hiyo miaka ni mingapi alikuwa waziri na kama ujamsikia miaka yote basi wewe ulizaliwa 90s. Alikuwa waziri 1982 - 1995.
ReplyDeleteHuyu ni mmojawapo wa watu walioidumbukiza nchi yetu sana. Nina uhakika huko baadae kati ya watu tutakaohitaji kuvifanyia uchunguzi vichwa vyao ni pamoja na huyu tusibiri tu muda ufike.
ReplyDeleteDuuh mnyalu kafanya bunge ni biashara yake binafsi yaani siamini kaanza ubunge toka sijazaliwa hadi sasa najiaandaa kugombea kiti changu duu bongo bwana
ReplyDeleteKumbe MOI kinda, nawa miguu ukalale kima wewe.
ReplyDeletemaskini makweta alimkosea nini Mkapa? nikajua labda watamuonea huruma this time kumbe tena ana bifu na kikwete pia mhh kweli nyee iumisa swela ela be kokoo mwee ila kwa kifupi wewe anony wa hapo juu nataka nikuhakikishie kwamba makweta haachi ubunge mpaka anakufa ana historia njombe huyo alijenga mashule hivyo kumuenzi ni kumuachia nafasi mpaka atakapotaka mwenyewe kuacha au Mungu atakapompumzisha...
ReplyDeleteAnony wa august 15, 2006, 12:03, keep it nimependa comments zako mzee
ReplyDeletebaba-ko asante kwa kuniita kinda inaonyesha ni kiasi gani kichwa chako kimesha anza kupoteza uwezo wa ustaarabu. pole sana ndugu yangu....nilikuwa nadhani ukubwa ni busara ila nasikitika kungudua kuwa sio kwa kila mtu....
ReplyDeleteI concur with Trio Kaka. We do not have the right to disparage Makwete's long tenure in parliament while we, wananchi, are the ones who DEMOCRATICALLY keep him in office. Additionally, it is logical to put cap to tenures of higher offices, like President's, PM etc. But these constituency Member of Parliaments let them RULE OVER us if we so choose.
ReplyDeleteA bit of travia: Tam Dalyell took over from Ted Heath as 'Father of the House'.
Whether or not they are capable to handle the intricacies of the modern Politics is another matter! Some have been photographed taking a snooze in the middle of the Parliamentary sitting.
Fadhili, huyu jamaa alinunu Mashamba kule kwako njombe kutoka kwa Wamishen, ambayo yanasadikiwa kuwa na Dhahabu .Sasa akianza kuchimba huyu ndio tutaujua umasikini wake..
ReplyDeleteNadhani wote mtakubaliana na mimi kwamba wenye matatizo siyo huyu bwana MAKWETA ila watu wa jimbo lake ndiyo hasa wana matatizo kwa mtazamo wenu. Huyu bwana ni MSOMI anawakilisha jimbo lake la uchaguzi BUNGENI kwa miaka hiyo 30+ kwa sababu watu wa jimboni kwake bado wanaimani naye kuna vingunge wengi tu wamepoteza ubunge baada ya wananchi wa hayo majimbo kuona hawafai Mfano kina Pius Ng`wandu na wengine. Sasa kama wananchi wake wanaona ndiyo mtu anaye faa kuwaongoza hata akikaa miaka 50+ jimboni kwake sioni sababu ya nyie Vihiyo kumsakama. Nendeni Jimboni kwake muwa convince wapiga kula wawachagueni kuwa wakilisha bungeni kama mabwana mdogo akina Serukamba walivyo fanya kwa akina kaborou wa jimbo la kigoma mjini. Mzee Malecela alikataa kugombea katika awamu hii lakini wananchi wa jimbo lake walienda kumchukulia form za kugombea kwa kuchanga pesa wenyewe na akapita ubunge sasa sioni kama huyu bwana Makweta kama anatatizo lolote. Mimi namsaport kwa nguvu zote ukizingatia kwamba anaimani kubwa kwa wapiga kula wake. Ukifika muda hawezi kuwaongoza wananchi wake atapumzika. Pia sioni sababu za msingi kusema eti ana bifu na Mkapa ama kikwete Tanzania ina wasomi zaidi ya million 5 sasa sasa hizi nafasi za uwazili ziko kama 40+ tu siyo lazima kila mtu arudi eti kwa sababu amekaa madarakani muda mrefu ama alikuwepo katika awamu fulani? Mheshimiwa Kikwete anamamlaka ya kuteua mtu yoyote anayeona atamfaa katika position furani kumbe katika hao watu 5 millioni atachagua 40 tu sasa ambaye ataachwa siyo swala la bifu ni kwamba ni utawala mwingine na mambo mapya. Hata wewe mwenyewe unaye lalamika leo ukiwekwa madarakani utafanya vivyo hivyo. Acheni malalamiko someni na ninyi mpate madalaka mwendeleze nchi yenu. Jackson Makweta ni msomi na ana fanya kitu ambacho jimbo lake la uchaguzi linapenda. wewe mpiga debe jiangalie upo wapi na unafanya nini, huna jimbo na wewe ukaliwakilishe? Je umefanikiwa kwa kiasi gani mpaka umwone makweta hafai? Ushauri Nenda shule ukatoe UJINGA then you can come back and talk trash...
ReplyDeleteKabada Kabinda ni mtu mzuri wa kutoa hoja vile vile ni mtu mzuri wa kuchanganya mambo. Kwa mzee makweta kuna shule ngapi za sekondary?. Kipindi cha miaka 30+ watoto waliosoma/waliopata elimu kupitia mgongo wake walitakiwa kuwa ni kama kata tano hivi, Je ni wangapi wamekwenda shule mpaka Elimu ya kubobea?(nafikiri utakuwa umeelewa hapa), Tukilinganisha kwa mfano na Mwandosa kwenye jimbo lake wapi zaidi? Mwandosa amekaa muda gani ukilinganisha na yeye? Je unakumbuka malalamiko yaliyokuwa jimboni kwa Makweta wakati wa uchaguzi. Ulisikia wananchi walisemaje? Nafikiri ashukuru mzee wa watu na wengine kama yeye watanzania bado wanaipenda/Wanaogopa CCM, pia Rais Kikwete alikuwa chachu katika kuwabeba la sivyo wangelisombwa na Elinyinyo.
ReplyDeleteNashukuru kama utakuwa ulifanya analysis wakati wa uchaguzi na kugundua kuwa wabunge wengi walipita kwa mgongo wa Mweshimiwa Rais ambaye watu walikuwa na imani naye, akiwepo mweshiwiwa aliyeko hapo juu.
Pia suala la Mzee malcera, nafikiri kidogo ukizungumzia huyu inahitaji ujasiri wa aina yake kwenda kuchukua form kwenye jimbo lake ndio maana wananchi wanaamua kumchukulia tu. Hila yote tunaitaji maendeleo akiyaleta siyo tatizo.Kwa kweli malicera mpaka atakaposema hataki tena ndipo atajitokeza mtu.
nasikitika kwa kuchelewa kuona hoja iliyo kuwepo mezani, kwani nafikiri ningewapa mfano mzuri juu yake kwan mi natoka katika jimbo lake. Kuna mmoja ameeleza vizuri tu juu ya viongozi wengi wanao changuliwa tz kwa kutumia njia zisizo halali. naamini hata wanao mtetea Jackson wanaelewa vivuri tu mazingira ya rushwa yaliyopo TZ na jinsi vigogo wanavyo yatumia vizuri kubakia madarakani, kimsingi tangu mwaka 1975 alipo ingia bungeni kwa mara ya kwanza mpaka sasa alicho kifanya hakilingani na umri alio kaa bungeni.km mlifuatilia uchaguzi wa safari hii kama si kifo cha mgombea mwenza wa Chadema sijui kama angekuwepo bungeni tena maana hata yeye anasema hilo. Ktk kipindi hicho ndipo CCm ilipo peleka nguvu zake zote na baadhi ya watu kutishiwa kuwa amani ingeharibika endapo asingechaguliwa. Ukienda kijijini ukawaambia amani itapotea wote wanabadili msimamo, hata kama ulikuwa unawadanganya
ReplyDeletemichuzi uko safi,
ReplyDeletemsg zote zinatokana na uelewa wa mtu, kwangu naona ni bomba kuwashtua wazee, kwamba kukimbia ni rahisi unapokua kijana, maisha yanapita tu na wewe sapoti jinsi unavyoweza ktk nafasi uliyonayo. fanya kazi bila kusukumbwa hata ikiwa ni kazi yako binafsi,