Inside a Chagga tembe in in one of Moshi rural's 'Vihanga'

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Hao ng'ombe wanaonekana wamenona kweli kweli! Michuzi, give us more pics of rural lifestyle please!

    ReplyDelete
  2. Hivi kweli kuna sababu hasa ya Kisayansi kwa ngo'mbe hawa kufugwa ndani ya vibanda?...
    Aaaah! ndio Uzungu tena mfugaji kapata Phd yake Ulaya basi hata kufuga ngo'mbe wetu wenyewe (Zebu)ni umaskini.

    ReplyDelete
  3. wewe anon hapo juu kuna sababu nyingi tu za kufuga ng'ombe ndani ya banda, mojawapo ni uhifadhi wa mazingira.

    ReplyDelete
  4. Kaka,
    picha zako hazina viwango babu,unakuwa kama amateur bwana wakati umefanya hii kazi kwa miaka sijui mingapi! Tunategemea kujifunza taaluma hii kupitia wakongwe kama wewe lakini kwa kweli picha zako naona hazina viwango kabisa.Yaani mashindano ya blogu za picha Michuzi hatuwezi kukuingiza kabisa.Changamka mzee.Na ni maoni tu,constructive criticism babu,au sio?

    ReplyDelete
  5. we anony hapo juu... fungua basi we blog yako yenye picha zenye viwango

    ReplyDelete
  6. Tatizo letu wabongo tumejaa ushabiki tu,ndio maana hatuendelei.Kumuambia Michuzi aboreshe viwango ili awe proffessional zaidi haina maana mbaya kama unavyodhani wewe.Pia haina maana kama kitu kibaya basi jawabu ni wewe nawe kuanzisha chako.Kama kitu hakina viwango vya kutosha hatuna budi kusema.Naamini mwenyewe Michuzi atakuwa ameelewa na atalifanyia kazi suala hili.Upambe nuksi.

    ReplyDelete
  7. Asante sana Michuzi kwa kunikumbushia kwetu, yaani we acha tu naomba uongeze picha kibao , achana na huyo anae kuambia picha zako hazina viwango ana lake jambo kama sijakosea naona ana kuonea donge, ukisikia viumbe wazito ndo huyo, songa mbele Michuzi.

    ReplyDelete
  8. we anony wa 2 (2:58PM). Hata kama kungekuwa hakuna sababu za kisayansi; tatizo liko wapi la kujenga kibanda?

    ReplyDelete
  9. enhee we unayedai viwango. Hebu tuelezee basi mapungufu yako wapi

    ReplyDelete
  10. Michuzi,
    Ukiamua kuwasikiliza wapambe,fanya hivyo.Ila kama unataka kuboresha zaidi utaalamu wako(tayari unao kiasi) basi sio mbaya kama ukiangalia blog za wengine za picha kama hizi hapa

    http://photoblogs.org/hot/

    Au angalia wenzio kama kina damonce.com nk.Mimi nia yangu ni kukujenga zaidi Michuzi,sio kukuponda kama ambavyo wapambe wako wanadhani.Kazi kwako mzee!

    ReplyDelete
  11. maneno kama
    - picha zako hazina viwango
    -unakuwa kama amateur
    -mashindano ya blogu za picha Michuzi hatuwezi kukuingiza kabisa
    ndio naona yamefanya baadhi ya watu wasione kama unatoa constructive criticism bali uonekane unaponda.

    Kupeana mawazo ya kimaendeleo na kukosana ni vizuri, lakini inakuwa vema ukijaribu kutumia maneno kwa namna ambayo mtu ataona unakiheshimu alichokifanya kwa sasa, na kisha kutoa maoni kipi kirekebishwe.

    Maneno uliyotumia ndugu yangu naona yalifanya watu waone kama unajidai we mtaalamu na unaponda tu. Na naonelea ingekuwa vema ungemtumia michuzi barua pepe kumpa ushauri wako kwa faragha.

    Sio upambe au upinzani, ni ushauri wangu tu kwako anony hapo juu

    ReplyDelete
  12. Peter,somo la busara ulisomea wapi? nategemea watu wanajifunza kupitia kwako, keep it up, Mungu ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  13. Huwezi kumwambia Michuzi kwamba picha zake hazina viwango bila kumwambia aongeze viwango kwenye nini

    ReplyDelete
  14. Michuzi, unanikumbusha mbali sana maana na mimi nilikuwa mfugaji wa ng'ombe wa maziwa kama huyo mzee wangu hapo juu

    ReplyDelete
  15. Peter,
    Nashukuru kwa busara zako.Ninachofurahi ni kwamba kimsingi wengi tunakubaliana kwamba Michuzi anahitaji kuongeza zaidi ujuzi wake.Hilo ndilo la msingi.

    ReplyDelete
  16. Anony 11:24, 11:57 and others with similar comments. I accept the fact that my work is below standard and that’s why I have only over a 150,000 visitors, as compared to those with the so called first class photos.

    The problem is that I do this for fun and try to make you out there afford a smile or two as you hark back to what is happening back home, NOT to compete.

    After all what do you expect from something that you get free? Are you aware that posting a photo of over 300 dpi takes ages? Kindly bear with me as I am quite sure you are aware that what’s good for the goose is bad for the hen…

    Thanks, anyway, for visiting this blog and taking the trouble to jot down some comments.

    ReplyDelete
  17. Kwa mara ya kwanza Peter umemwaga busara tu. Sasa nitaanza kusoma comments zako tena. Nawewe mporipori unayedai kimsingi wengi tunakubaliana kuwa michuzi anahitaji kuongeza ujuzi sijui kiwango, tafadhali usitutilie maneno akilini mwetu. Hayo ni mawazo yako

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...