najifunza kuogelea

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Haya bwana ogelea tuu lakini angalia usizame.
    Bwana Michuzi naomba umwambie JK kuwa nchi yetu haina jeshi hapo, jeshi letu ni zee, limechakaa na kiwango finyu. Kwa wale wanaofuatilia mambo nadhani wanakumbuka jinsi mwaka jana Musaba aliposema tukimletea usenge na kuingilia mambo yake ya ndani, basi atatuchapa. Wengi mtashangazwa na hili lakini ukweli ni kwamba Jamaa jeshi lake liko Gado kuliko letu kwa hivi sasa. Mwambie JK afanye mkakati, ingawa hatuna adui, hii isitufanye tuwe dhaifu.

    ReplyDelete
  2. Ndio museveni jeshi lake kali lakini sio kuzidi Tanzania nchi iliyo kubwa ktk East Africa.

    Jeshi la Tanzania linatumia zaidi ya US Dollar 21.6 Million kwa mwaka ktk kulipatia nguvu. Sasa museveni anachofanya ni kupokea pesa za misaada anayopewa na nchi kama UK kwa ajili ya maendeleo ya taifa na yeye ana amua kununua ndege za kivita na silaha nyingine kutumia hizo pesa.

    Mwambie museveni akitaka kujalibu kupigwa na mkubwa aweze kwanza kumpiga Joseph Kony ndio aje kwetu maana ime mchukua decades kupigana naye na ameshindwa na kuamua kuomba truce naye sasa ataweza Tanzania? Mwambie kwamba sisi ndie tuliye muweka madarakani na tuna uwezo na nguvu za kumtoa dakika yoyote sasa aweze kuheshimu wakubwa! Hasione ana chezea RDC (République Démocratique du Congo au The Democratic Republic of the Congo) na Sudan ndio aweze kuzani ndio sawa sawa na Tanzania basi atakuwa amepotea.

    Tanzania ni moja ya nchi iliyo fiti kijeshi ktk Africa na tupo fiti ktk East Africa.

    Ukitaka kujua uondo wa ngoma ingia ucheze, Ukitaka kujua nguvu za Tanzania chokoza nyuki, Ukitaka kujua makali ya Tanzania iba ardhi ya mipaka ya Tanzania utakiona cha moto. Ukitaka kuona mvua kali isiyo isha, vamia anga au ardhi ya Tanzania.

    Nashukuru.

    ReplyDelete
  3. Faza MK hapo juu, unaongea fantasy babaake. Musaba yuko fiti kuliko Bongo kwa hivi sasa. Na ukikata kuamini kuwa Bongo sasa hivi heshima yake imeshuka, ziwa Nyasa limeshachukuliwa na Malawi. Mara ya Mwisho bongo umesikia lini jeshi linaajiri wanajeshi wapya?

    ReplyDelete
  4. Michuzi vua basi nguo hizo uvae nguo za kuogelea nije nikufundnishe.

    ReplyDelete
  5. Aaah kaka michunzi mbona umetoa ile picha ya wewe na my nanii wako, umeogopa wajanja awsije wakaanza kubeep. lakini ndio vizuri kila mtu analinda kilicho chake....

    ReplyDelete
  6. Michuzi yaelekea wewe ni mtaalamu sana wa miondoko ya mayenu,naona umepiga style hiyo mpaka baharini.

    ReplyDelete
  7. Unajifunza kuogelea au unajifunza kutembea majini?

    ReplyDelete
  8. sawa sawa blaza hujifunzi kuogelea kwa maji ya unyayo, tusipelekanepelekane Michuzi Kaka!!

    ReplyDelete
  9. Hivi inawezekanaje mtu uzaliwe Dar-es-salaam, na usiweze kuogelea? Au ulikuwa unaogopa chunusi utotoni? Au michuzi umezaliwa Sigimbi nini?

    ReplyDelete
  10. Kuogelea ni mchezo mtamu sana kama football, kikapu, drafti, chesi na mingineyo. Kwa baadhi yetu tuliozaliwa maji chumvi tumepata bahati ya kuzaliwa majini, kwa hiyo kama alivyosema anony hapo juu, kama ulizaliwa karibu na maji na hujui kuogelea basi huna wa kumlaumu isipokuwa ni wewe mwenyewe.
    Siri ya kuogelea ni kwamba, tunaogelea ndani ya maji na siyo juu ya maji. Watu wengi wasiojua kuyakata maji ukimuingia majini tuu basi anataka awe juu ya maji kitu ambacho hakiwezekani. Ongeza bidii kaka michuzi.

    ReplyDelete
  11. Hakuna cha kuzaliwa sehemu za bahari wala nini watz kwa kifupi hatuna utamaduni wa kuogelea,hili labda liwe moja ya somo mashuleni,lakini watu tumezaliwa pwani na nakumbuka tunaenda beach kutembea ukiogelea kibano unachpewa home hurudii tena,labda kama baba yako alikuwa mvuvi na akapenda urithi uvuvi sasa akawa anakufundisha

    ReplyDelete
  12. wee anony hapo juu acha kuongea takataka hapa, kama kwenu hamjui kuogelea huo ni uzembe wenu na hasa kama kweli umezaliwa pwani. Itawezekanaje uzaliwe pwani halafu usiweze kuogelea?

    ReplyDelete
  13. kwani uonge watz wengi wamezaliwa pwani na hawajui kubisha unabisha nini wabongo kwa kubisha,mnabisha mpaka ishu kama ya mapanki wakati ni kweli

    ReplyDelete
  14. mi sikuzaliwa pwani ila nilihamia nikwia mdogo na nimejifunza kuogelea toka siku nyingi.. lakini kilichosaidia ni kuwa skauti. Tulifundishwa tukiwa camp, na baada ya hapo ilikuwa tunatoroka sana tukiwa wadogo mimi, bro na washkaji wkenda bichi ingawa ilikuwa maza akishtukia tu kazi mnayo!!! hehe...
    ila ukweli ni kuwa kuna waTZ chungu nzima Bongo hawajui kuogelea. Nina marafiki zangu tani tulikuwa tunaorganize trips wakati nipo shule Moro kwenda sehemu 1 inaitwa Tangeni; na pia Bongo tulikuwa tunaenda Kigamboni sometime, na masela walikuwa wanashangaa mzee nikiyavaa maji wao bila bila. Na wamekulia Dar kwenye bahari.

    Na kuna walitoa comments za watu kuzaliwa pwani.. unajua ukitembea mikoani (kwenye miito kama moro, etc) watoto wanaogelea kuliko Dar.
    Ukiacha watoto wa mitaa ya bonde la msimbazi, watoto wa kigamboni na msasani kidogo. Wabongo wengi hatujui kuogelea.
    Tofauti na wenzetu Uganda na kenya hata baadhi ya shule za public wana pool au kama hawana shule inaweza organize trips every now and then kwenda ktk public pools. Tofauti na sisi, tunaona maji ni ya wavuvi tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...