chifu mazengo wa wagogo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Tutengeneze sinema kuhusu machifu wetu. Hivi kuna sinema inayohusu historia yetu kweli? Na si zungumzii zile sinema za Mogambo na, African Queen na Hatari za Mkoloni.

    WaAfrika Kusini wanayo sinema ya Shaka Zulu na zingine kuhusu Zulu wars.

    ReplyDelete
  2. Naunga mkono kabisa wazo lako Chemi che-Mponda.Hata documentary za hawa machifu sijawahi kuziona. Labda ni maswala ya kukosa ma producer wakibongo na pia gharama za kutengezea hizi filamu. Kwa maana waigizaji tunao, na ma Directors tunao.

    ReplyDelete
  3. Kaka Simon,

    Huenda Tanzania Film company walitengeneza. Ingekuwa vizuri kujhua sinema zao ziko wapi. Tatizo ni kuwa sinema zao ziko kwenye reel na joto la Bongo, huenda zimeoza sasa. Kama zipo basi wazipeleke kwenye restoration.

    Ni kweli, kutengeneza sinema ni ghali sana.

    ReplyDelete
  4. Hapo kwa Chifu Mazengo umenikuna kisawasawa nimewapelekea taarifa wana wa uzao wake. Sasa humo namo ndugu yangu hebu tuangushie series yao Kina Mtemi Mkwawa, Mirambo, Chabruma, Marealle, Makwaia tena huyu ndiye mjumbe/mbunge wa kwanza wa Kitanganyika katika Legislative Council of Tanganyika akiwakilisha Federation of Sukuma People, na wengineo wa kariba yao. Pia kama inawezekana naomba utuletee picha ya Kinjeketile Ngwale, Mmatumbi aliyebuni na kuongoza 'sokomoko' la Maji Maji. Mjomba hii mishababi ilikuwa ni moto. Mungu Awalaze Pema, Amen.

    F MtiMkubwa Tungaraza.


    Post a Comment ~ Rudi Mwanzo

    ReplyDelete
  5. Watu na hoja zao, mitusi siioni hapa...hivi tatizo ni shule au....?

    ReplyDelete
  6. Tatizo ni u-toto. Ukitaka kujua hilo angalia zile picha za shule za Tambaza na Shabaan Robert ndio utajua. Utaona mara miaka sita pale 1998- 2003, mara form six 2004 na kadhalika. Sasa unategemea nini hapo?

    ReplyDelete
  7. watoto wa mikocheni!! mnajijua babu yenu huyo......!!!

    ReplyDelete
  8. hivi huyu ndio babu yao kina Mwaja na wengine,bado wako mikocheni mnaofahamu au wapi?

    ReplyDelete
  9. Fide, mti mkubwa, vipi babu, mbona hujawataja kwenye LEGCO wajumbe wengine kama kina Chifu Shangali, Chifu Fundikira, kina marehemu Paul Bomani, Chifu Adam Sapi? hawa wote nao walikuwamo katika hilo baraza.

    ReplyDelete
  10. LEGCO alikuwapo pia Mzee George Kahama. Nimemtaja Chifu Kidaha Makwaia kama Mtanganyika wa kwanza kuwa mjumbe wa LEGCO.

    Mtaala wa somo la historia unapaswa kuundwa upya ili kuwapa Watanzania ueleo wa kina wa Historia yao. Tukilisoma somo la historia kama lilivyo sasa linaenda mwishoni mwa miaka ya 1880 wakati wa mapambano na Wajerumani, linarukia 1905-07 vita vya maji maji, linaruka hadi 1954 kurudi kwa Mwalimu toka Edinburgh na kuibadilisha TAA na kuanzisha TANU, halafu uhuru, baadaye 1964 mapinduzi ya Zanzibar na Muungano, na kuishia 1967 Azimio la Arusha. Kabla na katikati ya matukio hayo kunaachwa na mapengo mengi sana ya kihistoria ambayo ni muhimu sana katika kujenga dhana ya utaifa na kitaifa.

    F MtiMkubwa Tungaraza.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...