kila mwaka wakati wa baraza kuu la umoja wa mataifa joji kichaka hukaribisha rais mmoja toka kila bara duniani kwa mazungumzo. safari hii toka bara la afrika jk ndo aliyealikwa. doooh! acha watani wetu wa jadi waje juu kwa wivu. mara ooooh, jk anatuchamba, mara ooooh, waandishi wa nchi yake wanamlamba miguu. yote hii ni ile mikelele ya mkosaji. hivyo wabongo msiambiwe chochote na yeyote. mambo yenyewe ni mwendo mdundo tu... na bado - watasema sana, we ngoja tu! hahahaaaa!!!!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. ALIECHORA KATUNI NI MWENZETU.....YAANI MTANZANIA ANAEFANYA KAZI HUKO KWENYE HILO GAZETI LILIOTOA HIYO KATUNI....

    ReplyDelete
  2. Ni dhahiri shahiri, hili swali linaweza kuleta uharibu wa mambo hasa kwenye jumuiya yetu. Nimefuatilia kwa karibu mno haya malumbano, kweli yanadhihirisha namna mvutano uliopo kwa baadhi ya raia wa Kenya na Tz. Hivyo, kwa vile sasa tupo kwenye harakati za kuimarisha diplomasia ya kiuchumi,vi vyema tukawajibu hawa jamaa kiplomasia huku tukiangalia saana maslahi ya Tanzania kwa ujumla. Zaidi ya yote is better to stay silince than arguing with a fool one

    ReplyDelete
  3. Dooh Kikwete umekaa kama mkojo umekubana vile? Tulia huyo ni rais kama wewe ingawa ni Big Boss lakini tulia kwenye kiti, ni vizuri kuwa free wakati wa maongezi siyo kama tumbo linakuuma ama unataka kujamba! Kwa ujumla nakupa FIVE maana huyu Jamaa big boss mpaka amekuzimia lazima kazi yako ni nzuri. Kibaki naomba mumwache tu, huyu jamaa kajizeekea watu wanakula kila kitu Kenya hajui where to start kazi kusinzia tu mikutanoni, that is another Banda. Juzi Juzi Senator Barack Obama alikwenda Kenya hakutaka hata kuonana na Mwai akaishia kuonana na kina Kalonzo Msyoka wa Upinzani sasa huyu Babu nasikia kapandwa na pressure ile kinoma. Kikwete Hongera kazi nzuri, keep it up brother you are the only good guy we got in AFRICA NOW!!
    Michuzi in your part keep doing a good job it is your job to let the people know how you personally think of Kikwete and that is what you are doing so far and everyday. people will always say something negative about you but it is good you accept there critics and move on, when they get tired they will stop.

    ReplyDelete
  4. Yes, but the question here we should ask ourselves, is, was JK correct in commenting the political status of another country? I believe diplomatically it was not correct of him to comment like that.

    ReplyDelete
  5. Michuzi, hawa watani zetu siunajua tumewaacha mbali sana Wenzetu hawa majirani bado wako na zile enzi za kuchagua rais kutoka kabila fulani wakati sisi hatupo kabisa katika karne hiyo, hawa jamaa tusubiri tu kesho si ajabu wakawa kama Burundi ama jirani zao Somalia...
    Basi na wao wamlambe miguu Mtukufu Mwai Kibaki na zile fungus kwenye miguu doooh!!

    ReplyDelete
  6. rais yeyote anaweza ku comment any political situation za nchi nyingine, bush amekuwa aki comment political situation za irani,iraq,cuba,venezuala, nk. iran ime comment kuhusu britain na marekani, india ime comment kuhusu pakistan, nyerere alicomment kuhusu marekani na zaire wakati wa mobutu kumbe ni halali marais kuongerea kuhusu political situation za nchi nyingine, ukumbuke hata bush aliongea kuhusu hali ya kisiasa ndani ya urusi/chechnya juzi juzi sasa kwa nini kikwete asiongee kama anaona kuna issue/moto unawaka kenya na sisi ndiyo majirani?

    ReplyDelete
  7. Waandishi Wakenya wanamsema vibaya Raisi wetu sababu aliwatimua wakenya waandishi wahabari waliokuwa wamejificha kwenye lundo la takataka za magazeti bila vibali vya kuishi nchini,Pia wana hasira sababu majambazi yao ya Kenya yameng`ang`aniwa kooni na Kikwete wakati nchini kwao Kenya mla Rushwa mkubwa Kibaki aliyaacha yatambe !!!Wakenya hawaingiii kienyeji kama walivyokuwa wamezoea sasa wana hasira na Raisi Kikwete! Wakenya mlie tu.

    ReplyDelete
  8. Ilikuwa halali Kabisa Kikwete kuzungungumzia Kenya sababu kuna uwezekano mkubwa wa Kenya kuzalisha wakimbizi watakaofurika Tanzania wakati wa uchaguzi mkuu wao unaotarajiwa kufanyika mwakani kutokana na watu kuchoka serikali iliyo mikononi mwa wakikuyu toka uhuru.Siyo siri hali Kenya ni mbaya kwa wazi na kwa siri.Bush na Kikwete walikuwa na haki kuzungumzia nchi ambayo muda si mrefu yaweza geuka kuwa Rwanda au Burundi.Siasa zao za kipumbavu ndani ya nchi zinaelekea kuleta madhara na usumbufu kwa majirani.Hongera Kikwete kwa kuliongelea na Bush achana na mpuuzi Kibaki!!

    ReplyDelete
  9. wakenya hawana maana watabakia hivyohivyo wakati jk anapeta.na jk kasema hana mpango wa kuwajibu .yaani kelele za za...hazi.....,wameona jk anauzika ukianzia sura personality alafu ni kijana,sasa huyo wa kwao anayesinzia kila saa mpaka aamshwe pole zaooooooo ha ha hhhhhhhhaaaaaaa uwiiiiiiiii

    ReplyDelete
  10. we kaka bingwa uliyesema hapo juu kua Kikwete amekaa kama anataka kujambajamba umenifurahisha kweli, hapa mbavu sina

    ReplyDelete
  11. Wakenya walio na akiri ndogo ndio wanamsema vibaya JK, Mimi nimekutana na wakenya wengi sana baada ya hiyo comments. wanaoelewa siasa za dunia/dunia hii inavyokwenda hawawezi kumulaumu JK pale anapokutana na kilanja wa dunia na kuanzisha mjadala fulani.

    Wengi wanakubali kuwa kama umekutana na Bush akaanzisha mada fulani huna jinsi ya kumpinga isipokuwa unazungumza kadili unavyoweza halafu yanabaki pale pale. Huwezi kupoteza muda mwingi kupingana naye.

    Pamoja na kwamba wakenya waliowengi wanachukulia kwamba marekani inawaingilia kwa sababu kidogo kale ka sefu kao wanaona kanaelekea pazuri kiasi kwamba hawana shida na marekani.

    Kwa hiyo marekani imeishalijua na ndio maana inawapiga vita. Lakini vile vile wanaoelewa msimamo wa Tanzania pamoja na kwamba hatujawa na uchumi imara sana hila wanajua kuwa bado tuna nguvu katika jumuiya ya kimataifa na kiburi pia. Ambacho ndicho rais kama JK anasimamia. Hiyo haiwezi kuisha kwa sababu baba wa taifa alituachia msingi huo. hata hivyo sitegemei waandishi wa kenya wamseme vizuri JK maana walimuanza zamani.

    Pia walifikiri katika kuanzisha Africa mashariki wangeweza kutuingilia haraka kupata oportunities lakini pia wamegundua tunaweza kupambanua mambo na hatuna haraka na kaujanja kao.

    Anaway ni jirani zetu lakini pia wao wana tabia mbaya sana wewe watu wakutoka sehemu tofauti hawasalimiani. wala hakuna haja ya kuwajibu wakenya waache tu na pamoja nasi kuwa na matatizo yetu lakini wao yako mengi sana kutuzidi.

    ReplyDelete
  12. Jamani hila nafikiri mimi Michuzi na wanablog kenya media imetuchallenge vibaya sana na ni dhiaki kabisa mpaka nasikia uchungu. Nafikiri hiwe changamoto kwa watanzania na raisi kikwete na wadau wote hii ni dhiaki let us wake up jamani watanzania fanyeni kazi nimesoma magazeti mengi nimejisikia vibaya sana, kizunguzungu.

    Story mojawapo"East Africa will not survive effects of this scramble. Moreover, despite the signs that the region is moving to closer ties among its member-countries, national policies remain largely different".

    For instance, while Tanzania is moving away from its Nyerere-era socialist ideology to closer identification with the capitalist West, Kenya has been courting more of the East in recent years, especially China.

    Uganda is a mixed grill of jumbled policies. President Museveni identifies himself with socialist ideas while donning a capitalist jacket more capitalist than even the capitalists themselves. hapa kigongo.

    For Kenya, it used to be a commercial kingpin in this region, the region’s manufacturing basket, extending its commercial influence all the way down to Southern Africa. By then Nyerere’s experiment with socialism in Tanzania had bogged down development. Idi Amin was wrecking havoc on the Ugandan economy and the dastardly apartheid made sure that Southern African independent nations would not trade with the economically giant of South Africa.

    http://www.timesnews.co.ke/08oct06/nwsstory/opinion3.html

    ReplyDelete
  13. Katuni kutoka Kenya ina ujumbe mkali sana kwa TZ MEDIA.Sio kwamba wanatuonea wivu wa TZ.Enyi waandishi wa TZ Jitaidini kueleza hali halisi ya TZ na sio kila kukicha JK. Watanzania tunawategemea nyinyi kwa kuandika ukweli bila kuogopa kukosa ulaji.Kazi ya gazeti la Uhuru sasa inafanywa na nyombo vyote vya habari. TZ MEDIA msipobadilika mtakua IDARA uenezi habari ya Chama Tawala.

    ReplyDelete
  14. Uzuri wa magazeti ya Tanzania hayasubiri yapewe rushwa ili yatoe habari za chama tawala au habari za vyama vya upinzani kama ilivyo kwa magazeti ya kenya ambayo habari iwe ya chama au serikali haitoki gazetini hadi wakatiwe rushwa.Huko ndiko kuwa mwandishi mzuri wa kenya hawako tayari kuwa waenezi wa habari ya yeyote asiyetoa mshiko! Kwa kenya huko ndiyo kuwa mwandishi bora usiyekuwa na upande wowote.Wakenya kwa Rushwa au ufisadi ni kiboko!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...