Home
Unlabelled
meza
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Ni vyema viongozi wetu wa sasa wakajifunza jinsi baba yetu wa taifa alivyokuwa hapendi makuu. Sasa hivi pamoja na kuelezwa kuwa furniture watakazozikuta maofisini ndizo hizo, viongozi wetu wa sasa hivi hasa mawaziri hilo somo halijawaingia akilini kabisa. Jk aende akatembelee nyumba na ofisi za mawaziri hasa wale ambao wa mashirika ya serikali chini yao ajionee ubadhilifu uliopo.
ReplyDeleteMichu-Boy, najua wahusika wa Jumba la Makumbusho wanaahamu umuhimu huu, na wamekuwa wakifanya hivyo, ila si vibaya wakikumbushwa kwamba hii meza (kama yalivyohifadhiwa yale magari yake ya serikali uliyotuonyesha picha yake siku zilizopita), ingelikuwa murua kama vingezungushiwa uzio ili visishikwe-shikwe na wanaopita makumbusho. Bin-adam tuna vitabia na hulka ya ajabu, mathalani, yupo mtukutuku akaamua kiichora hiyo meza na kuharibu nakshi zake, ama kwa bahati itayaitwa mbaya, akatokea mmoja na kuimwagia kimiminika kama wino na kuondoa ule uhalisi wake. Kwa hiyo kaka, ukipata nafasi, naomba utuwasilishie ombi hili. Bin-Shukran.
ReplyDeleteKukalia meza moja hiyo miaka yote hiyo ni udhibitisho tosha kuwa alikuwa Mchawi.Maofisi ya serikali yana watu wachawi ambao hata wakihama hupenda kuhama na meza au viti sababu vina hirizi au uchawi wao.Nyerere naye alikuwa mchawi kwa taatifa yenu msiojua historia ya kile Kifimbo chake alichokuwa anatembea nacho alipewa na mchawi mkubwa wa Sumbawanga ambaye alikuwa Baba yake Mzazi wa Chrisant Mzindakaya ambaye ni mbunge sasa hivi ambaye anaendelea kuwanga bungeni.
ReplyDeleteAnonymous mmoja hapo juu amesea ukweli juu ya utunzaji mzuri wa historia ya nchi yetu! Hivi ni kwanini kandarasi za kujenga ama kuhifadhi mambo muhimu ya kitaifa hawapewi watu wenye uzoefu na uwezo wa kufanya hivyo? Kumbukumbu za baba wa taifa ni muhimu mno kuachiwa kampuni shenzi za ujenzi (makumbusho ya mwalimu Butiama), makapenta wa hovyo (wale waliojenga yale mabanda ya "kutunza" magari aliyowahi kutumia Mwalimu pale makumbusho Dar)na hao wapuuzi walioweka deski la Mwalimu ili watu waandike "fulani kapita hapa"! Sitashangaa kama vitu hivi havitakuwa vimejaa vumbi nk!
ReplyDeleteTafadhali sana wahusika tazameni jinsi wenzetu nchi za nje wanavyohifadhi historia zao vizuri katika makumbusho zao!
Picha hii imenikumbusha tena picha nyingine nilizoziona katika blogu hii, picha ya magari aliyowahi kutumia mwalimu jinsi yalivyowekwa katika banda pale makumbusho! na picha ya majoho ya Mwalimu kama mkuu wa chuo kikuu cha Dar yalivyo"hifadhiwa" ndani ya fremu za mbao kule Butiama. Hivi mpaka siku moja magari haya yawekwe juu ya mawe au deski hilo lipauke na kuchorwa grafiti au majoho yale yapigwe vumbi na kuchafuka ndio mtafurahi?
Tafadhali zitumike pesa za kutosha kuhifadhi historia hii! Tutoe kandarasi kwa makampuni yenye uwezo wa kusaidia kuhifadhi historia hii vyema hata kama ni aghali kwani watanzania walio wengi hawatachukia iwapo pesa zaidi itatumika kutunza vyema historia hii kwa sababu ikiharibika hatutoipata tena!
Ni yangu machache!
Asante!