jk, makamu wake na waziri mkuu na mawaziri wakubwa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 38 mpaka sasa

  1. Waziri Basil Mramba yafaa anga'tuke...Waziri Mungai yafaa anga'tuke...(ale kustaafu kwake na wajukuu)... Waziri Wassira hafai kuongoza Wizara ya Kilimo
    ...aliwahi kuwa Waziri Mdogo wa Kilimo wakati wa hayati Rais Nyerere...Huku nikimsifu kwa bahati yake, ukizingatia kuwa huyu alikuwa amemaliza darasa la saba tu...na kukumbwa na kimbunga cha Chama cha Ushirika (alikuwa Meneja wa Union ya Pamba ya Ushashi)huko katika Wilaya yake ya Bunda, Mara, na kuwa Mbunge hadi Waziri Mdogo, hakuleta mafaniko katika Wizara ya Kilimo. Alihamishiwa Washington Ubalozini alipopata nafasi ya kusoma kufikia digii ya M.A.


    Post a Comment ~ Rudi Mwanzo

    ReplyDelete
  2. JK sasa imani yangu kwako yaanza kunitoka.Si tu kwa ajili ya kfanya mabadiliko katika cabinet yako,la hasha ni kutokana na kuzirudisha kundini sura ambazo tumezichoka.Naomba nieleweke si tu kuzichoka sura zao bali pia hakuna lolote la maana watakalofanya hawa wateule wako.Bila shaka huko wanakotoka wameisha chafua na ndo maana unawaondoa,lakini hapa ni kama unahamisha uchafu kutoka sehemu moja kwenda nyingine.Wangepumzika hao waliochoka kwani kuna damu nyingi tu za moto TZ.

    ReplyDelete
  3. Policia anasema inaanza kumutoka imani mimi ishanitoka na sasa nasema hivi Tanzania hata kama unakimbia mbia za marathoni 1000km/hr haitafika wakati iendelee. naona staili iliyofanya uchumi wa tanzania kupolomoka ndio hiyo hiyo bado viongozi wa sasa wanatumia.

    watu ambao ni wakereketwa hawataweza kuvusha tanzania katika kipindi hiki kigumu cha ushindani wa sayansi na technologia.

    Mimi nafikiri watanzania wataweza kuendelea tu pale watakapoweza kujikomboa na kuondoa watu waliokuwa na mawazo ya lazima ni sisi. Kama watanzania watangoa CCM madarakani, maendeleo yatapatikana la sivyo watanzania itabidi wavumilie. Kuna mtu mmoja katabiri kama CCM itaendelea kukaa madarakani kizazi/vizazi vya sasa visahau kabisa kitu kinaitwa maendeleo.

    samahani nasema hii sentensi lakini sikutakiwa kuisema hapa. Kama mtaendelea kulindana CCM itakufa kifo cha gafla *aitaugua'

    ReplyDelete
  4. Hivi jamani mlitegemea jipya gani kwa JK? Vyeo vyenyewe ni vyakupeana kulipa fadhila za uchaguzi uleeee1 Sasa hapa ngoma ni kuwa tutaona badala ya kufanya kazihawa mawaziri watamaliza mwezi mzima wa kukutana na watendaji wao ili kufahamiana na baadaye Rais wao naye atatembelea Wizara hizo kwa muda wa mwezi mzima ili kukabidhiana majukumu kama alivyofanya mwanzoni mwaka na hatimaye mwaka unaisha. Kilichofanyika? Washabiki wa Kikwete wanajua.

    ReplyDelete
  5. Nadhani wote tunakubaliana kuwa huyu Kikwete ni mbabaishaji na Msanii mkubwa. Hakuna lolote atakalofanya kuleta maendeleo Tanzania kwani kwa huu mwaka mmoja tu toka aingie madarakani ameonyesha ni jinsi gani alivyo Rais bomu na jinsi gani CCM (Chama Cha Majambazi) Kinavyozidi kuwanyonya na kuharibu uchumi wa Tanzania.

    Hebu chukulia mfano huyu Ibrahim Msabaha, huyu hakufaa kupewa wizara yeyote bali alitakiwa afukuzwe kazi mara moja kutokana na uzembe wake wa kufanikisha deal ya generators kutoka kwa Messr Richmond Company. Yaani Tanzania hakuna accountability kabisa kwani viongozi wanafanya wanavyotaka wakijua hakuna consequences zozote zitakazotokana na kuboronga kwao.

    Balozi wa Tanzania USA Andrew Daraja ambaye inasemakana nae ameshiriki katika kuipatia hiyo kampuni fake ya Richmoind deal inabidi nae awajibishwe lakini kama unavyojua Kikwete kutokana na usanii wake hatofanya chochote.

    Yaani inatia huruma kuona walalahoi wa nchini mwetu wanavyozidi kuteseka kutokana na hawa majambazi wa CCM wanavyoimaliza nchi kwa rushwa na uzembe wa hali ya juu katika wao wa Kazi.

    Sina Imani na Jakaya Kikwete na sina Imani na Serikali Yake.

    ReplyDelete
  6. Nakubaliana kabisa na Geeque.

    Siju nishauri: Waziri Msabaha na Katibu Mkuu wake, kwaheri ya kuonana, kutokana na kazi mbaya ya kizembe ya kuzorotesha jitihada za kumaliza tatizo la umeme nchini, hasa jijini Dar!

    Anyway, Waziri Msabaha na Katibu Mkuu wake wanajua wazi. Tanesco inajua wazi. Benki ya biashara ya CRDB (iliyokuwa eti idhaminie "letters of credit" kwa ajili ya mambo ya "export and import, documentary collections, shipping guarantees and collections"), Wizara ya Fedha, na Balozi Andrew Daraja na maofisa wake wa juu hapo Washington, pia wanajua kwamba kampuni ya Richmond Development Corporation ya Houston Texas - ya akina Mohamed Gire (Mhindi Mtanzania) na Mohamed Haque, Ph.D. (Mpakistani Mwanauchumi) - ni ya uwakala tu. Inafanya biashara za ki-tenda. Haina genereta zake za umeme!

    Ni hivi majuzi tu Tanzania imeugua na dili ya namna hii na mojawapo ya nchi za Southeast Asia.

    Hivi ni lini tutajifunza kutokana na uzembe wa baadhi ya wakubwa? Mnakumbuka hapa awali tuliagiza miaka ya 1979/80 mi-dege ya abiria mizee kutoka Amerika – mi-dege ya ambayo iliishia hapo Kilimajaro na Gatwick (Uingereza).

    ReplyDelete
  7. Mimi namjua kikwete vyema ,
    Msabaha ni mshikaji wake kishenzi kutoka alipokuwa mbunge wa bagamoyo ontop of that waganga wa kikwete wote msabaha anawajua !!!Kumbuka ni watu wa bagamoyo hawa what do you expect?

    ReplyDelete
  8. maana mi kila siku nasema hawa watu watakufa lini (samahani kama nitakua nimemuudhi mtu) maana hawa viongozi wetu sioni cha maana wanachokifanya zaidi ya kudumisha maendeleo ya nchi yetu, kusema ukweli mimi naipenda sana nchi yangu na inatia uchungu sana pale unapoona watanzania wenzako wanavyoishi kwa shida huku viongozi wetu na mawakala wao wanavyoishi kama wafalme. hivi hawa viongozi wetu ni kwamba hawatujali sisi wananchi wao au ni vp? maana kwa upande wangu mi naona serikali ina hela ila sema hawana mpangilio mzuri, maana hizo hela wanazotumia kwa masafari yenye utitiri wa watu kama kijiji,au wanazoziiba zingetumiwa vizuri nadhani zingeweza kuleta maendeleo hata kiduchu lkn ni maendeleo, maana kwa kuangalia picha za Tanzania (hasahasa kwenye blog ya mjengwa) maana yeye ndiye anayeonyesha hali halisi ya tanzania ilivyo, sio siri inasikitisha sana. Tatizo jingine ni sisi watanzania ambao kila siku tunawachagua hawa viongozi (hasahasa CCM)pamoja na kujua ubaya wao. kwanini tusibadilike na tuone watu wengine wakoje ( ila mimi kwa upande wangu naona kwa sasa vyama vya upinzani bado, wanahitaji waamke, sijui kwa sasa maana sijakuwepo nchini kwa muda kidogo)lkn pamoja na hivyo inabidi tubadilike, maaana mi nakwambia hapa hata kama kikwete akifanya vibaya kwenye hii awamu yake na kudumisha maendeleo, bado kama akigombania uraisi miaka ijayo, watu watamchagua tu tena atashinda kwa kishindo kikubwa, mimi hapa ndio huwa nashangaa, je sisi watanzania tunachagua watu kutokana na jina au kutokana na ufanisi wa kazi?

    ReplyDelete
  9. Kwa kweli hapa JK kachemsha. Hivi tutaendeleza watu kutokuwajibishwa mpaka lini? Hiyo kasi mpya, nguvu mpya na ari mpya ipo wapi? Tatizo ni kujaza baraza la waziri kwa kufuata undugu, urafiki, na ufuska. maana hapo wengine ni mabibi za watu fulani hatutaki tu kuwataja. sasa baraza likijaa watu wote wanaokuhusu matokeo yake ndiyo hayo, ni kuwapanga hapa na kuwapeleka pale ili mradi siku zinaenda na fedha za walalhoi zinazidi kupotea na umasikini kwa wengi unazidi wakati kwa wachache waliokaribu na ufalme wa JK na Lowassa wao mambo safi.

    JK kuwa na huruma na hii nchi.

    ReplyDelete
  10. Watanzania ni watu wa ajabu na wanafiki kupindukia ! wakati JK akigombea urais kuna mtu hata mmoja aliyetaka kujua historia yake na nini amekifanya kipindi chote alichokuwa mbunge na waziri ? Hakuna mtu aliyejali kufanya hivyo tulikimbilia kusema kikwete mtu wa watu anajichanganya na sura ya mvuto wa ajabu !Sasa wakati umefika wananchi inabidi walipe sasa .

    Huu ni ujinga , sasa matatizo yake tunayaona ndungu zetu wanalala bila umeme huko nyumbani , majenereta ndiyo hayo watu wamekula hela na hakuna mtu anayechukuliwa hatua watu wanabadilishwa wizara tuu , sio tuu ni jambo la ajabu bali inasikitisha. kwa mtu yoyote anayemjua msabaha vizuri asingethubutu atakumpa ukiranja wa shule let alone uwaziri. Ni lini sisi wadanganyika tutajifunza ? ni lini hawa viongozi wetu watajua ya kuwa kampeni za uchaguzi zimeisha ? Ni lini tutapata viongozi wanaowajali wananchi kwa VITENDO ?

    Hatuwezi kuendelea kusema JK ni mtu wa watu wakati watu wanaoibia serikali mamilioni ya shilingi anawakumbatia , watanzania amkeni huko mliko kutembelewa na kina jayz , ja rule sio maendeleo hayo .....

    Hawataki kuwakopesha watoto mavyuoni lakini wao wanaendelea kula hela na kubadilishana wizara ! si majuzi tuu JK aliwapa kozi hawa mawaziri ...sasa mbona hata mwaka haujafika tayari anabadilisha tena ?

    Halafu baadhi ya watu wanawashauri watu warud nyumbani , hutarudi sehemu ambayo hauna uhakika nini kitatokea ?

    ReplyDelete
  11. Fadhili ,

    Usituletee imani za dini hapa , sisi hapa tunazungumzia masula yanayohusu mstakabali wa taifa letu. Dini aina nafasi kabisa katika hii hoja !

    ReplyDelete
  12. Wewe Fadhili usituletee zako hapa hakuna mtu yeyote aliemtuhumu JK kwa udini bali udhaifu wake katika uongozi ndio unaotufanya wengi wengi tuchoshwe nae. Miezi 10 ni muda tosha kabisa katika kutathmini mwelekeo wa nchi yetu chini ya utawala wa kiongozi yeyote. Kuna mambo mengi yanayoashiria kuzidi kuzama kwa uchumi wetu na huduma mbalimbali za kijamii. Mabadiliko yanatakiwa yafanyike sasa kabla ya Viongozi kuendelea kuboronga na sio kusubiri baada ya miaka mitano.

    Msabaha hafai period na ingebidi awe fired na sio kuhamishiwa Wizara nyingine. Kuwa kwake Mkuu wa Chuo cha Diplomasia sio kipimo cha uongozi wake bora.

    ReplyDelete
  13. Ndugu zangu watanzania,naomba tutumie busara tunapotoa maoni yetu kwenye hii blog.Ni miezi kumi tu imepita tangu tumchague Rais Kikwete lakini naona kama watu wengine wameshakata tamaa na utendaji wake!Tumpe muda tafadhali.Unapokuwa na wadhifa wa Urais suala la kuteua watendaji wakuu,hasa mawaziri ni gumu.Ndio maana Rais Kikwete anatwateua akina Wassira,Mramba,Mungai kwa sababu ni watu anaowafahamu utendaji wao wa kazi.Ninaamini kabisa kaona bora kuwateua hao kuliko watu baki asiowajua.Sikatai kwamba wako kwenye system kwa muda mrefu sasa.Narudia tena tumpe Rais wetu muda wa kuleta mabadiliko.Marekani haikuendelea kwa siku moja.Ninachomshauri Rais ni kuongeza mishahara ya wafanyakazi maana njaa ndio chanzo cha rushwa.

    ReplyDelete
  14. Naona kuna malalamiko mengi sana kuhusu uteuzi wa mawaziri.Watanzania wenzangu,labda imefikia wakati wa kujadili baadhi ya vifungu vya katiba yetu,hasa vifungu vinavyozungumzia madaraka ya Rais.Kufuatana na katiba yetu,Rais akishamteua kiongozi wa ngazi yoyote kinachofuatiwa ni kuapishwa na kushika wadhifa.Nadhani imefikia wakati hawa wateule wawe wanajadiliwa kwanza bungeni(kama vile wanavyojadiliwa na senate hapa marekani)na kupitishwa kwa kura kabla ya kuapishwa.Naamini hiyo inaweza kusaida kiasi fulani umma kujua uwezo wa utendaji wa wateule hao,na hivyo basi kuwa na imani nao kabla ya kushika nyadhifa zao.Katiba yetu inampa Rais madaraka makubwa mno,yaani anakuwa tu kama Mungu wa Tanzania!

    ReplyDelete
  15. Jamani nimechoka nasikia uchungu mpaka machozi yananitoka,kwanza mungai amechemsha mpaka hata hajiwezi jamani,amezungushwa sasa mambo ya ndani kwa kweli watu kama ni kubebwa mungai ni namba moja,alafu mungai ni rafiki sana wa lowassa pete na kidole hamna sherehe yoyote hta ya kifamilia mungai atakosa kwa lowassa,kwa hiyo sisi tulie tu.
    huyo msabaha naye ndio rafiki wa kikwatw kufa na kupona mpaka wanashea waganga wa jadi ambao wanawaweka madarakani .jamani hata huyo masha naye ni kubebwa tu.jamani hivi tunapelekwa wapi sisi jamani?????

    tukienda kwa wasira amejichokea anaweza hata akaanguka muda wowote jamani tanzania yeeetu inaenda wapi???

    diallo naye nasikia amechoka ,upendeleo ulizidi sana kwenye nafasi yake,aliweka watu ambao hawafai hata kidogo kwenye bodi yake ya utalii.

    mramba naye alishindwa hata kupresent budget yake bungeni kwa kigugumizi kikali kwa jinsi ambavyo hajiwezi,naye ametegeshewa bomu hajijui ila ameshachokwa kabisa,

    ngoja tuone huyo chenge na maghembe kama wana jipya mana wao ni wageni na karamagi

    MUNGU IBARIKI TANZANIA YETU NA WATU WAKE.AMEN

    ReplyDelete
  16. Haki ya baba sikio la kufa halisikii dawa, kama ni shabiki wa timu ya mpira kocha atowapo mchezaji ndani ya dk kumi ni kiashirio cha kuwa majeruhi asiyefaa kucheza hivyo haitakiwi kumrudisha akalinde gori au akatafute mabao lilopo ni kumtoa.
    Nasikitika kuona kuna Wadanganyika wenzangu wanajaribu kusema eti miezi kumi haifai kupima utendaji wa mtu, ni kweli kiuchumi hatuwezi kupima lakini sidhani kama tutakuwa wapumbavu wa kushindwa kupima hata maendeleo ktk sector zisizo hitaji muda mrefu kama Afya na Elimu, kushuka kwa kiwango cha rushwa na ufujaji wa pesa za umma. Enyi mliopendekeza kuwa muda hautoshi hata katika maeneo haya bado hamsadiki kua muda watosha? Binafsi namuona president wangu hapo kafanya uzandiki wa kiutendaji. Kikubwa atuondeleo hao wasikuwa na uchungu wa nchi yetu.

    ReplyDelete
  17. FADHILI yaelekea akiri yako ina matatizo katika kupima muda wa kiutendaji, kwanza JK katafuna mwaka tayari, anza kuhesabu tangu shughuli za uchaguzi ziliposimamisha maendeleo mengine ya Mdanganyika mwezako. Pili kuna anony hapo juu nadhani amekuelekeza jinsi ya kutathimini maendeleo kwa muda mfupi mfano ktk hizo sector mbili. Hawa jamaa waliopanguliwa inaonekana hata pesa zetu za semiar ya Ngurudoto walikula bila uchungu wa kweli kwa Mdanganyika mwenzetu. Ukioa, na kuona mwenzi wako ndani anamaliza miezi hata mitano akiwa anaweweseka juu ya mpenzi wake wa zamani usiku jua hakufai, hivyo kama hawa jamaaa bado mpaka sasa wanaweweseka katika utendaji basi hawatufai!!!!!!!!!!jamani.

    ReplyDelete
  18. Hapa katika mabadiliko Kuna Wizara Nne ambazo ni failures zilizosababisha mabadiliko..soma Mwananchi ya Jana "Rais Apangua Wizara Nne" wakati ni mawaziri kumi, kuna wanne waliosababisha uhakika...Failure Namba 1) Nshati na Madini(DK.MSABAHA) AU Mh. Megawati 2)Miundombinu (PESAMBILI AU KIGUGUMIZI BUNGENI)/Shekilango Road Haiishi 3)Kilimo (MUNGAI)AU KASHFA YA SHAMBA LA MBARALI 4)Utalii (Diallo) au "Waziri ambaye kila maamuzi hubatilishwa na Waziri Mkuu", kapelekwa Mifugo (huwezi kukosea huko)...
    JK katika Mawaziri anaowaamini ni Karamagi, Wasira, Prof. Maghembe na Kawambwa (Wachapa Kazi).....Hawa ndio wanaziba mapengo ya Failure au Kushikilia Wizara zile nyeti zenye budget..1) Karamagi--Nshati & Madini 2)Wasira--Kilimo 3)Kawambwa--Maji
    4) Chenge--Miundombinu (huyu sijui kwanini, "sio hands on" alafu alimpinga JK kuwa Rais waziwazi) ila wanasema mpende adui yako!! kasoma Harvard Lakini..... alafu Prof Maghembe--Utalii kwa Diallo
    Sasa inasemekana kuwa shake-up itakuja, ila Msabaha kwenda EAC ni demotion, ye ni kama naibu wa Asha Rose Migiro, Dialo Mifungo! Mramba Viwanda & Biashara aliwahi-fanya, Mungai Mambo ya Ndani, Yeye na naibu wake Masha ni target za failure (watch out)!!!! HAPA HAKUTAKA KUWAPA WAPINZANI SILAHA, ILA KUNA FAGIO LA CHUMA LITAKUJA HASA HASA BALOZI DARAJA AJIANDEE HUKO WASHINGTON, DC--MAREKANI HUWA KUNA THANKSGIVING WANATOA TURKEY KAFARA, BALOZI WA MAREKANI???? RICHMOND BRIEFCASE COMP YA HOUSTON, TX WHAT? HAMNA HATA PHYSICAL ADDRESS! THANKSGIVING NI NOV FULANI..HEEE, YETU MACHO

    ReplyDelete
  19. Fadhili nafikiri bado anataka wote tuwe na akiri ya wendawazimu.

    Wewe watu wameambiwa leteni bajeti zenu mara tu ya kwanza kwa sababu walizaliwa kiraracha bajeti zote zinazohusu tanzania nzima zimejaa kiraracha. na bado wanaonekana wanafaa kuwa mawaziri.

    Mimi imani imenitoka hakuna cha uzoefu, uzoefu huwa unamsaidia mtu aweze kungamua mambo. mara tu walipochaguliwa haikutakiwa kufanya hivyo.

    Pili ktk nchi zetu kitu manupulation ndio tu kazi zinazofanyika na hawa watu hakuna utaaalamu wowote ununuzi wa magenerator unadhihilisha hivyo vitu vinavyohusu taifa vinakuwa ni dili za watu namna hii. Sham kwa nchi kama tanzania kila siku tunaonekana kama hatukusoma. Ni aibu hii.

    ReplyDelete
  20. Pole sana Raisi Kikwete kwa kulizwa na Mwislamu mwenzio Msabaha na Waislamu feki wa kampuni ya kitapeli ya Richmond Development Corporation ya Houston Texas akina Mohamed Gire na Mohamed Haque.Jitahidi kuepuka tenda za kupeana misikitini.Kuna watu wana tasbihi na sigda kubwa sana usoni ukiwaangalia kwa macho utadhani waswalihina lakini kumbe mashetani wengine walishakumbwa na kesi za Ubakaji bungeni mfano mzuri ni huyo Waziri Msabaha.Jihadhari Kikwete na Watu unaokutana nao misikitini.Kuna maharamia ya kimataifa yanayojifanya maswalihina.Uwe makini sana tafadhali.

    ReplyDelete
  21. kwani watanzania mlipopiga kelele na kushangilia siku 100 za mafanikio ya malaika JK mlikuwa na maana gani? mbona hamjawahi kushangilia siku 100 za Yesu au Mtume?
    Mnaposema eti amepata kura nyingi asilimia zaidi ya 80 mlikuwa na maana gani? Mbona Nyerere ambae alikuwa maarufu na anapendwa na watu wengi mno, na alikuwa hapambanishwi na wapinzani hakuwahi kupata 80% ya kura zote?
    nawaomba mkubali kwamba JK sisi wengine tulimjua tangu mwanzo na tulijitahidi kupinga uteuzi wake, alheri angebaki mzee Salim Ahmed Salim. Ila kwakuwa timu ya JK ya kampeni ilijaa wezi (akina Alex Masawe), warafi (akina Lowasa) na wahindi woote wafanya biashsra nchini, pia wawekezaji woote walioangusha uchumi wetu, ambao JK aliwatafuta kwa miaka 10 akiwa waziri wa mambo ya nje, aksihirikiana na Ben. basi ndo wakaamua kuvinunua vyombo vyote vya habari ili kuwalaghai wananchi. pia wakawaibia hata kura zao chache walizowapigia wengine, wakatamba eti amepata 80% ya votes.
    Angalieni, watu wake waliomzunguka, akina Cisco Mtiro, yule mvaa kihereni wakati wa uchaguzi mdogo wa ubunge kule Temeke, akashindwa na Mrema. akina January Makamba, yule mtoto wa Makamba wa kwanza wa Makamba kwa mke wa nje yule wa kihaya. nk.
    bado hamkuweza kugundua tu pale alipolijaza baraza la mawaziri kufikia 60?
    HUYU JK SI MTU, BALI NI MHUNI KAMA MHUNI YULE ALIYEPITA.
    kuna mtu alishawahi kusema, eti "KASI MPYA, NGUVU MPYA NA ARI MPYA.............kutakuwaje na Kasi wakati GARI LENYEWE BOVU?"
    alimaanisha kuwa woote waliopo na waliomzunguka ni wabovu, maozo na matakataka.
    JAKAYA MRISHO KIKWETE HUTUFAI!!!!

    ReplyDelete
  22. Mtu wa watu, mzuri, ana mvuto, Nabii HIZI NDIO SABABU ZILIZOWAFANYA WATANZANIA WAMPIGIE KURA. Ukiwauliza watu aliifanyia nini nchi hawatakupa sababu za msingi. Zaidi hudhani alifreeze a/c za Prof Malima Ulaya KITU ambacho sio kweli.

    Wana mtandao wake na wanausalama kama Michuzi wamebaki kuwaambia wapenda nchi na wenyekuitakia mema nchi mambo yanapoenda mlama KAMA WANAWIVU WAJINYONGE na kwamba Mwaka mmoja katika safari ya miaka mitano ni mdogo. Hiki ni kichekesho.

    Leo hii muulize mtanzania na hata waziri nchi inaelekea wapi, watakuambia habari za mkukuta ambao tayari tafiti zinaonyesha we are far behind from meeting deadlines set in it na watakuambia election manifesto ambayo imeandikwa kwa kutafsiri mkukuta. Serikali haina jipya.

    Mwaka sasa bado mtu anapanga safi yake ya uongozi na kufanya seminar elekezi ambazo kama hii ya mwisho alichelewa Ngurudoto kwa siku nzima na kufanya wakuu wa wilaya wale per diem za bure kwa siku nzima.

    Nchi inaenda vibaya la historia itawashitaki wote waliotuletea rais huyu Bomu asiekuwa na vision na mamluki wote wanaomsupport sababu ya kupewa ukuu wa wilaya na perdiem za safari anapoenda safari zake ndefu ambazo hupoteza hata maana ya state visit (Rais utakaaje nchi ya nje kwa mwezi).

    Mabadiliko haya ya mawaziri naamini ameeanza kuona mambo magumu. Mtandao unahisi watu ni wajinga na unaweza wasilence kwa propaganda na matisho ya ajabu. Sauti za umma hunyamazishwa kwa muda lakini sio siku zote.

    Kwa serikali iliyokuwa na nafasi ya kufanya vizuri ni hii ya JK. serikali inasaidia bajeti ya mataifa na mashirika ya nje kwa kiwango kikubwa. Hailipi madeni kama ilivyokuwa kwa BM, na imekuta natinal reserve nzuri tu, LAKINI UBABISHA ULIKITHIRI NDIO UNAFANYA TUWE HAPA. KWANZA kwa haya aliyoyakuta tulitakiwa tuwe mbali mno kwa miezi kumi kuliko hapa tulipo.

    ReplyDelete
  23. Annonymous wa October 17, 2006 9:32:15 AM zaidi ya yale uliyoandika...RICHMOND BRIEFCASE COMP YA HOUSTON, TX WHAT? HAMNA HATA PHYSICAL ADDRESS!..napenda kukutaarifu kuwa hiyo kampuni ya wakala ina PHYSICAL ADDRESS ifuatayo:

    5825 Schumacher
    Houston, Texas 77057

    Kutokana na habari za kuaminika, Mohamed Gire ana dada yake huko London na ndugu yake hapo Dar.

    ReplyDelete
  24. Wadanganyika wenzangu, mi nadhani hata tukilia mpaka machozi ya damu yakatutoka haitasaidia chochote! Mimi nakumbuka saaana wakati wa uchaguzi wakati watu walihamasishwa sana wawape kura na upinzani pia. Hata kama upinzania bado ni mchanga, basi wangepewa atleast nafasi wabunge na madiwani kwa wingi, huo Urais apewe JK. Lakini hapana, hili likapuuzwa, na kwa vihela vidogo, T shirt na kofia walivyopewa wakulima na walalahoi wa nchi wakatoka wakaenda wakazitoa kura zote kwa CCM (80%!!!). Ona sasa hiyo serikali yao imewafikisha wapi?? Wanaodhurika zaidi na matatizo haya ya nyumbani ni haohao walalahoi waliohongwa vipesa kiduchu wakati wa kampeni.

    Kuwepo kwa upinzani madhubuti bungeni na kwinginepo kungesaidia kuipa serikali challenge. Just imagine wabunge 25% - 40 % mfano watoke upinzani, mambo yangeenda kiholela namna hii? ( Matumizi mabaya ya pesa za umma kwenye hizi safari, kutokuwajibishwa unapokosea - Msabaha et al etc). Ona sasa hata watu wenye machungu na nchi yao hawana platform ya kupiga kelele tumebaki kulalamika hapa kwenye Blog ya michuzi ( Michuzi mwenyewe ndo walewale). Hii yote ni weakness ya kutokuwa na Upinzani hapa nchini.

    Sasa ndugu zangu kwa mwendo huu hatutaweza kufika popote, tutaishia kulalamika bila kusikika na tutakuwa kama vile tunampigia mbuzi gitaa, kwani miaka mitano ijayo CCM itatumia tena economical muscle kuwalaghai walalahoi na kuingia tena madarakani with another landslide victory.

    Haina budi kwa sisi watanzania tuliopo ughaibuni kuisadia nchi yetu tuipendayo kwa kukuza upinzani nyumbani – hii inaweza kuwa kwa michango au kwa mawazo, lasivyo CCM itaendelea kutupeleka mputa tu wakijua wao ndio wao

    ReplyDelete
  25. Wewe Anon hapo juu nadhani hujui nini maana ya kampuni feki , watu kusema kampuni ni feki aina maana ya kuwa aina physical adress , wanayo ila hiyo kampuni ailipi tax yoyote kwa state ya Texas . Jamani tuacheni ushabiki usio na maana kamaa hii ishu ingekuwa ya uongo Msabaha angepinga kwenye vyombo vya Habari lakini hata hajathubutu kusema lolote, kwa sababu anajua ni kweli.

    Physical adress hata mimi ninayo , lakini aimaanishi ya kuwa nina own kampuni ! unajua nini marekani suala la kujua kama kampuni ina exist au ni famba ni NO BRAINER kabisa .Unapiga simu tuu unapata taarifa zote au unaweza kubofya dakika moja tuu na kupata data zote .

    Viongozi wetu sasa hivi wana shida moja kubwa kwamba watanzania sasa hivi wameelimika na zaidi wana exposure kubwa kwa hiyo ni vigumu kuwadanganya .

    ReplyDelete
  26. Tukubaliane tu kwamba Watanzania ndio viumbe wa ajabu sana waliopata kutokea kwenye sayari hi ya Mola. Ndio maana mpaka sasa hivi bado kuna watu wanakuambia kuwa miezi kumi ni michache sana kumpima kiongozi na hivyo tuendelee kumpa muda.
    hawa ndio watu ambao unakuwa na uhakika kabisa kuwa itakapofika mwezi mmoja kabla ya uchaguzi watakuambia kuwa tumpe tena miaka mitano amalize kazi zake kwa vile miaka mitano iliyopita alikuwa anajiandaa!!! mind you, hii ni baada ya kugaiwa makanga na mafulana na makapelo na mapilau!!
    Watanzania tuamkeni! hivi suala la kumuwajibisha waziri anayemuuzia mdogo wake nyumba nalo linahitaji muda? na lile la kununua generator hewa ya umeme? watanzania, tuamkeni......

    ReplyDelete
  27. Rais regan mwaka 1980 wakati akigombea urais aliwauliza wamarekani JEE Hali yenu kimaisha kwa sasa ni nzuri kuliko ya miaka ya nyuma ? Hakuishia hapo akaendelea kwa kusema kama basi jibu ni hapana....basi ni kwa nini muichague Democrats ?

    Swali hilo inabidi tujiulize watanzania , jee hali yetu kimaisha inazidi kuwa nzuri au kuwa mbaya ? na kama jibu ni kuwa inazidi kuwa mbaya then kwa nini tuendelee kuikumbatia CCM

    Mimi kwa mtazamo wangu nadhani tatizo kubwa ni elimu , kwani mtu asipoelimika hawezi kujua hata thamani ya kura yake ndio maana inakuwa raisi kudanganywa na pilau.

    ReplyDelete
  28. ina maana severe wa maliasili na utalii ni mkubwa zaidi ya waziri? maana yeye alikuwa demoted kwa kutoa vitalu zaidi ya nusu kwa foreigners lakini akamkatalia waziri na akawa backed up na luhanjo(chief secretary)!hii reshuffle kila mtu aliingia kwa gia yake matokea yake kukawa na mvurugano na kugusa interest za wazee(rais na chief secretary!)
    saivi tunaambiwa reshuffle hata semina elekezi haijapita miezi sita...kaazi kwelikweli!

    ReplyDelete
  29. mimi nadhani pia inabidi Upinzani ulaumiwe. Kwa mfano: Gharama alizotumia Mbowe na mahelikopta nk kwa kujipigia kampeni ili awe rais wakati akijua wazi kwamba atashindwa, ile nayo ilikuwa kiini macho kwa watanzania.
    Mbona mwaka 1958 katika harakati za kuondoa uongozi ulio madarakani, mwalimu alipigania zaidi kupata kura nyingi za baraza la kutunga sheria (Bunge), sasa nawashangaa wanasiasa wetu wa upinzani wa leo, ambao wao wanajua wazi kabisa kwamba inakuwa vigumu kwenda ikulu iwapo kuna baadhi ya sheria ambazo zinapitishwa tu na akina Amina Chifupa wasio na mawazo mapya yoyote, na sheria hizo zinaubana upinzani na mchakato mzima wa uchaguzi huru wa kuwawezesha wao kushinda.

    sasa basi tunahitaji wanasiasa wa upinzani kujiimarisha katika chaguzi za majimbo kabla ya kutumia ruzuku ndogo mnayoigombania kila siku kwa kutaka muwe IKULU. kwa hilo ndipo tutaona upinzani wa kweli ndani ya bunge. siyo kuwaachia wasioelewa kitu, walalavi, na wanaopenda umaarufu tu kwa kuwanunulia vijana wa CCM card za bahati nasibu ya mfuko wa Nyerere, badala ya kutoa hizo pesa kwa ajili ya elimu, afya na mambo mengine ya maendeleo.

    Serikali ya JK, ya CCM, na wengine wanaofagilia wizi, tumeichoka watanzania. Wapinzania kama hamuwezi kupingana kikweli, nanyi Historia itakuja kuwasuta. Mnapenda Umungu Mtu tu kama Mrema, Lipumba, Mapesa Cheyo na wengine.

    Hivi unadhani kweli mimi na uvuvi wangu ntakupa kura yangu wewe Lipumba? au Mrema? waachieni wengine waongoze upinzani na uwe wa kweli, nyie kuweni waasisi tu.
    mbona akina Abdul Sykes, Ally Sykes, Dossa Aziz,na akina Mzee John Rupia hawakulazimishia kuongoza, ingawa wao ndiyo walimwalika Mwalimu kwenye chama chao cha TAA? Hata Karume, hakutaka kulazimishia kuongoza Jamhuri ya Muungano.

    Nyie wapinzani mliolala katika jangwa la Founderlism syndromme, mstuke, dunia inakwenda. Acheni kuwa kama Museveni. tanzania ina watu wengi wenye uwezo wa kutuongoza katika upinzani, na siasa za kweli, tena wazalendo wa kweli, na siyo wale wanaolilia sera za UZAWA, tunahitaji UZALENDO. wazawa wengi wametuangusha, mpaka wageni wanatuonea huruma, na wageni wamekuwa WAZALENDO. usijivike jina la uzawa ili tukupe nafasi, mbaguzi mkubwa we.

    ReplyDelete
  30. Jamani haya ni matatizo tuliyoyataka sisi wenyewe watz.JK hana jipya huyo mtu.Hivi kitendo cha kumkumbatia Msabaha,Mungai na Mramba ni kweli anawajali watanzania huyu?Hii panga-pangua imefanywa kiushkaji zaidi kwa ajili ya kutunza heshima za wababaishaji.Walah naweza kutabiri muda si mrefu magazeti yatatawaliwa na vichwa vya habari kama hivi.PANGUA PANGUA YA WAKUU WA MIKOA-12 WABADILISHWA VITUO.Mkwasa(Betty),Dialo,Salome Mbatia wapeta ukuu wa mkoa.
    Semina elekevu walizopata hao mawaziri naona hawakuzielewa na sasa JK anarudi tena sijui safari hii ni Ngurudoto au wapi kwenda kwaelekeza tena huku mamilioni ya Watz yakiangamia.Najua Misupu huta kosa kuwepo na tunategemea kuziona picha toka huko.AMA KWELI JK SASA UMEKUWA KJ.

    ReplyDelete
  31. Huree wacha watu wajipongeze maana kazi waliyofanya Desemba mwaka jana ilikuwa pevu. Wakati f'lani palikuwa na ukumbi wa mjadala kwenye website ya majira nafikiri Nyaulawa yule mmliki wa Business times na mbuge wa Mbeya mjini aliufutilia mbali akitarajia kupewa uwaziri na JK. Mle watu walishajua tangu awali Kikwete ni bomu ni bomu ni bomu. Ombi langu kwa Kijana wa Kikwete maana najua huwa anapita humu bloguni ampelekee ujumbe Pops wake kuwa; ataitendea Tanzania haki kama ataamua kuishia miaka mitano tu. Kama ni hamu ya kuwa Rais si imeshaisha?

    ReplyDelete
  32. nimesoma maoni mengi hapa juu, na nimegundua wengi tunakubaliana kwamba Kikwete ni bomu kabisa. sasa sisi kama watanzania tufanyaje?maana inavyoelekea nchi inaelekea pabaya kabisa, ujue wakati wa uchaguzi wa raisi wafanyakazi wengi wa serikalini walikua wanasema huyu kikwete ni bomu, lakini walikua wanashindwa kutamka public, ujue mi nina uhakika kwamba kura nyingi alizopata kikwete ni kutoka huko vijijini au vijana wa mitaaani ambao wengi walikua wanamuona kikwete kama ni Mungu( nilivyosema haya makundi naomba msinichukulie kama siwaheshimu au nawadharau haya makundi)lkn ukweli ni kwamba wengi hawajui siasa ya nchi yetu inavyoendeshwa kwa sababu wengi hawana access na media, au kuna siku moja nilikuta vijana wa vijiweni wanavyomsifia kikwete kwamba atakua raisi mzuri kwa sababu anajichanganya na watu, sijui kwamba anaenda kwenye maconcert, yani nilishangaa sana hivi sisi tunachagua Rais kutokana anaenda kuzindua maconcert ya wanamuziki wetu au tunachagua mtu kutokana na utendaji wa kazi?au wengine wakawa wanasema bwana huyu Kikwete ni kijana sio mzee kama wanasiasa wengine, hapa ndio nikasema kweli vijana wetu wanahitaji elimu ya siasa, hawajui kbs nchi yao inavyoendeshwa, sasa hawa ndio walewale ambao wanaenda kupiga kura na kuichagua ccm,maana mimi nina uhakika wafanyakazi wengi hawaendi kupiga kura kwa sababu wanaona ni upotezaji wa muda, sasa majambazi wakichaguliwa tunalalamika lkn kumbe ni uzembe wetu kabisa, umefika muda wa watanzania kuamka bila kusahau ni kweli bwana kikete anabebwa sana na magazeti au television, kila siku anapambwa kikwete kafanya hiki mara kile, hivi haya magazeti yanaandika kweli hela za mamilioni za watanzania zinavyochukuliwa bila huruma?maana kama ubaya wake ungekua unaandikwa watanzania wengi wangekua na mwanga wa uendeshaji wa nchi yetu na hawa majambazi. halafu wewe unayesema kwamba kikwete amekaa serikalini miezi 10, wewe kibaraka wake nini?bwana nyota njema hung'ara mapema, huyu Raisi wetu bado kabisa yupo kwenye giza na sijui itang'ara lini

    ReplyDelete
  33. Anony wa 7:25:30, Asante sana ndugu, vigezo vilivyotumika kumchagua huyu Rais feki ni vya ajabu mno, mara kijana, mara mzuri wa sura, mara anajichanganya na watu ni upuuzi mtu ukiangalia. Sasa Watanzania tunaula wa chuya kwa uvivu wa kupembua. Kibaya zaidi nikuwa itatucchukua miaka kumi ijayo kuondokana na huyu mchovu. Na who knows labda jamaa atabadilisha katiba awe rais wa maisha maana anajua kuwa kuwa anasupport ya Watanzania.

    ReplyDelete
  34. Nyie watanzania kazi yenu ni kulalama halafu mnatawaliwa kiulaini tu. Wakati wa uchaguzi hawa wote wanaopiga kelele huwa waangalizi tu.

    Ni watanzania wachache vijana ambao kweli wana upendo na tanzania acheni wazee wale ppf yao sasa hivi mnajifanya mna uchungu na kuanza hoo JK bomu hoo mawazili bomu nk. wakati mnaona katika chaguzi watu kibao wamebeba blungutu la noti nyingine zikitoka kwa majambazi wakienda kuomba kura kwa wananchi. Sasa wameisha tumia mitaji yao wanataka kurudisha faida zao nyinyi hoo sijui nini?

    Watnzania na kulalama ndio zao tu hawa wote wanaolalama hapa hakuna hata mmoja ni mpiga kura ndio maana CCM wanatembea kifua mbele na mabao ya visigino. Tanzania mlie tu maendeleo mtayasikia kwenye Luninga tu na internet siyo kwenye nchi.

    Subiri miaka ishirini ijayo hata Uganda, Kenya, Shelisheli wote watakuwa ndiyo wawekezaji tanzania baada ya south Africa kushika mikampuni minono.

    Nyie mnaona hata East Africa Uganda wanapinga kwamba hatujiungi na Tanzania kwa sababu elimu yao Manpower yao ni duni. Nyie kaa kulalama tu pole sana wenzangu.Suala hapa ni kuhakikisha kama mnataka maendeleo maendeleo hayaji kwa kirahisi hivi hivi. fanyeni kazi kuwa tayari kuwahakikisha katiba zetu zinalenga ktk kureta maendeleo siyo kutoa chambo kwa akina lipumba, mrema eti wapinzani wakati vijana lukuki mnakimbilia nchi za nje.

    ReplyDelete
  35. Ukitaka kujua kama serikali iko kazini angalia on the ground. Ni vazi kuwa JK anayo nia njema lakini wachovu wake wa tangu enzi za Sr. Edward Twinning wanamzidi kete.

    Nenda sehemu kama Muhimbili inayoitwa eti "National Hospital" mambo ni vurugu tupu. Muhimbili unaweza kuiita “an extended dispensary”. Muhimbili inafanya kazi zinazoweza kufanywa kwenye zahanati yoyote hata ya kule Kasulu. Walimfukuza Mzungu aliyeleta maendeleo makubwa sasa wako hoi. Sasa wanataka kumuweka mtu aliyekuwepo na kusaidia kuiua Muhimbili eti huyo aifufue. Hii ni akili kweli? Mfu anaweza kumsaidia marehemu?Wapo watanzania wanaoweza kazi ya ukurugenzi lakini historia zao zinaonyesha hawawezi kuruhusu mgao 10% kwa wakubwa. Kwa hiyo hawawezi kupewa nafasi.

    JK anaangukia pabaya kwa kuwa safu ya watendaje wake hawana uwezo wa kutafsiri falsafa za maneno yake na kuyaweka kwenye vitendo. Haya yalimkumba pia Rais wa kwanza Mwl. JK.

    Watu anaowapa kazi hawaonyeshi work plan "WP" zao na deliverables ambazo zingalitumika kupima ufanisi wa kila mmoja. Uliona wapi udanganyika huo nchi nyingine ile duniani! Sisi watanzania inatubidi tukubali kuitwa " WADANGANYIKA" maana hakuna mechanism ilyowekwa ili wananchi wamshauri Rais na waziri mkuu bila kupitia kwenye system za serikari (mawaziri na usalama wa Taifa).

    Watanzania wako wengi wanaoweza kufanya kazi vizuri kuliko akina MSABAHA, lakini JK anapaswa atumie kichwa chake mwenyewe maana washauri wake wengi wako wenye mtandao wa walaji waliobobea. Kwa hiyo asitegemee kupata ushauri wa kuleta manufaa kwa nchi mbali na ule wa kusaidia kujaza matumbo ya wanamtandao huo, mfano ni ule wa RICHMOND KULETA UMEME TOKA MAREKANI.

    JK upo, je jumbe hizi unazipata au tunapoteza muda...sisi tungalikuwa washauri wako wazuri tu. Tuma vijana wako waminifu wachunguze na wakuletee vijana wenye vision wakusadie kusukuma kazi vizuri katika maeneo mabali mbali kuanzia taasisi za uma hadi mawizarani na pia wafichue uozo wa wakubwa uliowaweka madakani lakini na wewe uchukuwe hatua za kuondoa wabovu wote.

    Mwisho JK, uwe mwangalifu na UDINI. Mwl. JK alikuwa na dini yake na alikuwa na imani nzuri tu ndani ya dini yake, lakini dini hiyo ilibaki kuwa ya kwake tu na katu hakuifanya kuwa ya WADANGANYIKA WOTE. Dalili zinaonyesha punde si punde watu wataanza kukatwa mikono katika ka-nchi alikoanzisha mzee mchongameno (Mwl. JK). Watch out Sir JK. Historia itakulaani.

    ReplyDelete
  36. Trio kaka nafikiri hapa kinachogomba siyo mzee au kijana ndiye ataleta maendeleo kikwazo kikubwa cha maendeleo tanzania tumekuwa na mfumo uliozoeleka, watu waliozoeleka ambao wamekuwa ktk system muda mrefu wamezoea kutawala wamezoea kuwa viongozi wamekuwa professional viongozi nafikiri umenielewa.

    Sasa ukiwa mtu wa namna hii huwa mara nyingi huwa ni vigumu kubadilika. Hii ni sawa sawa na wale mafundi mchundo. Hawa jamaa huwa wakisha jua kuwa hapa huwa tunafunga kamba mashine inakwenda huwa ndiyo hivyo huwa hawabadiliki. Lakini akija mhandisi baada ya muda anasema no hebu jaribu hivi kesho yake yake mambo yanabadilika. Sasa ukiangalia katika serikali ya tanzania kuna watu wamekuwepo vijana tunazaliawa mpaka sasa vijana wanafika kuwa maprofessor bado wapo vile vile.

    Kuna wengine huwa wanajitahidi kubadilika kuna wengine akishajua yeye kazi ni kutoka nyumbani, kufika ofisini na kufanya kazi ABC kwa mtindo fulani hata kama atabadilishwa kutoka sehemu moja kwenda nyingine huwa inakuwa vigumu sana kubadilisha mfumo.

    ndio maaana inatakiwa watu fulani wangatuke waletwe wengine wajaribu pia mifumo yao.

    Kuna wazee wengi sana hata nafikiri vijana wa sasa hawawezi kuwafikia. Hila kilichosemwa kwa waliosema vijana ni kwamba vijana hasa hasa ndio wanalalamika, wakati wao hata kura huwa hawapigi, kazi ni kufikiri kuwa watu wa kijijini/vijijini waabadilisha mambo. sasa ninachojua wengi wanaotoa challenge wanazitoa ktk wakati mgumu/mazingira magumu hawawezi kufika mbali. Ndio maana vijana bado wana nguvu challenge zao zinaweza kufika/kutufikisha mbali lakini hili linawezekana kama tu itaonekana labda wanafikiri kuna jambo fulani halijafanyika wakati wana uwezo wa kulifanya.

    lakini kama hakuna initiative mpya, ambayo ndiyo inaweza leta mabadiliko tunyamaze.

    ReplyDelete
  37. Hebu sasa tuzungumzie lifuatalo:

    Kampuni ya kimataifa ya Wahahudi ya Tiffany, yenye makao makuu yake hapa New York, ndio iliyobatiza zoisite gemstone kwa jina la tanzanite; madini yanayopatikana Tanzania peke yake. Tiffany ndiye mnunuzi mkubwa wa tanzanite.

    Biashara ya madini haya ni ya kusitaajabisha kutokana na habari kuwa nchi nyingi zisizo na madini haya ndizo zinaouza Tanzania nje kwa kampuni ya Tiffany na nyinginezo. Biashara hii pia iliathirika kutokana na ukweli kwamba kati ya wadau wake walikuwa ni wanachama wa El Qaida ya wakina Bin Laden kuhusishwa na biashara hii. Tiffany walisusia kidogo biashara hii hadi hapo wakina Bin laden walipoondolewa.

    Kuna msukosuko mwingine. Shirika la Umoja wa Mataifa linapambana sana dhidi ya mambo mawili: utumwa na uajiri kazi kwa watoto wa umri mdogo. Kupitia mojawapo ya ofisi zake - Ofisi ya Kuratibu Masuala ya Misaada (Office of Coordination of Humanitarian Affairs) - hivi majuzi ilitengeneza filamu dhidi ya kuajiri watoto kama hao katika machimbo ya tanzanite ya Merereni, yenye kichwa cha habari, Gem Slaves: Tanzanite's Child Labour. Filamu hii ilizinduliwa Septemba mwaka huu hapa kwenye Umoja wa Mataifa wakati Rais Kikwete akiwa hapa. Hii si mara ya kwanza kwa ofisi hii kutengeneza na kuonyesha filamu za namna hii.

    Hatujamsikia Rais Kiwete akilaani filamu hii, kama alivyofanya kuhusu filamu ya Hubert Sauper, Darwin’s Nightmare! Mbali na shutuma za baadhi ya wadau wa Kitanzania wanaohusiana na tanzanite, hakuna hata Wabunge wetu waliokuja juu dhidi ya filamu ya Gem Slaves: Tanzanite's Child Labour! Kisa: Aidha, hii ni filamu ya Umoja wa Mataifa au pengine kuna ukweli bayana ndani yake.

    Juzi juzi, gazeti moja la nyumbani liliandika kuwa mwakilishi wa kampuni ya Tiffany alifanya ziara nchini kwa minajili ya kujibu wito wa Rais Kikwete wa kualika wawekezaji nchini. Lakini yatubidi kupanua mawazo yetu. Isije ziara ya mwakilishi huyu wa Tiffany ikwa ni sababu ya kuja kutathimini ukweli way ale yaliyomo ndani ya filamu ya Gem Slaves: Tanzanite's Child Labour! Maana filamu hii, licha ya yaonekanyo kwa macho yetu (contents), ina maana kubwa sana yanapoumbiwa sura nzito (context). Si kuajiri tu watoto wenye umri mdogo, bali, pia ni utumwa!

    Kampuni ya Tiffany kamwe haingependa kujihusisha na vitendo nivavyoendeleza njama za kudhalilisha na kudurru tu na fia za kupanga, kutekelza, kupanua, kuotesha, kupalilia, kumwagilia maji mimea ya utumwa, na uajiri wa watoto wenye umri mdogo kazini. Ukweli utakaopatikana unaweza kuathiri tena biashara ya tanzanite. Pengine mwakilishi wa kampuni ya Tiffany amekuja kuzungumza na wakubwa jinsi ya kuendeleza uchimbaji wa tanzanite bila ya kuwatumikishs watoto wadogo, kama watumwa.

    ReplyDelete
  38. mmeongea mengi kuhusu uozo wa baraza jipya, umeme, na mengi... yote ni kweli kutokana na mitazamo ya kila mmoja.
    swala la wamachinga, maduka, majengo yanayobomolewa sasa hivi na ambayo haizungumziwi kokote, si kwenye radio, tv, magazeti na kwingineko, mnalichukulia vipi
    wana blogger.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...