Home
Unlabelled
lexus
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Kaka Michu sasa ume-advance kwenye fani.Umenifurahisha kuruhusu picha zako kutumwa kwa rafiki.Binafsi nafikiri si ku-admire tu ila Waziri Ally anaonekana kuukubali huo mkoko wa babu njenje.Keep it up Michu.
ReplyDeleteMiss Tanzania atoweka nyumbani
ReplyDeleteSaleh Ally na Vicky Kimaro
VODACOM Miss Tanzania 2006, Wema Abraham Sepetu ametoweka nyumbani kwao tangu juzi asubuhi na juhudi za familia yake kumpata zilikuwa zimeshindikana hadi jana jioni.
Wema anadaiwa kuaga nyumbani kwao juzi asubuhi akieleza kuwa alielekea kwenye "shughuli zake za kila siku" lakini hakuweza kufanya hivyo hadi jana mchana, hali iliyofanya baba yake mzazi, Abraham Sepetu kuamua kutoa taarifa katika kituo cha Polisi Kijitonyama Mabatini, Dar es Salaam.
Hofu iliingia kwenye familia yake baada ya mawasiliano ya simu na mrembo huyo kukatika usiku baada ya simu yake kuzimwa wakati mawasiliano na dereva wake yalikatika jana alfajiri.
Akizungumza nyumbani kwake jana, Sinza Mori jijini Dar es Salaam, baba huyo mzazi wa Wema alisema wamekuwa wakimsaka bila ya mafanikio na baadaye kuamua kumtafuta kwa simu ya dereva wake.
"Dereva wake naye hakupokea simu muda wote ila tukaelezwa alionekana pale Mori sehemu ya kuoshea magari muda wa saa 4.00 usiku. Wanasema baadaye walituambia kuwa aliaga kumuwahi bosi wake (Wema)," alisema Sepetu.
"Tuliendelea kumpigia simu bado ikawa kimya, leo (jana) saa 11 alfajiri dereva alipokea simu na kusema alikuwa sehemu akimsubiri bosi wake kwa kuwa alikuwa kwenye sherehe na wenzake.
"Lakini baada ya hapo hakupokea simu tena hali iliyonifanya niende kituo cha polisi saa 2.00 asubuhi kutoa taarifa kwa kuwa yule ni bidanamu. Huwezi kujua amekutwa na nini."
Sepetu alikuwa mfano kwa wazazi wakati wa mashindano ya Miss Tanzania baada ya kumuunga mkono mrembo huyo kuanzia ngazi ya kitongoji.
Alisema baada ya kutoa taarifa Polisi amekuwa akisubiri matokeo baada ya kuahidiwa kuwa wanalifanyia kazi.
"Wamesema wameshaanza kulifanyia kazi na wote vikiwemo vyombo vya habari tunaomba tusaidiane katika hili," alisema.
Katika kituo hicho cha polisi cha Kijitonyama, askari mmoja wa zamu alisema hawezi kutoa taarifa zozote kuhusu tukio hilo hadi apate ruhusa ya kamanda wa mkoa wa Kinondoni, Jamal Rwamboh, ambaye pia hakupatikana.
Jana, muda wa Saa 11:45 Mwananchi ilishuhudia gari la Wema aina ya Toyota Rav4 aliloshinda baada ya kutwaa taji la Miss Tanzania, likiendeshwa kwa kasi na dereva wake maeneo ya Sinza, Afrika Sana huku muziki ukipigwa kwa sauti ya juu sana tofauti na wakati mrembo huyo anapokuwemo ndani.
Wema alianza kazi ya kusaka taji la Miss Tanzania lililokuwa linashikiliwa na Nancy Sumari akitokea kitongoji cha Dar Indian Ocean alikoshika nafasi ya pili na baadaye kanda ya Kinondoni alikoshika nafasi ya pili tena.
Boko!
ReplyDeleteNi faraja ilioje kuiona gari ya Babu Njenje, wewe na mandahli ya Njenje plaza!
Swahiba!
Huu mkoko sio Datsun 120J? Hizi ndio zilikuwa gari miaka hiyo ya mwishoni mwa 70 na mwanzo wa 80.
ReplyDeleteKipindi hicho magari ambayo yalikuwa yanatamba kwenye barabara za Bongo ilikuwa ni pamoja na Peugeot muundo wa 404!
Mzee Michuzi kuna watu wanabisha Bongo hakuna Range Rover mpya nyingi!Sasa hivi zipo kama 40 Dar peke yake. Naomba uende yard ya pale fire uwawekee picha za hizo range zipo kibao pale. Jamani Bongo ni pesa yako tuu kwa sasa kila kitu kipooo.
ReplyDeleteVipi Wazir, lini tutarajie nyimbo mpya?
ReplyDelete