kama kawa mabango yenye ujumbe mbalimbali yalikuwepo kwenye maandamano ya leo ya cuf yaliyoandaliwa kushinikiza kuwepo na serikali ya mseto zenj

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Kwanza kabisa napenda kukupongeza kaka yangu michuzi kwa kazi yako nzuri, Keep it up. Pili kaka siku hizi umeanza kuwa mzito kuweka mambo hapa tunakusihi kaka blogu hii ni kisima cha habari halisi kutoka bongo kwa sisi wa ughaibuni hivyo tupe issue za home kaka. Unasalimiwa na mazrui na amasha kaka

    ReplyDelete
  2. Chifupa: Najitoa mhanga

    Na Mwandishi Wetu, Dodoma

    MBUNGE wa Viti Maalum, Amina Chifupa (CCM), amesema yuko tayari hata kufa lakini kamwe hatakubali janga hilo la dawa za kulevya liwateketeze vijana.Chifupa alitoa msimamo huo jana baada ya kuombwa kuwasilisha serikalini taarifa alizonazo kuhusiana na maeneo, majina ya wauzaji na watumaji wa dawa za kulevya anayodai kuwa nayo.Alishauriwa ayawasilishe majina na taarifa hizo kwenye kamati maalumu iliyoundwa na Rais Jakaya Kikwete ili kuchunguza biashara ya dawa za kulevya nchini ili yaweze kufanyiwa kazi.

    Mkuu wa Kitengo cha Uhalifu wa Fedha na Mali katika Wizara ya Usalama wa Raia, Samson Kassala, alimshauri mbunge huyo kwenye semina ya wabunge kuhusu jinsi fedha haramu zinavyohalalishwa na udhibiti wake iliyofanyika mjini hapa jana.
    Baada ya ushauri huo wa Kassala uliotokana na mada iliyohusu mbinu mbalimbali zinazotumiwa na wahalifu katika kuzalisha na kuhalalisha fedha haramu, Chifupa alidai kuwa maeneo na watu wanaojihusisha na biashara ya kulevya wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam, yanafahamika, lakini hakuna hatua zozote zinachokukuliwa dhidi yao pamoja na wananchi kulalamika juu ya suala hilo.

    “Haya mapambano dhidi ya dawa za kulevya ni kama mchezo wa kuigiza kwa sababu maeneo na watu wanaojishughulisha na biashara hiyo wanajulikana hata kwa watoto wadogo. Wakati wa Bunge la bajeti nililieleza hili, lakini hadi leo hakuna hatua zinazochukiliwa. Alisema : "Nipo tayari kusaidia kuwatambua wafanyabiashara wa dawa za kulevya na maeneo yaliyokubuhu kwa biashara hiyo endapo nitatakiwa kufanya hivyo." Hata hivyo, kauli hiyo ya Chifupa ilionekana dhahiri kuwashtua baadhi ya wabunge wenzake waliokuwa wakishiriki semina hiyo wakihofia usalama wake kwa madai kuwa wafanyabiashara hao wanaweza kumdhuru kwa kuhofia kuumbuliwa. “Jamani huyu mtoto anajitafutia balaa. Kwanini anahatarisha maisha yake, hawa wauzaji wa dawa za kulevya ni watu hatari sana wanaweza kumdhuru kwa kauli zake anazotoa,” alisikika akisema mbunge mmoja kwa kunong’ona wakati Chifupa akiendelea kutoa maoni yake.

    Alipoulizwa na Mwananchi Jumapili kuhusu maoni na kauli yake hiyo kuhusiana na wasiwasi waliokuwa nao wabunge wenzake alijibu: “Mimi nimeamua kujitoa mhanga kwa ajili ya kuwaokoa vijana wenzangu wanaoteketea na dawa za kulevya. Siogopi hata kufa kwa kusema ukweli, kwani kama nimeandikiwa nife kwa ajili ya dawa za kulevya, basi nipo tayari kwa hilo, lakini sitaacha kukemea maovu katika jamii yetu” alisema mbunge huyo. Alisema yeye akiwa kiongozi aliyeaminiwa na Watanzania kiasi cha kupewa wadhifa huo wa ubunge, dhamira na nia yake vinamtuma kujitokeza mstari wa mbele katika kusaidia mapambano dhidi ya biashara ya dawa za kulevya ili kuwaokoa vijana ambao ndio waathirika wakubwa wa dawa hizo.

    “Sitaogopa kusema yanayowaumiza wananchi, wanaoumia ni watoto wetu kwani hawa wauzaji wapo mitaani ambako pia watoto wetu ndiko wanakochezea na kuishi. Hakuna wa kuwanusuru kama wote tutaogopa kupiga vita jambo hili na mambo haya ndiyo yanayoharibu nchi yetu,” alisema. Alishauri zitungwe sheria kali za dhidi ya biashara na watumiaji wa dawa za kulevya ili kulinusuru taifa na tatizo hilo ambalo alisema kama halitasimamiwa kidete litaangamiza vijana ambao ndiyo muhimili wa taifa. Awali, Kasalla, alimtaka Chifupa kushirikiana na kamati iliyoundwa na Rais Jakaya Kikwete, kuchunguza tatizo la dawa za kulevya nchini ili aweze kutoa taarifa alizonazo ili zifanyiwe kazi. Hivi karibuni Rais Kikwete, aliunda tume hiyo kuchunguza tatizo la dawa za kulevya pamoja na kupewa orodha ya majina ya watu wanaodaiwa kujihusisha na biashara hiyo haramu.Hii ni mara ya pili kwa mbunge huyo kutoa madai kama hayo, mara ya kwanza ikiwa ni wakati wa kikao cha Bunge la bajeti kilichokutana kuanzia Juni hadi Agosti mwaka huu.

    ReplyDelete
  3. Tanzania haitengenezi dawa za kulevya,Chifupa na Bunge tukufu inabidi wajue kuwa dawa za kulevya hazizuiliwi kinondoni,zinazuiliwa mipakani.

    ReplyDelete
  4. Nimeshukuru sana michuzi kwa taharifa hii mimi nampongeza mweshimiwa chifupa vile vile napata taabu kujua kama kweli serikali kweli ina dhamira ya kutatua tatizo hili maana inapata kigugumizi sana.

    Mtu anakwambia huyu anauza madawa unasubiri nini?

    wanaouza ukisema suala kama hili wanasema unajitafutia matatizo. Nchi zetu haziwezi kuondokana na majanga kama hatutapata watu wa kujitolea. Nafikiri sasa Amina anafanya kazi yake kama alivyotumwa kuwa kiongozi wa vijana ambao ndio wanaoumia

    ReplyDelete
  5. Ongela AC, lakini waswahili wasema kikulacho ki nguoni mwako, kwanza anza kwa kusafisha nyumbani kwako kabla ya kwenda kwa jirani.

    ReplyDelete
  6. Majina ya vigogo yanazidi kulundikana kwa JK na Waziri Mwapachu. Isije ikawa kama yale ya Ripoti ya Tume ya Warioba kuhusu rushwa nchini! Waandishi wa habari hawana budi kuzitingisha dola zinazohusika kuyaanika ipasavyo majina ya vigogo wanaochochea matumuizi ya madawa ya kulevya. Lazima kuna watengenezaji. Lazima kuna wasafirishaji wa kuyaingiza nchini. Lazima kuna wapokezi uwanja wa ndege, poti baharini, njia za panya, mifuko ya kibalozi (diplomatic pouches), na walimaji wa bangi (uvutaji wa wazee kama zamani - vijana walikuwa hawavuti bangi kule nitokako - ingawa serikali ya wakoloni na ya uhuru i(li/na)piga vita tabia na desturi hii. Lazima kuna meja distributazi distributasi. Lazima kuna pakejazi na wasindikaji wa kuyaweka katika vitita. Lazima kuna wachuuzi wadogogo wa kuyawasilishwa kwa walaji ambao mwishoni wataonekana kama zombi hadi miili yao ionekane kana kwamba wamefuliwa kwa blichi!

    ReplyDelete
  7. asante sana michuzi kwa kuwa unatupatia habari za kila siku kutoka huko nyumbani hila mimi nataka kusema huyu chifupa hasije hakawa na chuki binafsi ya kutaka kutumia hako kanafasi haliko pewa ka,ubunge kusudi kuwapakazia watu bila kuwa na huakika na yale anayo yasema mimi ninanvyo jua haya madawa ya kulevya hayakuanza leo au baada ya yeye kupata ubunge yalikuwepo na alikuwa anajua kuwa yapo na serika zote zilizo pita walikuwa wanayapiga vita kwanini hakusema au wakatiuo aliona hakuna umuhimu?? mweshimuwa chifipa mimi nakushauri wacha pupa nenda taratibu najua rais anajua kuwa upo kama nafasi ya kuongezewa cheo atakupatia lkn sio kwakutaka kuja kuwapakazia watu kusudi wewe uneemeke kwa migongo ya watu,tunajua kuwa watu wapo na wanajificha wacha vyombo ya serikali vifanye kazi yake kwa umakini na sio kuwafanyisha kazi za chuki binafsi ushauriwabure nakupatia mw, chifupa

    ReplyDelete
  8. Bango hilo ni ushahidi kuwa CUF imejaa washirikina.Mambo ya kuaguliwa kwa waganga wa kienyeji yalikuwa enzi za kale.Siwalaumu CUF.Hawana wasomi.Wasomi hawataki kujiunga nacho.Chama kizima nchi nzima kina PROFESA mmoja tu.Profesa Ibrahim Lipumba.Ambaye naye siku hizi hata akihutubia maneno yake hayana tofauti sana na Profesa Maji Marefu ambaye ni Mganga wa Kienyeji wa Handeni.Kukubali bango kama hili kwenye maandamano kunathibitisha kuwa siku hizi hata Profesa Lipumba anakumbatia Ushirikina.Hii ndiyo taabu ya chama kikiwa kimejaa watu ambao elimu ya juu kwao ni madrasa ya dini ya kiislamu tu.

    ReplyDelete
  9. Ww anony hapo juu acha ushamba.Umeambiwa kuaguliwa ni ushirikina pekee?Hivi mtu hawezi aguliwa kisayansi?Lo!!! mbona unaumwaga hadharani ufinyu wako wa kutokuelewa mambo.Unatakiwa na wewe uka-aguliwe labda utapata nafuu.

    ReplyDelete
  10. Kimbia mwanangu, kimbia
    Huyo si mganda aminia!
    Kimbia hilo sindano atalodungia
    Na dawa yake ndani kukuingia
    Ni kukubali tanzia!

    ReplyDelete
  11. Nenda kwenye Kamusi uangalie neno la Agua maana yake nini.Liko linked na ushirikina moja moja.Jua kali penda kusoma kabla hujatetea wasiopenda elimu wa CUF.Kachukue kamusi ya kiswahili haraka!

    ReplyDelete
  12. Toka lini Mpemba akaenda hospitali? Ni rahisi kumwambia afunge biashara kuliko kumwambia aende hospitali kama anaumwa.Akiumwa mpemba spidi huondoka kwenda kuaguliwa.Wapemba wengi huishia kuaguliwa na waganga wa kienyeji.Hilo bango linawasilisha hasa imani kuu kabisa ya toka moyoni ya kile wanachokiamini hasa, yaani kuaguliwa kwa waganga wa kienyeji kila wanapoumwa au kupata tatizo.

    Ushauri wa bure nawapa siku ingine kuwe na kamati ya kuyasoma mabango na kuyapitisha kabla ya kuingia nayo barabarani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...