mafundi wakifanya kazi usiku na mchana pale ubungo tanesko kuhakikisha mitambo ya richmond inaanza kuzalisha umeme chap chap

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 28 mpaka sasa

  1. Hawa jamaa wamekaa kama hawafahamu wanalotakiwa kufanya.
    Sidhani kama wana blueprint kamili ya jinsi ya ku-install hiyo jenereta. Tusubiri uone kama hii kazi haitakamilika mwakani mwezi wa nne!

    ReplyDelete
  2. waaaaaaaaaaaaapiii wewe hizo stori tumezisikia toka september kua ufungaji utakamilika mwishoni mwa november lakini wapiii? acheni kufagilia kila kituu!

    ReplyDelete
  3. UMEME NI TISHIO BONGO;SASA HII RICHMOND WATAFANYA KWELI AU NDO LONGO LONGO?

    ReplyDelete
  4. Dr Ibrahim Msabaha na Dr Lawrance Masha si vibaya mkipitia hii website, bei ya turbines ipo wazi hapa,transport ipo wazi hapa antonov.com cantact zao zipo hapa, commission/mlungula upo wazi kwani jamma wanotoa bei ukiwacontact.....Mlishindwa nini kuongea moja kwa moja na hawa jamaa wa GE/General Electric? au mliogopa kidhungu mpaka mkawatafuta hawa madalali wa Richmond/ apart from parcent yenu hapo. Inatia uchungu sana.

    ReplyDelete
  5. hawa jamaa deadline imeshapita na umeme hakuna.....mkataba hauwabani kulipa demages???

    ReplyDelete
  6. It's such a shame that after almost half a century since independence, the capital city of a nation lacks electricity! The dependence on water by itself is archaic, the corruption with which the leaders and its highly educated personnel commit is a thing of surprise!

    ReplyDelete
  7. MUDA UMEFIKA KWA BONGO SASA KUWA NA NISHATI YA KUHAMINIKA. YAANI SIAMINI MPAKA LEO HATA DAR YENYEWE HAINA UMEME..WAKATI HAPA MAREKANI HATA WAKATI WA KATRINA BADO KULIKUWA NA UMEME. JE TUTAFIKA NAMNA HII?? WAKATI CEO WA TANESCO ANALAMBA $50,000 KWA MWEZI??

    ReplyDelete
  8. Unategemea nini wakati karibu viongozi wote wa Tanzania wamesoma University of Dar es Salaam shule ambayo inatoa graduates wajinga na mambumbumbu ambao kazi yao ni kutia saini mikataba mibovu na kula rushwa. Sijapata kuona nchi ambayo ina viongozi wajinga kama Tanzania yaani ni aibu tupu.

    ReplyDelete
  9. Serikali yetu ni ya kijinga sana, sana, sana tu....nimecheka mno kuona hizo jenereta ni za GE....anonymous umenifurahisha sana.

    ReplyDelete
  10. Hawawezi kufanya kazi usiku na mchana kwa sababu kuna mgao wa umeme, na hii kazi ya instalation inatumia umeme kwenye drill na vifaa vingine hah heh heh inachekesha maana hata tanesco kwenyewe pia kuna mgao wa umeme

    ReplyDelete
  11. Hamna ummeme hapo ni utapeli tu. Serekali inachukua hatu za gharama kiasi hiki, walishindwa nini kuingia mkataba na Zambia wakatuuzia umeme. Hizi jenereta sio reliable maana unaweza kuwasha leo kesho ikawa na tatizo, je hii itatufikisha wapi. Exposure ya viongozi wetu ni finyu. Wewe mtu ametoka mitaani hana hili wala lile anapewa jukumu la kuiongoza wizara, hajui a wala Z, Unategemea nini. Makatibu wa wizara ambao ndio watendaji wakuu, ili kuhakikisha kila kitu kina enda inavyotakiwa wanatakiwa watu waliopiga shule na ambao wana fani inayoendana na wizara husika na experience ya kutosha.

    Sasa kama hii kampuni imeshindwa hata ku install hii genereta, iweje wamepewa tenda nyingine ya kuagiza jenerator nyingine South Africa. Hii ikiendelea miaka 20 itakayokuja Tanzania haitakuwa ya watanzania tena ila ya watu wengine, watch out. Viongozi muwe na focus, msiwe short minded. Msipende vijisent ambavyo hatima yake inaiweka Tanzania pabaya. Fanya kitu ambacho hata mbele ya mungu utapewa thawabu. Mnatutia aibu sana viongozi, ila hamlioni hili maana hamna akili wengi wenu. Hamna akili ni ujinga tu umewajaa na ubinafsi. Na watananzania amkeni msishangilie huu ujinga wa viongozi ila wawajibishwe ipasavyo. Tuwe wamoja kupigana na hawa watu wachache wajinga wanaotokomeza Tanzania. Mungu ibariki Tanzania na wananchi wake na tunaomba ubadili utendaji mbovu unaonuka walionao wengi waviongozi wetu maana unanuka na kutia aibu kubwa. Kila mjanja sasa hivi anakuja Tanzania kuvuna maana watu wamelala usingizi wa mfu.

    ReplyDelete
  12. HIZO NI SHUGHULI AMBAZO WATOTO WA VIGOGO WAMEPEWA DILI ALAFU WANALETA UOZO,ALAFU BABA ZAO WANAWANYAMAZISHA WATU BUNGENI ETI WASIONGELEE HILO SWALA,INATIA HASIRA SANA WATU WALIVYO WALAFI WAKATI WAMESHAKUWA MATAJIRI.

    ReplyDelete
  13. michuzin unauzi sana wengine sisi comment zetu huweki kwa nini umeweka hii blogu??sasa ngoja utaona mambo yakikuchenjia ndio mana siku hizi imepooza sana watu hawaipendi tena.

    ReplyDelete
  14. ushenzi wa hali ya juu jamani kweli nchi hii imekwisha.kwaherii.

    ReplyDelete
  15. ushenzi mtupu.

    ReplyDelete
  16. Angelikuwa hai Jabali la Muziki, the Late Marijani Rajabu, nina uhakika kabisa angerudia ule wimbo wake wa "Dunia imani imekwisha", nyoyo za watu zimebadilika, wanadhulumu hata watoto yatima". Yaani jinsi viongozi wetu kwa mikataba feki na tamaa ya fedha wanathubutu kuidhulumu hata nchi maskini kama TZ. Unajua hata ule utangazaji wa tender yenyewe ambayo Richmond alishinda ulikuwa ni wa kutatanisha! Mimi nikafikiri hizo zitakuwa ndo hizo NGUVU Mpya, ARI Mpya na Hiyo KASI Mpya. Kwani deliever and commissioning time ilikuwa ndani ya miezi mitatu, yaani August 2006 ilibidi 40 MW ziwe generated pale na 60 MW ziwe generated Ubungo. Lakini leo naona wanaongelea 20 MW. Halafu zinafanywa deal kama nini sijui. Ni nini 20 MW??? Hivi kwanini hatutafuti Long term solutions na siyo hizi issue za ZIMAMOTO. Na hizi issue za ZIMAMOTO ndo zinatoa mianya ya RUSHWA na ufujaji wa pesa za wanyonge! Mimi nipo tayari kuandaa "long term plan" kwaajili ya kumaliza matatizo ya umeme Tanzania, hata kama kuleta wawekezaji ambao hawatatoa wala kupokea 10%. MUNGU IBARIKI TANZANIA.

    ReplyDelete
  17. viongozi wote Wa Afrika ni wapumbavu tu. Kikwete anaenda ulaya kutafuta vitega uchumi wakati Tanzania hamna umeme wala maji, barabara mbovu, sheria za biashara na mahakimu inanuka rushwa. Hawa viongozi kweli wamesoma uchumi? Mimi binafsi nimeamua kutoendelea na uraia wa Tanzania kwa kuwa Tanzania hamna maendeleo na haitaendelea kwa kuwa tuna viongozi wapumbavu na wananchi wajinga wasiofanya lolote kuwapa presha viongozi wabadilishe sheria na kuingia katika karne ya 21 badala ya karne ya 17 tulionayo sasa. Bora pesa zangu niziweke hapa Marekani kuliko kuzipeleka Afrika, sioni mabadiliko yoyote Tanzania, maendeleo tunayoyaita maendeleo ni mambo ya 1970 an 1980. Tunachekelea supermarket utafikiri biashara ya supermarket ya mlimani itatuweka katika ramani ya dunia kibiashara. Mpaka serikali ikiwaleta wafanyabiashara wenye hadhi duniani kama watengenezaji magari na ndege, ndio tutaweza kusema kwamba tuna maendeleo. Hapa tunafurahia kuwa na Supa inayo uza bidhaa za nje, wakati viwanda vyetu vinashindwa hata kuzalisha chupi kwa kuwa hatuna umeme wala akili. Akili tuliyo nayo ni ya kutukanana na kutayarisha Ms tanga, Dar, Upanga, utadhani itatusaidia kutufanya matajiri. Wenzetu akina Singapore na Korea Kusini walikuwa masikini kuliko sisi miaka ya 1960, lakini angalia walipo, sidhani kwamba walikuwa wanapoteza muda wao kufanya Miss temeke na kuwaita akina Jay Z kutupotezea muda wetu, Je Jay Z kajenga kitu kuwasaidia wananchi wapate kazi au kaweka kitega uchumi wowote? tusiwe wapumbavu jamani, tuamke na kuwatimua viongozi wapumbavu. Nataka kuona Tanzania inatengeneza IPOD na PC yake mwenyewe kabla hatujapitwa na akina Vietnam na Mayanmar.

    ReplyDelete
  18. Mtoa Maoni, Anonymous, Monday, November 27, 2006 4:13:23 PM, usiingize sana antanov katika ili ya Richmond Development Corporation. Antanov, kama nijuavyo, ni kampuni ya ndege za cargo. Baada ya Richmond kushinda (sijui kwa tenda ama vipi) kuipatia Tanzania jenereta za umeme, ilibidi watafute msafirishaji wa bei nafuu, kama antanov (Rusian mafia)!

    Je, hizo jenereta za G&E ni mpya?
    Je, ni za umeme wa masafa yapi (240 (umeme wa Tz) au 110 (umeme wa USA) Voltage/

    Kwani kama ni 110V itabidi waweke tena booster ya kuuwezesha kufanya kazi ki-Tanesco. pengine ndio maaana ya kuchelewesha kuziunganisha!

    ReplyDelete
  19. Ama JK ana kazi kweli kweli maana watendaji wake sio wakweli hawana uhakika kile wanacho kifanya. Ndio maana hawana taarifa kamili lini genereta hizo zi
    takamilika - TENGA

    ReplyDelete
  20. Wazungu wanaendelea kututawala, sasa kwa akili ya kutudanganya pamoja na viongozi wetu wa juu. hosea

    ReplyDelete
  21. Born Again Pagan, nakubaliana nawe kuhusu kiasi cha voltage level ambayo hilo generator litazalisha. Hatu- boost voltage level, bali tuna-transform kwa kutumia transformers. Zaidi ya hayo voltage level ni kitu cha msingi kabisa unapo design generation, distribution hata consumption, hivyo nafikiri hilo si tatizo la kuchelewesha. Tatizo la kuchelewesha ni technical know-how ya hao Richmond na maswala ya kutafuta MBUZI aliyeKONDA kwa bei KUBWA.

    ReplyDelete
  22. HIKI NI KICHEKESHO. KWELI TUMEKWISHA. UKITAKA CHUNGUZA HIYO PICHA. UNAONA HIZO CONTAINER NDOGO MBILI SAMBAMBA NA HILO BOX LA JENERATOR HAPO KWENYE PICHA? HAYA YALIKUJA SAMBAMBANA NA HICHO KIJENERATOR KUWAPUMBAZA WATANZANIA KUWA NI JENERETOPR KUBWA! JUST UMAGINE KUKODISHA NDEGE KWA AJILI HIYO, KAMA NI CONTAINERS YA MAINGINEER YA KUHIFADHIA VIFAA MBONA HAPA DAR ZIMEJAA TELE? ILISHINDWAJE KUSAMBARATISHA HIYO INGINE NA KUILETA IKIWA NA UJAZO MODOGO, HIVYO WAKATUMIA NDEGE YA KAWAIDA? WALIFANYA MAKSUDI ILIKUONYESHA NI JENERATOR KUBWA LAKINI UKWELI NI NDOGO TU NA SIO YAKUTISHA. WASIWASI MKUBWA NI KAMA ITAWAKA, AU ITATOA KIWANGO CHA 20MW WANAZOSEMA.

    ReplyDelete
  23. Suala hapa siyo kusoma wapi suala lililopo tanzania ni uzandiki na ufisadi wala hakuna chochote rushwa itaendelea kututafuna mpaka nchi iote vidonda hakuna cha nani wala nini.

    hakuna asiyejua matatizo tuliyonayo tanzania yanasababishwa na nini hata ukisoma havard University hata Zile University zilizoko mass hatutaweza kufika tanzania ukaendeleza nchi hiyo hapo.

    Tatizo kubwa tulilo nalo tanzania sheria zote zilizopo kwenye ile nchi ni sheria zinazotamanisha (Zinamaindisha) rushwa, sheria ambazo hata wanazozitunga, wanazozisimamia wanazielekeza siyo kwa masilahi ya nchi hila ni kwa mtu aliyeshika madaraka(aliye kwenye kitengo husika) hakuna anayejua kuwa leo hii anaweka sheria ambayo inaweza kulinda nchi hata vizazi vijavyo.Sheria zinabaki kwenye mwenye madaraka muda huo. Nchi zilizoendelea sheria zao ziko wazi. Sisi hata wanaozisimamia hawazijui vizuri(hapa ni makusidi/matamanisho/kukaa ofisini na kusubiri kusaini makabrasha tu na lazima yawe na cha juu)

    Kwa hiyo haya makampuni unaona hapo watu wako bussy, unaweza kuwaona mwezi ujao hivyo hivyo bussy au wakiweka umeme unakuwa kila siku ni wa kuunguza tu vifaa vya wananchi husika (kuleteana umasikini hata kuunguziana tu tv/radio) "ngombe wa masikini Hazai".

    ReplyDelete
  24. YAANI KUISHI BONGO NI AFADHALI NIKAISHI BAGHDAD ANGALAU KUNA UMEME JAPOKUWA HALI SI SHWARI. YAANI KAMA KUNA KUZIMU BASI TANZANIA NDO YENYEWE? GHARAMA ZA SIMU, UMEME, MAJI NI KAMA WHOOOAA HALAFU NA HAZIPATIKANI? HII NI AIBU?

    ReplyDelete
  25. Hata Grinaker - LTA inajenga barabara ya to Nzega - Isaka , Tinde Mwanza yenye km 200 usiku na mchana na wanatumia majenereta makubwa kwa hilo sio tatizo!!!, Ok twende kwenye mada Mnazi bay itakamilika hivi karibuni yenye uwezo wa mW 376 it means bado mW 224 kukamilisha mahitaji!!, kwa hiyo inmaana shida ya umeme ndio itakua imekwisha!!!?? Na mimi niwezi kurudi bongo!!

    ReplyDelete
  26. Ndege ya kirusi ilileta generator! Serikali haiwajui warusi.Warusi sasa hivi ni machinga wauza silaha maeneo yote ya vita barani Africa na yale yenye wahuni wanaotaka kuibua vita.Kikwete kaa mbali na warusi.Vita Africa mashariki na kati hazitaisha ukiwa karibu na warusi au wafanyabiashara waliokaribu na wenye urafiki na warusi.Ukiwa karibu na warusi au wafanyabiashara wenye uswahiba na warusi ujiandae kuona kuzagaa silaha za kirusi badala ya generator za Tanesco.

    ReplyDelete
  27. Wakati bado tunahangaikia umeme nimesikia baadhi wanatabiri kuwa nchi itakuwa imeendelea kufikia miaka 15 ijayo!!!!!?????.

    Nawaoneeni huruma waliona ndoto hizi kuwa wanafuata njia za korea, china na japan huu ni udanganyifu mkubwa kabisa. Na kufikiria kureta wawekezaji wakati hata shule zetu hazina kiwango chochote cha kimataifa. Hivi ni wawekezaji wa kuuuza karanga na manchungwa au nini?

    Nimefurahia leo kusoma the guradian nafikiri waliochangia pale ni watu wanaoona mbali. hakuna research hakuna maendeleo. Watu wanafikiria kuwa ukienda ukawakuta wamachinga wee mwaga pesa, mama ntilie mwaga pesa, wakulima wa tumbaku wewe mwaga pesa, wafagia barabara mwaga pesa.

    Haki ya nani ukisikia kupigwa chini ni pale ambapo unaanza mipango ya mitindo hii bila utaaramu. Pesa za nchi zinakuwa ni za kugawana tu kuwekeana mifukoni bila hata planning zinazoonyesha nchi inategemea kufanya nini? Kama ni kupeana mifukoni kwa nini watu wasome?

    ReplyDelete
  28. Mmiliki wa Richmond Mpakistan na Msafirishaji Mrusi,Tusubiri tuone. Anyway vigazeti uchwara vya ulaya vinasema hilo dege la mizigo la Urusi halina kibali cha kuweza kutua Marekani Hivi hizo Generator walibebea wapi? Zilikuwa Marekani au nchi gani? Maana sisi tuliona tu likitua uwanja kimataifa Dar es salaam.Lilikotokea hatujui.Watu wa viwanja vya ndege muwe mnatangaza hata ndege za mizigo zikija mutuambie zinatokea nchi gani labda hili nalo mtusaidie.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...