dada ailinda sawe mmiliki wa nyumba ya mitindo ya afrika sana akimfunga bintiye kilemba. huy
u mama anasifika kwa mitindo na mavazi ya kiafrika

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 28 mpaka sasa

  1. Msichana mdogo kavaa Tasbihi(Rosary) ya kikatoliki Shingoni akimlilia masaa 24 Maria wa Rosary apate mume maana biahara ya vilemba imekuwa ngumu. Wanablogu wanaume mhurumieni jamani pamoja na mtoto kuvalishwa kilemba aonekane mstaarabu!! bado tu hajarusha ndoana? nyie vipi.Msipite karibu na Afrika sana nitawapiga rungu kama hamtaki kuoa.

    ReplyDelete
  2. BWANA MICHUZI NINGEPENDA KUKUULIZA SWALI NA PENGINE NINGEPENDA KUPATA MAJIBU KUTOKA KWAKO. HIVI WEWE NI MPIGA PICHA WA SERIKALI AMA MPIGA PICHA BINAFSI? MAANA NASHINDWA KUELEWA, KAMA KWELI WEWE NI MPIGA PICHA WA SERIKALI NA UNASAFIRI NA MSAFARA WA RAIS NA NDEGE YA RAIS KWA KUTUMIA FEDHA ZA WALIPA KODI UNAWEZAJE KUTUMIA MIANYA HIYO KUJINUFAISHA MWENYEWE KWA KUPIGA PICHA BINAFSI NA KUZITANGAZA KATIKA WEB SITE YAKO? HATA KAMA HATULIPI KIASI CHOCHOTE KUANGALIA HIZI PICHA LAKINI UNAITANGAZA BIASHARA YAKO YA PHOTO POINT KUPITIA HII BLOG. NA KAMA UNAPO KUWA NA MSAFARA WA PRESIDENT UNAKUWA KWENYE CLOCK, SASA IWEJE USITUMIE MUDA HUO KUFANYA MAMBO YALIYO KUPELEKA KWENYE HUO MSAFARA UNAANZA KURANDA RANDA MITAANI KINSHASA KUPIGA MIPICHA YA WATU WAKO KWENYE DALA DALA, WENGINE WALIO KUFA KINA PEPE KALLE, HICHO NDICHO KILICHO KUPELEKA KINSHASA? KWA NINI USIENDE MWENYEWE KWA GHARAMA ZAKO NA USAFIRI WAKO MWENYEWE UNAPO KUWA LIKIZO AMA NJE YA CLOCK? ARE YOU PAID TO DO YOUR OWN BUSINESS BY GOVERNMENT? HUONI KAMA KUFANYA HIVYO UFANYAVYO NI KUWAIBIA WALALAHOI WALIPA KODI WANAOCHANGIA GHARAMA ZA WEWE NA MSAFARA WA RAIS? SIDHANI KAMA MHESHIMIWA RAIS AMEKUWEKA KATIKA HUO MSAFARA ILI WEWE UENDE KUZULULA MITAANI KUTAFUTA MATUKIO MBALI MBALI YANAYOTOKEA CONGO ILI UTUWEKEE ILI TUJIONEE KULIKONI,NILIDHANI UNAKWENDA KIKAZI KUPIGA MATUKIO YANAYO HUSU ZIARA YA MHESHIMIWA RAIS! MICHUZI JALIBU KUTUMIA MUDA WA KAZI KUFANYA KAZI NA MUDA WA BIASHARA KUFANYA BIASHARA. NI KWA SABABU UNAFANYA KAZI NA WASWAHILI LAKINI KAMA UNGEKUWA HUKU MFANO AMERIKA SIKU NYINGI ULIKWISHA TIMULIWA KAZI. ETI MPIGA PICHA WA SERIKALI/IKULU ANASAFIRI NA BUSH NA SIYO MPIGA PICHA WA CNN HALAFU ANAENDA MITAANI KUPIGA MIPICHA HALAFU ANA POST KWENYE BLOG YAKE ILI WATU WATOE MAONI? MBONA SIKU NYINGI KIBALUA KILIKWISHA OTA MBAWA!! HAKUNA KINGINE KWENYE HII BLOG BALI NI UMBEYA NA WATU KUKOSA KAZI NA KUANZA MAJUNGU...NAOMBA UPOST HAYA MAONI ILI WATU WATOE MAONI YAO USIONE HAYA HUU NI WAKATI WA UWAZI NA MIMI NAONA YOU PERSONALLY ARE CORRUPT AND YOU SHOULD BE FIRED SO THAT YOU CAN DO YOUR JOB WHICH IS TO FIND FUNNY AND EMBARASSED EVENTS SO THAT PEOPLE CAN SEE AND LAUGH, YOUR GOAL HERE IS NOT TO EDUCATE ANY TANZANIANS BUT TO HUMILIATE THOSE WHO APPEAR IN YOUR BLOG. I ASK THOSE WHO HAVE APPEARED IN THIS BLOG WITHOUT THEIR PERMISSION AND ENDING UP CURSED TO FIND THE WAY TO SUE YOU. LIKE PRIME MINISTER DAUGHTER PAMELA, OR TAUSI AND CYNTHIA, YOU REAL DESTROY THEIR IMAGE AND I THINK YOU SHOULD PAY SOMETHING OR GO TO JAIL. I WISH YOU CAN PUT MY PICTURE WITHOUT MY AUTHORIZATION AND SEE WHAT COME UP NEXT! POST MY COMMENT!!!

    ReplyDelete
  3. Huyo mama si aliwahi kuwa YWCA Dar?

    ReplyDelete
  4. Naanza kuelewa kwanini michuzi inabidi uya edit baadhi ya maoni ya wadu wa hii blogu, watu kama dada betty hawakupaswa kupewa nafasi nashangaa anaulizaje maswali ambayo ana majibu yake sisi kama watanzania tuishio nje ya nymbani tunafarijika na picha za kaka michuzi suala la yeye kuwa mserikali ni kitu cha kawaida sana siku hizi ni kama kuwa daktari na uka wa na zahanati yako ni njia ya kujiongezea kipato inashangaza dada betty hajui hulka ya watanzania kusaidiana kitu kama kupewa lift kwenye ndege ya Rais ni jambo la kujivunia ni vitu ambavyo utavipata Bongo tu angalia watu wa mataifa mengine kama kenya na hata Nigeria wanavyohusudu Umoja wetu labda dada beti ameathiriwa na Uzungu itamchukua muda kutuelewa watanzania

    Usikatishwe tamaa Michuzi Hongera kwa kupost picha ya 2ooo , pia ukiwa pale RG kwa mlatie chukua picha unatukumbusha mbali sana hata pale JJ ikiwezekana ufike ni karibu na kwa mzee wa macharanga

    ReplyDelete
  5. Wewe unayejiita betty korrasa, Kama umekosa cha kuandika nenda kampikie mme

    ReplyDelete
  6. Betty angalia upande mwingine wa faida tunayopata kutokana na blogu hii km historia ya nchi,matukio muhimu,maendeleo ya nyumbani,umoja wetu kama wabongo,mawasiliano kupitia hii blogu ,taarifa na picha kv mazishi ya dereva alieditopeliwa,etc. Michuzi anachofanya ni ujasiriamali,dunia ya sasa iko leveled na watu binafsi wana uwezo wa kufanya mambo makubwa hatuhitaji makampuni wala serikali(soma kitabu the world is flat).
    Ni kweli watu wamekashifiwa na michuzi binafsi hafurahii hii tabia ndo maana akaanza kuchuja maoni ya matusi na kashfa. Hivyo Da betty toa maoni na kuboresha zaidi blogu acha hasira.Lakini imeonyesha tabia yetu mbaya watz ya majungu na uzushi hivyi ni nafasi kwetu kujijua kupitia hii blogu na kujirekebisha.
    Mwisho dunia ya sasa ni ya uwazi na kushindana kwa hoja na pia kukosolewa hadharani na ndo tunavyofanya hapa,acha watu wakosolewe hapa waziwazi inasaidia wengine kujirekebisha.
    Mwisho kabisa hii blogu ni burudani tosha na inagusa nyanja zote za maisha na kutuunganisha wabongo,sisi tulio nje tunajiskia nyumbani sana kupitia hii blogu,ku update kiswahili chetu,etc,etc,etc.....
    Michuzi keep it up!Liverpool imekeep it up too!

    ReplyDelete
  7. Dada Bety Korrasa,

    Pole sana maana inaonekana kama una matatizo kwenye ndoa yako sasa unaona kila kitu kwako kina kasoro,yani umechanganyikiwa akili.

    Kwanza unaonekana ni limbukeni sana kufananisha nchi ya Tanzania na Marekani,are you out of mind????? Hauoni hata katiba ni tofauti na uchumi ni tofauti kabisa kuzifananisha!!!!!!

    Pia si sahihi kuingilia shughuli za watu,Michuzi anakuhusu nini kuhoji utendaji kazi wake?kama hawajibiki vya kutosha basi ni wajibu wa mwajiri wake kuona hilo na kuhoji lakini sio wewe au hangekuwa anawajibika basi angefukuzwa kazi.Ina maana wewe ukisafiri kikazi hautatoka kwenda popote mara baada ya kazi au semina? Wacha ujinga wewe mama usichanganye atatizo yako ya nyumbani na shughuli za watu,au unaona michuzi anafaidi sana huku wewe unabeba mabox?!!!!!!!!!!!!!!!!!

    Acha Majungu betty hayana faida.

    ReplyDelete
  8. Naomba Michuzi weka picha ya Betty Korrassa usiandike chochote zaidi ya jina lake halafu tuachie wanamtandao wa blogu tuliosambaa dunia nzima tu-commend kweli tupu kumhusu bila kuweka uongo hata punje moja.

    ReplyDelete
  9. Bi betty uko dunia ya ngapi dada yetu? Halafu unaonekana wewe una roho mbaya sana! haiwezekani utoe maoni yenye kuonyesha jinsi gani usivyoridhishwa na kazi ya mwenzio.. Unaonekana ni mbinafsi sana. Mungu akubariki ujifunze kukubali kazi za wenzako na sio kutoa maoni ya aina hiyo siku nyingine.

    ReplyDelete
  10. nakubaliana na betty. kwa kweli kwa wengine kinachofanyika ni the famous but degrading "punch" iliyokuwepo UDSM. ina humiliate baadhi ya watu it aint fair.

    ReplyDelete
  11. Betty, Michuzi anaonyesha alivyo makini katika kazi yake. Maana upigaji wa picha imemuingia saana, badala ya kuwa kazi imekuwa hobby na vice versa....

    ReplyDelete
  12. BETTY, INABIDI UKUE BWANA, MBON AUNAKUWA HUELEWI MAANA YA BLOG??? NAOMBA UFANYE RESEARCH NA UJUE ZAIDI HOW BLOGS WORK, SIYO TU KUMLAUMU MICHUZI, KWANI KAMA ANAFANYA KAZI SERIKALINI NDIYO ASIWE MWANA-BLOG? GROW UP...

    ReplyDelete
  13. Maoni yote yaliyotolewa chini ya picha hii ni ya 'WENDAWAZIMU' maana hayaendani na picha! Watu wanahitaji kukua kichwani! Tuache kufuata upepo, angalau tujue kusoma na kuandika maoni yanayoendana na picha, sio kukurupukia mijadala isiyo na kichwa wala matako!

    ReplyDelete
  14. Wewe Betty,Haya sasa uliomba Michuzi apost maoni yako na watu watoe maoni bila shaka umeyapata maoni kwelikweli?
    Tatizo umetumia chuki na jazba mno kutoa maon yako. Siku nyingine usijeandiaka utumbo wako hapa kabla hujautafakari kwa kina, Sawa? Kakojoe ukalale sasanayambafuu we!

    ReplyDelete
  15. Betty uwe makini wakati wa kuandika information itakayosomwa na public, maana kuna watu makini wanaweza kusoma ndani ya ubongo wako unavyojieleza na kufahamu lengo lako la kuandika waraka. Huenda ulikuwa na mood sio nzuri ukaamua kumshambulia michuzi leo, sasa vuna ulichopanda dada yangu. Michuzi hiyo kamera isilale njaa lete vitu vitu mwanangu. Camera iwe ya serikali au ya Michuzi kama inatunzwa vizuri hakuna shida kuitumia. Sioni kama michuzi anashindwa kuwa na kamera yake maana anavyosafiri nafikiri anapewa allowance, isitoshe maana ni fani yake lazima atakuwa na vitendea kazi, sioni kama ataopna kamera nzuri katika kusafiri kwake ashindwe kununua camera? Tandika kazi mzee michuzi:

    ReplyDelete
  16. Kulikuwa na mdau mmoja ambaye alimwomba Michuzi atundike tarehe 10/13/2006 yafuatayo (mdau huyo na Betty Korassa wanakerwa kisawa):

    Ndugu Michuzi,

    Salamu.

    Ninayo yangu matano : Kwanza, wewe ni mwandisi wa magazeti (mpigapicha). Sawa. Kuna kitu kinaitwa kwa lugha ya Kiingereza, "intellectual property", na kinalindwa sana kwa heshima na askari wa doria aitwaye, "copyrights". Kwa muda mrefu, umekuwa ukitundika, tundika mapicha mengi ambayo mengine ni copyrighted. Na baada ya kuyatundika, naona unayalinda na askari wa doria hao hao, kama copyrights yako. Pengine, sielewi. Lakini huu ni wizi mkubwa.

    Pili, ki-journalism, kuna kitu kinaitwa “freedom of expressions”. Lakini wengine tunaamini kuwa uhuru wa kusema au kuandika kitu chochote, in the name of “freedom of speech” bila social nidhamu, ni wendawazimu mkubwa. Ndio maana una-threaten waandikaji wa maneno machafu, machafu kwenye blogu lako, ambao hujigamba kuwa ni uhuru wa kutoa maoni na kuwasiliana (kutuma na kupokea news, information and propaganda nzuri au mbaya - propaganda ambazo wakati mwingine wataalamu wa mambo ya communication huita “political and social propaganda”. Lakini kwa upande mwingine, we must be very informed when we attempt to trudge on this thin-cutting edge: censorship! For time may come when vya wale walio “high priests” tu ndivyo vitapokelewa na kutumwa ili visikike – a one-way information generation – na ku-control minds za walalahoi au walio nje ya mainstream.

    Tatu, unapendelea sana u-paparazi wa vilivyo vizuri tu - monuments nzuri. Tuletee picha za walala hoi pia kwa wingi tuone the daunting Tanzanian condition, na tujaribu ku-contribute to resolve the obtaining ugly situation. Tuelemishe bila ya kutupaka na one-sided stories. You may not be feeding us with news, information or education but numbing propaganda, which may numb us to death! Nina uhakika kuwa wana-blog wana ability ya kupambanua na how to remain sane katika ulimwengu wa sasa in which we are bombarded with instantaneous information. If some cannot, let us educate them; they have the ability and capacity for such functionally informative education.

    Nne, sina ubaya na yale uyafanyayo. Hii inatusaidia sana sisi Watanzania wa ughaibuni katika kuona yale yatokeayo nyumbani ki-picha. Na pia husaidia wa nyumbani kuona yale yatokeayo ughaibuni, hususani, safari za viongozi wetu na wawakilishaji wetu. Picha, bwana, huzungumza mara elfu moja kuliko maneno ya kuandika. Picha ni "gestalt" - inapenya moja kwa moja hadi kwenye kiini cha "psyche". Ndio maana ni rahisi kwa washiriki wa blogu hii kupenda sana kuandika, andika "comments" zao. Maneno ya kuandika, kwanza lazima ujue kusoma neno moja, moja. Halafu utunge sentenso na para kabla ya kuunda picha (kuelewa) kile usomacho. maneno ni "linear". Lazima kuyatunga moja, moja, kama shanga!

    Mwisho, wewe ni mpigapicha wa Gazeti la Daily News (gazeti la serikali au la umma). Nielemishe, kama nimekosea. Sijui kama kila wakati unatumia kamera yako ama ya kazini na pia kupata picha ambazo wakati mwingine tunaziona kwenye blogu lako. Kutumia kamera ya kazini kwako na kwa kuwa wewe una uhuru wa kupata picha kutoka kwenye archive ya Daily News - picha ambazo mimi siwezi kuzipata kwa urahisi bila kibali na kuzitumia - huoni kuwa hapa kuna kile kiitwacho katika business transactin environment, "conflict of interest" au kujinufaisha?

    Kwa kuwa haya niliyoandika yana uzito mkubwa ki-blogu, napenda sana yasomwe pia na waheshimiwa wana-blogu. Tuzidi kupanuana constructive mawazo; ni maarifa mazuri.

    ReplyDelete
  17. KWA TAARIFA YENU MICHUZI HANA GUTS ZA KUWEKA PICHA ZANGU NITAMSHUGHULIKIA KISHERIA.SIONI SABABU YA YEYE KUPIGA PICHA BINAFSI WAKATI WA ZIARA YA MTUKUFU RAIS. ANAPASIKA APIGE PICHA ZINAZO HUSU HIYO ZIARA. MIJITU MINGINE HUMU HAMUNA AKILI NI MAJI TU NA PUMBA NDIYO ZIMEJAA, ETI AWEKE PICHA ZANGU NYOO MBONA NITAKWENDA NA SHERIA? WAKINA PAMELA LOWASSA NA TAUSI MBONA WAJINGA MNAKUBALI KUTUKANWA HIVYO, HATA CYNTHIA SIJUI KWANINI MNAKAA KIMYA? MWAMBIENI ASIWEKE MIPICHA KAMA ANARUHUSU MITUSI HUMU NDANI, KUVUNJIANA HESHIMA NA MIBABA IMEKALIA KUTOA MITUSI KAMA HAINA AKILI ITAFIKILI HAINA DADA WALA MAMA, SHENZI KABISA!

    ReplyDelete
  18. Wewe Betty uliyeandika mzalendo unagomba humu ndani,inakuhusu nini michuzi kuwa mpiga picha wa lolote??hayupo marekani so hawezi kufukuzwa kazi,anachofanya Its his bussiness it shouldnt be your problem at all, unaona hafai then usiangalie anachoweka thats it thats all!uvivu tu unakusumbua

    ReplyDelete
  19. Michuzi kweli hii blog ni burudani sana inatufanya tunapata fya kwa kucheka,mbavu zangu hazina kazi kwa comments za watu ha haaaaaaa haa,nakupongeza Mzee,hii safi sana

    ReplyDelete
  20. Huyu betty naye anatishia mahakamani kama vile ni yeye tu ndiye anayekujua! humu ndani ya blogu mna majaji,mawakili maarufu,mahakimu na wanasheria pia kibao.Humtishi mtu kwenye hii Blogu.Michuzi weka picha ya Betty Korasa mpige hata akiwa kwenye kundi halafu tuletee tum-identify wenyewe.Inaelekea anafikiri kwenye blogu kumejaa wahuni tu hajui kuwa hata maprofesa wa sheria wamo.Mlete huyo bibie weka picha yake michuzi.Unamuogopa au unamtaka Michuzi? Kama huleti picha yake tutakubadilikia michuzi tukugeuzie kibao.Maana yake lugha anayotumia betty inaonyesha kama kamama kalikograduate juzijuzi tu sasa kanajitutumua na tumaterial twa notisi kalikofanyia mtihani karibuni.

    ReplyDelete
  21. Dada Betty naona unatoa ushauri mzuri wakuto kutoa matusi kwenye hii blog inayo tembelewa na watu wengi, hili ni jambo la busara, ila cha kushangaza tena hii comment yako ya mwisho imesheheni tena matusi??? Hata kama umewakasirikia watu walio toa matusi au kutoa comments za ajabu, onyesha mfano kwakujibu hoja bila matusi na kustick kwenye points. Nafikiri wanaopenda matusi ndio watapata mwanya wakukushambulia zaidi ila nawasihi waache kufanya hivyo maana sio ustaarabu. Pole lakini maana haya mashambulizi sio ya kawaida dada yangu.

    ReplyDelete
  22. Anonymous wa leo 12:18:54PM Umenichekesha kwasusema huyu dada ame-graduate juzi juzi. Au kwa vileumeona amejikanyagakanyaga na katu-english kaliko toboka toboka hapo juu unaona ndio kaimshomile. Ka inglish bwana hata mlevi akisha weka maji safi kanatokatokamo kidogo, hivyo kasikufanye ukamwona anayekitoa toa kainglish kuwa ni inshomile.

    ReplyDelete
  23. Kaka Betty,

    Naomba kwanza upunguze munkari.

    Ungemuhoji kwanza Kaka Michuzi kama huwa anaenda kupiga hizo picha kwa baraka za mwajiri wake au anatoroka tu.

    Mimi ninavyoelewa fani ya uandishi wa habari inabidi uingie mtaani kutafuta habari. Huwezi kukaa ofisini ukatayarisha habari umekaa kwenye deski. Tena kwa mpiga picha anapaswa zaidi kuwa mtaani akijaribu kunasa picha za matukio mbali mbali.

    Sidhani kama Michuzi akiambatana na msafara wa rais kama mpiga picha/mwandishi wa habari kwa pesa yetu ya kodi anapaswa kuwa amesubiri tu muda wote apige picha watu alioandamana nao. Nadhani anasababu za msingi kabisa kurandaranda mtaani akitafuta habari au matukio anayoweza kuandikia makala atakaporejea ofisini kwake.

    Kwahiyo nakuomba Kaka Betty, usiwe na wasiwasi, nina imani kwamba wakubwa wa Michuzi wanatambua umuhimu wa fani yake na wanampa baraka zao mara zote anapokuwa mtaani iwe majuu au bongo darisalama, akitafuta habari.

    ReplyDelete
  24. Sista Betty mara ya mwisho umeDate lini? au kuombwa namba ya simu? inshort ushatongozwa hivi karibuni? maana unasound hujalifaidi for a while!!!! hasa nyie watu wa ughaibuni mnapiga sana schedule. Try to take care yourself okay? Trust me u will be fine

    ReplyDelete
  25. I totally agree with Betty japo kuwa small minds zimemcriticise sana.....Betty has a point.Michuzi go back to Rioba for more ethics.

    ReplyDelete
  26. wee betty mbona hamna mtu aliyekulalamikia kama hufai kitandani lakini wewe unawaambia wenzako hawajui kazi zao wee vipi au tutaje majina ya watu waliosema parformance yako poor.

    ReplyDelete
  27. betty, u sound really frustrated with something (or someone) and u are venting it out on kaka michuzi. if i can analyze you properly u must be a mid aged woman with sexual frustrations (not married yet huh?) either due to the fact that u dont get enough or you cant get any at all...u seem somehow learnt but you are claerly very angry with the male gender and hide behind the little education you may possess...u want attention but dont know where to get it (or how) because if i guess correctly you must be a sight for sore eyes (ugly) and naturally this must be why u arent gettin any....did ur parents ignore u as a child, didnt guys want to date u...talk to me i promise i will listen....free your p****y and the rest will follow darling...

    ReplyDelete
  28. Betty chukua dakika tatu nzuri, fikiria ulichoandika kama ungependa kiandikwe juu yako...hebu kaa kimya anza kufikiria sasa...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...