UZINDUZI WA TAWI LA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) LONDON.

Ndugu wananchi na wapendwa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Kutakuwa na mkutano wa Watanzania wote ambao wangependa kuwa wanachama wa CCM hapa London kujumuika pamoja katika mkutano wa kuzindua chama hicho siku ya Jumamosi tarehe 6/01/2007.

Mkutano huo utafanyika katika hoteli ya Holiday Inn iliyopo Brend Cross Shopping Centre. Mkutano huo utaanza saa tano. Tafadhali zingatia muda.

Agenda ya mkutano huo:

1.Wana CCM kuchaguana na kuunda uongozi wa muda.
2.Mikakati ya kukiimarisha Chama hapa London
3.kupanga tarehe ya uchaguzi
4.Mengineyo

Kufika kwako ndiko kufanikisha tawi la CCM hapa London.
Tafadhari orodhesha jina na anuani yako kamili na namba ya simu kwa ajili ya kujiandikisha kupata kadi ya CCM ili Jumamosi uweze kupata kadi yako.
Tumia barua pepe ccmlondon2007@yahoo.co.uk.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na waandalizi wa mkutano huo kwa namba ya simu:07765697578
"KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI"

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Ndugu Michuzi,

    Post hii inanifanya nijiulize swali moja, hivi inawezekana kweli kwa chama cha siasa kilicho katika nchi nyingine kufungua tawi katika nchi ya kigeni? Tawi hilo litasajiliwa kwa shughuli zipi hasa? Nakumbuka hapa tulikuwa na ofisi za FRELIMO, MPLA, Pan African Congress n.k. lakini hawa tuliwatambua kama wapigania uhuru, ndiyo maana tukawapa ofisi na kuwahifadhi, vipi kuhusu CCM au CUF kuwa na matawi kule ughaibuni? Taratibu za kimataifa zinasemaje? Inakubalika? Kwamba kuna wanachama wa vyama mbalimbali vya siasa pande mbalimbali za dunia, hilo si jambo geni, lakini kuwa na tawi lenye uongozi kamili wa tawi katika nchi ya kigeni? Naomba wadau mnielimishe. Hili ni jambo jipya kwangu.

    Asanteni.

    ReplyDelete
  2. hello wana ccm, tunashukuru kwa kuwaza jambo la maana la kuimarisha chama. Tunaomba mtupatie address kamili na station y6a kushukia na nani atakua mgeni rasmi

    ReplyDelete
  3. Michuzi asante sana kwa kazi nzuri unayofanya, niko London lakini ajabu napata habari nyingi zinahofu watanzania hapa kupitia blog yako hii. Habari kama mkutano wa wa Tanzania, miss eastafrica n.k. Usengwile
    Sufa Mpunga

    NB:Ukiwa London usikose kututembelea Lewisham. mpunga@hotmail.com

    ReplyDelete
  4. hao waasisi wa hilo tawi mbona hawajitaji majina?

    pia kuna wasi wasi kwamba hawa wanataka kujijenga wakati rais kikwete atakapofanya ziara hapa mwezi januari.

    lakini ndiyo siasa zilivyo.ukitaka kushikana mkono na rais kavu kavu huwezi, lakini ukitaka anzisha shughuli ya kumvutia mambo yako yatakunyookea.

    sawa sisi tupo, tuone na caf wakianzisha kama watu watanuniana.

    ReplyDelete
  5. wow! hii mpya sikujua kuw achama kinaweza kufungua ofice nchi za nje. sasa je kama chama hicho hakitawali nchi kwa wakati huo si ndio kuanza kujenga magaidi? Ila serikali iwe makini kwa sababu ni vyama vingi vitafungua office nchi ya nje na who knows nani watakua wadhamini wao. Afadhali chama kikiwa na office kwenye nchi inakuwarahisi kuki monotor na kujua ni nini kinaendelea. Ina maana wananchi hao wiwa wanavote wata vote kutumia residency address za TZ au watakua wanatumia na absent ballot? Naomba mnifumbue macho. I am very politics challenged

    ReplyDelete
  6. Hujaulizwa hupo wapi ANYOMOUS acha pumba kijana kila mtu yupo kiwanja hapa sasa tulia kijana na mabox yako!!

    ReplyDelete
  7. We Gegedu sio kila mtu alio kiwanja anabeba mabox. Kuna wa Tanzania wako kiwanja na ni madaktari, engineers, wengine busimessmen, wengine hata huo uTanzania wameuacha na wamekuwa maraia, wana passport ya dark blue yenye eagle. Kwa hiyo hiyo concept ya kubeba mabox, ni fikra finyu mno.

    ReplyDelete
  8. we gegedu acha ulimbukeni kwa kuwa mmabo na mambo ya zamani ya kudhani kwamba miloko ughaibuni ndi wajanja, kwa sasa nyie ndio malimbukeni wajanja walionaazo bongo huku, huku kuja matanuzi kwa muda tu.

    ReplyDelete
  9. Wewe michuzi na siasa zako humu unaanza mwenyewe. Kwenye siasa kuna matusi. Watu wakicheza siasa unaanza kulalamika na kuanza kuchuja maoni ya watu. kumamamako mbichi hata ukichuja haya yangu lakini utakuwa ushayasoma. CCM na London wapi na wapi?
    Wewe unapenda kujipendekeza kwa "wakubwa" wa kibongo, na ndo maana kila siku una "post" kale ka picha kako unamuendesha JK kwenye mtumbwi kwenu Nyegemba huko.
    Shauri zako.

    ReplyDelete
  10. Anony wa 5:35:42 AM. points zako za mwanzo kumpinga GEGEDU ni nzuri, lakini unaposema watanzania wameuacha u-tanzania na kupata pasipoti nyingine sijui unamaanisha nini. Kwani hao kwa mujibu wa sheria ya Tanzania, si watanzania tena. Hatuna "dual citizenship" Tanzania. Labda tuuanzishe mjadala huu wa dual citizenship.

    ReplyDelete
  11. Hata mie nikipata uraia wa eagle wa blue, naukana utanzania. Hakuna kitu muhimu kama kuwa raia wa U.S., kwani ukiwa nje ya U.S. ukakwama, unaenda embassy na embassy inahakikisha una rudi U.S. hata kama huna hela ya nauli, hawaachi raia nje hata siku moja. Idumu U.S. milele.

    ReplyDelete
  12. Achana na huyo fala ana mawazo bado ya kizamani eti kuwa na passport,unaona raha sana kuitwa mtumwa siyo au kwa kuwa huna kitu kichwani huko unaona raha kabisa mustarehe

    Falaa wewe ANONYMOUS nenda shule na ujue nini na ufahari ya mtuu kuitwa mtanzania au USA AU UK,pimbi kabwala wewe!!

    Eti doctor,doctor gani anaweza kutoa mawazo pumba kama hayo yako?wewe mchambishaji wazungu tuuu hapo nitakuelewa cunt!!

    ReplyDelete
  13. Jiungeni.Wengine kupitia huko mtajulikana na kuweza hata kuteuliwa na kugombea vyeo mbalimbali msaidie kujenga Tanzania.Hiyo ni Platform yenu ya kupandia ngazi za uongozi kuanzia katika chama au serikali itumieni msibeze tu.Watakaowahi kuitumia wakifanikiwa msije wengine kupiga yowe!

    ReplyDelete
  14. Safi sana, nimefurahia jambo hili kwani nyumbani ni nyumbani. Tunafahamu kwamba dunia imekuwa ndogo, kwahiyo haya yote yanawezekana. Kuishi London hakutotofautiana sana na kuishi Dar, Tanga, Mwanza, Beijing au Tokyo. Kwahiyo basi unaweza kufanya mengi tu hata kuendesha biashara zako ili mradi unatumia fursa zilizopo kikamilifu. Kama tunavyojua treni la utandawazi linapita, kama hutapanda utaachwa tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...