
nikiwa newala na wadau ambao walinipa taff sana ughaibuni.
naomba idhini ya kubandika picha hii katika muendelezo wa mjadala wa faida/hasara ya uraia wa nchi mbili. nawashukuru waliochangia nawakaribisha tena wao na wengine kuuendeleza, nikiwa bado sijaridhika na wachangiaji waliosema kuishi ughaibuni ni bora kuliko bongo.
naomba niulize; hivi kuna aliyekatazwa kuchakarika akiwa bongo kama anavyochakarika akiwa ughaibuni? yaani nguvu kazi hiyo na ujasiriamali unaotupwa huko vikifanyika kwenu kuna ubaya gani?
roma haikujengwa kwa siku moja. kuna mahali walianzia hao waroma, kwani pamoja na shida zilokuwepo 'hawakuzamia' kwengine, wakabaki kwao hadi roma ikajengeka. sasa kama watu mnaingia mitini mnamtegemea nani awajengee bongo yenu, huku mkisahau kwamba huko kuna waliovuja jasho na damu hadi kukawa kama mlivyokukuta? hapo sizungumzii walio masomoni na nia ya kurudi baada ya kuhitimu. nazungumzia nyie mliomaliza masomo na kukacha kurejea kwenu kwa visingizio kibao!
nyumbani ni nyumbani tu, hata kama ni pangoni!!
hebu chungulia hapa: Introduction Video ya Investment in Tanzania
Wewe noma. Inaonyesha upeo wa mawazo yako. Hivi unazania hatu inverst bongo. Unazania basi tunakaa huku tu.
ReplyDeleteKwasababu sasa hivi sio hata mambo ya uraia tena ni oooh mkimaliza shule mnazamia. Wewe shukuru mungu ulipata hicho kikazi na sasa hivyo vihela mnavyopewa mkiwa njiani umefungua photo point. Angalia majority ya watu walioko huko wamemaliza shule wanamaendeleo gani huko na hao wasomi tu ambao wako TZ wanafanya kazi tuuu lakini hela haipo. Maneno mengiiiii kila kukicha nitafutie shule basi nije huko. ...Hao wanaotaka kuja huku wamemaliza mlimani sasa wewe unachosema ninini??? Kwanini watu wametumia elimu ya bure na baada ya hapo wanakuja tena kuzamia huku? Watu wangapi wamesoma mlimani nasasa hivi wako huku????
Kuna mtu ameondoka bongo amemaliza muhimimbi na amefanya udoctor kidogomuhimbili. Amekuja huku kafanya mtihani na sasa hivi hela anayoipata kwa siku ni hela aliyokua anapata kwa mwaka muhimbili. Sasa utamlaumu?.
Kama unaona home unamake zaidi it is better ukae huko na kama nje ya nchi unapata zaidi ni bora pia. Sioni kwa nini unataka watu warudi nyumbani wakati hamna kazi za kufanya. Hivi unazania tukimaliza shule basi tunaishia kubeba babox tuuu. Mabox tunabeba tukisoma...
Use your brain man...it is your blog but you put it in public for everyone to read and the more you express your feelings the more you show how low you can go and how less knowledge you have.
Mara unaita watu wakimbizi, wazamiaji what is the point? Unaona watu tunaoishi nchi za nje wajiiiiiiiinga....Utajiju...
Don't blame the piper when your children starve
mimi niko nje miaka nane sasa sina mengi ya kukujibu ila linalonikera mimi ni ubabaishaji wa serikali zetu,ubinafsi wa viongozi wetu namaanisha rushwa iliyokithiri miongoni mwa viongozi wa ngazi zote za serikali,mwisho huduma mbovu za jamii naanza na shule,hosipitali na sizungumzii dar pekee bali hadi mikoani ambako hali inatisha,nikuulize michuzi kuna sababu ya msingi tanzania haina maji safi ya uhakika na tuna kila vyanzo vya upatikanaji wa maji,na kwa nini tanzania haina umeme na tuna kila resource,na kuna awamu nne zimepita zimefanya nini? kujenga magorofa dar,viongozi wetu wanapaswa wabadilike na wawe wabunifu kutatua matatizo kama hayo,na viongozi wengine wanaamishwa kutoka wizara hii kwenda nyingine na hakuna mabadiliko yoyote,na wamekuwa serikalin tangu mimi natambaa.kwa hiyo michuzi hivyo vitu vinakera kinoma,kwa hiyo kuvujwa kwa jasho kuanzie kwa hao viongozi, wawe mfano bora kwa jamii.
ReplyDeleteKwa ninavyojua mimi TZ unemployment bado ipo juu, kuna wasomi wengi wapo bongo ambao hawajapatiwa ajira ktk fani walizo somea. Walio nje ya nchi warudi tu pale watakapo hakikishiwa ajira , pia isiwe anapewa ajira tu kwa sababu kasomea nje. kama kuna mtu amesomea fani hiyo hiyo yupo Bongo basi apewe kipaumbele kwanza.
ReplyDeleteWalio nje wanaweza kuchangia uchumi kwa kuwekwza Bongo, kitu ambacho kita ongeza mzunguko wa hela. Nasikia pamoja na Marekani kuwa na matajiri wengi wawekezaji wao wengi wanatoka nje, ule mzunguko wa hela ndo unainufaisha nchi na sisi tunakimbilia huku kutafuta ajira. Labda mfano wa pili unaweza mchango wa Wamexico walio marekani illegally, nasikia wanachangia millions of dollars ktk uchumi wa nchi yao.
Kwa hiyo mi nadhani kama kutakuwepo na uraia wa nchi mbili itasaidia kuwapa watu options ya nini wanataka kufanya wakiwa wapi.
Kuna faida kubwa sana ya kubaki U.S. baada ya kumaliza shule. Kama umepata kazi baada ya shule, inalipa zaidi ya kazi za Tanzania. Kwani hata huko Tanzania watu wanafanya kazi kwa kutegemea kulipwa mwisho wa mwezi. Sioni tatizo kama mtu ataamua kubaki hapa na kufanya kazi ambayo itamsaidia yeye, na familia yake. Mtu huyo huyo akienda Tanzania kwa elimu aliyonao, hatalipwa mshahara wa kuridhisha. Kama mtu aliyemaliza technical college anaweza kupata/kulipwa Tsh.30 million kwa mwaka, kwa nini mtu mwenye college degree ambaye ana chance ya kulipwa zaidi ya hapo asibaki U.S. Kitu kingine, kama hujawahi kuishi U.S., utakuwa na idea za ajabu ajabu kuhusu watu kurudi nyumbani, lakini ukishaishi humu, ukalinganisha na Tanzania, ndio utaelewa umuhimu wa kufanya kazi U.S., na zaidi ukiweza kuupata uraia, ni bora zaidi.
ReplyDeleteSABABU ZA KUAMUA KUKAA UGAIBUNI NA KUTO RUDI NYUMBANI MIONGOINI MWA WATANZANIA WENGI;
ReplyDelete1. DOCTOR BONGO MSHAHARA $ 500.00 USA DOCTOR MSHAHARA $ 10,000+
2. NURSE BONGO MSHAHARA $ 65 USA NURSE MSHAHARA $3000+
2.MUOSHA VYOMBO BONGO MSHAHARA $ 10 USA MUOSHA VYOMBO $ 2500+
3. MATIBABU BONGO LAZIMA KULIPIA LAKINI USA MATIBABU BULE KAMA HUNA INSURANCE
4. ACCOUNTANT(CPA) BONGO MSHAHARA $ 2000+ USA ACCOUNTANT(CPA) $6000+
5. MBEBA BOX BONGO MSHAHARA $25+ USA MBEBA BOX $ 2000+
6. NYUMBA YA KUPANGA BONGO YENYE KIYOYOZI, HEATER, NA UMEME WA UHAKIKA $ 800 USA $ 375-700
7. BONGO MAGONJWA KAMA TYPHOD, KIPINDUPINDU,MALARIA,AMIBA, NGOMA TUNAONGOZA NA DAWA HAKUNA KWA WAATHIRIKA USA HAKUNA TYPHOD, MARALIA, AMIBA, NA UKIMWI TUKO CHINI DAWA KIBAO KWA WAATHIRIKA.
6.CHUO KIKUU HAKUNA CHAKULA, MADAWATI, MIZENGWE YA WALIMU NA SERIKALI MINGI. USA HAKUNA MIZENGWE, DARASA NA MADAWATI VINAENDANA
SASA MICHUZI NAWEZA KUORODHESHA VITU VINGI TU MPAKA UKACHOKA KUSOMA ILA NINACHOWEZA KUKWA MBIA KAA CHONJO TUNAWEZA KUJA NA KUANZISHA STUDIO YA PICHA MPAKA YAKO IKAIONA NI MAVI KUMBE FUNGA DOMO ENJOY KUDANDIA NDEGE YA KIKWETE!
Uraia wa nchi mbili na Kuishi nje ya nchi ni mkakati wa kupata nguvu ya mtaji wa fikra,fedha na teknologia ya kuwekeza nchini kwako pia.Wajapani walisambaa dunia nzima lakini baadaye wakarudi Japani na sasa Japan ni tishio la kiuchumi na kibiashara.Walichota mawazo,Technologia,na uwezo wa kifedha wakarudi wakautumia kuibadilisha Japan kila eneo.
ReplyDeleteNchi nyingine ni China.China imepeleka watu wengi dunia nzima wenye una sasa wanarudi na kuwekeza nchini kwao na imeanza kuwa tishio kubwa kiuchumi na kibiashara kuanzia sekta ya umma hadi ile ya binafsi.
Sekta binafsi ya India inasomesha sana wataalamu mfano wa Computer nchi mbalimbali duniani na wengi wanarudi na kujiajiri India.Na ni tishio dunia nzima.Makampuni makubwa ya komputa duniani yanawafuata huko huko India na kuwapa tenda za mabilioni.
Uraia wa Nchi mbili ni msaada katika hili.Uraia wa Nchi mbili si mbaya ila tujipange vizuri.Tuwe na mkakati kama nchi.Tunahitajiana wale wa ndani tunawahitaji wa nje na wa nje wanatuhitaji kinachotakiwa kuwe na kiunganishi kizuri (linkage)ya namna ya kuunganisha juhudi za ndani na nje ili tujenge nchi yetu.
koloboi@yahoo.com
MICHUZI KAMA MAANONY WOTE HAPO JUU WALIVYOZUNGUMZA TZ KUNA VUNJA SANA MOYO MTU AMEJITAHIDI NA SHULE KAFATA SHERIA ZOTE ZA KUPATA MAFANIKIO LAKINI MWISHO WAKE NI KIMSHAHARA CHA $500 AKAFANYIE NINI? HUKO KUCHAKARIKA UNAKOKUITA WEWE BONGO KUFAFANUE VIZURI KWAMBA UWE MJANJA KUIBA MALI YA UMMA(WIZI)UKIIBA UKIJENGA GHOROFA NA KUWA NA KAAINVESTMENT FULANI BASI KILA MTU ATASEMA WEWE MJANJA.....LAKINI KWA WENZETU SIVYO UKIUMIA LEO LAZIMA UTAKULA KESHO KAMA ALIVYOSEMA ANONY HAPO JUU INATIA UCHUNGU SANA KUONA KUNA WATU WENGI SANA WANAKULA KIULAINI BILA KUCHAKARIKA KWA KUTUMIA MIGONGO YA WENGINE NI WANGAPI BONGO WAMEFANIKIWA KWA HAKI? LABDA ASILIMIA 1 TU NA WEWE UNALIJUA HILO SASA MICHUZI HAKO KA PHOTO POINT ULIKOKAFUNGUA BAADA YA KUPATA EXPOSURE TOKA UGHAIBUNI NA VIHELA VIWILI VITABU ULIVYOIBA NA ALLOWANCES ZA TRIP ZA KIKWETE UNANGUVU YA KUANDIKA KWA KASHFA KABISA ETI WAZAMIAJI!!! MICHUZI WEWE UMEPATA NAFASI YA KUCHUKULIWA NA JK KAMA MPIGA PICHA WAKE SASA UNAJITUTUMUA,NI WANGAPI WANAPATA NAFASI KAMA YAKO? UNAJISIFIA MWENYEWE INDIRECT KWA VIJIENDELEO ULIVYOPATA HA HA HA HA.
ReplyDeleteAMA KWELI BINADAMU HANA SHUKRANI HATA UMPE NINI YAANI MICHUZI HIZI NDIZO FADHILA UNAWEZA LIPA WATU? KWA KUWATUKANA KIASI HICHI HAKUNA CHA MJADALA HAPA WALA NINI MF. MICHUZI ALITEMBEA SANA USA MWAKA 2006!!!! KTK MATEMBEZI HAYO NA KUTEMBELEA WABONGO WOTE WALIOMKARIBISHA KWENYE NYUMBA ZAO KUMPIKIA UGALI NA BAMIA NA MAHANJUMATI YOOOTE,
ReplyDeleteKUMPA ENTERTAINMENT ZOTE HIZI NDO SHUKRANI ZAKE KWENU.NAWASILISHA NA NAOMBA SANA UTOE WATU WASOME WAKUELEWE.
Hivi hoja hapa ni uraia wa nchi mbili au kurudi nyumbani?
ReplyDeleteBinafsi kabla sijatimka nilikuwa mfanyakazi serikalini, yaliyonikuta ni aibu kusimulia !
Personnel manager alikata msharara wangu kwa sababu binafsi hakuna aliyemnyooshea kidole ! hata baada ya kumaliza kozi kede kede sikupewa promotion ,sasa kama una face vitu kama hivyo kwa nini usiondoke? Pamoja na kuitwa wazamiaji ,wakimbizi majina yote lakini through vijimiradi vyangu bongo i managed to create employment to more than 25 people! Which i never dreamt of when i was in Bongoland, created accommodation to 8 families ,madalali nao walijipatia chao .
Lets be realistic tujue zaidi uzuri na ubaya wa double nationality mfano mtu yoyote ambaye ni criminal hii sio option kwake, ni kwamba ukiharibu Bongo na una uraia wa Holland huwezi kurudishwa kufungwa jela ya Holland ule kuku na TV utawekwa segerea ulikoharibu! Hii ni kuangalia mikataba ya kubadilishana wafungwa baina ya nchi na nchi.
Kwa investors inafupisha process za registration ya kampuni , kuapply kwa ajili ya TIN numbers ect, na mambo ya land ownership.
Nafikiri hata huu msemo wa ‘’nyumbani ni nyumbani’’ wengi wetu hatuuelewi vizuri matokeo yake tunapotosha tafsiri yake hasa.
People wake up and let’s focus on what we can do for our Tanzania! No matter where you are it can be done if each one of us plays his/her part.
Naona historia imekuponyoka kidogo kaka Michudhi. Roma haijajengwa na waroma. Usiione Roma inavyopendeza vile ukasahau kuwa hilo ni jasho la mababu zetu. Waswahili wasilisema mchumia juani.... Si vibaya tukiwasaidia mambabu zetu kulia kivulini.
ReplyDeleteKuhusu suala la kurudi Bongo baada ya kuhitimu masomo, ni gumu kidogo. Nyumbani ni nyumbani ila kinachoangaliwa saana ni maslahi. Ilhali sheria haivunjwi sioni tatizo. Wengine wanasoma kwa mikopo, leo hii wamehitimu na kurudi bongo unafikirii itawachukua muda gani kulipa hiyo mikopo??? Mikopo ya wanafunzi wa mlimani yenyewe (ambayo haifikii hata robo ya gharama za shule huku) kazi kuilipa kwa maisha ya bongo.
leo hii waliomaliza shule ughaibuni wote wakarudi Bongo unafikiri kutakuwa na photo point (za uhakika) ngapi?
Wazo la bure Kaka Michudhi... Fikiria mara mbilimbili (ikiwezekana fanya utafiti) kabla haujatoa maoni na kushutumu.
Kheri ya mwaka mpya kaka.
Roma imejengwa na mababu zetu, jasho la mababu zetu lile. Mchumia juani..... Sio vibaya tukawasaidia mababu zetu kulia kivulini.
ReplyDeleteKwa kozi za kawaida BA hapa US (Hadi kuhitimu) tunaongelea si chini ya $ 35,000, hapo haujala haujavaa, haujalipa pango nk. Nimekopa hizo hela ili niweze kusoma, leo hii nimemaliza nikarudi bongo, unafikiri ni sehemu ngapi ninaweza kupata kazi ya kulilipa hilo deni?, kwa muda gani? fanya uchunguzi ujue ni idadi gani ya wahitimu wa vyuo vya bongo wame(na)lipa madeni (mikopo) waliyopewa kujisomesha, halafu ujiulize kwa nini kuna wanaoshindwa kulipa mikopo hiyo.
Je unafikiri wahitimu wa ughaibuni wakirudi Bongo ajira za wahitimu wa vyuo vyo bongo ikakuwa vipi? sasahivi yenyewe wahitimu kibao wenye taaluma zao wanafanya kazi zisizo za taaluma zao, tena zenye maslahi kiduchu. (Leo hii wapiga picha wote wakatazwe kupiga picha, unafikiri kutakuwa na makonda, wapiga debe wangapi??? )
Kaka Michudhi nafikiri ingekuwa busara ukafikiria marambilimbili kabla ya kutoa maoni yako na kutoa kashfa.
Kheri ya mwaka mpya wanablogu wote.
Michuzi husiwe one sided, jaribu kutumia kipaji chako sijui cha uhandishi wa habari au kupiga picha. Kila mtu anataka akae Tanzania lakini mazingira ndo yanafanya watu wakimbie au wakimaliza elimu zao wakae huko huko hata kama watafanya kazi tofauti na fani zao. Kumbuka nchi kama Philipine, 60% ya income inatokana na remittances zinazotumwa home kwao toka nje na wafilipino tena wanafanya kazi za ovyo (Kumbuka Lebanon juzi alipopigwa na Israel, over 20,000 people toka filipino wanaofanya kazi za kuosha vyombo and whatever wanafanya kazi Lebanon). Point si kuchakalika Tz, bali ni kuinvest home.
ReplyDeleteBwanaa Michuzi unajua sasa hivi tupo kwenye globalization era, yaani ni kujichanganya pamoja na investment(whatsoever level of investment). Hata kama hutaki, huwezi epuka globalization (hata wewe pia ndo maana una hii blog na studio). So acha jamaa ambao upeo wao uko mbele wachume na baadaye wanalia TZ.
Kwanza TZ kazi nzuri wanapeana watoto wa vigogo, tenda wenyewe kwa wenyewe, wewe shukuru mungu umetoka mbali na Kikwete ndo maana tutakuona kila sehemu anapoenda Kikwete ( fikiria mpiga picha mwenzako ambaye safari yake ndefu ni kwenda Kibaha tumbi hospital ikitokea ajali). So nafikiri jaribu kuwa na positive thinking and fresh and beautiful mind. Hawa jamaaa wanaokaa nje wape muda ila wakirudi mtabanana kwenda mbele.
Du naona michuzi leo wamekuweza kuongezea tu viongozi wetu waache tamaa angalia serikali ya awamu ya nne kushika madaraka tu Tsh imeshuka kichizi kwani hata ma-investors wamestuka kuona watu wale wale wenye kupenda rushwa wameingia tena...hicho ni kipindi cha mwaka mmoja tu wewe utaniambia eti nirudi na elimu yangu wakati viongozi wetu hawapendi kukosolewa especially in this modern technology era...ndio maana watoto wangu waendelee kusoma huku ughaibuni nitakuja kama mtalii na kuacha vidola vyangu ila bado nakumbuka bongo ilivyonitesa...
ReplyDeleteasante sana kwa msemo wako michuzi lkn mimi ninachotaka kukukumbusha ni kwamba hata wewe hukuzaliwa hapo dar es laam ninavyojuwa humetokea kijijini ambako kunaitajika sana na nguvukazi tena wanasema kilimo ni uti wa mgongo kwanini hurudi kwenu kijijini na ukawasaidia wanakijiji kukiendeleza badala ya kugangania hapo dar? hila mimi ninanvyojua wewe uliona huko kijijini mambo hayakuendei vizuri ukaamua kuwaterekeza nduguzo pamoja na wanakijiji wenzio kusudi hukasake maisha dar namungu kakujaria umeweza kujichanganya sasa wacha kutupiga madongo maisha ni popote wacha izo michuzi
ReplyDeletemawazo yako yanawakilisha watu wachache sana hapa Bongo kwa kua wewe umenufaika hapa sio wengi wetu wenye hiyo bahati ndio maana kwenye blog yako watu unaowasifia ni walewale kama wanne hivi.
ReplyDeleteMichuzi, kuwa na nidhamu ya kisayansi katika kuprozi your risechabo question! Wewe una-generalizi kwa ku-insinuate kwa inuendozi kuwa wengi wanapenda "kukacha kurejea kwenu kwa visingizio kibao," kwa sababu wanaonekana kuwa ni wakimbizi wasio na uzalendo.
ReplyDeleteWanafunzi wengi wamekuja na skolashipu za umma, wengine wanajisomesha wenyewe. Wengine wamebakia ugaibuni kwa vibali vya serikali ya Tanzania!
Kwa nini unawasakama tu wanafunzi walioamua kubaki ugaibuni bila kuwasakama maafisa wa kibalozi wanaoamua kubakia kufanya kazi na mashirika ya kimataifa baada ya kuambiwa kurudi nyumbani? Na wengine kuchukua utaifa, kwa mfano, wa Kimarekani!
Hello Michuzi.
ReplyDeleteUnajua hizi mada unazopandisha zinaanza kuonyesha ni jinsi gani wewe mwenyewe unavyoanza kuaribu profile ya blog yako. Blog yako ni ya picha na sasa unaanza kuleta hoja ambazo kwangu mimi naona hazina msingi. Kuishi nje na kuishi nchini Tanzania yote ni choice ya mtu. Wewe unaye ishi huko hatujawahi kuleta dharau kwamba ni mjinga au haufaidi. Hakuna aliyewahi kufanya comparison kama hiyo until wewe unapoamua kupandisha hii hoja. Wengi wetu tunaoishi huku tunasidia ndugu na jamaa walioko huko. Sasa wewe unapoleta kauli zisozo na msingi nashindwa kukuelewa kabisaaaa!!!!!
Hata China imenufaika na Uraia mara mbili. Kweli masikini akipata .......
ReplyDeleteWell!! Nyie achacheni kumpaka MICHUZI, Hata Mimi niko VIWANJA (mwaka wa tisa huu), kinachosemwa hapa siyo kwamba mrudi nyumbani ila tupakumbuke,, Dunia imebadilika if you are smart you can make money and enjoy life anywhere. Tusaidie kujenga nchi yetu,, invest ,, there is money there (Mimi nimesha invest na faida zake nimeziona nakwenda BONGO kila mwaka sometimes twice) nyumbani ni nyumbani ,,,
ReplyDeleteKwa Sisi wahindi nyumbani ni popote unapopata chakula au riziki yako pawe India,Tanzania,Uingereza,Canada,au Kwa Mfuga Mbwa pale Buguruni cha msingi ukiona Canadakuna chakula unaacha uraia Tanzania unaenda Kanada.Lakini kwa waswahili ni shida nyumbani ni pale babu zenu wamezikwa.Mnapenda sana kukaa na makaburi.Washirikina sana nyie Waswahili.Ndio maana kuhamia sehemu ingine mnaona shida shauri ya kuendekeza kuwa karibu na makaburi ya babu na bibi zenu ambao hawakuleta chochote cha maana cha maendeleo katika nchi.Na nyinyi mtakufa maskini kama babu zenu na bibi zenu kama hamtakuwa tayari kwenda mataifa mengine kutafuta riziki.
ReplyDeleteSwali linalopaswa liulizwe na hasa wewe Michuzi ambaye uko karibu zaidi na wakubwa wa Tanzania, ni kwanini wanatuambia kwamba shule za Tanzania ni nzuri, na kwamba kuna kila kitu Tanzania lakini watoto wao, na ndugu zao wengine wote wanawapeleka kusoma South Africa au ughaibuni? Na kwanini wanakwenda shopping New York? Kama kila kitu kiko nyumbani kulikoni?
ReplyDeletemwandishi hapo juu, bwa michuzi hailizi unaenda kutembe Tz mara ngapi kwa mwaka . Anataka urudi Bongo , kwa sababu roma haikijengwa kwa siku tatu . Michuzi ameanza kuchanganyikiwa, kisa ameweza nunua kamera kadhaa
ReplyDeleteMICHUZI,
ReplyDeleteIWE NI URAIA MMOJA AU 'DUAL', SWALA NI KWAMBA NAWAUNGA MKONO WOTE WALIOSEMA MAISHA NI POPOTE. SITAKI KUHARIBU WALIYOSEMA YOTE MAZURI KUHUSU KUCHACHARIKA UGENINI. Kifupi, uko sehemu gani siyo issue, ila unafanya nini ndio cha maana. Ndio maana watu wanakimbilia Dar es Salaam toka mikoani wakitafuta maisha bora, japo hayapo. Ila nia yao ni njema ya kutafuta ubora. CCM imewadanganya siku zote wabaki waliko vijijini ikidai ndiko kwenye uti wa mgongo sijui, lakini wapi.
Sasa Michuzi ukiwavutia nyumbani wabongo kwa hoja tu ya uzalendo wa kuonekana Bongo, utakuwa sawa na hao wazee wa CCM. Hata rais wako amekuwa akililia walio nje wafungue mianya ili wabongo wenzao wajipatie kazi huko. Unadhani hajajua Bongo ni noma? Bongo hakuna promose ya life kama walivosema waungwana wengi. Waliobaki hapo wamebahatika kuwa na nafasi, au wamepewa na 'god fathers'.
ASANTE.
Madaktari Tanzania watimkia Dafur,Afghanistan
ReplyDeletehttp://www.mwananchi.co.tz/mwananchisite/Mwananchi/Habari/Habari0.asp
chonde chonde wabongo wenzangu tulioko majuu,tuache kumshambulia michudhi binafsi bali tushambulie au kujadli hoja anayoileta kwetu.mimi sidhani kama yeye ni mjinga sana au labda ana wivu na sie kuwa huku kwasababu nina uhakika hata yeye ana uwezo wa "kuzamia" na kuja "kubeba maboksi" huku ng'ambo,ila nashawika kuamini kuwa lengo lake ni kujaribu kuchokoza mada tu yeye akiwa kama fanani ili sisi hadira tuingie kuanza kuicheza.hata serikali inapokuwa inapita kukusanya maoni kwa wananchi tayari inalo jibu kichwani ila inataka kujua watu wengine wanawaza nini juu ya hilo jambo.inawezekana kabisa kuwa ndugu yetu michudhi ameshakula tenda ya kimyakimya ya kukusanya maoni ya watanzania wa ndani na wa nje kuhusu uraia wa nchi mbili au uwekezaji nchini kwetu na watanzania walioko nje.sioni sababu ya jazba,chuki au matusi na dharau hapa.ni ukweli usiopingika kuwa kazi nyingi nje ya nchi yetu zinalipa zaidi ya kufanyia nyumbani na hata mazingira ya kuishi na kufanya kazi ughaibuni ni bora zaidi ya yale ya kule kwetu.tujifunze kupokea mada na kuijadili kwa hoja nzito kama walivyofanya wadau wengine hapa ambao wameorodhesha kabisa ubora wa vitu na huduma nje ya nchi na kulinganisha na nyumbani.safi sana.mada nyingine zinaweza kukukera na kukuudhi ila uungwana na ustaarabu ni kuziendea kwa hoja na mifano madhubuti.nakataa kukubali kuwa alie nje au ndani ni bora zaidi ya mwenzake,pia si kweli kuwa wote walioko nje hawatak kurudi nyumbani kuwekeza au hawawekezi kabisa tanzania.vilevile naona ugumu kuamini kuwa wote walioko nyumbani hawawezi "kuzamia" huku na kujitafutia maisha.kila mtu ana mtazamo wake wa maisha,wapi aishi na vipi aishi.haya maneno kama mzamiaji,mkimbizi au kubeba boksi sioni kama ni mabaya hivyo kama ambavyo wengine wetu wameyachukilia hapa,nadhani ni sehumu tu ya kupandisha watu munkari ili kupendezesha mjadala.tusitukanane na kudharauliana watanzania,michuzi ni muandishi wa habari tumuelewe jamani.pia tuache kukanyagana wenyewe bali tukanyage mpira-tuishambulie hoja na sio mtoa hoja.hata hivyo huyu ndugu ya ngu hapa juu amenisikitisha sana kwa dharau na matusi yake dhidi ya watanzania,hasa ndugu zetu walio bongo.hivi ndivvyo wahindi mlivyo? lakini ujue kule kwenu India,Pakistani,Bangladesh,Burma,Sri Lanka,Maldives,n.k kuna shida sana na nyie na sisi wala hatuchekani.kwa ambao tumewahi fika mijini na vijijini India tunajua maisha yenu kinagaubaga,na ushukuru sana mungu tanzania imekuwezesha kupata visenti vya kuja huku ng'ambo;yote tisa,kumi unatafuta nini ktk mjadala huu wa watanzania? MUNGU IBARIKI TANZANIA,MUNGU WABARIKI WATANZANIA POPTE PALE WALIPO. JJ,UK.
ReplyDeleteMichuzi umechemsha vibaya sana. Kuchachalika bongo maana yake ni kuwa mwizi, mfujaji wa mali ya umma, muuza unga, kufadhili majambazi na watu kama wewe kumsifia Kikwete na Lowasa hata kama wanaingia mikataba kama ya Richmonduli.
ReplyDeleteWewe annoy 5:07;39 pm akili yako ndogo tu pia. Kwani hata ukikaa miaka 100 na kwenda bongo mara 2 kwa mwaka ndio nini? Jinga tu...watu wanaenda kila two months wamenyamaza kimya wewe kwenda mara mbili kwa mwaka unaona basi tena. Wewe kukaa miaka 9 unaona mingiiiiiiiiii..... Wenzio wanawa jukuu huku. Jinga tu. hebu ongea swala lililoulizwa na michuzi. Kwanini wabongo wakimaliza shule hawarudi nyumbani??? Wewe ni wale ungambire stupid infront of my wife nini??? You must be....
ReplyDeleteRiziki ni popote,kazi ni kazi na nyumbani ni nyumbani,Kila mtu ana upeo wake na kila linalofanyika japo halitudhuru basi na liwe heri kwetu kwa nduguzetu na nyumbani kama walivyowakilisha wadau hapo juu viongozi wa tz wakibadilika kila mtu atapenda kurudi,kwa nini tusitafute na kujifunza mengi tukiwa nchi zingine kuliko kulumbana nao mwisho wa siku huna maisha?
ReplyDeleteMichuzi usitishwe na wengi waliochangia hoja ambao wameonekana kukupaka sana.Ukizingatia utakuta kwamba karibu wote wanazungumzia kuajiriwa na kupata mishahara mizuri kama wanayoipata ughaibuni.
ReplyDeleteWanachopaswa kufahamu ni kwamba mtu ukielimika maana yake ni kwamba akili yako imepanuka na inategemewa kuwa na uwezo wa kuangalia maisha kutoka "angles" mbalimbali.
Kama mazingira ya kupata ajira Bongo mtu haridhiki nayo kwa nini asitumie elimu au ujuzi alionao kutengeneza uwezekano wa kuwa na ajira binafsi? Hakuna siku ambayo kila Mtanzania anayetaka kazi ataipata na kwa mshahara anaoutaka yeye.
Badala ya kung'ang'ania mishahara mizuri ambayo mwajiri wako atakupa kwa nini usijiamulie mwenyewe maisha yako kwa kutumia ujuzi wako kujiajiri? Being your own boss has never been a crime.
Ni kweli kwamba mazingira ya Tanzania si mazuri lakini hiyo haimaanishi mtu ukitumia busara huwezi kufanikiwa,hao walioko Tanzania na wanafanikiwa je wote ni wabadhirifu? Hapana, tatizo ni kwamba Watanzania tuliharibiwa na siasa ya ujamaa iliyodumaza uwezo wa binadamu wa kufikiri na kuchakarika ndiyo maana hata nchi zingine za palepale Africa zinatushinda kwa mfano kibiashara na uzalishaji.
Watu jifunzeni kuangalia mbinu zingine za kuishi msipigie mahesabu kuajiriwa tu,dunia ya leo haiendi kwa mwendo huo peke yake!
Poa muhindi point yako imefika lakini usitutukanie babu zetu. Mimi nipo India sasa hivi but I can't wait to finish what I am doing and come back home. You know why I rather live na hayo makaburi ya kwetu kuliko hapa India. Sisi huko hatuwabagui lakini hapa mmezidi... mambo yenu ni kwa class tu...the country is dirty, crowded and so forth lakini sijawahi kukutukania huyu babu yako mchafu hapa ambaye kikwapa kinamnuka kama nini. Okay Thanks
ReplyDeletenjoo ulaya wewe michuzi wacha wivu kila siku attack zako ooh ugaibuni ooh sijui nini we right here and will never go no where
ReplyDeleteWhat is the point of dual nationality? If the Tanzanian High Commission in London do not answer, or return our calls, why bother with dual nationality. Kama Ubalozi unatutelekeza hakuna haja ya kuendelea na Uraia wa Tanzania. My Tanzanian passport expired years ago and I did bother to renew it when new ones were issued. When visiting my folks in Tanzania I just apply for a visa with my British Passport. No hussles. I visit Tanzania as often as I want.
ReplyDeleteThe country should put more effort to look after her own citizen. If she does not fulful her obligation even abroad, people have no option but to renounce thier citizenship.
However, It should be born in mind to acquire another country's nationality does not mean one has forsaken his/her Tanzania roots. I am Tanzania through and through. Even in Tanzania we have "Tanzanians with Asian oring" who still maintain and are proud of their roots. Most of them came to Tanzania when their forebears came to contruct the colonial railway networks. Majority have not even set thier feet in Indian but still they are Indian by roots and culture.
mlokole unatudanganya sasa. how could you renew a tz passport while you already have a british passport? ...lol...you can't hold a tz passport at the same time you have another's country citizenship...that is what people are talking now "dual citizenship". Au ndio nyie mliojifanya wasomali nini sasa hivi hata hukumbuki wapi ni wapi....
ReplyDeleteMlokole hiyo passport itumie vizuri rudi shule it is free with your passport....hiyo english duhh.....
ReplyDeleteMICHUZI, ZAIDI YA ASILIMIA 70 YA MA-ENGENEER SILICON VALLEY NI WAHINDI, OUTSOURCING YA MABILLIONI YA DOLLAR IMEISHIA BANGALORE, INDIA! MADINI YOTE TANZANIA YANAUZWA NA WAGENI, WANAOFAIDI FAIDA KUBWA YA SIMU ZA MKONONI HAPO BONGO NI WAGENI(BEI A BONGO KBWA KULIKO UGHAIBUNI), KINA CELTEL, VODA, ETC. DUNIA YA LEO SIO KUKAA HAPO ULIPO, NI KUSHINDANA DUNIA NZIMA!!
ReplyDeleteMimi sioni kwa nini Michuzi anatukanwa kutokana na kuanzisha mjadala huu.
ReplyDeleteKama wewe hau fit hiyo categorization ya waliozamia je kinakuuma nini? I think kuna umuhimu wa kufikiria vitu alivyosema. Tatizo letu sisi watanzania mtu akianzisha topic ambayo ina ukweli tunaanza kutukana - Kumbukeni kwamba sio lazima ku-agree, na it is okay to disagree, na pia sio lazima tufikie makubaliano. Kila mtu aseme anachofikiria bila kumtukana michuzi. This is a valid topic kwa sababu hata serikali imeanza kuzungumzia hili swala.Kwa kusoma vitu walivyoandika watu wengine tunaweza kujifunza kutoka kwa watu wengine.
Mimi nimekaa nje ya nchi kwa karibu miaka 11 sasa, nilikuja kusoma na sasa kinachonibakisha hapa ni kumalizia kulipia elimu yangu na pia mwenzi wangu naye anamalizia kusoma, then tunarudi bongo for good. Nina degrees tatu, na nimejaribu kuwasiliana na kampuni nyingi tu kuona kama kuna uwezekano wa kufanya nao business as contractors na most of them wako interested. Pia tumekuwa tunaangalia uwezekano wa kuanzisha biashara zetu wenyewe, na uwezekano ni mkubwa sana. Just be creative, fikiria nini unapenda kufanya combined with your education, than come up with some ideas, talk to people and see if you can come up with some moneymaking ideas.
Ukiangalia some of the comments above, wengi wanazungumzia kukosa ajira, mishahara midogo, viongozi wala rushwa - hii ndiyo mentality yetu sisi watanzania, badala ya kufikiria kujiajiri, tunafikiria kumfanyia kazi mtu mwingine. Tunalalamika viongozi wetu wala rushwa je tunategemea nani atakayerekebisha hayo mambo nyumbani?, Je tulimwacha nani nyumbani atufanyie hiyo kazi? Tunakaa kwenye forums tu tunalalamika na kutukana, instead of doing something about it. Tunategemea nani ataleta mabadiliko na maendeleo katika nchi yetu?
Watu tunafikiria kutengeneza hizo dollars sijui pounds chache ndiyo kuukata and then what? Kuna watu ambao wanatengeneza $20K per year anajiona ameukata, wakati hawezi ku save hata $50 per paycheck - hela yote inaishia kwenye bills. Wengine wanafanya kazi ili waweze kujirusha on weekends - Shame on us. Mtu akishakuwa na gari na apartment anajiona ndiyo mwisho wa dunia. Afadhali hata wanaonunua nyumba wana akili kwa sababu hiyo ni investment that can go a long way. I understand kwamba maisha nyumbani ni magumu, lakini kama uko nje ya nchi chukulia kama hii ni opportunity ya kutengeneza hela - SAVE MOST OF YOUR MONEY na kujifunza kutoka kwa wenzetu, halafu turudi nyumbani tukasaidie kuendeleza nchi yetu.
Najua kama kawaida yetu mtanitukana but i could care less
Hakuna sababu ya kumlaumu michuzi. Yeye ni mchokoza mada ili tuijadili.
ReplyDeleteNionavyo mimi suala la ulaia wa nchi mbili lichukuliwe kama ktk kuhama kwa wanyama au ndege kutoka kwenye ukame kwenda kwenye neema. Ukame ukiisha wanarudi. Kwa hiyo tusiwalazimishe watu warudi kwenye ukame kabla haujaisha na pia tusiwazuie kurudi ukame ukiisha. Mbona miaka ya nyuma watu walikuwa "hawakimbii" nchi kama sasa? majibu tunayo. Kwa hiyo, kutokuwa na dual citizenship kwa dunia ya leo ni kuwanyima mianya ya maendeleo wananchi na nchi kwa ujumla. Kuna mambo mengine ya maendeleo huna haja ya kuumiza kichwa, bali una transfer knowledge toka nchi moja kwenda nyingine.
Nataka kwenda marekani au Kanada kusoma hivi ni vyuo gani vya bei rahisi? Dar mikwala vyuoni mingi.Roho mbaya nyingi.Mara mwalimu asije lakini mnapewa Coursework marks za bure ili kuwafurahisha.Mimi nataka elimu hasa sitaki marks tu Sababu najilipia mwenyewe. Nataka niende nje ya nchi tu nipate elimu ya uhakika.Vyuo gani niende? Nisaidieni wanablog.
ReplyDeleteNashangaa watu wanamshambulia Michuzi kwa kuanzisha mada muhimu. Baadhi wamejaribu kuonyesha uzuri wa kuishi ughaibuni eti kwa sababu mshahara wa ughaibuni ni mkubwa kuliko mshahara wa bongo kwa profession ile ile. Tofauti ya mishahara nakubaliana nayo. Lakini swali ninalojiuliza ni je mbona hawasemi juu ya matumizi ya mishara hiyo? Je, bei ya chakula ya ughaibuni, pango la nyumba, matibabu mtu akiugua au hata kumwona daktari tu, na matumizi mengine ni sawa na bongo au pungufu kuliko bongo? Tunaweza kuona figure ya mshahara wa ughaibuni kuwa kubwa kuliko ya bongo lakini kumbe kimahesabu kwa kuzingatia matumizi yake isiwe na tofauti na bongo. Ni kweli kuwa wapo kweli WaTz waliofanikiwa kwa kuishi ughaibuli, lakini sehemu kubwa ni walala hoi tu wanaoishi kwa shida na wengine kulala kwenye gheto watu kibao. Watu wa namna hiyo wanasota kila siku kutafuta mlo wa siku.
ReplyDeleteNinaheshimu sana comments zilizotolewa na baadha ya waBongo hapa. Hawa wameonyesha hata kukaa kwa ughaibuni kumewasaidia na mawazo yao yanaweza kuijenga nchi. Lakini wapo wachangiaji wengine ambao kwa maoni waliyotoa unagundua kuwa huko kukaa kwao nje ya nchi hakuna faida yoyote kwao wenyewe na kwa nchi pia. Hawa ndio ambao Michuzi nawaita "wazamiaji," na kwa kweli hakukosea.
ReplyDeleteunajua nyumbani ni pale unapoweza kufanya maisha yakawa mazuri na kwamba ukawa na uwezo wa kuwasaidia watu wako kuna wengi wetu hali ya maisha imebadilika ukifananisha na maisha tuliyokuwa nayo bongo na maisha ambayo tunayo sasa kuna tofauti kubwa kiuwezo, kuna ambao wameshindwa sababu nyumbani baba anazo au familia ina uwezo imebidi warudi bongo sababu ndinga ya kupanda ipo akirudi nyumbani mwajuma kishapika sasa huku anapelekwa mbio anaona tabu kidogo lakini kama mtu ulikuwa unakwenda mbio bongo na jua kali lazima huku uone poa kila mtu anandinga hapa hakuna cha mwajuma kila mtu fridge open misosi ovyo ovyo nyumba ya kuishi kila mtu anaishi vizuri hapa sio bongo mpaka uwe fulani au baba yako awe mwizi fulani kwa maana hiyo kila mtu ana sababu yake inayomuweka nje na isiwe ugomvi kama mambo yako mazuri bongo tangulia mungu akijaalia tukija tutaonana
ReplyDeleteMwema, umechangia vizuri sana! Ninakubaliana na point yako kuwa sisi wantanzania tunatabia ya ku focus on the problems instead of the solution.
ReplyDeleteMimi niliishi Marekani miaka 9 nikiwa katika masomo pamoja na kufanya kazi. Uamuzi wa kurudi nyumbani haukuwa rahisi kwasababu kama watu wengine wengi, matatizo ya huku Tanzania kama kutokuwa na ajira, hali ngumu ya maisha, rushwa na kadhalika vilinifanye nisite sana. Lakini baada ya kupanga mikakati mizuri, nyumbani kulirudika na mwezi wa tano ninatimiza miaka 10 baada ya kurudi nyumbani.
(Friends and family faxed to me job advertisements which appear in the local newspapers; I applied for the jobs, was interview over the phone by several companies, and received two job offers before I had set foot in Tanzania) Mwanzo ulikuwa mgumu, na nilikwezeka sana na urasimu, mfumo dume na rushwa iliyozoeleka hapa Tanzania, lakini malengo yangu hayakuwa kumfanyia mtu kazi for the rest of my life. Kwa sasa nimejiajiri tena ninafanya kazi niliyoisomea na kuipenda (na nimeajiri watu pia) maisha niyakustruggle kama ilivyo sehemu nyingine yoyote duniani lakini I don’t regret one bit and if I had to do it again I will not change a thing.
Opportunities ziko nyingi sana hapa nyumbani na hata kama tuta criticise namna gain, serikali inajaribu kuwawezesha wazawa. Lakini kama wazawa hao hawatakuwepo basi watu wengine wata-take advantage ya hizo policies. Focus on the solutions, have the right mentality plus your education and “exposure” you can make it in Bongo.
Mwema, mwenzi wako namtakia kila la heri katika kumaliza masomo yake na nawakaribisha sana Bongo.
michuzi wewe bongo lazima uione nzuri kazi yako nzuri unakaa karibu karibu na jk akisafiri anakuchukua ukapige picha ukirudi unawapelekea picha wananchi yaani ni celebrity fulani hivi lakini miaka 20 iliyopita labda na wewe ulikuwa unaona bora nje sasa hivi lazima upige mawe sababu labda na wewe ni mtu wa ambae kwamba lakini tumekushtukia hatutaki utuonyeshe picha na sisi tunataka tutokee kwenye hiyo picha
ReplyDeleteMaoni ya Mwema na Anonym wa 11:09:30 yamenifanya nijisikie kutoa machozi. Huo ndiyo ukweli wenyewe. Mimi nipo hapa USA na nimemaliza shahada ya udaktari wa falsafa hivi karibuni. Wakati wa kukaribia kumalizia shule, nilianza mawasiliano na vyuo vikuu vitatu (SUA, UDSM na UCLAS) juu ya uwezekano wa ajira kama mhadhiri. Guess what????
ReplyDeleteKila idara niliyowasiliana nao wamenitaka niandike barua ya maombi ya kazi nikiwa bado huku, na nimeitwa kwa interview sehemu zote hizo tatu!!!!!!! Na kabla ya hapo nilifanya maongezi ya simu na wakuu wa idara hizo kabla hata ya barua kutumwa, na wote walidhihirisha nia ya kuniajiri, na kunitaka kurudi haraka maana Tanzania inatoa opportunities nyingi sana wakati huu, na serikali ya jk imepandisha mishahara na kuwa at least $1,000 (Elfu moja)kwa mwezi, ambayo si mbaya kwa maisha ya TZ, ukizingatia pia kazi hiyo inakuwa na opportunity ya kufanya kazi zako binafsi kwa kutumia utalaamu wako, ambazo zinaweza kukuingizia pesa zaidi ya za salary. Kwa hiyo niko njiani kurudi bongo na nikifika tu nitakutafuta michuzi ili tusaidiane kuelimisha wa TZ wanaoogopa challenges!!
kwa wale waliowahi kuangalia movie ya Sister Act 2 ya Whoopi Goldberg, kuna mahali anasema 'If you see a challenge infront of you, and you think that running away is good solution, then you will be running away all you life, because challenges are part of life............kama nimenukuu vizuri.
Ndiyo, ukilinganisha kipato cha hapa US ukaongeza na sifuri tatu ili kupata equivalent ya kitanzania, utaona ni pesa nyingi, lakini je Bills zinakula %ngapi ya pesa hiyo. Mwisho wa mwezi unakuta ni 100% imekwenda. Mtu unaishi paycheck to paycheck (hii ina apply kwa zaidi ya 70% ya watu walioamua kuishi huku, awe mwanafunzi au mishen town). Na hii naongelea hata kwa maprofesa, siyo tu waosha dishes!! Cheki isipoingia benki, profesa anataka kuua watu maana mkopo wa SUV (gari), nyumba (mortgage), TV set, makochi atashindwa kulipa. Wanaishia kula junkies ambazo baadaya zinawapa maradhi. Zaidi, ni professionals wachache sana wenye asili ya kitanzania wanaoweza pia kufanya consultancy hapa, sana sana waanzishe kampuni za kudeki vyoo!
kwa hiyo bado wazo la kurudi bongo ni zuri kama waliotangulia walivyotoa maoni, cha muhimu ni kuwa tayari kwa challenges zinazoambatana na transition hiyo
Tuna safari ndefu ndugu zangu
We mwema acha kujichanganya. Mara useme watu hawawezi ku save hata dola 50 mara save most of you money kipi ni kipi hapa? Tusidanganyane hapa kujiajiri Bongo? umeme, barabara na maji hakuna. Majambazi kila sehemu. Hao utakaowaajiri utawalipa elfu 80 kwa mwezi halafu wataishia kukuibia ni lini utaweza kutoka.
ReplyDeleteHalafu unatwambia eti unasubiri mwenzi wako amalize shule, kwani asiende kusomea Bongo? Baadaye utatuambia unasubiri watoto wako wamalize shule.
Nyumbani ni popote pale utakapoweza kufanya maisha yako. Kama ni bongo kama ni southpole hiyo ni juu ya muhusika. Hivi mmekaa mkajiuliza wale wazee wanaostaafu wanaishia wapi? mafao ya wafanyakazi wa EAC iliyovunjika mwaka 1977 walikuja kulipwa lini? Kuna mambo mengi sana ya kisenge samahani lugha yangu na ninadhani neno hilo ni sahihi kulitumia hapa. Rushwa tangu katibu kata mpaka raisi wa nchi. Mnaosema inabidi turudi nyumbani ili tutatue hili tatizo mnamkumbuka Horace Kolimba? Yupo wapi sasa hivi? Sio kila mtu anaakili ya biashara ndio maana kuna wanasiasa, wanaharakati,wafanyabiashara n.k. Bongo inabidi kuhonga hata kupata pensheni yako ambayo ni jasho lako sasa kama sio usenge ni nini? Viongozi wanajua wazi kuwa kuna rushwa kali sana na wao ndio vinara wa kula rushwa. Wewe kama unaona bongo kunakufaa basi tia timu kivyako usijidai kushawishi watu waende huko kwani sidhani kama ulimshawishi mtu kuja huku aliko. Kwa kifupi mtoto wa kabwela nafasi ya kufanikiwa huko bongo ni finyu sana yaani ni karibia na sifuri. Bongo hata uwe na hela huduma kama za afya ni mzozo. si unaona wazito wa nchi wakiumwa wanakimbizwa nje ya nchi? Wewe kama unaona bongo ni poa basi wewe nenda tuu na hakuna atakayekuuliza.
ReplyDeleteMimi sitaki kusikiliza chochote kwasababu I learned from my dad. Baba alikua huku 75-80. Akarudi tz na maisha aliyoyaishi hakuwa milionea. Lakini mwenzake ambaye alikata kurudi na my dad walipomaliza shule yeye ndio alinipokea nilivyokuja hapa marekani. yeye ameweza kuinverst so much back home while he is still here. Sasa wanaosema wanaona ni bora wote turudi home....noooooo.......hapa ukifanya kazi kwa nguvu na ukiwa na malengo utafanikiwa. Sio wote wanaorudi na kumake a big deal. Tumewaona na wewe unayesema umerudi na kujiajiri sasa lakini before ulikua na mtu wakuku hook mahali sasa kama ukoo wangu wote wako shinyanga nani atanihook nikifika na mashahada yangu? Ukweli tuangalie tusieme tu....easy come easy go jamani .why they say "american dream" Mimi ndugu zangu wamemaliza masters zao india hata siwaoni wanafanya cha maana huku tz. Sirudi kuishi ng'o huko hata mseme vipi. Mimi nakuja mara moja kila miaka miwili.
ReplyDeleteMichuzi huna akili wewe, tena limbukeni wa maisha, na una wivu wa maendeleo.
ReplyDeleteSawa, hata kama tunabeba mabox ughaibuni, at the end of it tuna pata sent kiasi, tunafanya mambo nyumbani Tanzania, tunaipendezesha nchi yetu na tunasaidia familia zetu, kulikoni kubaki Bongo kazi sina japo elimu ninayo.
Angalia serikali yetu, (Ooops, nimesahau wewe ni kada) but hell with you! Ni kwamba viongozi ni wale wale (recycle) tangu nazaliwa, kubadilishana tu wizara/ofisi, unless afe but still kunakuwa na back-up wanaojiita "Manaibu", leo mimi fulani japo nina elimu hata huo ubalozi wa nyumba kumi kumi nitaupata? Si bora nikae huku nipate yangu shilingi nijiendeleze Bongo na kusaidia familia yangu Bongo kwa kuwatumia pesa za shule, matibabu na matumizi kwa mengine.
Ahaaaaaaa, kitu kimoja nimegundua Michuzi, hujabahatika kuja huku kuishi muda mrefu zaidi ya Kikwete kukuoshea jina walau hata umejua kupanda ndege, tena umshukuru sana, kakuokoa huyo mshamba wewe.
Umesahau enzi zile in 1990's unapita mtaani (Kurasini) na kamera yako shingoni sole ya kiatu choka mbaya, leo na wewe unanyanyua pua jamani lol.
Ehe, na unasemaje kuhusu hao raia wengine wa nchi zilizoendelea walipo Tanzania, na wao ni watumwa ama wapo kwenye kundi gani?
Amka baba, acha ushamba. Nyumbani ni pale unapoishi, sio lazima ulipozaliwa ama kukulia.Na ukija huku nilipo hatutakumind wala nini.
Acha wivu na majungu!
NAWAKILISHA!
jamani eeh msameheni michuzi next time ukija iishia huko sheraton tusikuone kwenye majuba ya watu
ReplyDeleteThis comment has been removed by a blog administrator.
ReplyDeleteCongrats, Mzee Michuzi.
ReplyDeleteI can see that you have removed one comment. I am always impressed by your photojournalism. As the old adage goes 'a picture speaks a thousand word'. Your blog is my first port of call of news from Nyumbani. But, I sometimes get slightly peeved at some of the comments given by Watanzania wenzangu which are devoid of cogency and full of profunities.
Keep up the good work Bro. Keep us posted of what is happening nyumbani.
Michuzi ,
ReplyDeleteMimi naamini ya kuwa watu wengi katika hii bodi ni watu wazima na wanajua nini ni kizuri au kibaya kwao . Sidhani kama kuna haja ya mtu au kikundi cha watu kujifanya wanajua ni kitu gani ni kizuri kwa watu wengine.
Mimi kwa mtazamo wangu naona ni kuishi nje ni kuzuri kuliko nyumbani kwa sababu zifuatazo ;
a) Huduma za afya ughaibuni jamani ni nzuri kuna watu wengi sana Tanzania wanakufa either kutokana na magonjwa au ajali lakini ukiangalia kwa undani utagundua ya kuwa ni kutokana na huduma mbovu za afya ndio maana wamekufa . Nitatoa mfano mdogo mtu akipata ajali hapo Dar atapakiwa kwenye gari na sio ambulance kukimbizwa muhimbili ! Na akifika muhimbili anaweza asipate huduma zinazotakiwa mpaka safirishwe nje ya nchi ...Sasa waungwana sidhani kama kila mtu ana uwezo wa kwenda nga'mbo kutibiwa?
b)Mimi nina watoto na sio kwamba najisifu watoto wangu wanaenda kwenye moja ya shule nzuri na sio hivyo tuu wana uhakika wa kusoma mpaka chuo kikuu kutokana na mipango mizuri iliyowekwa. Sasa mtu anaponishauri nirudi nyumbani hatanihakikishia vipi kuhusu elimu ya watoto wangu.
c) Tanzania leo hii kama hauna elimu ya chuo basi chances zakuwa successfullkimaisha ni ndogo sana. Ughaibuni hapa mlete mtu aliyemaliza form IV na baada ya muda utaona mambo hatakayofanya hapo bongo.
Itaendelea...
Nashauri wanaume warefu wajiunge kwenye timu za Basketball wengi watajikuta Marekani Wkiwa serious na mchezo wa basketball.
ReplyDeleteMarekani wanapenda sana wacheza basketi warefu kama huyo mheshimiwa katikati kwenye picha.Hii si utani.Umbo pia ni mtaji.Nawaombeni watanzania warefu sana jaribuni eneo la kucheza basketball mtafanikiwa wengi wenu.Jiungeni kwenye timu za basketball na mcheze kwa juhudi.mtajikuta mko mbali.Naomba shule na vyuo na serikali za mitaa na serikali kuu ziwashauri watu warefu sana kupenda basketball tunaweza fanya maajabu pia kama nchi kwenye eneo hilo na tunaweza saidia wengi kwenda marekani kiajira kwenye timu.Hili ni eneo tunalotakiwa tulitilie mkazo.Tuna watu warefu sana wengi wako idle tuwa-mobilize tuwaundie timu za basketball tuwafundishe na kuwahamasisha.
Nawaomba wawekezaji katika michezo eneo hili laweza lipa baadaye kwa kuuza wachezaji timu kubwa za marekani au kwenda mashindano yenye kuingiza pesa nyingi Marekani.Anzeni kuwekeza kwa watu warefu sana.Hata kama watu hao si wachezaji na hawapendi basketball wasaidieni kuamka.
Huu ni ushauri serious sio kitu cha mzaha.
koloboi@yahoo.com
Michuzi huwezi kufananisha quality ya maisha ya mtu average marekani na bongo. Angalia zaidi huduma za jamii ndio utaona maendeleo ya nchi sio kuangali mtu kapita na Landcruiser na mziki wa juu ukasema watu wanatanua bongo... Hell no! huyo jamaa akishuka garini mwake anaumwa na mbu kibaao kutokana na madimbwi ya maji machafu yasiyoenda hapo nnje ya nyumba yake kesho ana malaria!!Bongo watu hawaishi kwa mishahara kwa kuwa haitoshi sio kama watu wanapenda kulima mchicha uwani mwa kila nyumba na kuleta harufu ya mbolea mpaka sebuleni.. Bongo watu wamejaa ubinafsi hasa viongozi. Watu wa namna hii hawajui kuwa hawawezi kuinjoy vizuri ingawa wanaona ufahari kuwa kila mtu anawakodolea macho mtaani na kuwaona wana uwezo. Huwezi enjoy mpaka wanaokuzunguka nao wana hali bora na mazingira yao yako bora pia. Tofauti hizi zinasababisha sasa hivi wenye visenti bongo wanaishi maisha ya kutolala usiku kwa kuogopa majambazi na vibaka! Maisha ni kumake popote ila tuu tusihau kufanya kitu nyumbani hata kama haturudi kuishi kwa muda mrefu.
ReplyDeleteMichuzi,mbona hivi sasa hii blog imejaa mambumbumbu?jitu linalinganisha mishahara ya US na bongo by converting dollars to Tshs.How come?Unatakiwa ucheck maisha yakoje?unaweza ukapata dollar nyingi lakini na bills nazo ni nyingi na bongo mtu akapata pesa kidogo lakini life kwake ni cheap.mbumbumbu jingine linalinganisha nyumba za US na UK,wapi na wapi?UK ni kakisiwa kadogo hivyo nyumba zao zitaendana na eneo lao sio kama US,Hivyo bruv Michuzi mie naona watu wadiscuss vitu vya maana kwa maendeleo yetu na sio kulinganisha vitu vya kipumbavu ambavyo havitusaidii kimaisha.hollaa.
ReplyDeleteCha mtoto weewe ndio mbumbumbu. Hata ukilinganina gharama ya maisha UK na TZ ni tofauti sana. Gharama ni nyingi sana UK, bills kila kukicha lakini kutokana na mshahara unaopatikana kuna tofauti kubwa sana. Tunalipa bills na tuna jisomesha, na kidogo kinachobaki tunawasaidia familia zetu nyumbani na pia tunajijenga kimaisha TZ na huku pia.
ReplyDeleteNi wangapi TZ madoctor lakini wameshindwa kupangisha nyumba karibu na mjini na saa wanapangisha Mwanerumango na Boko? Ni wangapi wakiwa shuleni bongo wanaweza kujenga pia hata kibanda cha mbuzi? Ni wachache sana tu compare na majority ya watu walio nje. 75% ya watu walio Ulaya kama hawa jisomeshi wanafanya something back home compare to 5% ya hao unaosema maisha ni mazuri TZ.
Common give me a break.
Na kama kazi zipo bongo kweli ungeita watu mambumbumbu. Huwezi kucompare gharama ya maisha au kuyalinganisha kama huja compare na ajira zenyewe. Yeah TZ gharama ni ndogo sana ya maisha lakini kazi ya kulipia hata hayo maisha ya gharama ndogo iko wapi.
Michuzi katusaidia kufungua huu ukumbi na ni vyema kuelimishana. Ni kweli maisha magumu lakini ukifanya kazi kwa bidii ni maisha mazuri sana kuliko kwa huyo mbeba mabox hapo TZ.
Wewe usikurupuke tu na kuita watu mambumbumbu kabla hujafikiria.
It is okay aliyecompare maisha ya London na ya USA ni sawa na yule aliye compare maisha ya TZ na UK. Ndio kazi zipo London lakini wanaoishi maisha USA ni afadhali kidogo kuliko tunaoishi London. Sio uongo na it is not something to be ashamed of. Sasa I guess mjinga ni wewe unayekataa ukweli na kutoa vitu kufuatia na sample ya watu wachache unaowaona Dar tu wameendelea. Wakati majority ya watu wanashida hata kama wamelimika vipi.
Don't dare to call people mbumbumbu because you real don't know them and you don't know their situations. You have the right to give your opinion but don't call other people names.
Inaonyesha jinsi ulivyo na machungu rohoni. Find a therapisty. Kam unaishi UK au USA na still huwezi kulipa bills basi wewe ndio wale watoto waliozoea kila kitu baba amfanyie ndio maana unataka kurudi home ukarithi cha baba yako. Ni lini utatengeneza cha kwako na watoto wako wajivunie. Make something for yourself. Make your own name. Hata watoto wako wataitwa wajukuu wa so and so...instead of watoto wa so and so. Ndio maana unajiita cha mtoto kwa vile hutaki kukua. Hapa UK ni parrallel ukitua tu kwenye hii ardhi sahau kuwa wewe ni mtoto wa nani bongo. Hamna cha mtoto wa fulani au fulani hapa wote tunaishi maisha sawa na ni nguvu na akili yako inayo determine your destiny.
I need some witness here.
KIMSINGI NIKWAMBA TUNASHINDWA KUELEWA BADO.UNAJUA KUCHUA URAIYA WA NJE SITO UPOTEA NIKUJENGA NCHI YAKO BADO. WENZETU WAZUNGU WAO HAKUCHUA URAIYA SIKUHIZO KWASABABU NDIO WALIO KUA WATAWALA WANCHI NYINGI ZAKIAFRICA THAT TIME. KWAHIYO WALIKUA NAUWEZO WAKU KOMBA MALI BILA HATA KUULINZWA KUJENGA NCHI ZAO. HIYO ROM MNAYO ITAJA NK. UNAJUA UKIWA NA URAIYA WANCHI NYINGINE NI BADO UNATILIA PATO NCHI YAKO, KWANI KILA WENDAPO NYUMBANI BADO INA KULAZIMU KUITILIA PATO NCHI KIASI CHA DOLLA 50 KWAMIAJILI YA VIZA.KWAHIYO MKIPATIKANA WATU MIA MOJA NCHI TOFAUTI MLIONA URAIYA WANJE, KWAKIPINDICHA MWAKA KWENDA NYUMBANI BASI MTAKUA MMEWEZESHA KUIJENGA NCHI VYAKUTOSHA, KWAHIYO SIONI SABABU YAKULALA MIKA KUA NILAZIMA TUWE NA URAIYA MBILI KWANINI WAKATI TUNA TILIA PATO NCHI. MIMI NAONA KAMA NCHIULIO INA MASLAHI YAWEWE KUA NA RAIYA MOJA NI BORA UFANJE HIVYO, KWANI NYUMBA HAWAKUKATAZI WEWE KWENDA ILAKINACHOTAKIWA ULICHANGIE TAIFA KWA DOLLA 50 TU. JEHILONIBAYA? NADHANI TUSINGELIKUA NAMJADALA KWENYE SWALAHILI. MNACHOKIFURAHIYA NIKITUGANI KWENYE RAIYA MBILI? SASA MNATAKA NCHI IKAE VIKAO WAPOTEZE PESA KWAKUJADILI SWALAHILI AMBALO LIPO WAZI? MIMI NADHANI ULIPO NDIO PAKO HALAFU UTAKUA UNAKWENU PIA, MBAKO HUKATAZWI KWENDA KUJENGA KIBIASHA NK. MIMI NAONA HAKUNA CHAKU PIGANA MADONGO HAPO SWALA LIWAZI.
ReplyDelete